Elections 2010 Dr. Slaa anguruma BBC redioni: Nimeshinda Uraisi kwa kura milioni 15...

Mambo mengine yana chosha akili kabisa..!! Ukimsikia mtu mwenye akili timamu ana support utawala wa Mh. Jakaya Kikwete ni shida kubwa na ina leta mashaka sana!! Inanisumbua kichwa kusoma post za ajabu ajabu za kumsupport huyu bwana.

Kwa kupoteza viti vya ubunge ni ishara kubwa kwamba watu hawampendi Kikwete, Hilo halina Mjadala ndani ya nchi ya Tanzania. Uongozi wa JK umekuwa na mashaka mashaka sana, Na chanzo kikubwa cha kuanguka kwa Wabunge wengi si kitu kingine bali yeye JK ndio Mhusika mkuu na mlengwa mkuu hapa. Inashangaza kuona mlengwa mkuu amepata kura nyingi wakati Mbunge wake amesha ondolewa kule jimboni kwake kwa tofauti ya kura nyingi !!!

Hatukatai kwamba inawezekana kwamba wananchi wakamchagua Mbunge toka chama kingine na rais akatoka chama kingine. Hili lipo na linafanyika sana kwa nchi za Ulaya na kwingine. Lakini kwa Tanzania niijuayo mimi, Mwananchi akichagua chama basi inakwenda sambamba kuanzia kwa diwani ,Mbunge na Rais. Na kama kutatokea tofauti basi ni kwa kiasi kidogo sana ambazo si zaidi ya Kura 50 hadi 100.

Chama Cha Mapinduzi baada ya kuliona tatizo hili la kuanguka kwa mheshimiwa JK wamejaribu kuleta hili igilizo la wenzetu wa Nchi zilizoendelea ili iwe kisingizio cha kuweza kujitetea. Kwamba Inawezekana kabisa Wananchi wamemchagua mbunge toka chama kingine na Rais toka chama kingine....HILI KWA TANZANIA BADO HALIWEZEKANI. ELIMU HIYO WATANZANIA TULIO WENGI HATUNAYO.... Kuweni wa wazi the source hapa ni Rais Kikwete. People they dont like him...Akubali au akatae. Kipindi cha miaka mitano ya mwanzo watu walimpokea vizuri kwa ushindi wa Kishindo lakini si kwa Kipindi hiki cha mwaka 2010. Hii ni sawa na wenzetu wa Marekani. OBAMA alishinda vizuri na watu walimpokea vizuri sana. Ndani ya Miaka miwili hii watu wamekuwa very dissapointed kiasi cha kuanza ku vote in other direction.

Basi na sisi Watanzania tukubali hilo.Hakuna ulazima wa mtu ambaye tunaona wazi kwa macho yetu kwamba kashindwa kutawala kumpa muda wa kuendelea kuitawala nchi wakati uchumi wa nchi unazidi kuteketea..Tumemchagua 2005 tumeona alivyo tudharirisha kwa kutukimbiza kwenye misaada wakati nchi yetu inao uwezo mkubwa wa kujiendesha endapo kutakuwa na udhibiti mzuri wa mali tulizo nazo. Ya nini tuendelee kuwa na Rais ambaye amebakiza kutuvua nguo mbele za wazungu? Kila kukicha misaada, Misaada ,Misaada. Obama kasema atatusaidia.Ili iweje? .Mtu wa jinsi hii ni wanini katika kipindi hiki tulicho nacho cha maisha? Watanzania tunataka kujitawala na kujitegemea wenyewe. Huu ukilitimba wa budget ya nchi kutegemea misaada toka nchi zingine hauna manufaa kwetu. Nchi hii inateketea..!

Nasupport chama chochote chenye kuweza kutupeleka pale ambako tuna stahiri kufika. CCM / Kikwete hatatufikisha popote. Chama hiki kimekuwa tegemezi kwa baadhi ya watu/ matajiri wachache ambao kwa manufaa yao binafsi wamekuwa wakikitumia. Watu hao hawana jema lolote kwa watanzania maskini walio wengi.

KWA UCHAGUZI HUU NAUNGA MKONO NA KUSUPPORT KUTOKUKUBALI KWA MATOKEA ALIKOKUZUNGUMZIA DR SLAA KWA MANUFAA YA TAIFA NA SI KWAMANUFAA YA CHAMA.
 
Si kiwamba tu Dr Slaa anapinga matokeo, hata sisi wananchi tunapinga matokeo hayo maana ni sisi tumempigia kura za kishindo. Ukweli ni kwamba mara baada ya hesabu ya kura vituoni kukamilika taarifa za kila kituo zilirushwa harakahara kuelezea hali halisi na maagizo yakatolewa usiku ule ule - kuchakachua!!

Na wewe unayeleta figure mbofu mbofu ya 15 mil nani kasema, nilimsikiliza Dr hajasema hivyo. Acha kuleta vurugu hapa, umetumwa wewe.
 
jamani tunataka taarifa za uhakika tupeni data tusiigeuze JF ikawa sehemu ya kuchakachua taarifa
 
Dr Slaa Songambele Wazalendo wa nchi hii tupo nyuma yako..just say a word:A S angry:
 
Back
Top Bottom