"Dr" Shayo kuwania ubunge wa Afrika Mashariki!

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,211
113,520
009.JPG

dr.hildebrand shayo (kulia) akirejesha fomu zake kuwania ubunge wa afrika mashariki kwa ofisa wa ccm katika ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho jijini dar es salaam. Dr. Shayo ni mhadhiri wa uchumi na amerejea nchini baada ya kuishi uingereza kwa miongo kadhaa akifundisha. Katikati ni mh makongoro nyerere ambaye naye amejitosa kwenye kibeneke hilo lenye ushindani mkubwa. source

smh.
 
hiyo ''Dr'' umeifungia kwenye hizo alama basi hata inanipa wasiwasi...

Nadhani simfahamu kivile kwa kweli. Ila ulivotikisa kichwa sasa ndo najiuliza kunani tena na Daktari mgombea ubunge?

Aah mie siasa na wanasiasa wake wamenichosha kwa kweli!
 
btw: naona wabeba boksi wanashuka kuja kujitutumua kwenye kugombea ubunge wa EAC
wewe lini?
 
siku hizi deal ni ubunge...na usomi wote mtu anauweka kando na kugombea uwizi(ubunge)
 
Tunalalamika hatuna walimu wengi wakufundisha huku wataalam waliobobea mnawapele kwenye siasa!
 
Dr.Shayo amenisikitisha sana yaani anatoka uingereza moja kwa moja anakwenda kujiunga na kundi la mafisadi ili nae aanze kuitafuna nchi ni masikitiko makubwa kwa watu kama hawa wanaojua ukweli jinsi CCM ilivyoanagmiza nchi letu wakaamua kuweka yote hayo pembeni ili ale nchi. ungetegemea kijana kama shayo angekuwa tayari kusimama imara na kuwaambia wahusika ukweli kuhusu kuzorota kwa uchumi wa nchi yetu ili tusonge mbele lakini ameamua kuwa sehemu ya mafisadi huku akijua wazi kuwepo kwake ndani ya chama hicho kilichozeeka hakuna tija yeyote. yaani ni masikitiko kwa mtu aliyesoma kama huyu kuangalia kwanza mkate na siagi huku akiliona taifa linateketea shame on you shayo.
 
Wote ni ma-f-i-s-a-d-i katika mengi tu. Makongoro Nyerere anajua ubunge unaweza kutenguliwa wakati wowote kwa hoja ya kuchakachua matokeo. Ameingia plan B ya kisiasa. Dr. Shayo sifahamu sana lakini kwa sasa naanza kuwatilia shaka wanaokaa nje kwa muda mrefu halafu wakaibukia CCM wanakuwa wameona mahala pa kupitia tu.
 
Mwanzoni nilishawahi kujadili hapa na kusema huyu jamaa udokta wake ni makapi na chuo alichosoma ni London South Bank University ni bure hadi wanafunzi wake wanalalamika hawapati kazi. Nadhani maneno yangu yalikuwa sahihi huwezi kuwa PhD holder ukaacha taaluma ya academia kwenda kuwa mwanasiasa kama sio wewe ni mtupu kichwani.

Huo ni uganga njaa na usanii. Anyway nilishaamua sitamjadili tena maana wengine walisema labda nina ugomvi nae ila huo ni mtazamo wangu. PhD holder unatakiwa uwe katika vyuo ukifundisha au nafasi za utendaji ukionyesha umahiri wa fani yako uliyosomea na sio kuwa mwanasiasa. Na tunawaomba akina michuzi warekebishe huyu jamaa kasomea forest management na sio economics tafadhalini sana economics amevamia fani isiyomuhusu huyu sio mchumi.
 
Kwa hiyo una maana Dr. Slaa ni mtupu kichwani? ama dokta yake pia ni ya kuchakachua?
 
Mwanzoni nilishawahi kujadili hapa na kusema huyu jamaa udokta wake ni makapi na chuo alichosoma ni London South Bank University ni bure hadi wanafunzi wake wanalalamika hawapati kazi. Nadhani maneno yangu yalikuwa sahihi huwezi kuwa PhD holder ukaacha taaluma ya academia kwenda kuwa mwanasiasa kama sio wewe ni mtupu kichwani.

Huo ni uganga njaa na usanii. Anyway nilishaamua sitamjadili tena maana wengine walisema labda nina ugomvi nae ila huo ni mtazamo wangu. PhD holder unatakiwa uwe katika vyuo ukifundisha au nafasi za utendaji ukionyesha umahiri wa fani yako uliyosomea na sio kuwa mwanasiasa. Na tunawaomba akina michuzi warekebishe huyu jamaa kasomea forest management na sio economics tafadhalini sana economics amevamia fani isiyomuhusu huyu sio mchumi.
Kwa hiyo wakina Lipumba na Mgiro nao ni watupu?
 
Hao watakuwa watupu kwa sababu ni ccm na cuf, cha kuuliza na je
Dr Slaa? sijawahi kusikia mtu akishauri ama kuhoji msomi huyu aliyebobea kwanini ameiingia
ktk siasa badala ya kwenda chuoni kufundisha.
 
Dr. Shayo ana haki ya kugombea ubunge au madaraka yoyote kama raia wa Tanzania.

Ila swala la uwezo wake kitaaluma lilipoletwa hapa kwa mara ya kwanza mwaka 2007 sikuona sababu yoyote ya kuquestion academic gravitas yake; ila sasa hivi baada ya transition kutoka LSBU kwenda OUT na kuwania ubunge mara moja inaanza kunionyesha kuwa watu waliokuwa waki-question uwezo wake wakati ule huenda walikuwa sahihi. Kuna mtu aliyeandika hapa kuwa Dr.Shayo alikuwa ameajiriwa LSBU kama research associate na alikuwa akitembea kwenye kamba hapo LSBU kwa kuwa kibarua hicho lingeota nyasi wakati wowote. Mtu huyo aliyesema hivyo huenda alikuwa sahihi pia.

Kwa vile karudi nyumbani kutumia taaluma yake kuendeleza nchi, tusiendelee kuwa negative sana; mwacheni afurahie matunda ya uraia wake.
 
Huyu "Dr." kihiyo si ndiyo yule "mother of all plagiarists"? Masikini Watanzania, hawaelewi kitu hapo na "Udokta" wake wa chuo feki cha Wanigeria, Wahindi na Wapakistani cha London South Bank University.
 
Kufundisha mtu yoyote anaweza kufundisha aliyeomea hiyo fani lakini sio kila mtu anaweza kuwakosesha mafisadi usingizi
 
Huyu "Dr." kihiyo si ndiyo yule "mother of all plagiarists"? Masikini Watanzania, hawaelewi kitu hapo na "Udokta" wake wa chuo feki cha Wanigeria, Wahindi na Wapakistani cha London South Bank University.

A big, brazen plagiarist!!
 
Dr. Shayo ana haki ya kugombea ubunge au madaraka yoyote kama raia wa Tanzania.

Ila swala la uwezo wake kitaaluma lilipoletwa hapa kwa mara ya kwanza mwaka 2007 sikuona sababu yoyote ya kuquestion academic gravitas yake; ila sasa hivi baada ya transition kutoka LSBU kwenda OUT na kuwania ubunge mara moja inaanza kunionyesha kuwa watu waliokuwa waki-question uwezo wake wakati ule huenda walikuwa sahihi. Kuna mtu aliyeandika hapa kuwa Dr.Shayo alikuwa ameajiriwa LSBU kama research associate na alikuwa akitembea kwenye kamba hapo LSBU kwa kuwa kibarua hicho lingeota nyasi wakati wowote. Mtu huyo aliyesema hivyo huenda alikuwa sahihi pia.

Kwa vile karudi nyumbani kutumia taaluma yake kuendeleza nchi, tusiendelee kuwa negative sana; mwacheni afurahie matunda ya uraia wake.

Kichuguu, why are you giving this plagiarist a pass? Aren't you aware of his plagiarism?
 
Sasa akale wapi? Polisi?

Akale London South Bank Uni. huko....

Halafu siku hizi Tanzania kuna ma "Dr" wengi sana. Yaani humo serikalini ndo usipime kabisa! Raisi ni dokta, makamu wake ni dokta, raisi wa Zenji ni dokta, bado Pinda tu! Naye muda si mrefu atakuwa dokta.

Kwenye baraza la mawaziri ndo balaa. Nadhani karibu robo tatu nzima ya mawaziri na manaibu wao wote ni madokta.
 
Back
Top Bottom