Dr. Slaa AMKIMBIA Wilson Mukama katika mjadala?

nakubaliana na wewe.....inawezekana CCM wamezusha tu. kwani ikizingatia taarifa hiyo imetolewa kwenye front page ya UHURU. inawezekana magazeti mengine yametarifu suala hili lakini UHURU ndo imebeba Ukrasa wa mbele

yaani mkuu nimeufuatilia huu mjadala kwa umakini sana, kumbe source ni hayo makaratasi ya maandishi (wenyewe wanaita gazeti la uhuru) ah mkuu hapo inabidi unitake radhi kwa kuiteka attention yangu.
 
Dr.slaa nadhani ana dharura kama alialikwa!mimi ningekuwa yeye wala nisingekubali kuongea na wehu ambao hawana nia njema na nchi hii.
 
huo ni mdahalo ulioandaliwa na kamati kuu ya ccm na kuitafutia kipindi cha kukichomeka TBC1, wakapiga kura kati ya nape na mukama nani mwenye kumbukumbu, hatimaye mukama kashinda. Taarifa kapelekewa mtayarisha wa kipindi kwa maandalizi. Lengo ni kujisafisha mbele ya watz kwa matukio yalifanyika Igunga.
 
Kipindi cha jambo leo hakifai kuwasilisha mijadala ya watu muhimu kama Slaa yeye anatakiwa na kipindi cha dk 45 au zaidi ili atoe maelezo na wananchi waulize maswali au kutoa maoni. Maana hiki kipindi tena siku za kazi wanaangalia mahouse girl wengine tunakuwa njiani kwenda maofisini. Hata hivyo nani mwenye kuwahoji ni huyo Hasan?
Hoja muhimu kwasasa kwa viongozi makini ni kujadili matatizo ya wananchi siyo propaganda kujadili hoja za Mkama ni kupoteza muda maana huyo bingwa wa fitina hadi chama chake wanamjua kawatia hasara Igunga 3bilioni zimetumika kwasababu ya sera yake isiyo na mashiko popote.

Slaa tafuta air time nzuri nenda na makamanda wako eleza wananchi kuwa nchi inaangamia tuiokoe maana kila kitu mgao kuanzia umeme maji hadi sukali.
 
No...No...No...Tujaribu kuwa watu makini kidogo kwenye maamuzi,tufikirie kidogo kuhusu
mambo ya msingi ambayo yangewafanya kuingia kwenye mjadala huu ni kama haya:
1.Mwenendo wa Uchaguzi wa jimbo la Igunga-Ni vigumu kuzungumzia uchaguzi wa Igunga wakati unajiandaa
kupeleka kesi mahakamani kupinga matokeo.
2.Tuhuma mbalimbali ambazo zimejitokeza kwenye uchaguzi Igunga ziko mahakamani-Ni wazi kuwa watakuwa
wanaingilia uhuru wa mahakama kwa mtego wa Mukama(ccm) lakini Dr Kashtukia issue.
3.Tuhuma za makomandoo zimeshagonga mwamba na kuonekana ni za uzushi,sasa mukama anataka kubadili
mkakati wa kujeuza maneno kwa kupitia mjadala na Dr Slaa akijua kutakuwa na watu wengi wa kusikiliza.
Ni mawazo yangu tuu.
 
Dk. Wilbroad Slaa ameingia mitini licha ya kuthibitisha kushiriki kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa na TBC1 ambacho kililenga kumkutanisha na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama. Wote walithibitisha kushiriki lakini ghafla Dk. Slaa akaingia mitini.

Haiwezekani hata siku moja Slaa amkimbie Mukama. Mukama na CCM yake wana jipi la ajabu la kuwaambia WTz? Mfano uchaguzi wa Igunga ni ishara kuwa CCM imeporomoka kutoka kukubalika 100% wakati wa Rostam ambapo alipita bila kupingwa uchaguzi uliopita, na miezi michache tu baada ya uchaguzi mkuu kinakuja chama ambacho hakijawahi kusimamisha mgombea jimbo hilo kinaporomosha ushindi wa 100% hadi 50%. Hii ni ishara mbaya hata CCM hawatakiwi kujisifu sana kwa ushindi huo.
 
SHULE ZA KATA KAZINI!DR Phd,amkimbie bwana udenda?????crapp!sidhani kama inawezekana, kama ni kweli dr kama kawa atafunguka muda si mrefu!pigeni porooooooooooooooooooooojo zenu zote ILA MWISHO MJUE WATU WAMEWACHOKA NA MUANZE KUFUNGA VIRAGO TARATIBU!!!!!
 
Mukama hata mimi aliwahi kunikimbia mimi Arusha na Nepi wake...sasa ataongea nini na Dr wa ukweli sio wa kupewa kama jk???...Big up Dr Slaa wakufuate nyumbani kwako kwa ushauri
 
No...No...No...Tujaribu kuwa watu makini kidogo kwenye maamuzi,tufikirie kidogo kuhusu
mambo ya msingi ambayo yangewafanya kuingia kwenye mjadala huu ni kama haya:
1.Mwenendo wa Uchaguzi wa jimbo la Igunga-Ni vigumu kuzungumzia uchaguzi wa Igunga wakati unajiandaa
kupeleka kesi mahakamani kupinga matokeo.
2.Tuhuma mbalimbali ambazo zimejitokeza kwenye uchaguzi Igunga ziko mahakamani-Ni wazi kuwa watakuwa
wanaingilia uhuru wa mahakama kwa mtego wa Mukama(ccm) lakini Dr Kashtukia issue.
3.Tuhuma za makomandoo zimeshagonga mwamba na kuonekana ni za uzushi,sasa mukama anataka kubadili
mkakati wa kujeuza maneno kwa kupitia mjadala na Dr Slaa akijua kutakuwa na watu wengi wa kusikiliza.
Ni mawazo yangu tuu.
Kama kuna UKWELI kwenye hoja hizo kwa nini asitumie platform aliyopewa na TBC kuueleza umma kilichojiri Igunga? Unasema Slaa anajiandaa kupeleka kesi Mahakamani. Kesi haijafika Mahakamani sasa uhuru wa Mahakama unaingiliwaje?
 
Hayo matusi yanadhihirisha ulivyokosa hoja za kumtetea Slaa.

Nina swali kama hicho kipindi kiliandaliwa kwa nini Mukama hakuongea live tukamsikia? Nyinyi mmezoea kurecodi na kuchakachua ndio mnatuma hewani upupu ndio maana kaona anapoteza muda wake. Hata nyinyi mngeweza kufanya huo mdahalo na Mukama kwa sababu mnajua hali ya watanzania.
 
Hizi ni propaganda za CCM tu na magazeti yao na mafisadi wake wa Dowans kwani mbona wao walikimbia kwenye midahalo nchi nzima kipindi cha uchaguzi lakini hatukulalamika mpaka ikafikia wakamfitini boss wa TBC na kumwaribia kibarua chake.




Deni la Dowans hatulipi ng'o
 
Nimeona katika gazeti moja la kila siku. dk Slaa amekacha mjadala uliipangwa kufanyika hapa kwa kushirikiana na chombo kimoja kikuu cha habari yaani TBC1 katika kipindi cha JAMBO LEO.
Katika mjadala huo ambao Mukama alipanga hoja za msingi na kutaka kumuonyesha dk slaa kwamba anayozungumza mengi hafanyi utafiti.lkn pia kuzungumzia magaidi waliongizwa na CHADEMA IGUNGA na mengine mengi juu ya CHADEMA
katika hali isiyoyakawaida katika Chama cha chadema. Dk slaa amekacha mjadala huo.
Jee Dk slaa ameanza kuogopa mijadala ya wazi?
What next?

Kuna uhusiano gani kati ya kipindi cha jambo leo na
gazeti la Jambo leo?
Hata mimi nisingeenda maana ni ushuzi tu
 
Mmmmmmmmmmmm mkama siyo saize ya Dr slaa.
Labda mtatiro wa cuf ndo saize ya mkama.
Mkama anatafuta umaarufu kufanya mdaharo na DR
 
ata kama angekwenda hakuna jipya hapo kwa Mukamasi..
siasa za uzeeni bana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom