Elections 2010 Dr. Shein aibuka kidedea; kuiwakilisha CCM urais Zanzibar 2010

Wakuu tujuzeni yanayojiri huko Idodomya.
Moshi mweupe unaelekea kumfunika nani?
 
Sina haja hata ya kujua. Atakaye kuja huyo huyo tutakutana kilingeni. Najua Seif kajiweka tayari kumkabiri bila kujali sura wala wasifu wake.
 
Mkuu Halisi:

Macho yetu leo hayabanduki hapa:

Dr. Shein v/s Dr. Bilal : ni kama fainali ya Woza
 
dOKTA Shein ananikwaza maana nasikia hakuwa na nia ya kugombea, kashawishiwa na Kikwete na pia nimesikia nyuma yake yupo Rais WA Znz, sasa kama yeye bi chaguo la viongozi walioshindwa na yeye automatically amefail kabla hajaanza , maana anaomba mamlaka amabayo nafsi yake haina haja nayo, atatuangusha.
Bilal na wagombea wengine hatujaambiwa kama ni vipenzi vya makundi ya Watawala, ni heri ajitawalaye kifikra maana huyo anajua kwanini anataka madaraka makubwa visiwani.
 
Hivi Zenji wanawake hawaruhusiwi kugombea urais? maana utaona wanasukumana kwenye ubunge wao wanaita uwakilishi. Hata uwaziri kiongozi tu hawawezi pewa?
Wanadanganywa tu kila siku kuwa wao pia wapewe upendeleo. Tumia akili za mbayuwayu.
 


Teh Teh Teh Teh Mkuu inabidi wategemea kweli kuna kula kweli leo maana twangojea kwa hamu sana kujua ni Kiongozi yupi atatukwamua huko Zenji.

Kweli twahitaji kiongozi shupavu mwenye busara hekima na msikivu kwa wanchi wa Zenji na Bara pia twahitaji mabadiliko na maendeleo sasa nadhani katika vuguvugu hili CCM wanapaswa kujipanga vyema kuboresha Chama nadhani mambo yako wazi nyakati hizi, watu wasikimbilie Uongozi bora uongozi twahitaji viongozi wawajibikaji

Tupeni Detailz pindi mpatapo kutoka DOM.

Eeeeh kwli nimesikia Ati Mr.Sitta Ameiuliza serikali ya CCM kama inadhamira ya kuhamia DOM na anashangazwa kuwa serikali yaendelea jenga nyumba za Mawaziri Dar?

Kwanini Hili laendelea CCM wanashindwa timiza sera hiyo toka 1980's kweli ?????? hiii napenda iende kwa vijana kama wakina January Makamba wanao sema wanakuja na chachu na kutaka kurekebisha MUSTAKABALI WA NCHI HII


In red....kwa kutumia kichwa cha Yusuph? no way.....huyo Sitta alishakuwa waziri wa CDA miaka hiyo ya 1980s.....alifanya nini?
 
mbona Bilali anafanala na Balali? Tuwe makini

Congruence Theory applies here?

Bilal ≅ Balali

Umenikumbusha hii Hesabu:
Side-Angle-Side (SAS)
Angle-Side-Angle (ASA)
Angle-Angle-Side (AAS)
 
UPDATES (Kutoka Dodoma):

Mpaka sasa tatu bora ni Shein, Bilal na Nahodha...

Poa mkuu.

Yaani sielewi kwa nini watu wanatumia muda wao kusubiri majibu yaliyo wazi kabisa. Naamini bila shaka kuwa mgombea wa ZNZ ni Dr Shein.

Ngoja wadau wasubiri confirmation.
 
Kama kawaida Tz bara tutaendelea kuwachagulia wazenj rais wao indirectly yaani watake wasitake....
 
Mbona News hai-Break?

There are currently 106 users browsing this thread. (28 members and 78 guests)

Obuntu,Limbani,MJM,abdu,Elli,Shalom,Junius,Jafar,Middle,blackpepper,Mkaguzi,Edo,Roya Roy,Dark City,Kyachakiche,Belo,Kinyambiss,lyangalo,Kilinzibar,chapa,Maisha,Mburahati,Kudi Shauri,Nyunyu,Akili Unazo!,Chiluba,kichenchele,Chimunguru,
 
Kama kawaida Tz bara tutaendelea kuwachagulia wazenj rais wao indirectly yaani watake wasitake....

Hii ni directly maana wakimaliza hapo atakayepita wataanza kumfanyia mpango wa kuiba kura kwenye uchaguzi na ndiyo CCm wanaita demokrasia. Kweli CCM yajenga nchi
 
Back
Top Bottom