Dr. Slaa anafanya kazi kupitiliza!

Msiogope Dr yupo fit kwa kazi hiyo lazima afanye kazi kwa nguvu si unajua T2015CDM.
 
Mie nadhani Slaa afanyi kazi kupitiliza kama anavyosema muanzisha hii thread, wengine wanasema kaamua kujitolea...Slaa anafanya kazi analipwa Milioni 7.5 kwa mwezi muacheni afanye kazi.

Kwani Mukama analipwa kiasi chote kile kwa kazi gani anayoifanya?? TZS 7.5M kwa Dr. Slaa kwa kazi inayoifanya ni kidogo sana kwa sababu kuna watu wanalipwa mpaka TZS 15M kwa kazi ambayo haifiki hata 1/2 ya kile anachokifanya Dr
 
Tanzania tumezoea kuona vitambi na sasa tunaanza kuamini kama hauna muonekano wa ki-John Komba basi wewe si mzima! Tatizo la unene ni kubwa sana hasa kwa viongozi wetu. Angalia vigogo wa polisi, wanahema kwa tabu tupu na siku zote naamini, if you cannot control how much goes into your stomach then you cannot control a lot of things. Just think about it.

Nakubaliana na wewe Mkuu,Unene ni hatari sana,ila ni Muhimu kwa Dr.Slaa kupata muda wa kutosha wa Kupumzika,sehemu zingine nafikiri ni muhimu kuwatuma Vijana!

We stll need Wilbroad for many more years,He is a great man!!!
 
kiukweli bila manjonjo ya kisiasa mzee amechoka sana,ukizingatia siasa zenyewe ameeanza umri umeshasonga.ukimwangalia hata ule mkono uliopata matatizo ndio haukunjuki kabisa,hata juzi mtwara mic alikuwa ameishika kiana,CDM hawawezi kumpumzisha kiukweli ndio mtaji unaokubalika kila kona,BORA PUNDA AFE MZIGO UFIKE ndio usemi unaoonekana kusimamiwa na chama,kwa ushauri wangu CDM wajipange vizuri kwa kumwandaa zitto kuwa mrithi wa huyu mzee kwa kuwa naye anakubalika sana katika jamii ya wadanganyika.
 
kwa kipindi
nilichomfahamu dr slaa kama mbunge na baadae mgombea uraisi nikiri kuwa
mwonekano wake umebadilika sana.dr.slaa amepungua sana yaani amekonda
mno isipokuwa ubongo wake ndio haujakonda kwani bado akisimama jukwaani
anatema cheche kama kawaida.

Mambo mengi yanaweza kuwa yamechangia mfano umri lakini nionavyo mimi
cdm wanamtumia sana huyu mzee wa watu kwa kiwango ambacho nahisi
hakizingatii wala kutambua hitaji la mzee huyu kupumzika na kujenga afya
yake.dr slaa yupo kila mahali kwa kila kitu.iwe mkutano iwe oparesheni
iwe kupokea wanachama na hata mikutano ya waandishi wa habari.anazunguka
mikoani kwenye mikutano isiyokwisha.anashiriki mikutano ya ndani na
kufungua matawi.ndiyo nakubali huyo ni katibu mkuu lakini kiukweli
nahisi dr slaa anachoshwa na kuzeeshwa zaidi na shughuli hizo.

cdm wanapaswa kuinua na kuwafunda makada vijana waende huko mkioani
kukomaa na ccm ana wapambe wao na sio kumwacha dr.slaa akihangaika kama
hakuna vijana.ni muda wa heche na viongozi wenzie wa bavicha kuacha
malumbano ya kwenye magazeti na kujikita katika ujenzi wa chama
mikoani.kazi hizo wapewe kina lema ,lissu mbowe zitto nassari na wengine
ambao bado ni vijana wadogo.

kama kweli cdm mnamuhuitaji slaa katika mipango yenu ya baadaye,huu ni
muda wa kutafakari namna ya kuutumia uwezo na kipaji alichopewa na mungu
.

Nawasilisha.

Hata mwalimu Jk Nyerere alikuwa na tabia hii, wananchi wakiwa na shida sana nja au vita alikonda pia kwani nae alikuwa anaishi kama mtz wa kawaida.

Siyo hawa kina Jk kichwa na nazi wananawiri katikati ya shida lukuki za wananchi.
 
ritz, Mukama analipwa kiasi gani, do you know?

Halafu mwambie a-quantify na benefits za Mukama bila kusahau lile V8 na gharama za kuliendesha...!! Akitoka hapo akamuulize Nape analipwa bei gani....!! Kisha amalizie kwa kuangalia output ya watu hao watatu (Nape, Mukama na Dr. Slaa).
 
Pia umesahau jambo moja la muhimu, Na yule binti wa miaka 36 aliye mpora kwa jamaa anaweza akawa chanzo kikubwa kwa Rais wetu kuchoka hivyo........ Mama J taratibu bana usije muua mzee wetu bado tunamuhitaji dose kwa kipimo tafadhali
 
asante dr.Slaa naamini kazi unayofanya sio kwa maslai yako bali kwa vizazi vijavyo. mungu akubariki kamanda.
 
Mie nadhani Slaa afanyi kazi kupitiliza kama anavyosema muanzisha hii thread, wengine wanasema kaamua kujitolea...Slaa anafanya kazi analipwa Milioni 7.5 kwa mwezi muacheni afanye kazi.


Mbona mnazungumzia sana hizo mil 7. Nyiye mmesahau kama maximo alikuwa anamlipa mil 23 na Nyumba na Gari kapewa?... Swali kwa kazi ipi aliyowafanyia waTZ zaidi ya kusafirisha mipira mingi sana kutoka Brazil kuja hapa???? au mnatufanya hatujui?...

Nadhani muaangalie mkurugenzi wa NSSF, TRA, etc wanalipwa kiasi gani ndiyo mje huku si mnakuja JF mmefunga taulo kiunoni na kupiga sarakasi mtaumbuka wenyewe...
 
Kuna hoja lakini katika asemacho. Dr kweli anaonekana kuchoka sana. Kuna haja kubwa sana ya kufanyika matumizi bora ya wabunge wengi ambao chadema imekipata. Pia kutumia vyema watendaji kama maafisa katika chama. Pia kuna wabunge ambao wanakuwa over-worked sana huku wengine wakiwa wanatanua tu mitaani bila kupiga mizigo ya chama ile kihaswa haswa kama vile hawana dhamira ya kuchukua nchi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom