Dr. Slaa aingilia kati Uchaguzi wa BAVICHA; Magazeti yalalamika

Hii habari kaandika yeye mwenyewe na kujijibu kwa kujiita ANONY.

Siyo gazeti hilo ila ni BLOG.......

Jamaa Msh***** sana huyu kwa kutumia jina la MAJIRA na kudanganya watu hapa....

Habari ipo hapa: GAZETI HURU LA KILA SIKU:: Heche aibuka kidedea BAVICHA

MAJIRA+MASTER+HEAD2.jpg
Sikonge kumbe huyu Bwn ni mhuni, yaani yeye mwenyewe kaandika tena kajijibu kama Anonymous. Mpuuzi kabisa hawezi kutuyumbisha ukweli ameisha upata, uchaguzi umeisha vizuri na viongozi wamepatikana, kelele za nini tena?????????
 
Mimi naona bora ukasome historia ya hao jamaa ndio uongee, Slaa kupanda juu ya jukwaa na kuropoka unataka kumfananisha na hizo number, kweli wewe unaupungufu flani.Slaa unatakiwa kumweka kwenye kundi la kina Cheyo na mtikila
Pilipili inalimwa shamba wewe kinachokuwasha nini? Kama mwananchi wameona walivyoona wewe ungana nao sasa makelele ya nini we kenge. mambo ya chadema yanakuhusu nini, mbona unashitukashituka au umekalia msumari? utakoma
 
Changuzi hii jamani haikuwa na TV ndani?, hiyo ndo funga kazi ya ubazzazzi huu. Kama Mwananchi ni waongo basi na Gazeti lao lilaniwe na kama wanasema kweli basi hakuna Chama mbadala wa CCM vyote ni CCM B, C, D, E etc mpaka viishe.
 
HATIMAYE uchaguzi wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) ulimazika jana kwa kumpata Bw. John Heche kuwa Mwenyekiti wa umoja huo.

Pamoja na kupatika kwa kiongozi huyo, uchaguzi huo uligubikwa na mizengwe mbalimbali ikiwemo rushwa na mambo ya 'kujuana' yaliyooneshwa wazi na viongozi wa chama hicho.

Kwa mujibu wa uchuguzi uliofanywa na Majira juzi usiku, uchaguzi huo ulifanyika huku kukiwa na makundi matatu, makundi hayo ni yale yanayomuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Zitto Kabwe na lile lisilomuunga mkono mtu yeyote katika chama hicho.

Uchunguzi huo ulibaini kuwa kundi linalomuunga mkono, Bw. Mbowe ndilo lilokuwa na nguvu zaidi na ndilo lilochukua kiti hicho kutokana na mwanzilishi wa chama hicho, Bw. Edwin Mtei kuliunga mkono kwa asilimia mia.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Baraza la Wazee kilidokeza kuwa, maamuzi ya kufanya uchunguzi wa wagombea yalifikiwa baada ya kugopa kivuli cha Bw. Zitto ambaye ameonekana kuungwa mkono na vijana wengi ndani ya chama hicho.


Kilisema kuwa baada ya kubaini uwezekano wa kundi hilo kushinda, baraza la wazee lilikubaliana kutafuta mambo yatakayowamaliza wagombea hao ili wasipitishwe katika kugombea kiti hicho.

"Ndugu yangu napenda kusema kuwa chama hiki sasa kinaenda pabaya walitafuta kila njia ya kuwamaliza vijana na njia waliyoipata ni kuwatutafutia tuhuma zitakazowafanya waondoke katika kuwania nafasi hiyo...lakini tulipigana na ikashindikana," alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.

Alieleza kuwa tuhuma hizo ni kundi hilo kutaka kuunganisha nguvu katika uchaguzi huo ili kumpigia kura mtu moja jambo ambalo kamati ya wazee ilipingana na suala hilo ikidai kuwa ni jambo linalowagawa vijana ndani ya chama.

Chanzo hicho kilisema kuwa katika uchaguzi wowote makundi lazima yawepo ndo maana mgombea hawezi kupata kura kwa asilimia mia moja hata akiwa pekee yake.


Alisema tuhuma nyingine zilizofanya kuenguliwa kwa wagombea hao ni kupokea wajumbe kutoka Zanzibar jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote lakini kutokana na mizengwe iliyoandaliwa na kamati hiyo ilibidi watu hao waadhibiwe.


Alisema kuwa tuhuma nyingine ilikuwa ni kupiga kampeni kabla ya muda uliopangwa na tume hiyo hali iliyosababisha kuenguliwa dakika za mwisho katika uchaguzi huo.


"Tuhuma nyingine iliyoelezwa ni wagombea hao kutaka kupindua chama hicho kwa kuhamisha agenda za chama hicho na wengine walihofiwa kuwa ni usalama wa taifa," kilisema chanzo chetu.

Hata hivyo Mjumbe huyo wa baraza la wazee alisema kwa upande wa Bw. Heche nako kulikuwa na tuhuma za kupokea wajumbe ambao kamati haikutaja kuwa wanatoka katika mkoa upi lakini alijitetea kuwa ni ndugu zake.

"CHADEMA tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa kigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anapokosea tunataka awajibishwe, sisi leo mtu anakosea wakati wa mchakato wa uchaguzi lakini tunasema tunafanya uchunguzi je akipata madaraka tunamchukulia hatua gani kwani atakuwa tayari amepata madaraka," kilisema chanzo.

Chanzo hicho kiliendelea kuhoji ni kwa nini mgombea huyo aachwe na kuchukua madaraka huku akiwa na tuhuma hivyo akataka haki itendeke kwa wote.

Naye Tumaini Makene anaripoti kuwa;

Kamati ndogo maalum, kwa ajili ya uchunguzi wa uchaguzi huo iliyoundwa na kamati kuu ya chama hicho ilibaini kuwepo kwa vitendo vichafu ikiwemo baadhi ya wagombea kutaka kuundwa makundi ili kudanganya wapiga kura kwa nia ya kutaka ashinde mtu wanayemtaka kwa hila zao.

Akizungumza na majira jana akiwa katika uchovu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, pamoja na kutotaka kuzungumzia tuhuma hizo za rushwa kwa undani akisema "mengine yanahitaji maamuzi ya juu", alisema kuwa wagombea hao watatu walioenguliwa baada ya kuthibitisha kuwa wamekwenda kinyume na katiba na kanuni za chama, kifungu cha 10, wamekiri pia kuwa wao walijihusisha kutengeneza agenda ya BAVICHA.

"Sasa hilo ni suala kubwa agenda ya BAVICHA ni suala la mkutano na haliwezi kuwa la wao watatu lakini walibainika kujihusisha na kundi la Bw. Habib Machange ambapo ilibidi chama kiingie gharama ikiwemo wajumbe wa kamati hizo kufanya kazi tangu saa saba usiku wa juzi mpaka asubuhi jana na baadhi ya wajumbe walishindwa kurejea kwao," alisema Dkt. Slaa.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Majira ilibainika kuwa mmoja wa wabunge wa chama hicho alijihusisha na kusimamia vikao vya usiku wa manane vilivyokuwa vikitumika kuwalubuni wajumbe kugawa fedha, kuwanunulia pombe usiku wa kuamkia uchaguzi akitaka kuweka mtandao unaodaiwa kuwa na lengo la kusambaratisha chama hicho.

Mbunge huyo machachari kutoka Kanda ya ziwa ametajwa pia kutoa udhamini wa mmoja wa mgombea aliyeenguliwa kwa lengo hilo ambapo imeelezwa kuwa suala lake pamoja na vituko vingine vitafikishwa mbele ya Kamati Kuu kwa maamuzi zaidi.

Alipoulizwa juu ya tuhuma kwa mbunge huyo (jina tunalo), Dkt. Slaa hakuwa tayari kulizungumzia na kusema kuwa liko ngazi ya juu ya kamati kuu.

Wakati hayo yakiendelea Bw. Heche alisema yuko tayari kufanya kazi katika nafasi hiyo akishirikiana na wenzake ili BAVICHA iwe sauti ya kupigania maslahi ya wananchi wanyonge.

Akizungumza na majira jana, Bw. Heche alisema kuwa BAVICHA itasimama kwa maslahi ya nchi na chama hicho kwa jitihada za kuchukua dola kwa ridhaa ya wananchi.

Bw. Heche alipata kura 147 sawa na asimilia 56 ya kura zote zilizopigwa 267 ambapo kura tatu ziliharibika.

Walioenguliwa katika uchaguzi huo ni Greyson Nyakarungu, Mwampamba na Bernard Saanane.



Source: GAZETI MAJIRA.


Comment iliyotolewa na anonymous:


Hakuna kitu hapo.hebu angalia hii undugu,kujuana, Rushwa na Viongozi kupanga Safu yao. Hawa wa Mbowe, hawa wa Zito. Waliobaki lazima walikuwa wa Slaa. angalia pia hili CHADEMA kila siku kelele kuhusu Rushwa, hivi kweli Mtu kama Mbowe ataacha hiyo? kama kwenye kampuni zake halipi kodi na kwenye Chama anawachakachua kwa kuwauzia Magari Chakavu itakuwa kwenye Uchaguzi wa Vijana? hakuna Demokrasia ndani ya Chadema ni Uhuni tu na Undugu uliojaa huko. Watanzania hatuwezi kufanya kosa kuwaweka Madarakani Chama kama hiki. Mbona Visiwani hamtii Mguu huko? inaeleweka Wazanzibar hawataki ubabaishaji walishawakataa Mapeema kabisa. hiyo pia inawanyima sifa ya kutawala. haya ni Machache tu, Siri na Mambo wanayoyafanya tunayo na tunayajua. 2015 kiboko ni kama 2010.

Duh, kweli gazeti la majira kiboko limeamua kuwabwaga Chadema baada ya kuona wanayo fanya siyo. Hongereni sana kwa kutuhabarisha wananchi, hiki chama cha CHAKushindwa tumeisha kielewa
 
first of all i would like to congraturate the chadema party cause they have proven that they are the only party in tanzania that can handle their conflicts by peacefull means,second to mr john heche for being elected as the head of the party's youth wing , in politics ,we may disagree on some issues but as long as the issue serves the interest of the tanzanian people as well as our party's there is no substitute to agreement.
 
Tungojee uchaguzi mkuu wa cdm tuone watamuundia zengwe gani mhe zitto zuberi kabwe maana naona cdm na wao wamekuwa wazee wa "zengwe"
Kwahiyo kazi yako kungoja mambo ya chadema tu! Huna la kufanya, macho yote chadema.
Wala hutaki kumsaidia boss wako lipumba kuimarisha cuf ili angalao ipate wabunge watano 2015?
Waswahili utawajua tu! Hana la kufanya. Anangoja apate la kuongea nyumba ya jirani.
 
Ndugu yangu ,
Narejea kikao chetu cha leo ubungo blue pearl hotel.
Nakushauri kuwa msimamo wako wa kujitoa ndani ya chama hauna manufaa yeyote kwa sasa.
Unakumbuka malengo yetu ya muda mrefu,hebu kaa na tafakari kwa kina kirefu kwani kama nilivyosema mchana na sasa narudia ni kuwa kufanya hivyo ni kujimaliza kwani hawa jamaa watatumaliza sisi waislamu kwani wamewaengua wakristo na kibaya zaidi mchagga tena mkatoliki.
Nimeona nipitie hapa kukushauri ili tuende salama haswa baada ya kukataa ushauri wangu leo mchana hotelini.
Tutafakari kwa kina kabla ya kuamua Habib.
NImeongea na PROF safari anasema kwa misingi hiyo atatupinga hadharani.
Wadau naombeni ushauri.
 
kwani aliyeshika nafasi ya pili ni dini gani? kwanini tusiamini mtu ameshindwa kwa merit badala ya kusingizia dini?
 
huyu mchange ndo nani?ndo alikuwa nawatumia wajumne mijihela kwa MPESA??? mwache aende kwenye lichama la wezi
 
Ushauri wangu.
1. Sungura akikosa zabibu husingizia mbichi.
2.Thread yako ya irekebishe imekaa kama mtu anae fikiri kwa miguu.
3.Jaribu wakati mwengine kuto "generalize"(waislam, wakristo) zungumza yanayo kuhusu.
 
Tunaomba utusaidie sisi ambao hatuwepo nanyi mchana ulipomshauri asijitoe kwenye chama,
  • kwanini Habib anataka kujiuzulu,wewe umemshauri asijitoe kwa misingi ipi?
  • kwanini Proffesa Safari amchane,si kila mtu ana uhuru wa kuwa mwanachama wa chama fulani anachoona yeye ni sawa?
  • unataka kutuambia kwamba CHADEMA watu wakitofautiana hawana namna ya kutatua tofauti zao kiofisi hadi iwe kwenye majukwaa?
Binafsi namkubali sana Habib,ningependa kujua grounds za yeye kutaka kujitoa ili aweze kushauriwa. Hatuwezi shauri bila kujua kwanini anataka kufanya hivyo...!!!
 
Nili kuwepo kwenye ukumbi wa P T A ambapo uchaguz wa vijana chadema ulikuwa unaendelea na nikagundua kuwa bado Zitto kabwe bado anatumiwa na mafisadi kwani katika uchaguzi huo kulikuwa na makundi matatu la mboye la zitto ,na lingine ambalo lilikuwa haliungi upande wowote.. .lile la zitto mara nyingi ndo limekuwa likileta matatizo kama utakumba kipindi kile wakina kafulila hadi wakaondoka kwenda NSSR MAGEUZ sasa kwenye ule uchaguz pia kund lile lilikuwa linataka pia kuleta matatizo . Lakini pia habari kutoka ndani ya chadema zieleza kuwa mbunge huyo amesha tangaza azma ya kugombea Urais hatua inayopingana viongoz waandamiz wachadema ambao kupitia maandamano wanamjengea tena Dr slaa nafasi ya kugombea tena nafasi hiyo.Jaman tusilale zitto bado anampango wakuiangusha chadema
 
Ushauri wangu.
1. Sungura akikosa zabibu husingizia mbichi.
2.Thread yako ya irekebishe imekaa kama mtu anae fikiri kwa miguu.
3.Jaribu wakati mwengine kuto "generalize"(waislam, wakristo) zungumza yanayo kuhusu.

Thank you!
 
demokrasia maana yake ni kuruhusu yeyote anayejiona anafaa kugombea

sio kusikiliza chama kinasemaje

zitto atakuja juta kwa nini hakuhama chadema mapema
 
Back
Top Bottom