Dr Slaa aacha historia kata ya Lwenzera-Geita

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,503
1,722
Tarehe 16 & 17 october 2012 zitakuwa ni za kukumbukwa katika historia ya siasa za vyama vingi katani hapa.

Katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo amefanya mikutano mikubwa kila kijiji katani hapa kwa siku mbili mfululizo bila kuchoka akimnadi mgombea udiwani wa chama chake ndugu Musa Ibugha na akitoa elimu ya uraia.

Hali hiyo ilipelekea kusimama kwa shughuli za kawaida na watu wengi kuhudhuria mikutano yake huku wakishangazwa na jinsi anavyomudu kuka jukwaani muda mrefu licha ya umri wake kuonekana mkubwa.Jumla ya watu 280 walirudisha kadi za ccm huku 678 wakijiunga na cdm rasmi

Hali hiyo imemfanya mwenyekiti mpya wa ccm- Geita bwana Msukuma kutia timu leo katani hapa ili ajaribu kukisaidia chama chake...ujio wake umewafanya ccm kuzindua kampeni rasmi leo.

Je nani zaidi SLAA AU MSUKUMA? Fuatilia mtanange huu mtamu hapa JF
 
ccm ccm ninavyokupenda nitakunywa sumu juu yako! ccm ninakupenda kama ugali na mchica, sintakuacha nitakuwa na wewe kama gari na betri
 
Dr Slaa, Mungu akubariki sana mzee...Kazi uliyofanya tayari ni kubwa, kwasasa unafanya ziada!
 
makamanda wa sikonge-Tabora walilalamika kuwa bado hawajapata sapoti toka makao makuu...kaeni mkao wa kula..babu yuko njiani...jana alikuwa kata ya mwawaza-shinyanga...leo atakuwa kata ya bugarama-kahama...then straight tabora
 
karibu sikonge Dr.uje tusafishe kila uchafu wa akina Nkumba n.k,sikonge wanakumbuka moto uliouwasha tokea mwaka jana.
 
Back
Top Bottom