Dr. Salim Ahmed Salim kuwa Obama wa Tanzania 2015?

Hata afufuke Nyerere sasahv, akigombea kwa tiketi ya ccm, hapati uraisi. Hicho chama kipo mochuari, kinasubiri maziko.
Mkuu Filipo hii nimeipenda. Pamoja na kwamb hayati mwalimu Nyerere alikuwa msafi unachosema ni kwamba akifufufuka na akagombania urais kupitia ccm hatapita kutokana na uchafu wa ccm.
 
Huyu mzee hawezi kukubali, maana chama kimechafuka mno naye anajua kwamba baada ya uchaguzi kitakua chama kikuu cha upinzani kikijitahidi sana. Haiwezekani chama kilipokua na mvuto wamtose halafu sasa chama kimekua maiti ndo wamkumbuke (kama tingatinga)

tena waliomchafua ni hawahawa wanamtandao wa JK ili kufanikisha azma ya eti leo ndo wanamuona lulu, imekula kwao
 
Hapana:
(a) Kikwete hawezi kufanya hivyo kwa kuogopa kuwa Salim atalipiza kisasi kwa aliyomfanyia mwaka 2005
(b) Salim hatakuwa tayari kujihusisha na chama ambacho kimeshakosa mvuto kwa watu wake. Atakuwa anajishushia heshima yake ambayo ni kubwa sana duniani
(c) Lowasa atapiga kampeini dhidi yake kuwa alienguliwa mwaka 2005 kwa sababu ya "madhambi" fulani ambayo bado yapo
 
Salim ni Mzanzibar, hatuwezi kuongelea swala la Mzanzibar kuwa rais wa Tanganyika na Zanzibar until the limbo of the Union gets resolved, bado hatujakubaliana kama tunaendelea na Muungano, na kama tunaendelea tunaendela na mfumo gani. Inawezekana kila upande ukawa na viongozi wake kivyao.

Kuna baadhi tunadai haki ya kila upande kuwa ni dola huru yenye mamlaka yake kamili, ndani na nje ya nchi husika.
 
Mkuu Filipo hii nimeipenda. Pamoja na kwamb hayati mwalimu Nyerere alikuwa msafi unachosema ni kwamba akifufufuka na akagombania urais kupitia ccm hatapita kutokana na uchafu wa ccm.

Kwanza Nyerere akifufuka CCM ilivyochafuaka hatakubali kujihusisha nayo kwa namna yoyote ile iwayo!!!!!
 
Ni upuuzi tena upuuzi sana hata kudiriki kufikiri kwamba ipo siku Mzee Salim A. Salim anaweza kuufikiria tena urais kwa tiketi ya CCM. Kumbukeni yeye ni miongoni mwa wahanga wa SIASA CHAFU zilizomwingiza Kikwete madarakani. Mwaka 2005 wakati wa wanachama wa CCM
 
Ni upuuzi tena upuuzi sana hata kudiriki kufikiri kwamba ipo siku Mzee Salim A. Salim anaweza kuufikiria tena urais kwa tiketi ya CCM. Kumbukeni yeye ni miongoni mwa wahanga wa SIASA CHAFU zilizomwingiza Kikwete madarakani. Mwaka 2005 wakati wanachama wa CCM wakitangaza nia ya kugombea urais, vyombo vya habari vilivyokuwa vimenunuliwa na kambi ya Kikwete iliyoanza kuutafuta urais tangu 1995, vilimtukana, vilimdhihaki, vilimdharirisha na kumrushia kila aina ya tuhuma ilimradi tu aonekane hafai.

Nakumbuka Mzee wa watu ilifikia wakati alilazimika kuitisha Press Conference kujibu tuhuma nzito zilzokuwa zimeelekezwa kwake na alitoa hata machozi mbele ya waandishi wa habari. Tangu wakati huo wa uchaguzi, sijamsikia tena Mzee Salim kwenye siasa za Tanzania. Ikumbukwe kuwa huyu Mzee Salim A. Salim ni miongoni mwa watendaji wa karibu kabisa wa Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere walioaminiwa sana. Inasemekana hata mwaka 1995 chaguo la Mwl. Nyerere lilikuwa ni Salim lakini kutokana na majukumu yake ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika, Mwl. Nyerere aliona ni bora aendelee na madaraka hayo kwani Mwl. Nyerere alikuwa ni muumini mkubwa wa PanAfricanism. Badala yake alimweka Bw. Benjamin W. Mkapa. Salim A. Salim alilelewa mikononi mwa Mwl. Nyerere kiuongozi na aliaminiwa sana na ndiyo maana sikushangaa niliposikia kuwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere Foundation).

Kwa historia hii ya 2005 yenye machungu yasiyofikirika aliyopitia Mzee wetu Salim, ni upuuzi tena uliokubuhu kudhani kuwa Salim bado anawaza kugombea urais wa nchi hii kupitia CCM. Ningeweza kushawishika kama ingedhaniwa kuwa atagombea kupitia chama cha ukombozi wa watanzania, chama kinachoaminiwa kwa sasa na watanzania chama kinachosambaa kama moto wa nyika CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO.
 
ili iweze kushinda kihalali ccm wanahitaji kumsimamisha malaika......... Lakini kwa kuwa wana mbinu zao mbadala za ushindi hata mwigulu, lusinde au nape wanaweza kusimamishwa kugombea uraisi
 
Heshima mbele wanabodi. Kwa muktadha wa siasa za CCM kwa sasa, ni dhahili kwamba Salim Ahmed Salim ndio right candidate wa urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa sababu zifuatazo:

1. Hafungamani na kundi lolote la wanamtandao, hivo baada ya makundi yote kupukutishwa, yatasahau tofauti zake na kuamua kunusuru chama na baada ya hapo kila kundi kujielekeza kwenye interests zake kupitia serikali ya CCM (japo haitakuwepo madarakani)

2. Salim ndie candidate kwa kuwa anatokea Zanzibar. CCM inahitaji uungwaji mkono kutoka zanzibar. Kufikia mwisho utawala wa kikwete, zanzibar itakuwa na miaka 20 haijatoa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. CCM itakuwa ime-neutralise bias kwa watu wa zanzibar na kudhoofisha mgombea wa ticket ya CUF na CHADEMA.

3. Salim inadiwa hana kashfa ya ufisadi kama walivo wengine kama akina Lowasa nk 4.Tayari ameshaandaliwa, amewekwa kwenye CC ya CCM strategically,hii ni kwa sababu ya kuwakabili vilivo wapinzani wake kwa kuwa ni member of the "vanguard few" Am ready to be corrected
 
mavi matupu...
yuko wapi kipindi hiki kuja kuwatetea watanzania wanaoteseka na ugumu huu wa maisha na mfumo mbovu na utawala mbovu uliopo chini ya Chama chake?
au ataleta pua yake na kuwaona watanzania ni wa maana sana pindi atakapokuwa anataka kura zao?
Ni mnafiki mkubwa.
 
Salim Ahmed Salim amekuwa mkimya sana. Watu hawajui ana msimamo gani katika masuala na matatizo yanayoisibu Tanzania hivi sasa. Huenda kweli Salim akawa suluhisho pekee ndani ya CCM, lakini nje ya CCM, je?
 
mavi matupu...
yuko wapi kipindi hiki kuja kuwatetea watanzania wanaoteseka na ugumu huu wa maisha na mfumo mbovu na utawala mbovu uliopo chini ya Chama chake?
au ataleta pua yake na kuwaona watanzania ni wa maana sana pindi atakapokuwa anataka kura zao?
Ni mnafiki mkubwa.

True, the guy has been useless...lakini haiepikiki kwa CCM no choice for them...
 
Wanyarwanda hawataki kumsikia huyo babu alishindwa kuchukua hatua hadi mauji ya kimbari huku akiwa katibu OAU
 
Back
Top Bottom