Dr Slaa amlipua rais Kikwete; adai hana ubavu wa kupambana na rushwa

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemlipua Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akidai kuwa hana ubavu wa kupambana na rushwa kwa kuwa chama chake kiliingia madarakani kwa rushwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Akihutubia katika mikutano ya hadhara katika Vijiji vya Kata za Kiloleli na Ipole, wilayani Sikonge, Mkoa wa Tabora, Dk Slaa alisema rushwa inazidi kukua siku hadi siku nchini.

Alidai kwa kuwa viongozi wa CCM waliingia madarakani kwa njia ya rushwa ndiyo maana hawawezi kulimaliza tatizo hilo.

Dk Slaa alisema Rais Kikwete anatania kuhusu tatizo la rushwa kwa kuzungumza tu majukwaani, huku akiwalinda washirika wake.

Alisema kama Rais Kikwete angekuwa mkweli angewakamata wamiliki wa Kampuni ya Kagoda ambao ni watuhumiwa wa wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Alidai kuwa ameshindwa kuwakamata kwa sababu fedha hizo ndizo zilitumika kumwingiza madarakani katika uchaguzi wa 2005.

Katibu mkuu huyo wa Chadema alisema vitendo vya rushwa vilivyojitokeza katika uchaguzi wa viongozi wa CCM ni kielelezo tosha kwamba, chama hicho hakina uwezo tena wa kupambana na rushwa.

"Tunawaambia CCM kuwa chama chao kimeoza kuanzia juu hadi chini, sasa mafisadi wameshika hatamu ndani ya chama hicho,” alisema.

Dk Slaa alisema, “Hivi Watanzania tunahitaji ushahidi wa namna gani ili kubaini uozo katika CCM na tuungane kukiondoa madarakani.”

Aliongeza, "Wakati chama hicho kinatopea kwenye lindi la rushwa na ufisadi, kiongozi wake mkuu ambaye Rais Kikwete naye anaishia kulalamika tu.”

Slaa alisema Rais Kikwete angekuwa na nia ya dhati
katika kupambana na rushwa, angeifanyia kazi orodha ya majina 11 ya watuhumiwa wakubwa wa ufisadi iliyotolewa katika Viwanja Mwembeyanga, jijini Dar es Salaam Septemba 2007.

Alisema kuendelea kulalamikia kuhusu rushwa bila kuchukua hatua yoyote, kunawashangaza wananchi ambao wanaona hata Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) bora ingevunjwa.

Hatuwezi kukubali taifa liangamie kwa sababu Rais anashindwa kuchukua hatua dhidi ya mafisadi na wala rushwa.
 
Ni hoja za msingi sana lakini yakija magamba hapa utaikia hana jipya Dr Slaa.
 
Ndugu umesahau hii kauli aliitumia wakati wa kampeni yake ya kugombea Urais mwaka 2012, kama na sasa anairudia basi ameishiwa ujumbe kwa wananchi.
 
Ni kweli rais wetu ameshindwa kukabiliana na rushwa, amesikika akilalamikia chaguzi za UWT kuwa zilikuwa na rushwa, sasa tunajiuliza kama yeye analalamika na sisi wakina yakhe tufanye nini?
Rushwa kila kona.
 
Ndugu umesahau hii kauli aliitumia wakati wa kampeni yake ya kugombea Urais mwaka 2012, kama na sasa anairudia basi ameishiwa ujumbe kwa wananchi.
Alaa, kumbe 2012 kulikuwa na uchaguzi ambao Slaa aligombea. Labda wa kugombania yule mwanamama.
 
Dr Slaa huna single mpya kila siku hii hii.

Take this.....up ....
ImageUploadedByJamiiForums1351351635.156298.jpg
 
Ni kweli rais wetu ameshindwa kukabiliana na rushwa, amesikika akilalamikia chaguzi za UWT kuwa zilikuwa na rushwa, sasa tunajiuliza kama yeye analalamika na sisi wakina yakhe tufanye nini?
Rushwa kila kona.
Timiza majukumu yako, basiiiiii.
 
Kamwe mtoa rushwa na mpokea rushwa hawezi kupambana na rushwa iliyokithiri nchi.

Raisi analalamika bila ya kuchukua hatua, Wanaichi wanalalamika. Bila shaka tunauongozi dhaifu
 
Kwa mawazo yake anafikiri yupo kwenye kampeni bila kujua huu ni mwaka 2012, na kujinadi kwa sera za mwaka 2010. Hivi hana mshauri au ndo Tundu Lisu aliyeshindwa kuhamasisha Wananchi wa Jimbo lake kushughulika na kilimo na maendeleo kwa ujumla, ila akabakia kuwashawishi wagomee kila kitu hata kama kitakuwa ni kwa ajili yao?. Sasa wananjaa huku Mbunge wao mpendwa anakura na kusaza bila kuwajali
 
Ndugu umesahau hii kauli aliitumia wakati wa kampeni yake ya kugombea Urais mwaka 2012, kama na sasa anairudia basi ameishiwa ujumbe kwa wananchi.

Naona Mkuu hapa wewe ndio umeishiwa, uchaguzi Wa uraisi 2012 nani aliuitisha?
 
Dr Slaa huna single mpya kila siku hii hii.

Mkuu Hii single haijachuja, kila siku tunapata chorus mpya!

Ongea na jamaa zako mfukuze wala rushwa, watoa rushwa Na mafisadi. Au wewe unawapenda na unafaidika nao?

Natumaini Hii sigle itachuja pale tu CCM itakapojivua gamba
 
Back
Top Bottom