hahaha dah umeuaUmejadili halafu umesema hutajadili,nimekupa mfano wa NOTTINGHAM,LEICESTER NA WARWICK kama mfano najua vizuri sana kwani siwezi kuifananisha OXFORD au Cambridge huko sio kwetu mimi na wewe ndio nikakupa Nottingham wajipime na chuo chako-Southbank.
kukusaidia kama najua nikupe ranking za mwaka huu 2009.
1.Oxford 2.Cambridge 3.Imperial College.4.London school of Economics-LSE. 5.ST.Andrews. 6.Warwick 7.University College London-UCL.
8.Durham University. 9.York 10.Bristol 11-King's College London. 12-loughborough 13-Exeter University. 14-Leicester University.
15-Bath University 16-Nottingham.
ninajua chuo kama OXford wazuri zaidi kwenye utawala,siasa etc wakati Cambridge kwenye sayansi.
Kings college London kwenye sheria na medicine, LSE ni wakali kwenye uchumi na siasa. Warwick wazuri sana kwenye sheria,UCL kwenye sheria n.k
Naomba usiwadanganywe watanzania Southbank sio chuo bomba au unapata kamisheni kwa kuwapeleka hapo chuoni?
kukusaidia University ranking league table 2009 timesonline.co.uk wameonesha kuwa chuo cha London Southbank ndio cha mwisho kwa kushika nafasi ya mwisho ya 113.
watanzania vyema tuwe tunafanya tafiti kwenye kuchagua vyuo wenzetu wazungu wana guide maalum kwenye chaguzi za vyuo-THE ESSENTIAL GUIDE TO PICKING THE RIGHT PLACE kwenye vyuo vikuu.timesonline wana huduma hiyo.jaribuni kupitia website ya chuo kimoja hadi kingine hata kama gazeti lingine litakuwa na mtazamo tofauti hauwi mbali wanaweza kusema LSE ni ya nne na Imperial ni ya tano. lakini hawawezi kuweka Southbank nafasi hata ya 90 lazima kiwe mkiani kabisa.
ukitizama michuzi blog kuna chuo anakitangaza London school of Commerce kuwa wanatoa digri kwa miaka miwili au MBA kwa pound elfu 3900 na wana intake sita kwa mwaka kitu kama hicho waTanzania inabidi tufanyie utafiti wa kutosha kabla ya kujisajili, kwangu mimi hakijanikalia vizuri chuo cha intake sita kwa mwaka na digri kwa miaka miwili.kama MBA ni £3900 bora mtu usome IFM wana masters kozi zina link na chuo cha UK kwa fikra zangu.