Dr. Slaa AMKIMBIA Wilson Mukama katika mjadala?

Dk. Wilbroad Slaa ameingia mitini licha ya kuthibitisha kushiriki kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa na TBC1 ambacho kililenga kumkutanisha na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama. Wote walithibitisha kushiriki lakini ghafla Dk. Slaa akaingia mitini.

Kiwango cha Dr. Slaa kipo juu hawezi jishushia heshima kwa kufanya mjadala na mukama
 
nakubaliana na wee kabisa, tena enzi za makamba ilikua mbaya sana

lakini je kamanda nae kaanza kuiga huo mfumo hasi?
Je huo mjadala ulikuwa na manufaa kwa wananchi au ni kwa manufaa ya magamba na ni kwanini sasa....
 
Malaria sugu anasema TBC ni "chombo kikuu cha habari" nchini, sina hakika ni habari zipi, za uongo au za kweli ukiachilia mbali coverage ndogo waliyonayo. Tabu yao wanachakachua sana habari hadi za JK zinakuja kutoka ndivyo sivyo. Hata ningekuwa mimi nisingeenda TBC ambao tayari wameshaonyesha "mrengo" wao kudhihirisha kuwa hawako huru. Halafu hayo mambo yaliyojiri kule Igunga, kama issue ya ugaidi, matusi na ukiukaji taratibu za uchaguzi yameshapelekwa Mahakamani, Dr Slaa aje kuyaelezea TBC ili iweje, au Mkama anatafuta possible defence to counter presented facts? Namshauri Mkama atulie Mahakama ifanye kazi, yakiisha mambo waliyoshitakiana Mahakamani midahalo itafanyika tu, muda upo mwingi. Asitufanye tuamini yasemwayo kuwa siasa ukizianzia uzeeni zitakusumbua sana.
 
Wewe kweli akili zako ni za mbayu wayu! Aongee kupitia TBC kweli? Ujuha ni ugonjwa mkubwa sana

kama haridhiki na waongozaji si angeweka masharti? na sisi tunaompenda, wenye uwezo wa kufikiri, si tungejua kabaniwa kutoa aliyonayo? si baadae tungeanzisha mjadala kuwalaani TBC?

UKIPENDA KITU Padre, kisikunyime nafasi ya kutafakari. kosa lingine hilo
 
Je huo mjadala ulikuwa na manufaa kwa wananchi au ni kwa manufaa ya magamba na ni kwanini sasa....
i dont know, lakini kama kwelia kasema sio vizuri, tusihalalishe yasiyofaa... ila nina imani kwamba kuna explanations
 
J.K alikimbia mjadala kwenye race za urais, sababu ni kuwa asingeweza kujibu maswali au hoja za Dk. slaa na Lipumba. Kwa lugha nyingine, media ingetumika kumchafua sana kikwete na kuwapaisha wapinzani wake. Ndo maana alikana kabisa kushiriki mdahalo huo.

Sasa nikuulize swali,
1.Dk. Slaa, amekacha kwa sababu sawa na za magamba kukacha midahalo?
2. Kwa nini athibitishe kuhudhuria na kisha kukacha tena yawezekana bila taarifa yoyote?
kakimbia nini? watanzania au mkama? nijuze crashwise.
Hivi Mukama anaweza kuwa na hoja za kumfunika Dr Slaa...hahaha.......kama alifikia kuthibitisha basi lazima kutofika kwake lazima kutakuwa na sababu na lazima atakuwa amewajuza wahusika labda tumulize mleta mada je alitoa sababu gani za kutokufika kwenye mjadala huo...
 
Kwa mawazo haya lazima unafanya kazi BAKWATA kwa mawazo haya.

nachelea kukujibu utakavyo nisije haribu mjadala halisi kwa kuibua mjadala wa dini tena. pitia mijadala ya bakwata iliyoshika kasi, utaona comments zangu na utajua mie niko upande gani
 
I don't trust the so called TBC, Inawezekana wamepewa maswali ya kuuliza kutoka kwa Mukama. TBC = CCM = Magamba, kwa hiyo ukienda mtu kutoka kundi tofauti na hilo ujiandae kwa mengi.
 
Unauhakika kutokuongea na TBC1 ni kutokuongea na wananchi?

ukiwa maeneo mbalimbali ya mwanza, TBC na ATN, ndo station pekee zinazodaka kwa kutumia antena za CDM. TV station nyingine aidha uwe connected na calbe tv, au uwe na dishi na kwa wenye kipato wana decoda za tin na startime
 
Dk. Wilbroad Slaa ameingia mitini licha ya kuthibitisha kushiriki kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa na TBC1 ambacho kililenga kumkutanisha na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama. Wote walithibitisha kushiriki lakini ghafla Dk. Slaa akaingia mitini.

Labda alikuwa bado anaandaa nyaraka za utetezi wa hoja za Mukama
 
kama haridhiki na waongozaji si angeweka masharti? na sisi tunaompenda, wenye uwezo wa kufikiri, si tungejua kabaniwa kutoa aliyonayo? si baadae tungeanzisha mjadala kuwalaani TBC?

UKIPENDA KITU Padre, kisikunyime nafasi ya kutafakari. kosa lingine hilo
nakuunga mkono lakini kwenye nyekundu sijakuelewa....
 
kuna kitu mmesahau wadau kuhusu mijadala ya wazi ya CDM na Mabunduki aka Magamba. Nani anakumbuka mjadala kati ya Wassira na Mbowe! Kama mnakumbuka basi. Dr. kasoma alama za nyakati Mabunduki hawachelewi kupandisha Jazba mjadala wanapokutana na kitu cha ukweli hasa joto la mjadala linapopanda.
 
Nimeona katika gazeti moja la kila siku. dk Slaa amekacha mjadala uliipangwa kufanyika hapa kwa kushirikiana na chombo kimoja kikuu cha habari yaani TBC1 katika kipindi cha JAMBO LEO.
Katika mjadala huo ambao Mukama alipanga hoja za msingi na kutaka kumuonyesha dk slaa kwamba anayozungumza mengi hafanyi utafiti.lkn pia kuzungumzia magaidi waliongizwa na CHADEMA IGUNGA na mengine mengi juu ya CHADEMA
katika hali isiyoyakawaida katika Chama cha chadema. Dk slaa amekacha mjadala huo.
Jee Dk slaa ameanza kuogopa mijadala ya wazi?
What next?

Hivi hawa magamba si walishapigwa marufuku kuhudhuria midahalo?? Sasa huu unafiki wa nini??? After all mukama wa magamba ataongea nini na Dr. Slaa????
 
Hivi Mukama anaweza kuwa na hoja za kumfunika Dr Slaa...hahaha.......kama alifikia kuthibitisha basi lazima kutofika kwake lazima kutakuwa na sababu na lazima atakuwa amewajuza wahusika labda tumulize mleta mada je alitoa sababu gani za kutokufika kwenye mjadala huo...

nimekosa kitufe cha like. nimependa majibu yako. kama alitoa taarifa halafu wakaifunika, tutajua hapahapa. tuendelee kufuatilia. lakini kama alithibitisha kushiriki halafu akasusa bila kutoa uzuru, ametukosea tunaomkubali
 
ina tija kwa maendeleo ya taifa? mukama akawavue gamba kama walivyoahidi siku 90
 
Hakuna cha excuse, kama aliahidi na hakufika then it is a bad sign... we want reliable leaders sio makamba style!!! I hope Dr. Slaa akakuja na clear clarification about this

bad stuff though

kwa jinsi ninavyomuamini dr. sidhani kama kulikuwa na kitu kama hichi, kuna uwezekano alialikwa lakini akatoa udhuru kuwa hatofika kwa sababu anazojua yeye ili wapange siku nyingine, ila waandishi uchwara kwa kuona hiyo chance wakaona waseme aliahidi kufika ili rep. yake ishuke, kiukweli angehudhuria Dr. Slaa nina uhakika wa 100% huyu mukama asingekuwa na ujasiri wa kufika pale, ni issue ilipangwa kuwa kwakuwa Dr. hatofika tutengeneze zengwe aonekane kaogopa.
 
Dk. Wilbroad Slaa ameingia mitini licha ya kuthibitisha kushiriki kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa na TBC1 ambacho kililenga kumkutanisha na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama. Wote walithibitisha kushiriki lakini ghafla Dk. Slaa akaingia mitini.

Inteligensia ya cdm imefanya kazi nzuri. mukama ni gamba sawa na tbc1. wote ni magamba, then what should you expect???
 
tatizo sio kuongea na mkama, alitakiwa kuongea na wananchi. kawakambia wananchi na siyo mkama. kosa hili

Inawezekana kabisa alikuwa tayari kuongea na wananchi. Tena ingekuwa fursa nzuri ya kuongea mengi na watanzania wengi kwa wakati mmoja lakini bila shaka alikuja kugundua kwamba it won't work because he was invited to a WRONG place.
 
Back
Top Bottom