Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 864
Mgombea Urais kipitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kesho ataunguruma Nyumbani kwake Karatu. Dr Slaa anakwenda kukutana na wanakaratu aliowatumikia kwa kipindi cha miaka kumi tano(15) akiwa Mbunge. Kabla Dr Slaa hajaenda tayari kuna timu moja toka Makao Makuu imeshakwenda jana kwaajili ya kufanya maandalizi kwa kushirikiana na Watu wa Karatu.
Timu nyingine ikiongozwa na Kamanda Freeman Mbowe inaondoka leo kuelekea huko.Viongozi wa ngazi ya juu wa chama pamoja na Prof Baregu ndio timu inayomsindikiza Dr Slaa. Baada ya kuzungumza na Wanakaratu Dr Slaa atacchukua fomu na kuzunguka nchi nzima kwaajili ya kupata wadhamani. Safari ya kuzunguka nchi nzima Dr Slaa atasindikizwa na Kamanda mwenzake Freeman Mbowe.
Wengine tumebaki Makao Makuu tukiendeleza mapambano.Leo tutakuwa na wawakilishi/mashujaa wa wanazuoni walisaini kutaka Dr Slaa agombee Urais kwaajili ya kupanga mikakati ya namna ya kumuunga mkono Dr Slaa kwa staili mpya kabisa. Mkutano huo unatarajiwa kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 7 mchana Makao Makuu Kinondoni Manyanya Mtaa wa Ufipa.Mnakaribishwa sana kwa wale mnaopenda kushiriki harakati hizi muhimu.
Find attachment hotuba ya Ufunguzi ya Mwenyekiti wa Kamati ya BAVICHA-Bw John Mnyika.
Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.
Angalia picha chini:
Dr. Slaa akikabidhi fomu kwa Mwenyekiti Mbowe
Karatu wakiridhia Dr. Slaa awe mgombea Urais.