DR Slaa aeleza sababu ya CHADEMA kususa

Huu ni upuuzi kabisa kwa wabunge wa chadema kutoka nje ya ukumbi

Kwa nini,Sababu wabunge hawa hawa wamekwisha pokea tsh milioni 200 kutoka serikali anayoiongoza Kikwete,kama wangechukua uamuzi wa kutopokea fedha hizo wangeeleweka kwa jamii,Je waliapa namna gani.

Tafadhari wabunge wa Chadema acha kuburutwa na baadhi ya viongozi wenu,tazama maslahi ya Taifa,Hiki chama kilianza vizuri vision yake lakini sasa nimeanza kuona tofauti.

binafsi nimechukizwa na uamuzi huo na maelezo ya dk slaa ktika face book ni mepesi mno yasiweza kuonesha ukweli wa tatizo

kaa ukiwaza ivo ivo! Ukweli utakufuata mpaka kwenu. Si ndo nyie watu wa kampeni za shuka kwa shuka. Subiri tu.
 
Let me congratulate Chadema and their leadership for their move. I wrote previous time of my view of implication of what then happened, JMK didn't listen! Dr. Knew many people were behind him but he didn't take advantage to take over! We could have been showering our beloved blood!

I thank God for such wisdom and patriocy! I loved your move but keep watching careful as sisi em are finding every trap they can to shut you up!

As long as your policy is Tanzania first, you have my support. big up Mbowe and the crew! You have made a history my wabunge! Now the fight have just started; aluta...
 
Namuunga mkono Dr. Slaa

Sidhani kama CCM wanajua madhara ya kuchukua nchi bila ridhaa ya wananchi.

Pia nawakumbusha wanaJF kuwa hakuna haki inayopatikana kirahisi, ile kutoka nche tena mbele ya Mabalozi na wageni wa kimataifa ni kutoa taarifa kuwa serikali yaijashinda kihalali nawao pia watafuatilia na kujua nini shida.

Kumbuka mapambani ndiyo kwanza yameanza... hadi kieleweke.
 
Huu ni upuuzi kabisa kwa wabunge wa chadema kutoka nje ya ukumbi

Kwa nini,Sababu wabunge hawa hawa wamekwisha pokea tsh milioni 200 kutoka serikali anayoiongoza Kikwete,kama wangechukua uamuzi wa kutopokea fedha hizo wangeeleweka kwa jamii,Je waliapa namna gani.

Tafadhari wabunge wa Chadema acha kuburutwa na baadhi ya viongozi wenu,tazama maslahi ya Taifa,Hiki chama kilianza vizuri vision yake lakini sasa nimeanza kuona tofauti.

binafsi nimechukizwa na uamuzi huo na maelezo ya dk slaa ktika face book ni mepesi mno yasiweza kuonesha ukweli wa tatizo

Umechukizwa kwani una upeo waa kufikiri wewe?
Avatar yako ina reflect kiwango cha upambanuzi wako. Wake uP!! sidhani hata kama unaelewa nimekwambia nini. Pathetic creature!
 
Dr. Slaa na CHADEMA ni lazima wamtambue Kikwete. Kama wana manumg'uniko yoyte,hayo manung'uniko yataweza kutanzuliwa kwa urahisi zaidi kama wakimtambua Kikwete. Kikwete amefanya ustaarabu sana. Hakuonyesha hasira wale watu walipotoka nje. Pia akasema labda anaweza kuwapa uwaziri katika Cabinet. Dr. Kikwete ameonyesha subira ambayo ndiyo hallmark ya CCM.
Sasa wanatokea watu wengine katika CCM ambao wanasema wanataka CHADEMA wafukuzwe kutoka kwenye Bunge. Kwa hiyo matatizo ya Uchaguzi badala ya kuisha,sasa ndiyo wanataka yaanze.
Babaji alisema kwamba ukweli ni lile jambo ulilolifikria kwanza kablaya kubadili mawazo yako. The truth is that which you thought first,before you changed your mind. Kwa sababu watu wengi,wakikaa na mtu siku chache tu,wanaanza kusema kwamba wamegundua kwamba huyo mtu ni mnafiki,mzandiki,siyo kama vile walivyofokiri kwanza.
Kama Ndugu Rais amesema kwamba labda atawapa CHADEMA cabinet post,that is the truth,hilo neno lililosemwa kwanza.
Wapo wabunge wengi katika CHADEMA ambao nadhani wanaweza kuchaguliwa kuwa waziri,kama vile Prof. Kulikoyera Kahigi,na wengine .
Kwa hiyo ni bora Ndugu Rais afanye kama alivyosema anaweza kufanya,na Chadema wakubali kutumikia katika Cabinet,kama bado malalamiko ya Uchaguzi,yatatazamwa baadaye.
Haiwezekani CHADEMA waseme kwamba hawamtambui Rais. Kwa sababu,siyo katika Bunge tu,Rais anaongea na wananchi sehemu nyingi sana,na wabunge watatakiwa kuwepo. Wakisusia kila mara Rais anapoongea na wananchi,watakosa sympathy ya wananchi.
Mimi naongea kama mwanachama wa CCM. Kadi yangu ya CCM ni na. AC 23552218 ya Kata ya Msasani,Bonde la Mpunga,na kadi hii haiondoki mfukoni. CCM peke yake ndiyo inayoweza kuwaongoza watu na kuwafanya wawe na moyo thabiti na kuleta maendeleo.
 
NAWApongeza wabunge wa CHADEMA kwa uamuzi waliochukua thats real mambo ambayo tunataka kwa watu kama sie ambao tunataka mabadiliko nasema big up wabunge wetu,Muwe hivyo ili kutoonyesha sisi tuliowapa kura zetu na kuibiwa na Mafisadi.Chadema tuko juuu sana tu,Tuzidi kumuomba Mungu ili 2015 tumpe Dr Slaa nchi hii moja kwa moja.Safi sana wabunge wa Chadema
 
CCM imewataka wabunge wote waliokiri kutomtambua rais kujitoa haraka bungeni vinginevyo wataondolewa na azimio la bunge hadi watakapotambua uwepo wa rais.

Katibu wa kamati kuu ya CCM, John Chiligati alisema kuwa kila mbunge amekula kiapo cha kutii na kulinda katiba na kitendo cha kutomtambua rais ni uvunjaji wa katiba na hivyo wabunge hao wanatakiwa kujiondoa bungeni.

Chiligati alisema kitendo cha Chadema kuruhusu wabunge na madiwani wake kuendelea na kazi wakati hawamtambui rais na serikali ni unafiki wa hali ya juu.

Chiligati aliwataka wananchi kukataa tabia za viongozi wanaokataa matokeo kwa kuwa ni tabia inayoweza kusababisha matatizo na kuchochea vurugu nchini.

Katibu mwenezi wa NCCR-Mageuzi, David Kafulila alisema kitendo hicho hakikuwa cha kiungwana huku akikielezea kuwa ni sanaa ya maigizo.
 
Wadau, JK kwa sasa anakanganywa na mengi, habari kutoka jikoni zinapasha kuwa ukiacha ule mkanganyiko wa Sitta kumgomea uwaziri (ingawa sasa naye inasemekana kashauriwa kama njia ya kumpa nguvu ya kupambana kusaidia kundi la haki kwa mwaka 2015 akubali uteuzi na atake wizara nyeti), imepashwa kuwa Lowassa amekuwa akimshinikiza 'msela' wake apate ama yeye binafsi au watu wake muhimu moja au zote katika wizara hizi nyeti ktk kujijenga kwa 2015.

Mambo ya Nje:Kujijenga kimataifa na kufahamika kwa wanadiplomasia
Mambo ya Ndani:Hii itampa fursa ya kufanya fitna nchi nzima kwa kisingizio cha kuzunguka kuangalia usalama wa raia etc.
Tamisemi:Huku Halmashauri, majiji na mitaa viko chini yake so madc na maRC wato watakuwa upande wao.
Miundombinu:Huku kuna uwekezaji mpana sana so kuna fedha zinazoweza kufanyiwa EPA zikaingizwa kwenye kampeni za kujiandaa, kununua wanamtandao wapya na kuwarejesha wa zamani walioparaganyika. Huu ndio mkakati wa Lowassa et al, wapambanaji kina Mwakyembe, Manyanya, Membe wanafanya nini, au ndio kina Manyanya wamerudi kundini kama CUF (rejea maswali ya Manyanya na Ole Sendeka Bungeni karibuni).
 
Ukiwaendekeza mafisadi ndo madhara yake ayo watakuendesha kama gari bovu kama usipokuwa na msimamo
 
Ni ugonjwa gani huu wa kutaka kutambua matokeo tu bila kujali mchakato wa matokeo hayo? Nadhani tusipoangalia tutaanza kuingia kwenye tatizo jingine ambapo hatujali upigaji kura, hatujali jinsi ya kuhesabu wala hatujali jinsi matokeo yanavyotangazwa. Tunachojali kitakuwa ni "matokeo".. tukipata matokeo "rasmi" tunaanza kuruka ruka kama kulungu!
 
Shida moja MKWERE hana analoweza kuamua yeye mwenyewe, anasaidiwa mpaka kufikiri, sijui huyu bwana uwezo wake shukeni ulikuwaje!!!
 
Watanzania wa sasa sio wale wa miaka ilee iliyopita.
Wawazuie wabunge tuliowachagua hapo ndipo historia mpya itajijenga nchi hii.
 
CCM imewataka wabunge wote waliokiri kutomtambua rais kujitoa haraka bungeni vinginevyo wataondolewa na azimio la bunge hadi watakapotambua uwepo wa rais.

Katibu wa kamati kuu ya CCM, John Chiligati alisema kuwa kila mbunge amekula kiapo cha kutii na kulinda katiba na kitendo cha kutomtambua rais ni uvunjaji wa katiba na hivyo wabunge hao wanatakiwa kujiondoa bungeni.

Chiligati alisema kitendo cha Chadema kuruhusu wabunge na madiwani wake kuendelea na kazi wakati hawamtambui rais na serikali ni unafiki wa hali ya juu.

Chiligati aliwataka wananchi kukataa tabia za viongozi wanaokataa matokeo kwa kuwa ni tabia inayoweza kusababisha matatizo na kuchochea vurugu nchini.

Katibu mwenezi wa NCCR-Mageuzi, David Kafulila alisema kitendo hicho hakikuwa cha kiungwana huku akikielezea kuwa ni sanaa ya maigizo.

Chiligati katika lugha ya kigogo "kiko ndani" hakiko hadharani. Kama hutoki ndani hata kuona mwanga ni tatizo. Tafsiri yetu wengine ni kuwa ccm wamedondosha taulo mbele ya wakwe zao wakitoka kuoga. Wameamini miaka yote wamefanikiwa kuficha mambo yao sasa yamewekwa hadharani kiaina.

Kafulila ndiyo ni mbunge lakini ni wa chama pandikizi. Yeye aendelee kucheza na nyimbo za ccm kama hajavuna mabua.

Ule sio mchezo wa kuigiza kwani umefikisha ujumbe na wananchi na wao sasa wana fursa ya kuchambua pumba na mchele
 
Uzuri wa gemu hii ni kwamba CCM wanajifunga wenyewe.
Kila wanachofanya kinawacost wao.
Walianza kwenye kura za maoni, wakaja kwenye uspika,
wakaja kwenye uteuzi wa wabungewa3, wakaja kwenye hotuba,
na sasa wanakuja kwenye uteuzi wa baraza la mawaziri.
 
Back
Top Bottom