Dr Slaa ajibu upotoshaji wa Mwandishi Mayage dhidi ya CHADEMA

Straatkasyambe;

Mkuu kama ulikuwa unafuatilia Statement za Dr. Slaa mojawapo ya mkakati aliokuwa nao kupitia CDM ilikuwa ni ku-overhaul system. Hili ni neno pana kidogo, lakini ukifuatilia zaidi juu ya sera za CDM utapata majibu ya maswari uliyoyarise isipokuwa la ushoga sidhani kama lipo maana hii ni la juzi la Cameroon lakini kwa kuwa vission ya CDM ni kujenga uchumi imara wa kujitegemea automatically this cancelled out! Are you there?.

Kuna mambo mengi ambayo ukiwa huna dola utayaangalia sawa na mcheza mpira reserve na hili ndilo linalotokea hapa. Ukisoma mfumo tulionao utaona hamna ambacho CDM kwa sasa wanaweza kufanya wakiwa nje ya serikali tofauti na kuikosoa. Kwa mfano CDM wanachukia ufisadi lakini lakini hawawezi kutunga sheria ya kudhibiti mafisadi-serikali ndiyo inatunga sheria na kuileta bungeni kama muswada ambapo wabunge huchangia kuhusu huo mswada ambao baadaye huwa sheria.

Kama CDM wangelikuwa na nafasi kama hiyo tungelitegemea muswada strict kuhusu ufisadi na si miswada ya ku accelerate ufisadi. Kumbuka mchango wa Mnyika kwenye mswada wa marekebisho ya sheria ya PPRA, he made about forty (40) ammendments kwenye mswada, kwa mantiki hiyo wakiwa wao ndo wanaotunga miswada, concern zako nyindi naona zitakuwa addressed.
 
Nampongeza Dr Slaa kwa kusikika baada ya kujificha kwa muda mrefu. Nimefuatialia majibu yake, but kinachonitatanisha ni kwamba, huyu dr hana sera mpya. Kwanini kila akiongea popote lazima atoe reference za EPA na Ufisadi?

Huu ni muda muafaka kwake kubadilika.
Wananchi tunahitaji kupata mapya kutoka kwake. Tunahitaji kusikia juhudi anazozifanya na chama chake kuleta maisha bora kwa kila mtanzania.

Wewe kijana wa kukuletea Maisha bora ni Dr Slaa kweli? Kwani yeye anaongoza serikali?
 
Nafasi ya chama kufanya zaidi hutolewa na wananchi na chama hakina uwezo wa kuinyakua. Kama umekiri kuwa kwa kiasi fulani wamefanikiwa na unaamini wanahitajika kufanya zaidi, suala sahihi la wewe kufanya ni kuunga mkono yale yaliyofikiwa ili ridhaa ya wananchi ipatikane, wapewe dola na waweze kufanya hiyo zaidi unayoitaka.

Kuna tofauti kubwa kati ya kukosoa na kuponda. Usipoijua hiyo tofauti utagombana na mama mkwe wako. Mayage ameconclude kwenye makala yake kuwa solution ni kuanzishwa chama kingine, huu ni ukosoaji? Yawezekana huna nia mbaya ktk comments zako, lkn yaelekea huna akili pia. Ni nini unachohitaji wewe kama mwananchi, siasa za kubwabwaja majukwaani na kusubiri uchaguzi au chama kilicho active wakati wote kikiwatumikia wananchi?

Uanaharakati ndio hasa msingi wa mabadiliko chanya ktk mataifa ya kidemokrasia. Ndio njia ya kupata haki toka kwa watawala dhalimu. Shida yetu watanzania ni uoga wa mabadiliko. Badilika kimtazamo, acha uoga na unga mkono harakati hizi za CHADEMA. Tanzania haitakuwa huru kwa uwakilishi wa wabunge wanaoorodhesha msululu wa matatizo ya majimbo yao halafu wamalizie kwa 'naunga hoja mkono kwa 100%'.

Na kama shida yako ni yale yanayohubiriwa majukwaani na CHADEMA, labda nikuulize: Ulitaka wajadili nini zaidi ya yale yanayotukwamisha tusiendelee?

Kuna kingine kinachotukwamisha zaidi ya ufisadi, mikataba mibovu, wizi wa rasilimali, uwajibikaji mdogo, kujuana na kufumbiana macho tunapokosea?

Ni vyema wananchi tukaaacha upuuzi, hizi nguvu za kuisakama CHADEMA tungeielekeza kwenye kuisakama serikali iwachukulie hatua wanaotufilisi. Kama tutagoma kushiriki harakati na kukaa tusubiri kuanzishwa kwa chama kitakacholeta maajabu kwa kukaa ofisini na kukomesha mabaya haya, basi hatutakuwa na tofauti na Mayage anayewaza kwa kutumia tumbo.
Wako ktk kupinga mambo ya kijinga na ukosoaji usio na mashiko,

Shizukan

Kuna namna fulani hivi ya tabia ambapo asiyejiamini na mtu aliye nyanyaswa kwa muda mrefu ili asikilizwe inabidi amsifie yule anayedhani ni boss (Mungu mtu)mtegemezi wake u name it, ili through huyo sauti yake isikike naye apate kukumbukwa kama mtu muhimu katika kundi la watumwa wa huyo mkuu/boss/Mungu mtu. Hii ndiyo tabia ya watanzania ambao baada ya kuwa opressed kwa muda mrefu hawajiamini tena kama wana weza kusimama na kutoa maoni yao yaliyo huru bado wakaendelea kubakia jinsi walivyo ama hata kuinua hali yao jua ya hapo walipo sasa. Wanasema wasicho amini na wanatenda kwa tahadhari sana ili wasije muudhi yule ambaye wanaamini anauwezo wa kuwafanya anachotaka na bado wao wasiweze kumfanya lolote.

Na moja kati ya hao ni huyo ambaye ume-respond post yake.
 
Kaka Rejao hii kazi ya kuhamasishana kufanya kazi kwa bidii tumeshaanza polepole si unajua tena walikuwa na mgomo baridi wa kutoingia drsn, kutia mboko wanafunz kisa serkali haijawalipa madai yao. Mwisho wa siku tukaona tunawaumiza watoto wasio na hatia na tunaongeza idadi ya mafisadi si unajua tena mtoto akikulia mazingira ya kifisadi tarajia kuwa fisadi nae. Japo wenzetu wa sec bado wana mahasira hawajalipokea sana hili la kufanya kazi kwa bidii hasa shule za kata. Kuhusu masaa 24 kuwa inter siunajua tena tuko likizo hivyo tutabanana hapahapa jf.
 
Nyie CHADEMA ni watu gani msiotaka kukosolewa???? Mayage katika makala yake aliwakosoa na kuwataka mfanye vizuri zaidi lakini mmeigeuza makala yake kuwa ugomvi kana kwamba amewatukana matusi ya nguoni. Ni nyie mnaolalamika hali ya nchi kwa sasa na kuhoji kama kweli Rais ana washauri. Nyie mnaukataa ushauri wa Mayage, je huyo Padri wenu aliyeasi akiingia Ikulu atamsikiliza nani?

Issue yenu ime ''backfire'' nendeni mkajipange upya...
 
Dr wa ukweli sasa kamwaga darasa, Mayange acha uandishi wa kishabiki kwa wale wanasiasa wa KUSADIKIKA uwapendao wewe akilini mwako peke yako kwa maslahi binafsi.
 
siku zote chadema tunasema ni chama makini chenye viongozi mahiri katika kujenga hoja, dr ndiye mwasisi wa mapambono dhidi ya ufisadi na chama chetu kitaendelea kusimamia ukweli huu huyu mwandishi anatakiwa atambue kuwa watanzania wanatambua kuwa chadema ndiyo mkombozi wa uchumi wa tanzania na tanzania tunayoitaka (tanzania we want)
kwani mayage mayage ni nani?? Ata atushauri tuwe na utitili wa vyama?? Hizi ni njaa tu zinawasumbua, kujipendekeza pia wanatumiwa na mafisadi, dr slaa tunamuelewa na kumkubali sana ivi mayage mayage amesikia matokeo ya uchaguzi uko mbeya vijijini?? Aaah kama hajui basi ajue tumechukua kijiji uko, natmai km anadhani anacapacity ya kutosha basi aanzishe icho chama aone mziki wake o/w aache mdomo anabwabwaja tu uyo.. Masab...li pia tokoilake lake....
 
Mayage mchumia tumbo anaishi kwa kutegemea makala halafu kwanini Jenerali Ulimwengu unampa Air Time mdwanzi kama huyu anaharibu gazeti letu makini, aendee kulekule Rai.
 
Ama kweli hili ni darasa tosha..mayage chukua notes, usome na kuelewa.
Next time ukirudia kupotosha itabidi uchapwe viboko hadharani..
 
dr slaa badili mifani... you can go deeper than that kwa ku refer hata nje ya tz

MTM

Kwa manufaa yako na wana JF Serikali yako imekabwa na wahisani kuhusiana issues hizo unazotaka Dr Slaa asizizungumzie. Kwa taarifa yako mambo hayo yote ndiyo kwanza yamepamba moto. Kikao kati ya serikali ya JMT na wahisani cha 24.6.2011 kilitoa action plan ya utekelezaji wa ufuatiliaji wa madeni ya EPA.

Taarifa ya sasa ni kuwa makumpuni kadhaa kama Ndovu Soaps,Bora Hotels and Appartments,Venus Hotels B.V.Holdings, VB Associates Kagoda Agricultre wamerudisha asilimia 100 fedha zilizofisadiwa. Jumla yote ni 70,725,425,541.39. Makampuni 13 hayajurudisha chochote.Kikao cha Troika kilitakiwa kukaa Taarifa ya kinachoendelea. Kwa taarifa ya wanaJF hata misaada inayopewa JMT iko conditioned kwenye matokeo ya EPA. Ndio maana narudia No Research no Right to speak.

Watanzania kweli wa ajabu, Wazungu wanafuatilia uwizi nchini kwetu sisi tunapiga porojo zisizo na tija. Alafu unaongelea maendeleo wakati hata hizo zilizorudi hujui zilirudishwa wapi. Maybe wanaobisha ni mafisadi au beneficiaries wa ufisadi.
 
Ni vizuri kafanya hivyo!

Sijalisoma bado la yaelekea anajibu kwa kuonyesha postive achievements za CHADEMA na hilo ni kosa!

Mayage kasema chama kina nafasi wafanye zaidi ya walivyofanya sasa! Sasa inaonekana watu hawapendi kukosolewa, hili nalo ni mapungufu ya kiuongozi! Ndo maana Dr Slaa naye hafai kuwa kiongozi wa nchii hii!

Haya ni maoni yangu kama mwana CHADEMA, unafiki kwangu hauna nafasi!!!

Hapo kwenye red: Ni macho yangu au ndo ulivyoandika? Ulitaka ajibu kwa kuonyesha negative achievements??? Otherwise, asante kwa kuthibitisha yale aliyosema kuwa kuna positive achievements hivyo CHADEMA ni chama makini.
 
MTM

Kwa manufaa yako na wana JF Serikali yako imekabwa na wahisani kuhusiana issues hizo unazotaka Dr Slaa asizizungumzie. Kwa taarifa yako mambo hayo yote ndiyo kwanza yamepamba moto. Kikao kati ya serikali ya JMT na wahisani cha 24.6.2011 kilitoa action plan ya utekelezaji wa ufuatiliaji wa madeni ya EPA.

Taarifa ya sasa ni kuwa makumpuni kadhaa kama Ndovu Soaps,Bora Hotels and Appartments,Venus Hotels B.V.Holdings, VB Associates Kagoda Agricultre wamerudisha asilimia 100 fedha zilizofisadiwa. Jumla yote ni 70,725,425,541.39. Makampuni 13 hayajurudisha chochote.Kikao cha Troika kilitakiwa kukaa Taarifa ya kinachoendelea. Kwa taarifa ya wanaJF hata misaada inayopewa JMT iko conditioned kwenye matokeo ya EPA. Ndio maana narudia No Research no Right to speak.

Watanzania kweli wa ajabu, Wazungu wanafuatilia uwizi nchini kwetu sisi tunapiga porojo zisizo na tija. Alafu unaongelea maendeleo wakati hata hizo zilizorudi hujui zilirudishwa wapi. Maybe wanaobisha ni mafisadi au beneficiaries wa ufisadi.
thank you very much dr. ninaamini hakuna executive leader wa ccm aliye na uwezowako na pia ambaye angejali kunijibu.

kama utafuatilia kwwnye ile thread waliyoweka makala yako, i called it "masterpiece".

lengo langu ni kukupa changamoto kwenye uchambuzi na ujengaji hoja uende beyond borders, mifano yote uliyotoa ina wenzake around the globe na ingekua vyema kuainisha na kuonyesha madhara, caveats au hata hao wezi/ mashetani walipofanikiwa ili tusiangukie kwenye takwimu

my message - goes beyond monotomy/repertition sometimes that you are used to: it was a constructive criticism coz we want a new horizon in our case studies, which in fact, ccm hawawezi kwa sasa labda wavue ngozi kabisa maana magamba yamewashinda [kuna kizungumkuti kinaendelea phillipines sijui watatokaje kutokana na viscious cycle ya ufisadi, we can learn alot), kuna ya thailand (thaksin na wenzake)

hitimisho, na wewe jifunze kuchukua challenges ppsitively, uliza kama hujaelewa na punguza povu na usiwe judgemental (alledgedly). Siwezi kuwa beneficiary wa epa uliza vijana wako wakuambie mimi nina msimamo gani kwenye hilo....na pia si mfanyakazi wala mdau wa serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania since march 29 2002, siku ya ijumaa [na sitegemei kufanya kazi kwa sasa kwani misimamo yangu inakinzana na watumishi wa serikali - mimi ni muwazi, siogopi na sio mnafiki]
 
MTM

Kwa manufaa yako na wana JF Serikali yako imekabwa na wahisani kuhusiana issues hizo unazotaka Dr Slaa asizizungumzie. Kwa taarifa yako mambo hayo yote ndiyo kwanza yamepamba moto. Kikao kati ya serikali ya JMT na wahisani cha 24.6.2011 kilitoa action plan ya utekelezaji wa ufuatiliaji wa madeni ya EPA.

Taarifa ya sasa ni kuwa makumpuni kadhaa kama Ndovu Soaps,Bora Hotels and Appartments,Venus Hotels B.V.Holdings, VB Associates Kagoda Agricultre wamerudisha asilimia 100 fedha zilizofisadiwa. Jumla yote ni 70,725,425,541.39. Makampuni 13 hayajurudisha chochote.Kikao cha Troika kilitakiwa kukaa Taarifa ya kinachoendelea. Kwa taarifa ya wanaJF hata misaada inayopewa JMT iko conditioned kwenye matokeo ya EPA. Ndio maana narudia No Research no Right to speak.

Watanzania kweli wa ajabu, Wazungu wanafuatilia uwizi nchini kwetu sisi tunapiga porojo zisizo na tija. Alafu unaongelea maendeleo wakati hata hizo zilizorudi hujui zilirudishwa wapi. Maybe wanaobisha ni mafisadi au beneficiaries wa ufisadi.
Ahsante Dr. Slaa, majibu yako yanajitosheleza,yenye hekima na yenye uchunguzi wa kina.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom