Elections 2010 Dr. Shein aibuka kidedea; kuiwakilisha CCM urais Zanzibar 2010

UWONGO!

Ni mpaka saa 11 jioni ya leo (mida ya Tanzania) ambapo CCM watampigia kura mmoja wa watatu ambaye ndiye atakuwa mwakilishi wa CCM kwenye uchaguzi wa urais wa Zanzibar 2010
Mkuu ni saa 11 au saa 10? maana kuna mtu yuko mlangoni anasema wanaingia ukumbini saa kumi
 
Uwiiiiiiiiii reo ni reo asikuwa na mutoto aereke jiwe mra. Bahati mbaya wazee wenye hekima CCM wameshaisha (eg Nyerere, Kawawa) na kwa sasa wamebaki wavulana tupu. Ngumi zinaweza kupigwa huko reo maana hakuna anayeogopwa kwa sasa. Bhamulawasu!!!!!!!! Jinsiku kabhajo jabhajile imbwa itamenya kwaika!!!
 
Kila la kheri CCM kwa yeyote mtakayempitisha maana sauti ya wengi ni sauti ya Mungu na isitoshe hakuna mtu anaweza kuwa kiongozi asipopewa haya mamlaka toka kwa Mungu.
 
Wakuu, kutokana na muafaka mgombea urais atakayeshindwa anakuwa waziri kiongozi.

Kama Shein atashindwa na seif, Shein anakuwa Waziri kiongozi. kwa Protokali, Waziri Kiongozi ni mdogo sana kwa makamu wa Rais. Hapo naona Shen kuchanaganyikiwa na hasa ukitilia maanani bosi wake sasa ni Seif. Sidhani kama Shein alilifikiria hili.

Mkuu naomba uelewe kuwa CCM ndo chama tawala na kulingana na taratibu zao zisizo rasmi hawawezi kukubali zanzibar itawaliwe na CUF. Kuna majambo yatafanywa ili CCM ichukue nchi. Futa kabisa mawazo ya Shein kuwa waziri kiongozi. Ameshahakikishiwa kuwa yeye ndo atakuwa raisi wa zanzibar vinginevyo asingekubali kuachia umakamu wa rais akaaishie kuwa waziri kiongozi.
 
Mie nadhani hapo Bilal ataambiwa awe mgombea mwenza JK na hivyo atapunguza msuguano Zenji. Wakati Shein ataukwaa urais wa Zenji. Wakishashinda then Bilal watakuja kumuweka pembeni mbeleni.
 
Mie nadhani hapo Bilal ataambiwa awe mgombea mwenza JK na hivyo atapunguza msuguano Zenji. Wakati Shein ataukwaa urais wa Zenji. Wakishashinda then Bilal watakuja kumuweka pembeni mbeleni.
Mgombea mwenza wa JK sio Salim Ahmed Salim?
 
Mgombea mwenza wa JK sio Salim Ahmed Salim?
Haitatokea! Kwa chama chenyewe CCM. Yeye si katika wao. Km hatampata katika hao walioomba kugombea Urais Zenji atafanya km Mkapa kwenda kumtafuta mtu asiyefahamika katika siasa ili iwe rahisi kumcontrol.
 
1. Shein akiwa rais muungano utimarika zaidi.
2.Yeyote atakaechaguliwa ana uwezekano mkubwa wa kushinda kwenye uchaguzi mkuu.
3.Wa unguja ni wengi kuliko wapemba,iwapo ccm ikimteua SHEIN lazima ielewe kuwa imejiongezea kazi kwenye uchaguzi mkuu ujao ili ishinde
ukichukulia maanani kuwa matokeo hutofautiana kwa kiasi kidogo sana.
4.Hivyo ccm wasingependa kupoteza hata kura moja.....SASA?wakimteua shein watakuwa wanajiamini nini hasa? au ni fidia ya wana cuf walioko pemba watakaompigia shein kwa vile ni mpemba mwenzao???????????
KAAAAAAAZI KWELIKWELI.
 
Wakuu, kutokana na muafaka mgombea urais atakayeshindwa anakuwa waziri kiongozi.

Kama Shein atashindwa na seif, Shein anakuwa Waziri kiongozi. kwa Protokali, Waziri Kiongozi ni mdogo sana kwa makamu wa Rais. Hapo naona Shen kuchanaganyikiwa na hasa ukitilia maanani bosi wake sasa ni Seif. Sidhani kama Shein alilifikiria hili.
Mzee The Good wakati unaogelea kujiokoa kwenye jahazi linalozama unachoangalia kwa wakati huo ni kama utafika salama ufukweni huangalii kama utatoka ufukweni na kikoi ua bila kikoi utakapofika ufukweni ndipo utajitambua kuwa uko uchi, kwa hiyo kazi moja ya Shein kwanza ni kuhakikisha anapita mchujo mambo ya protokali baadae.
 
majina matatu tu ndo yaliyopitishwa na mkutano wa kumpitisha huyo mgombea mmoja ni kesho, hizo ndo habari rasmi, chukuwa hiyo toka jikoni
 
aisee....... yetu maskio yaani huyu mzee chali tena kwa mara ya pili? duh shughuli pevu huko.

Kumbukumbu zangu zinanionyesha ni mara ya tatu 2000....2005.... na ikitokea leo 2010 itakuwa mara ya tatu, labda ajaribu tena 2015 hivi Bilal ana umri gani vile.
 
breaking news!
Dr mohamed gharib bilal nje,dr ali mohamed shein mgombea znz.
1.kama ndio hivyo,kilichomwangusha mzee bilali nadhani uvumi kuwa anakimbilia urais.....tofauti na maneno ya nyerere kuwa ikulu si mahali pa kupakimbilia....inatakiwa unyatie kidizaini....kama vile hutaki vileeeeee!!!!!!?
2.pili ni wale wapambe wake ambao nasikia tetesi walikuwa wanasema...''iwe mchana...iwe usiku,.....bilali atakuwa rais

nina wasiwasi na mambo hayo mawili, kama ni sahihi basi yawezekana ndio yamemwangusha.
 
Majina yaliyopitishwa na Kamati yao kuu kwenda kupigiwa kura kwenye NEC ni matatu nayo ni Dr Shein, Dr Bilali na Nahodha. Hilo ndilo lililopo sasa hivi.
 
majina matatu tu ndo yaliyopitishwa na mkutano wa kumpitisha huyo mgombea mmoja ni kesho, hizo ndo habari rasmi, chukuwa hiyo toka jikoni
Mkutano mkuu hauchagui mgombea unapitisha jina lililoletwa toka NEC kwa kura ya ndiyo au hapana, majina matatu yameshapitishwa na kamati kuu CC kinachoendelea sasa ni kikao cha NEC kinachochagua jina moja kati ya matatu yaliyopitishwa na CC kulipeleka kwenye mkutano mkuu kesho.
 
Back
Top Bottom