Elections 2010 DR. SLAA advised to reassure "ajira" to capable civil servants (kiswahili version).

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Watendaji wengi ambao kwa nyadhifa zao huteuliwa na rahisi sasa hivi ni tumbo moto wakihofia ujio wa utawala mpya wa Dr. Slaa.

Utafiti wangu umebaini ya kuwa wengi wao wanayafurahia mabadiliko hayo hususani watumishi wa ngazi za kati ambao wanawaona wakubwa zao wengi wao hawana sifa na ni mzigo kwa taifa.

Lakini hao wakubwa ndiyo wameshika mpini na wanaweza kutumia nafasi zao kwa hali na mali katika kulinda ulaji wao hapo serikalini katika kuchakachua matokeo ya kura.

Mwaka 1995, Augustine Mrema kosa alilolifanya ni kuwatishia wakubwa serikalini ajira zao badala ya kuwatoa wasiwasi ya kuwa watendaji wazuri serikali mpya ijayo itawajali na kuheshimu mikataba yao.

Kutokana na vitisho na jazba za Mrema, vibosile hawa walitumia nafasi zao kuchakachua matokeo na historia iliyofuata sote tunaifahamu.

Ushauri kwa Dr. Slaa, kwenye mikutano yake awaondolee wasiwasi haswa watendaji wazuri serikalini ili nao wapate uhakika wa ajira zao na hivyo kumsaidia kwa hali na mali.

Serikalini watendaji wengi wazuri wana manung'uniko sugu juu ya utawala dhalimu wa JK kwa sababu ajira na kupanda vyeo hakuzingatii sifa ila kufahamiana na wanachohitaji na kutarajia kwa Dr. Slaa ni kuhakikishiwa tu kuwa sera za ajira serikalini na kwenye taasisi zote za umma zitaheshimu kanuni za utumishi na wala siyo vinginevyoooooooooooo
 
Heshima kwako Mzee hilo ni muhimu sana,kunaumuhimu wa kuwahakikishia makundi yote ya kijamii kwamba pale wanapopatia mkate wao wa kila siku patatengenezewa mazingira bora zaidi ya ustawi ili kila mmoja wetu apate keki ya taifa
NCHI KWANZA VYAMA BAADAYE
 
Dr Slaa hakusema popote atawafukuza kazi watendaji wakuu wote, vita yake ni kwa mafisadi wa nchi hii.
 
Ila watendaji wale ambao wametumia nyadhifa zao kukandamiza upinzani lazime wafukuzwe kazi. Kwa mfano, watendaji ambao wamesimamia vizuri mikutano ya kampeni za CCM na kukosa kuitendea haki ile ya upinzani lazima waajibishwe.

Unataka kusema RPC anayeamuru wafuasi wa CHADEMA wapigwe mabomu ya machozi bila sababu ataendelea na kazi yake? No way! Au yule aliyemhamisha Mkurugenzi wa Arusha kwa uonevu wa kisiasa, au mtu kama Mhariri wa Daily News waendelee kudunda? No way!
 
NO way!
 
Back
Top Bottom