Dr slaa afunguka shinyanga na kuionya serikali wkati wa kampeni za uchaguzi wa kata ya mwawaza

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Kampeni za udiwani kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga mjini jana iliendelea kwa katibu mkuu wa CDM mh. Wilboard Peter Slaa kumsimamisha mgombea wa udiwani kupitia CDM mh. Anthony Peter Mhola kuweza kujinadi yeye mwenyewe huku akipima uwezo wake wa kujenga hoja tofauti na staili wanayo tumia vyama vingine kuwanadi wagombea wao na kuwaombea kura kama vile hawana midomo ya kuongea na wananchi.

Mkutano huu ambao ulifurika mamia ya wakazi wa manispaa hii ya Shinyanga mjini toka sehemu mbalimbali wengi wao wakitembea kwa miguu mile nyingi kwenda kumsikiliza kiongozi wa CDM ambaye wanaamini ndiye rais wa mioyo ya Watanzania.

Kampeni hizo ni mfululizo wa kampeni za uchaguzi wa udiwani wa kata ya Mwawaza mara baada ya kifo cha aliyekuwa mgombea wa kata hiyo.

Akiongea na umati mkubwa uliofurika kwenye kiwanja cha mpira wa miguu cha shule ya msingi Mwawaza Dr. Slaa alifunguka na kuzungumzia kwa mara ya kwanza suala la kutekwa Dr. Ulimboka na kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi huku akilaani serikali kuwaongopea wananchi wake tofauti na mipango yao ya maendeleo iliyowekwa kwenye vitabu ambvyo vimebaki kwenye makabrasha.

Akizungumzia suala la kutekwa Dr. Ulimboka alisema ameshangazwa sana na serikali kupitia vyombo vyake vya dola kushindwa kumwita na kumhoji Dr. Ulimboka lakini lilipojitokeza suala la mauaji ya kamanda Liberatus Barlaw serikali kupitia rais wa nchi imelikemea na kulitaka jeshi kuhakikisha watuhumiwa wote walio husika wanachukuliwa hatua za klisheriailihali tukio la Dr. Ulimboka limeachwa mikononi mwake kama vile hana haki ndani ya nchi yake.Alikwenda mbali zaidi kwa kumtaka rais Kikwete atoe agizo kali kama alivyofanya kwa kamada Barlaw vinginevyo ile dhana ya serikali kuhusika na utekwaji nyara wa Dr Ulimboka utakuwa na mshiko.Huku akizungumza kwa machugnu dhidi ya tukio hilo,
bila kumung'unya maneno kama ilivyo kawaida yake,alimtaja bwana Ramadhan Kigonda kuwa mhusika wa tukio la Dr. Ulimboka kama ilivyotabanaishwa na gazeti la Mwanahalisi katika uchambuzi wa tukio zima la kutekwa nyara na kutupwa nje ya jiji la DSM maeneo ya msitu wa Pande.

Akikemea kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi,Dr Slaa alishangazwa na uamuzi wa kimabavu wa kulifungia gazeti hilo bila kubainisha makosa yake,ilihali chombo pekee cha kusimamia haki ni mahakama.Aliishutumu serikali ya CCM kwa ubabe wake huo wa kuwanyima wananchi haki yao ya kikatiba ya uhuru wa kupata habari na kuitaka serikali ilifungulie gazeti hilo kipenzi cha wananchi kwa kufichua maovu ya serikali mara moja.

Alishangazwa na kitendo cha rais wa nchi kuendelea kustarehe nchini Oman ilihali nchini kwake hali ni tete,huku akimlinganisha na rais wa Afrika Kusini mh. Jackob Zuma kukatisha ziara yake akiwa nje ya nchi baada ya kupata habari za machafuko yaliyotokea chini mwake wakati wa saga la mgomo wa wafanyakzi wa migodi na kurudi nyumbani kulitafutia uvumbuzi.

Akiitaka serikali kumchukulia hatua na kumfikisha mahakamani bwana Ramadhani Kigonda ambaye ni afisa wa usalama wa taifa Ikulu,Dr Slaa alisikitishwa na matukio ya uvunjaji amani na mauaji yasiyo rasmi kwa wananchi wasio na hati huku serikali imekaa kimya.

Dr.Slaa alishangazwa na kuona serikali ikishindwa kuwalipa posho watoto 600 wa shule za msingi walio shiriki kwenye halaiki kama walivyoahidiwa wakati wa maandalizi ya uzimaji mwenge,sherehe zilizofanyika kitaifa mkoani Shinyanga.Huku akishangazwa na kuona watoto wa walalahoi tu ndiyo walio shiriki kucheza halaiki hiyo na kuwaacha watoto wa wakubwa wanaosoma Savannah Plain school wakiendelea kusoma na kupata elimu bora wakati watoto wa wanyonge wakipigwa jua miezi mitatu ya mafunzo mfululizo.

Akichambua hali ya uchumi inayokuwa kwenye makaratasi zaidi huku wananchi wakiendelea kutaabika na maisha kiasi cha kushindwa kupata bei nzuri ya mazao yao, Dr Slaa alinukuu takwimu za uchumi toka kwenye vitabu vya serikali alishangazwa na kuongezeka kwa bei ya pamba kwa msimu uliopita wa 2011/12 na serikali kuuza kiasi kidogo cha pamba wakati wananchi wakipewa bei ya chini.

Aliionya serikali kuacha kuandika mipango yake mizuri vitabuni lakini wakifika kwa wananchi wanaelezea tofauti na waliyoyaandika,huku wakiwadanganya wananch bei ya mazao katika soko la dunia imepungua ilihali vitabu vyao vya takwimu vinaonyesha bei iko juu kwa kuwa tu wananchi hawawezi kuvipata vitabu hivyo na kujua hali halisi.

Dr. Slaa aliishangaa serikali hii ya chama cha mapinduzi kwa kupata ushauri wa waganga wa kienyeji na kuacha ushauri wa wataalamu mbalimbali,huku akisisitiza kuwa yeye binafsi hakatai wala kuwabeza waganga hao,kinachotakiwa ni waganga kufanya kazi zao za kiganga na kuacha mambo ya uchumi yafanywe na wataalamu.

Akimuinua mgombea wa udiwani wa kata hiyo kupitia CDM,Dr Slaa alimtaka mgombea wake aeleze nini atawafanyia wana wa Mwawaza iwapo watamchagua.Kauli hiyo ilikuwa ni mtihani ambao alifuzu kwa kueleza mipango na mkakati wake kuhakikisha wananchi wake wa Mwawaza wanapatiwa huduma muhimu za kijamii kama vile maji na umeme ambao kwao ni kama nyota ya jaa.Huku akishangiliwa na umati wa mamia ya wananchi mh. Anthony Peter Mhola alisema yupo tayari kuwatetea wananchi wa kata hiyo hadi pumzi yake ya mwisho na kuwataka wananchi wa kata hiyo kutomuangusha.

Mkutano huo ulimalizika bila kuwa na vurugu wakati wote wa kampeni huku Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa CDM taifa mh. Rwekatare akiwataka Polisi wasimamie haki ikiwa ni pamoja na kuwaonya wafuasi wa CCM ambao wanatumiwa kuwashambulia wananchi wakati wanatoka kwenye mikutano yao ya kampeni,na mwisho w
a mkuatano zoezi la kujivua gamba liliendelea kama kawaida huku wananchi wakimchangia mgombea wao pesa za kuweza kufanikisha juhudi zao za kuikomboa Mwawaza mara baada ya kutelekezwa toka kuundwa kwa dunia hii
 
Umetueleza kama nasi tulikuwepo kufahamu yaliyojiri,pongezi kwako mleta mada na pongezi kwa wnanchi wa shinyanga kufahamu umuhimu wa kutetea haki yao kwa kuhudhuria wengi
 
Hakuishia hapo Dr. Slaa alifika mbali zaidi akiweka wazi mpango wa serikali kupitia bwana Nzoka na Ramadhan Kigonda wa kuhakikisha Dr Slaa ana kufa ikiwa ni mpango kabambe ulioandaliwa kwa kushirikiana na waganga wa kienyeji.Akitilia msisitizo suala hilo kwa kupata nakala toka miongoni mwa waandaji wa mkakati huo Dr.Slaa alisema kamwe hatorudi nyuma kuwatetea wanyonge na mwenye dhamana na uhai wake ni Mwenyezi Mungu pekee,akitaka afe atakufa
 
Sidhani kama kuna nchi duniani hata akhera ina rais kiazi kama hii ya kwetu. Kuna mtafaruku, watu wanauana, yeye anakwenda kupanda gari za kukokotwa na farasi!
 
Sidhani kama kuna nchi duniani hata akhera ina rais kiazi kama hii ya kwetu. Kuna mtafaruku, watu wanauana, yeye anakwenda kupanda gari za kukokotwa na farasi!


Lakini viongozi hao hao wa dini walimnadi kuwa ni chaguo la Mungu,basi kama kweli ni chaguo la Mungu basi ni chaguo la kuwaangamiza Watanzania.Rais haumwi kichwa kuona hali ya nchi tete,kila sehemu inanuka,machafuko nchi nzima vifo visivyo rasmi.Angalie sana mwenendo wake.Kuwahadaa wanajeshi kwa kuwalipa posho lukuki sio tija,kwani hata hao wanajeshi wana ndugu zao ambao wanao hitaji maisha bora.
 
Vasco Da Gama amewasili hali tete,lakini cha ajabu hatakubali kushindwa sia ajabu keshokutwa akawa safarini tena.
 
Hakuishia hapo Dr. Slaa alifika mbali zaidi akiweka wazi mpango wa serikali kupitia bwana Nzoka na Ramadhan Kigonda wa kuhakikisha Dr Slaa ana kufa ikiwa ni mpango kabambe ulioandaliwa kwa kushirikiana na waganga wa kienyeji.Akitilia msisitizo suala hilo kwa kupata nakala toka miongoni mwa waandaji wa mkakati huo Dr.Slaa alisema kamwe hatorudi nyuma kuwatetea wanyonge na mwenye dhamana na uhai wake ni Mwenyezi Mungu pekee,akitaka afe atakufa

Hakuna atakaye mgusa..Hata nywele zake hazitanyofolewa na yeyote....Analindwa na malaika wa Mungu 24/7.....Wala asiwe na mashaka kabisa!
 
Nani amuue Slaa? Anaweweseka hovyo tu huyo. Haamini kwamba yeye si rais na hatakuwa rais hivyo anatumia kila mbinu ya uchochezi. Domo panaaaaaa! Halafu alama ya v ya cdm maana yake nini vile!
 
Nani amuue Slaa? Anaweweseka hovyo tu huyo. Haamini kwamba yeye si rais na hatakuwa rais hivyo anatumia kila mbinu ya uchochezi. Domo panaaaaaa! Halafu alama ya v ya cdm maana yake nini vile!
Maana yake Vua Gamba lako, Vaa Gwanda! Umeelewa mpuuzi wewe? Next time do your homework thoroughly before you openly show up your stupidity! Pambaf!
 
Nani amuue Slaa?
Anaweweseka hovyo tu huyo. Haamini kwamba yeye si rais na hatakuwa rais
hivyo anatumia kila mbinu ya uchochezi. Domo panaaaaaa! Halafu alama ya v
ya cdm maana yake nini vile!

Povu la nini!
Ikiwa si tishio kwenu magamba acheni kumfuatafuata...!
 
kamanda huu ndo wakati mzuri kuwa shamba wao waache wagombane wakipatatana we kavune ushindi wa nguvu 2015
 
Hakuishia hapo Dr. Slaa alifika mbali zaidi akiweka wazi mpango wa serikali kupitia bwana Nzoka na Ramadhan Kigonda wa kuhakikisha Dr Slaa ana kufa ikiwa ni mpango kabambe ulioandaliwa kwa kushirikiana na waganga wa kienyeji.Akitilia msisitizo suala hilo kwa kupata nakala toka miongoni mwa waandaji wa mkakati huo Dr.Slaa alisema kamwe hatorudi nyuma kuwatetea wanyonge na mwenye dhamana na uhai wake ni Mwenyezi Mungu pekee,akitaka afe atakufa

Wamesaha yale ya Shekhe Yahaya eeh!ngoja kiwarudie wao
 
Nani amuue Slaa? Anaweweseka hovyo tu huyo. Haamini kwamba yeye si rais na hatakuwa rais hivyo anatumia kila mbinu ya uchochezi. Domo panaaaaaa! Halafu alama ya v ya cdm maana yake nini vile!

Makalio yako yana moto moto kama jina lako!


modz laana itawaandama mkinifungia, watu wanaudhi!
 
Back
Top Bottom