Dr. Slaa aiumiza CCM

Katibu wa itikadi na uenezi (Nape), bila itikadi kuwepo (CCM), ni tatizo kwelikweli. hatari yake unaweza kuwa vuvuzela, maana unazungumza bila falsafa au dira. Pole sana Nape CDM sio saizi yako.
 
Asante Doc,asante rais wangu.Nimefurahishwa na comments hizo kwaani mkakati umefeli tayari,wajipange upya.rip magamba
 
Siku CDM itakapoingia ikulu 2015 ndo watajua ni chama cha namna gani.
Nape anadhihirisha kuwa watanzania maskini, wanyonge wote wanaopenda mabadiliko kuwa ni watu wa kanda ya kaskazini, na Mafisadi na wezi wa mali ya umma kwake yeye ndo watanzania wa kweli.

Mungu Ibarikia Tanzania
Mungu Ibariki CHADEMA


Mungu wangu hajawahi kunidanganya, 2015 kitaeleweka tu.
 
Nape anafanya siasa za kizamani sana yani anadiriki kusema kwamba shibuda anapingwa sababu anatoka kanda ya ziwa,hivi haya maneno yatamshawisho nani,hata mtoto wa shule ya msingi hawezi kubali,propaganda za hivyo zilishapitwa na wakati

Huyu Nape ni sawa na mfa maji haishi kutapatapa. Wao ndo wanakuwa wa kwanza kuzungumzia ukabila halafu wanasema sera zao si za ukabila. Hawana mbinu mbadala hawa wameanza kuchoka
 
Tanzania Daima

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinadaiwa kuandaa fitina, mbinu na mikakati ya kukidhoofisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiwamo kumng’oa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.

Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa Dk. Slaa anaaminika ndiye amechangia kwa kiasi kikubwa kushamiri kwa CHADEMA na kudhoofika kwa CCM kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Hoja kubwa ya ufisadi na majina ya vigogo 11 wa serikali na chama tawala iliyotajwa na Dk. Slaa katika viwanja vya Mwembe Yanga vilivyopo jijini Dar es Salaam mwaka 2008 inasemekana ndiyo inayokitesa chama tawala.

Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa kitendo cha baadhi ya makada wa CCM kudakia hoja hiyo na kutaka wenzao watimuliwe ndani ya chama hicho imeleta mpasuko mkubwa na makundi yanayokinzana.

Inadaiwa kuwa kuaminika kwa Dk. Slaa katika jamii ndiko kulikoifanya izidishe chuki na kukosa imani dhidi ya CCM na viongozi wa chama hicho wanaodaiwa kushindwa kuandaa na kuitekeleza mikakati ya kumuondoa Mtanzania kwenye lindi la umaskini.

Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa hivi sasa CCM inamuona Dk. Slaa ni hatari kwao hasa kutokana na kiongozi huyo kutokuwapo bungeni.

Inasemekana kutokuwapo bungeni kumemuwezesha Dk. Slaa kuzunguka maeneo mengi kuimarisha CHADEMA na kuidhoofisha CCM ambayo inayumba kila kukicha kutokana na kutafunwa na uhasama wa makundi.

Inadaiwa baadhi ya vigogo wa CCM walikuwa wakiombea CHADEMA imteue Dk. Slaa awanie ubunge wa Arumeru Mashariki uliofanyika hivi karibuni ambao ungemfanya atumie muda mwingi kuangalia mambo ya kibunge, jimbo na hivyo kukosa muda wa kukiimarisha chama.

Slaa anena

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Dk. Slaa alisema anajua CCM wana mbinu nyingi chafu za kumdhoofisha pamoja na CHADEMA, lakini kamwe hawataweza kuzifanikisha.

Alisema hivi sasa akili yake imejikita katika kukiimarisha chama na ili azima ya kuing’oa CCM mwaka 2015 itimie.

“Hao CCM wewe waache waendelee na fitina, hila na mbinu zao chafu maana muda wao wa kukaa madarakani unaelekea ukomo, CHADEMA inajiandaa kuchukua uongozi wa nchi,” alisema.

Alipoulizwa kama haoni CCM inamtumia mbunge huyo kuivuruga CHADEMA, Dk. Slaa alikiri kuwa yawezekana, maana wana mbinu nyingi za hovyo, lakini akasisitiza kuwa hawako tayari kuruhusu migororo.

Ampuuza Shibuda

Dk. Slaa amesema hawezi kujibizana kwenye vyombo vya habari na Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda.

Kauli hiyo ya Slaa imekuja siku chache baada ya Shibuda kuingia kwenye malumbano mazito na Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha), kufuatia kauli yake ya kutangaza kugombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA, lakini akimwomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete awe meneja kampeni wake.

“Kwangu mimi, Shibuda sina la kumzungumzia, tunayo mambo mengi ya msingi ya kufanya, hivyo naimarisha chama si kuendeleza malumbano kwenye vyombo vya habari, tuna taratibu zetu za vikao, atashughulikiwa huko kama kuna hoja,” alisisitiza.

CCM yajitutumua

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alikana madai ya chama chake kumfanyia hila, fitina na mchezo mchafu Dk. Slaa na CHADEMA.

Nape, alisema hakijampandikiza mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda (CHADEMA) kukivuruga chama hicho.

Alisema madai hayo ni ya kipuuzi na Shibuda ana haki ya kuwania nafasi yoyote ndani ya chama hicho.

“Shibuda kama mwanachama ana haki yake kulinngana na katiba ya chama, hivyo wasimbague kwa kuwa anatoka Kanda ya Ziwa.

“CHADEMA inafahamika ni chama cha Kanda ya Kaskazini na suala hili lingeibuliwa na mwanachama anayetoka yuko wala mambo yasingefika yaliyopo, hivyo CHADEMA wasitafute visingizio vya kuondoa hoja hii na kumnyima haki yake Shibuda,” alisema Nape.

Alisema sheria za nchi zinaelekeza chama kiwe cha nchi nzima, lakini CHADEMA kimejieleza kuwa ni chama cha Kanda ya Kaskazini.

Mkakati na Dk. Slaa

Akizungumzia madai kuwa chama hicho kina mpango wa chinichini wa kumrudisha bungeni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, Nape alisema chama hicho hakimhitaji na iwapo CHADEMA kimemchoka kimfukuze.

Alisema kuwa katika vikao vyao hawana muda wa kumjadili Dk. Slaa kwa kuwa Watanzania wanafahamu kuwa ni mzushi.

Kati ya watu wanaozidi kukididimiza chama cha mapinduzi ni huyu bogus Nepi Nyauye na Mukama,ubaya ni kua mwenyekiti wao na hata wanachama wake walio wengi hawajaliona ilo,ni wachache sana wenye uelewa ndani ya c.c.m wameliona ilo na wameamua kukaa kimya!Nape uwa hana uwezi wa kujenga hoja kabisa za kuweza kukiletea uhai chama chake kwa wananchi wa Tanzania!yeye kazi yake amebaki na propaganda za kitoto,ukanda mara sijui vile,watu hawadanganywi kwa upuuzi kama huo,kwa nini hasijifunze kuwa na hoja zenye tija kuhusu matumizi ya rasilimali za nchi,maendeleo ya wananchi yaliyoletwa na chama chake,mfumo wa uchumi wa nchi n.k!haoni vijana wenzake kina Mnyika,Makamba,Zitto nk walivyo?nashindwaga kuelewa huyu Nape ame elimika nini!
 
Siku CDM itakapoingia ikulu 2015 ndo watajua ni chama cha namna gani.
Nape anadhihirisha kuwa watanzania maskini, wanyonge wote wanaopenda mabadiliko kuwa ni watu wa kanda ya kaskazini, na Mafisadi na wezi wa mali ya umma kwake yeye ndo watanzania wa kweli.

Mungu Ibarikia Tanzania
Mungu Ibariki CHADEMA


Mungu wangu hajawahi kunidanganya, 2015 kitaeleweka tu.

yap! Mungu si mwanadamu hadi aseme uongo.
 
Slaa hana jipya...yale yale ya 2008!
Haswaa, ni mheshimiwa Kikwete peke yake mwenye mapya kila siku, kama hivi jana kaahidiwa kujaziwa bakuli lake la kuombea na fedha za kuimarisha kilimo kwanza kama sio kilimo mwisho, ameshajenga barabara za kuning'inia Dar, ameshanunua meli kubwa na kuipeleka ziwa Victoria,amewateua mawaziri na wakuu wa wilaya wenye akili kuliko watanzania wooote! au vipi?
 
nape leo ana mtetea shibuda wakati walimpiga chini kwa mambo hayohayo ambayo yanalalamikiwa ya kuwa mnafiki wala hakumtetea, leo wanamtetea? kweli shibuda katumwa
 
Majibu mazuri sana hayo Dr Slaaa,,kiongozi mwenye busara utamjua tuu,,kama CCM walijua kuwa wakimshinikiza Shibuda kusema ujinga atasababisha mgogoro ndani ya chama basi ccm imekula kwao,,,MBOWE KIMYA,,SLAA KIMYA ila wanajua wapi pa kumkamata Shibuda,,,ama kweli njia ya mjinga nimeamini ni ndogo,,,
 
Kati ya watu wanaozidi kukididimiza chama cha mapinduzi ni huyu bogus Nepi Nyauye na Mukama,ubaya ni kua mwenyekiti wao na hata wanachama wake walio wengi hawajaliona ilo,ni wachache sana wenye uelewa ndani ya c.c.m wameliona ilo na wameamua kukaa kimya!Nape uwa hana uwezi wa kujenga hoja kabisa za kuweza kukiletea uhai chama chake kwa wananchi wa Tanzania!yeye kazi yake amebaki na propaganda za kitoto,ukanda mara sijui vile,watu hawadanganywi kwa upuuzi kama huo,kwa nini hasijifunze kuwa na hoja zenye tija kuhusu matumizi ya rasilimali za nchi,maendeleo ya wananchi yaliyoletwa na chama chake,mfumo wa uchumi wa nchi n.k!haoni vijana wenzake kina Mnyika,Makamba,Zitto nk walivyo?nashindwaga kuelewa huyu Nape ame elimika nini!

awali nilizani yusupu makamba aliondoka na kile kikundi cha kizua hili,,propaganda kale,,cha yulewa tmk aliye toka cuf,,,,,nani yule///////kumbe ndio broo nape karithi pochi,,,,,aibu,,,aibu,,aibu
 
Back
Top Bottom