Dr. Shein amesusia vikao vya cabinet, je wabunge wa Znz nao watasusia bunge la muungano?

Jamani hapa tunataka kujadili nini sasa hii habari ianaelea hewani!

Tunajadili kuwa kasusia, kwa ushahidi hupi wa habari ya kususia? au tunajadili hakuwepo kwanini? au tunataka kujadili speculations! hii habari haijakamilika mleta habari lete source ya kususia
 
Tokea Rais wa Zenj avuliwe umakamo wa rais SMT, imekuwa ni kama tabia kwa maprez hao wa Zenj kutohudhuria vikao vya kabineti... Mleta mada kaenda mbali zaidi kwa kudadisi iwapo rais wa zenj anasusa kwenye shughuli za maamuzi ya SMT, kwa nini na wabunge toka visiwani wasifanye hivyo!

Unaweza kuanzia hapo, pasipo kuwa na haja ya kujua chanzo cha habari hii!
 
Mkuu.
mimi naona kuwa kama kweli ameamua kususia vikao kwa sababu yoyote ile basi yeye ni mtu ambaye anafikiri na kutafakari.

Rais wa Tanganyika, muwakilishi wa watu wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar, muwakilishi wa watu wa Zanzibar waliunganisha mambo 11 yaliyoitwa mambo ya Muungano. Wote wawili wakawa na nafasi za kimaamuzi katika serikali ya Muungano.
Leo inapotokea muwakilishi wa upande mmoja awe hana sauti katika maamuzi ya serikali ya Muungano ndio kuna Muungano hapo?

kama kweli ameamua kufanya hivyo, mimi nachukulia ameamua kuwa yule mtoto aliyemwambia mfalme unatembea uchi, mfalme hana nguo.

kama ubabe hautatumika kumnyamazisha basi mjadala wa muungano unachukua sura nzuri.

Mimi naona kosa kubwa lilifanyika pale marekebisho ya katiba ya muungano yalipomvua madaraka rais wa zanzibar asiwe tena ndiye muwakilishi mkuu wa watu wa Zanzibar katika Muungano.Hili lilikuwa ni kosa kubwa kuliko lile walilolifanya wazenj kubadilisha katiba yao hivi karibuni. kwa maoni yangu mabadiliko waliyofanya Zanzibar ni response kwa mabadiliko yale ya Katiba ya Muungano.

Mabadiliko ya katiba ya Muungano yameleta sura kuwa serikali ya Muungano ni kama Central Gvt na Serikali ya Zanzibar ni kama local gvt kitu ambacho kwa uelewa wangu sivyo mkataba wa muungano ulikusudia. Kwa maneno mengine Bunge la muungano na serikali ya Muungano ilijinyakulia madaraka na mamlaka ambayo hawana. Ukipenda ,ita "ubabe".
 
Nonda said:
Mkuu.
Mimi naona amefanya jambo la maana kama ni kweli amefanya hivyo.Kama amesusia kuja kwenye vikao kama waziri asiye na wizara maalum. Hiki ndio cheo alichopewa rais wa Zanzibar kwa sasa katika Muungano au vipi?

Pia sioni mantiki ya wabunge wa bunge la Muungano kutoka Zanzibar kususia au kupanda boti na kurudi Zanzibar.

Nafikiri ni vizuri wawepo katika bunge la Muungano ili ikija hoja ya muungano au yale yanayowagusa wao kama Wazanzibari wayasemee au wayatetee.

Nilifikiri wewe JokaKuu utamuunga mkono Dr. Shein katika hili kwa sababu anasaidia katika kuleta mjadala wa wazi wa Muungano au hatutaki mjadala wa muungano? Au hatutaki Tanganyika?

Umeileta mada yako leo kwa ushabiki zaidi kulikoni kuangalia uzuri na athari ya anachofanya Dr. Shein.

Mkuu, Headquarters za AU ziko Addis, za EAC zipo Arusha,Leo headquarters za Muungano wa TZ zipo Dar na Dodoma. Na bado Muungano haujavunjwa rasmi ingawaje unaonekana haupo tena.

Hata wazanzibari wote wasusie hivyo vikao vya bunge na watangaze hawautaki tena muungano kwa Tamko la upande mmoja, Kikwete ataamuru JWTZ waishikilie Zanzibar.

Nionavyo ni vyema tuwatie moyo Wazanzibari wakaze kamba ili mjadala wa muungano na katiba mpya uwe wa uwazi ili utengano au ushirikiano uwe wa tija na wa maana kwa pande zote. Sasa hivi kila kitu kimegubikwa na usiri na ubabe na ujanja ujanja. Jambo ambalo linaleta manung'uniko kutoka "bara"(Tanganyika) na pia Zanzibar.

Nonda,

..serikali 3 zitaongeza mzigo wa gharama kwa walipa kodi wa Tanganyika.

..pia sidhani kama serikali 3 zitawapa wa-Zanzibar mamlaka wanayoyalilia kwa sasa.

..ktk mfumo wa shirikisho wenye serikali 3, bado serikali ya muungano itakuwa na mamlaka juu ya masuala ya fedha, ulinzi,mambo ya nje,ushuru na forodha, etc etc. kwa kifupi yale makubaliano yote ya mwanzo ya muungano yatakuwa chini ya serikali ya muungano.

..serikali itakayokuwepo Zanzibar haitakuwa na tofauti na serikali iliyopo Zanzibar sasa hivi.

..mabadiliko ya katiba ya 1994/95 wakati tunaelekea kwenye uchaguzi wa vyama vingi ndiyo yaliyomuondoa Raisi wa Zanzibar ktk umakamu wa Raisi. mabadiliko hayo pia yaliofuta uwezekano wa kuwepo na Waziri Mkuu ambaye pia ni makamu wa kwanza wa raisi.

..mabadiliko ya katiba ya 1994/95 yalipigiwa kura na wabunge wa Zanzibar waliokuwepo ktk bunge la muungano. je mmeshapata kujiuliza kwanini Wazanzibar walipiga kura ambayo leo inaonekana "kumdhalilisha" Raisi wa Zanzibar?

..binafsi sielewi kwanini wa-Zanzibar hawamheshimu Makamu wa Raisi wa sasa aliyepigiwa kura na wananchi wote. sheria zetu za uchaguzi zinaelekeza kwamba unapigia kura "ticket ya Raisi na Makamu wake." Je, Raisi wa Muungano akitokea Zanzibar na makamu wake akitokea Tanganyika, wa-Zenj watakuwa na malalamiko haya?

..kuna uwezekano kwamba Raisi wa Muungano na yule wa Zanzibar wakatoka vyama viwili tofauti. makamu wa raisi ndiye msaidizi mkuu wa raisi ktk shughuli za utawala, pia hukaimu nafasi ya Raisi, na mwisho ikiwa Raisi atashindwa kutawala huchukua nafasi hiyo. mazingira hayo ndiyo yaliyolielekeza BUNGE[lenye wawakilishi toka Zanzibar] kumuondoa raisi wa Zanzibar ktk nafasi ya makamu wa raisi.

..mwisho, makamu wa raisi ni jina tu la cheo, kitu cha msingi ni kuangalia madaraka na majukumu aliyonayo mhusika. raisi wa Zanzibar anaweza kuitwa makamu wa raisi hilo halina shida, tatizo lipo ktk kubainisha majukumu na mipaka ya madaraka aliyonayo.

NB:

..namuunga mkono Dr.Shein kwa kususia nafasi yake ktk serikali ya muungano. zaidi nawatia shime wabunge wa Zanzibar nao wasusie shughuli za bunge la muungano, ili Tanganyika na Zanzibar zizaliwe upya.

..naunga mkono Tanganyika mpya, na Zanzibar mpya, kuwa nchi marafiki, na wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (ya mwaka 1977 iliyojumuisha marekebisho hadi mwaka 2005) Ibara ya 54(1) wajumbe wa baraza la mawaziri ni makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa zanzibar na Mawaziri wote chini ya uongozi wa Rais kama atakuwepo.
Sijaona sehemu katika Katiba inayomtaka Rais wa Zanzibar kula kiapo cha Kuwa waziri asiye na wizara maalum hoja ya uwaziri usiokuwa na wizara maalum inatoka wapi?
 
Ebu sijawaelewa hapa, yaani rais wa nchi halafu aje kuwa waziri hapa bara, hata mimi nisingekubali, labda waje kumwapisha yule maalim seif maana ndio mpenda vyeo bandia na posho. awe anakuja maalim kumuwakilisha maana kule Zanzibar hana kazi mpaka apangiwe na Dr Shein, kwa sababu hata Rais wa Zanzibar akisafiri anaekaimu nchi ni makamu wa pili wa Rais.
 
ASK said:
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (ya mwaka 1977 iliyojumuisha marekebisho hadi mwaka 2005) Ibara ya 54(1) wajumbe wa baraza la mawaziri ni makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa zanzibar na Mawaziri wote chini ya uongozi wa Rais kama atakuwepo.
Sijaona sehemu katika Katiba inayomtaka Rais wa Zanzibar kula kiapo cha Kuwa waziri asiye na wizara maalum hoja ya uwaziri usiokuwa na wizara maalum inatoka wapi?

ASK,

..Raisi wa SMZ lazima ale kiapo kuwa waziri wa muungano.

..wote wanaoingia kwenye cabinet ama wameapishwa na Raisi, au Jaji Mkuu.

..Ofisi za Raisi na Makamu wa Raisi ni wizara, ndiyo maana wakati mwingine unasikia kuna mawaziri wa nchi ktk ofisi hizo.

..The president of Zanzibar does not have any portfolio in the union goverment. In swahili a minister who has no portfolio[minster without portfolio] is called "waziri asiyekuwa na wizara maalum."
 
Uwezo Tunao,

..Shein anapaswa kula kiapo kabla ya kuhudhuria vikao vya cabinet. je, umeona akifanya hivyo?

..anatakiwa aje Ikulu DSM na aapishwe na Jaji Mkuu kuwa waziri asiye na wizara maalum wa serikali ya muungano.
Duu! Hii umeipata wapi mkuu?

Katiba inasema hivi: Ibara ya 54(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri wote.

Maana yake ukishaapa kiapo cha moja wapo ya vyeo hivyo tayari ushakuwa mjumbe. Sijawahi kusikia "kiapo cha mjumbe wa Baraza la Mawaziri kinachofanywa na Jaji Mkuu." Pinda ambae anahudhuria Baraza la Mawaziri aliapishwa na Jaji Mkuu?

Mengine yote ya kuwatakia Wanzanzibar waende na salama tuko pamoja.
 
Taso said:

Taso,

..Waziri mkuu na mawaziri wa serikali ya muungano huapishwa na Raisi wa muungano.

..kulikuwa na utaratibu wa Raisi wa Zanzibar kuapishwa na Raisi wa muungano. Utaratibu huo ulibadilishwa baada ya kutokea malalamiko toka Zanzibar, na badala yake Raisi wa Zanzibar akawa akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania.

..I am not making these things up. kusisitiza tu Raisi Amani Abeid Karume aliapishwa na Jaji Mkuu Barnabas Samatta kuwa mjumbe wa baraza la mawaziri. unaweza ukafanya utafiti wako kuhakiki haya niliyoyaeleza.
 
Joka Kuu, Ok, kwa hiyo Rais wa Zanzibar anaapishwa na nani?

Kama na Jaji Mkuu, basi alishaapishwa. Sasa utasemaje bado hajaja Ikulu kuapishwa na Jaji Mkuu? Aapishwe mara ngapi?
 
Zanzibar wanachotaka hakitawezekana labda wajitenge tu.

1. Bara hawatakubali kabisa kuwa na uamuzi sawa na zanzibar wakati zanzibar ni 3.75% ya wananchi wa Tanzania. Zanzibar walichopewa kinatosha na wabunge wao waondoke bara warudi zanzibar.
2. Tuweke mkataba wa ulinzi wapige kura kama wanataka muungano au la. Hakuna haja ya kubadilisha katiba kwani haita wanufaisha wananchi wengi.
3. Kila mtu atakuwa happy lakini kusiwe na wabunge wa zanzibar bara, mawaziri wala mabalozi.
 
Tokea Rais wa Zenj avuliwe umakamo wa rais SMT, imekuwa ni kama tabia kwa maprez hao wa Zenj kutohudhuria vikao vya kabineti... Mleta mada kaenda mbali zaidi kwa kudadisi iwapo rais wa zenj anasusa kwenye shughuli za maamuzi ya SMT, kwa nini na wabunge toka visiwani wasifanye hivyo!

Unaweza kuanzia hapo, pasipo kuwa na haja ya kujua chanzo cha habari hii!

Umenichekesha sana Mkuu, yaani una ni-convince nijadili speculations! mleta mada kasema Dr. Shein Kasusia vikao, siyo kwamba ana dasisi, hii tungo yake ni kauri taarifa, Mkuu.

Ninachoweza kusema kuwa ana dadisi ni kwanini, Wabunge wa Zanzibar na M/Rais wao hawamuungi mkono Rais wao kwa kususia shughuli za muungano.

Mkuu mi bado nahitaji tupate source ya habari kuwa Shein ana susia shughuli za Muungano! labda mto maada mwenyewe atwambie kuwa pamoja na tungo kuonekana kama taarifa, lakini sivyo.
 
Muungano wetu huu ipo siku utakuwa Mtengano. CCM hawataki ujadiliwe kwa nini jamani? Japo sijafanya utafiti lakini naamini Watanzania wanataka ujadiliwe na kufanyiwa marekebisho kwa maslahi na ustawi wa pande zote za muungano. Haya mambo ya kuficha hata hilo lihati au limkataba la muungano yataupeleka muungano kaburini ungali hai japo mahututi.

2015 tuwape kura CDM kwa maana manifesto ya CCM kuhusu Muungano ipo wazi na haifurahishi wateja wa Muungano. CCM hawataki Muungano ujadiliwe kwa kua wanaamini huna ubabe wa kuwaadhibu na kuwapa kura CDM ifikapo 2015. CDM wana jibu zuri sana kuhusu Muungano - MAJIMBO. Zanzibar litakua jimbo linajitegemea, lenye nguvu na maendeleo makubwa chini ya CDM kwa kua WAZANZIBARI watakua na haki zote za kuendeleza jimbo lao kwa nguvu zao zote. Majimbo mengine kama Morogoro nk pia watafanya juhudi kujiendeleza.

Kama TZ tuna amani na utulivu, haitatokea CCM na mkewe CUF wakabadirika kua jiwe ktk swala la Muungano. Muungano ni nguvu.
 
Taso said:
Joka Kuu, Ok, kwa hiyo Rais wa Zanzibar anaapishwa na nani?

Kama na Jaji Mkuu, basi alishaapishwa. Sasa utasemaje bado hajaja Ikulu kuapishwa na Jaji Mkuu? Aapishwe mara ngapi?

Taso,

..Raisi wa Zanzibar ana viapo viwili tofauti. Kiapo cha kwanza mbele Jaji Mkuu wa Zanzibar kwa nafasi ya Uraisi wa Zanzibar, halafu kiapo cha pili mbele ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kuwa mjumbe wa baraza la mawaziri wa muungano.

..kwanini viapo viwili, naamini kwasababu kuna katiba ya ZANZIBAR na KATIBA YA MUUNGANO.

..sina taarifa kama Dr.Shein ameshaapishwa na Jaji Mkuu Ramadhani ambaye amestaafu, au huyu mpya Jaji Mkuu Mohamed Chande. pia kuna taarifa kwamba Dr.Shein hajahudhuria vikao vya baraza la mawaziri tangu uchaguzi wa October mwaka jana.

..huku kususa kwa Raisi wa Zanzibar kushiriki shughuli/vikao vya muungano nadhani ni muelekeo mzuri ktk kuipatia Zanzibar kile ambacho inakitaka, yaani mamlaka[jeshi,mabalozi,sarafu,...] yote yanayoendana na dola huru. pia napendekeza WABUNGE wa Zanzibar wamuunge mkono Raisi wao kwa kususia vikao vya bunge la Jamhuri.
 
..Raisi wa Znz, Dr.Shein, amesusa kuhudhuria vikao vya baraza la mawaziri wa serikali ya muungano.

..je, huyu anatunisha misuli kwamba Zanzibar hawataki muungano?

..je, wabunge wa Zanzibar kwenye bunge la muungano nao watamuunga mkono Raisi wao?

..au, kwanini wabunge wa Zanzibar hawajafuata msimamo wa Raisi wa Zanzibar kususia masuala ya muungano?

..hivi Makamu wa Raisi, Dr.Bilali, mawaziri toka Zanzibar, na wabunge wao, wakipanda speed boat na kurudi Zanzibar wakisusia shughuli za muungano, what will happen?

Jokakuu
Kwanza huyo Dr Bilali sio wakumuliza suali hilo, yeye kwa sheria ya Zanzibar 1984 na wzanzibar wenyewe hatumtambuwi cheo chake Zanzibar kipo kwa Maana gani?a.) b.) Jiulize wewe mwenyewe Jokokuu ikiwa Wzanzibar watasema ktk uchaguzi wa 2015 hawato piga kura ya Raisi wa Muungano wala Wabunge wa Muungano what will happen Muungano?.
Kwa sababu Dr Bilali sio kiungo cha Muungano kiungo cha Muungano kilichobakia ni Wzanzibar kushiriki kupiga kura za Raisi wa Muungano na wabunge ikiwa tutagoma basi ndio kufa kwa Muungano.
 
Back
Top Bottom