Dr Slaa afanyiwa hujuma Morogoro

acheni raia wasikilize wapime na waamue wenyewe, hii mambo ya kuwa treat kama watoto wa chekechekea inaleta picha mbaya kwa chama chetu ambacho kimsingi ndicho chenye sera nzuri kuliko za cdm.

Ungeenda Kumwelewesha Haya Maneno Joel Bendera!! Mheshimiwa Rais Alimtoa Huko Korogwe anapalilia Michungwa Baada ya Kubwagwa na wanajimbo sasa anailinda serekali kwa kutumia Upanga akitegemea ndio anamfurahisha Aliyemteua!! Why Only Morogoro?
 
kwa mwendo huu, CCM imefikia mwisho wa kufikiri na kupanga mikakati ya kujijenga. Mimi huwa nikipita Mikumi nalala pale VETA. Sitegemei tena kulala hapo kwani walichokifanya ni unprofessional. Nadhani CCM wanazidi kupandikiza mbegu ya kuimaliza 2015. Ukiona mtu kama Nape, ameishia kuwa Mropokaji ni hatari! Kasi yake ya kubwabwaja ni kubwa kuliko ya kufikiri!
 
Sitaki kuikubali hii habari kirahisi, Nina shaka na huyo mwandishi wa Mwananchi, hadithi imetiwa chumvi huenda mwandishi anataka kuvuta hisia.
Hivi karibuni waandishi wa gazeti hili walilalamikiwa na Tume ya Katiba kuripoti uzushi baada ya kunyimwa posho kule kanda ya Ziwa, sitashangaa hata hii story kuna kitu waletegemea wakakosa.
 
Safi sana CCM. Endeleeni kumfanyia vibweka vingi zaidi, hii inatupa nafasi wananchi kumpima uvumilivu wake, Hatutaki Viongozi waoga na waliotayari kujisubmit kwa watawala dhalimu sababu ya manyanyaso na mateso.

Angalizo
Wafanye kila kitu ila uhai wake tunawakabithi wao kuulinda usiku na mchana, kwa sababu chochote kitakachomtokea huu mzee, hata kama ni asilimia mbili ya walichomfanyia ulimboka, watajuta kuwa watawala, wao na vizazi vyao.
 
dalili ya mvua ni mawingu na dalili ya ukombozi ni misukosuko kama inayomkuta raisi anayeongoza nchi akiwa nje ya ikulu. Dr nakukubali sana keep it up usikate tamaa kwani ukombozi uko mlangoni unabisha hodi tutaendele kukusupport mpaka kielewe na by the time ukiwa magogoni ndo malengo ya ukombozi yatakuwa yametimia. peoplezzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz powerrrrrr, sauti ya umma ni sauti ya wanyonge
 
Nimeangalia huo umati unaosemwa na Molemo kwenye gazati la Nipashe imenibidi nicheke mkutano wa Dr Slaa anahotubia watoto wadogo...halafu umeme kukatika hakuna uhusiano wowote na mkutano wa Dr Slaa unataka kutuambia Mikumi umeme uwa haukatiki, mbona jana baadhi ya maeneo ya Kawe kulikuwa hakuna umeme napo kulikuwa na mkutano wa Dr Slaa.

Wewe endelea kubisha tu........

Pg.6.JPG
 
Kiongozi wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amefanyiwa hujuma kubwa mkoani Morogoro kwa kufukuzwa chumba cha kulala wageni ndani ya chuo cha ufundi VETA, Mikumi Kilosa.

Kiongozi huyo ambaye alikabidhiwa chumba hicho na viongozi wa CHADEMA kikiwa kimelipiwa kila kitu na akaingia lakini ghafla akaja Meneja wa hoteli hiyo Jacob Sumary na kumtaka Kiongozi huyo wa upinzani nchini kuondoka mara moja kwenye hoteli hiyo kwa sababu tayari ilishalipiwa na mtu mwingine.

Kwa ustaarabu mkubwa na kutokutaka mabishano Dr Slaa aliondoka.

Pia katika hatua nyingine umeme ulizimwa mji mzima wa Mikumi jana kuanzia asubuhi hadi usiku katika kile kilichoonekana ni hujuma ya Tanesco ili Dr Slaa ashindwe kuhutubia,hata hivyo mbali na kukosekana umeme mikutano ya Dr Slaa ilifurika umati mkubwa wa watu huku kiongozi huyo akiwaambia maelfu ya watu atawahutubia hata bila vipaza sauti.

Vitendo hivyo vya kihuni alivyofanyiwa Dr Slaa viliwachukiza wananchi wengi wa Mikumi na kusema watalipa kisasi kwa kuindoa CCM madarakani kupitia sanduku la kura.

Source: Nipashe/Mwananchi


attachment.php


What???? Ngojeni nikachukue panga langu kwanza!
 
CCM is digging it's own grave, and I'm sure it will shoot itself in the head and fall in! Tatizo watanuka sababu wakumfukia hatakuwepo.
 
Ukiona hila zinaongozeka ujue ushindi uko karibu sana. Morogoro ni wazi sasa inakwenda kuwa ngome ya CHADEMA.
 
katika ukombozi wa kweli vitu kama hivi mbona vipo sana kama Dr Slaa alikesha pale NMC huku mvua kubwa ikinyesha itakuwa huko kilosa hata kwenye gari lake alale tu lakini wakae wakijua mwaka 2015 atakuwa magogoni..na huyu sumary ni yupi au anakinyongo na kijana wao kugalagazwa na Nasari.
 
Sitaki kuikubali hii habari kirahisi, Nina shaka na huyo mwandishi wa Mwananchi, hadithi imetiwa chumvi huenda mwandishi anataka kuvuta hisia.
Hivi karibuni waandishi wa gazeti hili walilalamikiwa na Tume ya Katiba kuripoti uzushi baada ya kunyimwa posho kule kanda ya Ziwa, sitashangaa hata hii story kuna kitu waletegemea wakakosa.

Na Nipashe Je?
 
Inatakiwa wawe na standby generator kwa ajili ya mikutano na taa za solar. huyo summary anaweza kuwa ndugu yake Marehemu Mh. Sumari aliyekuwa Mbunge wa arumeru Mashariki bado ana Machungu ya kupoteza kiti kwa upinzani
 
CDM nunueni Generator kubwa.Matukio ya kukatiwa umeme yatazidi kuongezeka ili kujaribu kuwakwamisha.
 
Back
Top Bottom