Elections 2010 Dr. Slaa alikuwa anaongoza Kwa 61.6% - Marando

CCM walijua watu wanawapenda ndio maana walikuwa na jeuri hata ya kuwatukana wapigakura lakini walipoona matokeo ya kura wakashituka. Tukumbuke mwanzo matokeo yalipoanza kutolewa na vyombo vya habari waandishi waliopo maeneo husika walitangaza matokeo ya ngazi ya urais, ubunge na udiwani kama walivyotangazwa na wasimamizi. Baada ya CCM kuona mgombea wao anapitwa kwa zaidi ya asilimia 50-70 ( e.g. songea kikwete alipata kura kati ya 36-50 wakati Dk. Slaa alipata kura kuanzia 120 na kuendelea karibu kwa kila kituo cha kupigia kura) wamevipiga marufuku vyombo vya habari kutoa matangazo ya matokeo ya urais.
Shime watanzania wakati wa kuwaondoa mafisadi umefika
Mikakati katika bunge hili
1.kufuta na kubadilisha muundo Wa Tume Ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), kwa kumuondolea Rais madaraka ya kuteua Mwenyekiti na wakurugenzi wa Tume, bali mapendekezo ya majina matatu yawe yanawasilishwa bungeni na kuthibitishwa na bunge. Na bunge lipewe mamlaka ya kuwafukuza kazi na sio Rais

2. kufanya mabadiliko ya katiba kwa kufuta vyeo vya Mkuu wa wilaya na Mkuu wa Mkoa kwani ndio wamekuwa vibaraka wa ccm kuhakikisha kushinda kwa gharama yoyote ikijumuisha kuchakachua matokeo

3.kufuta utaratibu wa mtu kuwa mbunge ndipo awe na sifa ya kuteuliwa kuwa waziri. Bali nafasi za uwaziri ziwe zinagombaniwa kwa mfano wa ubunge, anayeshinda ndiye anakuwa waziri katika eneo analolichagua. Hii itaongeza uwajibikaji. Pia idadi ya wizara, mawaziri na manaibu mawaziri wa serikali inayofuata iwe inaidhinishwa na bunge kabla ya uchaguzi au baada ya uchaguzi.

4.kuwaondoa wakurugenzi wa halmashauri kuwa ndio wasimamizi na watoaji wa matokeo ya uchaguzi kwani hawa wanateuliwa na rais na kwa vyovyote vile hawawezi kukiuka maagiza ya rais. Bali wakurugezi wa NEC watakaidhinishwa na bunge ndio wawe wasimamizi na ndio watangaze matokeo ya uchaguzi(tujadili ili kujua idadi yao iweje)

5.kurekebisha sheria, ili kuruhusu vyombo vya habari kutangaza matokeo ya uchaguzi kama yalivyotangazwa na wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo husika,

6.kuweka masharti ya kutoajiri wastaafu katika Tume Ya Uchaguzi. Sababu kubwa ni kuwa uwezo wao wa kufikiri kwa haraka na kutoa maamuzi ni mdogo sana na hawana uwezo wa kusimamia ukweli.

7. Kuweka ukomo wa mtu kuwa mwenyekiti na Mkurugenzi wa Tume kuwa misimu miwili ya miaka mitano mitano

8. Ujumulishwaji wa matokeo ufanyike katika maeneo ya wazi ambapo kila mtu ataona, teknolojia hapa inaweza kutumika ili kuondoa malalamiko, hili liwe moja ya takwa la msingi la kisheria. mfano Marekani kila matokeo yalipotangazwa katika kituo cha kupigia kura yalionekana wazi katika screen/tv ya Tume ya Uchaguzi pasipo wao tena kuhitaji kutangaza.Hata walipojumulisha na kutangaza mshindi wa jumla hakuna aliyeyakataa matokeo kwasababu yalikuwa wazi kwa kila mtu na walijua nani ameshinda hata kabla Tume haijamtangaza mshindi.

9.Tuangalie na maeneo mengine yenye mianya ya ufisadi na uchakachuaji wa matokeo na kuona jinsi ya kuziba mianya hiyo kitaalamu

Bila haya kufanyiwa kazi ushindi kwa upinzani itakuwa ni ndoto na mwishowe tutakuwa kama wakenya na wazimbabwe, Mungu atusaidie tusifikie huko, maana inanitisha ninapoona watanzania waliokuwa wapole na waoga kwa vyombo vya dola sasa wanaweza kupambana na vyombo vya dola hadi vyombo vya dola vinakimbia na kujificha- rejea vurugu zinazoendelea kwenye majimbo ya uchaguzi ikijumuisha ya kibaha mjini
 
[Aidha taarifa hizo zinasema Dk. Slaa amepanga kuwakilisha ushahidi MZITO unaoonyesha uchakachuaji mkubwa wa kura za Urais ulivyofanyika. Ushahidi huo ni pamoja na matokeo halisi ya vituoni ambayo yanapishana na yale ya NEC.[/COLOR][/SIZE][/FONT]

Hatua zilizochukuliwa ni:


1. Kwenda NEC - kupeleka barua

2. Tunakwenda kueleza Nchi wahisani ambazo zimefadhili shughuli za Uchaguzi
3. Tunakwenda kuwaeleza wananchi kilichotokea kwa kuwaonyesha ushahidi kamili.

MWAGA USHAHIDI NA PANAPOHUSIKA....POROJO ZA MAJUKWAANI NA VIJIWENI HAZINA NAFASI. hivi kweli hakuamini ile kauli ya Daily News inayoshabihiana na hii ''...Slaa will never be our next President''.
 
Mkulima acha upupu. Huko Kyela na Kigoma Slaa alikataliwa wagombea wake wa ubunge. Lakini akaahidiwa kura za uraisi. Pia kuna jimbo moja Chadema wamelichukua, lakini wamepata diwani mmoja tu, wakati CCM wamechukua kata zilizobaki kama nane hivi au zaidi.

Kutoa ahadi ni jambo moja. Kutekeleza ahadi ni jambo jengine. Kumbuka mtu anaweza kushawishika leo, lakini kesho akabadili msimamo baada ya kupata ushawishi mbadala.
 
Wote asanteni mnaofahamu wezi kina nani . maziko ndo hayo ooo . sikujua bora umesema kumbe ccm ni dini hiyo ? pole chadema hakina dini . ni chama cha wapenda haki .pi ......mbi Ndo akili zake.
 
jambo lingine la kufanyiwa kazi ni

10 . kufanya mabadiliko katika sheria ya uchaguzi ili matokeo ya uchaguzi wa rais yawe na uwezo wa kuhojiwa na kutenguliwa na mahakama mara bada ya kutangazwa. Hii itasaidia kuondoa jeuri ya chama kilichopo madarakani kuchakachua matokeo, maana watajua matokeo yanaweza kufutwa na mahakama na kuidhinishwa mshindi halali au kuagiza uchaguzi kurudiwa ENDAPO YATAKUWA SIO HALALI.
 
THE PATRIOTS NEVER GIVE UP EASILY,LETS FIGHT 4 OUR STOLEN COUNTRY.........
Say NO to matokeo yanayotangazwa na NEC:nono:
 
But the National Electoral Commission chairman rejected the idea.
"There could be irregularities in terms of arithmetic in the vote tallying, but not enough to change the final results," Lewis Makame is quoted by the Reuters news agency as saying" Source BBC

Hayo ni maneno ya Jaji Lewis Makame kuthibitisha kuwa matokeo wanayotangaza siyo yaliyotangazwa vituoni. Ni ajabu kwa Jaji kufanya vitukama hivyo halafu utegemee kupata haki mahakamani.
Inauma sana, Mungu saidia Tanzania.

Kwa kweli inaudhi sana! Tena haiingii akilini! Sielewi ni kwa vipi NEC wanasahihisha hizo "irregularities", maana wao wanapelekewa matokeo ya vituo, sasa wanarekebisha nini? Huyu mzee (retired justice of appeal) anatakiwa astaafu kikweli! Akili zake zimeishachoka akapumzike! Aaagh!
 
Siasa za mfa maji hizo. Acha kutapata. Ni ndoto za mwendawazimu kuamini kuwa eti Dk. Slaa angeweza kumshinda JK. Huo ni upunguani kwelikweli.
Hivi Unategemea Marando- malaya wa kisiasa aseme nini. Kaivuruga NCCR na kuikimbia huku nyuma NCCRimeanza ku-gain power. Sasa amekwenda Chadema. Unategemea asemeje Wakili Mkuu wa kutetea wezi, mafisadi na wanyang'anyi wa haki za watu.
Marando huyuhuyu aliemtetea Mzungu aliyemtumia mbwa wake kumnajisi mwanamke wa Kitanzania. Tokeni kabisa na upuuzi wenu.
Kama mtu unatoa nukuu, zitoe kutoka kwa watu decent na sio watu wachafu wa aina ya Mabere Nyaucho marando.
Angesema Lisu, mimi ningenyanyua masikio yangu na kutafakari na sio kichaa wenu Nyaucho. Akome kabisa kuleta uchochezi hapa.
Umekosea aliyemtetea huyo mzungu alikuwa Lamwai na mara ya mwisho nilipotafitii niligundua kuwa bado yuko CCM!
 
Source: Mwanahalisi: Jumatano, Novemba 3-9, 2010

NEC inatuhumiwa kuhujumu matokeo ya Uchaguzi kwa lengo la kukinyima ushindi CHADEMA.

Madai hayo yamo katika barua ambayo CHADEMA kiliwakilisha jana NEC kulalamikia utaratibu mzima wa kutangaza matokeo.


Katika barua hiyo, Mwanasheria wa CHADEMA, Mabere Marando anasema NEC inatumiwa na CCM kuhujumu matokeo hayo ili CCM kionekane kinashinda. "Wamepanga kupora ushindi wetu, ndiyo maana kila ambapo CHADEMA imeshinda, CCM wamekataa kusaini karatasi za kura" alisema Marando.


"Hata pale ambapo kura za madiwani na wabunge zimetangazwa, matokeo ya kura za urais hayatangazwi". Marando alisema NEC inafanya hivi kwa makusudi kwani maeneo ambayo CHADEMA haikuwa imeweka mkazo, matokeo ya madiwani, wabunge na ya urais yanatangazwa haraka . . . .


. . . . . Lakini hata katika maeneo ambayo CCM imeshinda, Marando alisema matokeo yanayotangazwa na NEC hayaendani na yale yaliyotangazwa vituoni. "Huu ni Uchakachuaji". . . .


. . . . . Marando alisema hadi juzi Jumatatu matokeo ambayo tayari walikuwa wamekusanya kutoka katika maeneo mbalimbali ya Nchi, yanaonyesha Mgombea Urais wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa anaongoza kwa wastani wa asilimia 61.6%..


Aidha taarifa hizo zinasema Dk. Slaa amepanga kuwakilisha ushahidi MZITO unaoonyesha uchakachuaji mkubwa wa kura za Urais ulivyofanyika. Ushahidi huo ni pamoja na matokeo halisi ya vituoni ambayo yanapishana na yale ya NEC.


Hatua zilizochukuliwa ni:


1. Kwenda NEC - kupeleka barua

2. Tunakwenda kueleza Nchi wahisani ambazo zimefadhili shughuli za Uchaguzi
3. Tunakwenda kuwaeleza wananchi kilichotokea kwa kuwaonyesha ushahidi kamili.

Malalamiko haya yanakuja siku chache baada ya lori lililoingia nchini likitokea zambia kukamatwa mjini Tunduma likiwa limesheheni karatasi za kupigia kura zilizowekewa alama ya vema kwa Kikwete. NEC ilikanusha.


Lakini katika kituo kimoja cha kupigia kura wilayani Musoma, lilikamatwa Lori lililokuwa na karatasi za kupigia kura na tayari zilikuwa na zimewekewa alama ya vema upande wa Kikwete. NEC haikutoa maelezo kuhusu tukio hilo.


My take:

Kama hizi taarifa ni za uhakika, basi hakuna maana ya zoezi zima la uchaguzi na ni dharau kubwa sana kwa Watanzania. Bahati mbaya mshindi wa Urais akishatangazwa, huwezi kuupinga ushindi huo mahakamani.

Ni vema sasa jumuiya zote za kiraia zinazotetea haki za kidemokrasia na za binadamu, wanachama na wapenzi wote wa haki na wana CCM wanaokerwa na hili kupaza sauti zao na kupinga kwa nguvu zote uzandiki huu. Arusha, Mbeya, Mwanza, Kawe, Ubungo na Iringa wameonyesha njia.

Inawezekana, mambo mazuri yana gharama na si lazima gharama hiyo iwe ni kumwaga damu bali kupaza sauti na kukataa kutawaliwa na watu ambao watanzania hawajawachagua kwa haki.

data unazo au kelele tu?
 
Huyu Slaa naona ameishiwa sera yeye ni namba 3 halafu bado analalamika, wacha namba 2 kwanza aseme...

Hili swala la kushinda uchaguzi jamani si lele mama wewe ukurupuke tu leo kesho ushinde uchaguzi inatakiwa mipango ya muda mrefu . Maalim Seif amegombea Znz kama mara 4 mara zote anapata zaidi ya 45% lakini hashindi.

Slaa apunguze malalamiko na aanze kuonesha ukomavu wa kisiasa vinginevyo hata huo ubunge atakuja kuusikia kwenye redio tu!
 
jambo lingine la kufanyiwa kazi ni

10 . kufanya mabadiliko katika sheria ya uchaguzi ili matokeo ya uchaguzi wa rais yawe na uwezo wa kuhojiwa na kutenguliwa na mahakama mara bada ya kutangazwa. Hii itasaidia kuondoa jeuri ya chama kilichopo madarakani kuchakachua matokeo, maana watajua matokeo yanaweza kufutwa na mahakama na kuidhinishwa mshindi halali au kuagiza uchaguzi kurudiwa ENDAPO YATAKUWA SIO HALALI.

Kuwe na defined gap, kutoka kutangazwa kwa mshindi na kuapishwa kuchukua madaraka. Functioning of the government to be defined during the transition period so that handing over government activities are effected during this period and outstanding queries are sorted out.
 
Rasta! Na Botswana, Namibia iliwacost nini? Huko kwenye utulivu bila kumwaga damu. Tusiige mifano isiyofaa. Na mbona mifano yako imelala hapa hapa tu? Japan, Australia na Uswisi imewacost nini kujenga amani. Fikiri kama mtu mzima.......AMANI KWANZA
Iliwa cost uadilifu ndio sababu wana amani! Lakini uadilifu wetu inaelekea hadi damu itililike!
 
quote_icon.png
Originally Posted by CCM OYEE
Nendeni kanisani mkalalamike, waislamu oyeee, ccm oyee, tutaonana 2015. Udini wenu haukufanya kazi kikamilifu
Krapu
 
Huyu Slaa naona ameishiwa sera yeye ni namba 3 halafu bado analalamika, wacha namba 2 kwanza aseme...

Hili swala la kushinda uchaguzi jamani si lele mama wewe ukurupuke tu leo kesho ushinde uchaguzi inatakiwa mipango ya muda mrefu . Maalim Seif amegombea Znz kama mara 4 mara zote anapata zaidi ya 45% lakini hashindi.

Slaa apunguze malalamiko na aanze kuonesha ukomavu wa kisiasa vinginevyo hata huo ubunge atakuja kuusikia kwenye redio tu!

Acha pumba kijana sio lazima ugombee miaka 20 ndio ushinde hasa unaposhindana na mtu kama JK
 
Source: Mwanahalisi: Jumatano, Novemba 3-9, 2010
2. Tunakwenda kueleza Nchi wahisani ambazo zimefadhili shughuli za Uchaguzi

Labda hilo kidogo laweza kuleta matunda kwa amani, lakini pia nina wasiwasi! Kule Zanzibar walishuhudia wenyewe kilichofanyika na wakasema sana, lakini bado waliendeleza mahusiano mazuri tu na viongozi waliokuwepo! Mabadiliko huletwa na wananchi wenyewe! kivipi? Wananchi wakipiga kelele tunategemea wale walio madarakani wasikie. je, kama wameziba masiko?! hapo ndipo naogopa kusema ile njia ambayo itawaacha maelefu ya watanzania bila roho zao!! Inatia uchungu sana!!!
 
Back
Top Bottom