Dr. Saa ni kiongozi pekee aliye kwenye active politics anayeumwa na umaskini wa watanzania

mkuu hazina kwa kipi kuibia hela za kanisa au hazina kwa kudai pesa alipwe kama mbunge wakati yeye siyo mbunge?
 
Hahahahahaha.......Dr wa Gongo kwishney,amejizika mwenyewe,amesoma upepo akaona hata kura.alizopata 2010 hazitafika nusu......
Si ndo walijitangaza na DJ wake ndo atagombea 2015? au kasahau? UKAWA hamwezi mkayapita haya MaCCM,siyapendi ila hakuna upinzani murua Tanzania....enzi zile hii ndo ilikua dream team yangu.
1.Dr Wilbrod P. Slaa
2.Zitto Z.Kabwe
3.John Mnyika
4.Tundu Lisuu
5.Halima Mdee
Lakini baada ya chuki kuingia,baada ya shetani kuingia ,baada ya watu kuitwa wasaliti wengine kuitwa wahafidhina...niliamua kitu kimoja,"mstakabali wa maendeleo yangu uko chini ya mikono yangu" hayataletwa na maintarahamwe (MaCCM) au Ma-alshababi (MaCDM) hata haka ka pimbi kalikojileta ATC-Tanzania.
My fellow youths,your future is on your hands...
 
kumbe siku hizi kwenye jukwaa wapo wagonjwa wengi sana mtu anaongea mambo ya ajabu kabisa .
 
Imeandikwa na Daniel E Daniel


dk Slaa umelisaidia sanataifa.mapambano yako dhidi yaudhalimu wa CCM na ufisadi. Utakumbukwa na kuenziwa daima. Dk Slaa utabaki kuwa hazina Tanzania na Afrika kwa ujumla..

Katika miaka ya 2000's ni kwa mara ya kwanza nilikuwa nikipata hoja murua kutoka kwa wanasiasa makini wa upinzani watatu, nao ni dk Slaa, Zitto Kabwe na RashidHhamadi. Katika kipindi hicho serikali ya CCM ilishikwa pabaya sana katika uendeshaji wake ambapo kashifa nyingi za ufisadi kama kashifa ya Richmond, Kagoda,EPA,Buzwagi ,Kashfa ya BOT nk.


Kashifa hizi ziliibuliwa kwa kiasikikubwa na Dk Slaa,Hamad Rashid kamakiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungenina Zitto Kabwe.Katika Mapambano hayo ya kutafuta Tanzaniayenye neema,yenye usawa, uwajibikaji,uwazi,ukweli na kujenga Tanzania yenyemaziwa na asali kwa kuwapoka wakoloniweusi yaani Ccm na leo wanajiita Magambawapambanaji hawa walionesha ujasiri nauimara mkubwa sana.Cha kusikitisha ni kwamba wapambanaji hawawawili wakakakubali kuwa mateka waccm.Wakaamua kushusha silaa chini kablahawajafika katika uwanja wa Mapambano iliTanzania yenye asali na maziwa ipatikane.

Wawili hawa ni Zitto Kabwe na Hamad Rashidhuku Dk Slaa akiendelea kuwa katikamuelekeo ule ule wa Mapambano dhidi yaccm.Zitto Kabwe akaacha kushiriki operation zachadema kwa hoja kwamba yeye yupo kitaifazaidi.Kwamba yeye yupo bizze sana nashughuli za bunge hasa katika kamati yake ileiliyofutwa POAC.Hapo Zitto aliungana namakamanda wa chadema kwenda kutoanamba za simu za Job Ndugai na AnnaMakinda Temeke.Hapo ubize wa Zittohaukuonekana bali kufungua ama kuzinduaoperation ya M4c pale Jangwani Zitto akawabize.Kwenye operation ya M4c kusini yaaniMtwara na Lindi Zitto alikuwa bize.Kwenyeoperation ya kufanya kampeni Arumerumashariki Zitto akatangaza kugombea uraiswakati kwenye kampeni hakwenda..Wabunge wengine wa chadema walipotokanje ya bunge 2010 akasema ni utovu wanidhamu.

Wabunge wa chadema walipomlindana kupambana na udhalilishaji wa msemajiwa kambi rasmi ya upinzani Bungeni AikaelMbowe Freeman Zitto akasema hakwendabungeni kupigana.Wapambanaji wenzakewanaungana pale Jangwani kupambanakutetea katiba mpya kwa vyama vitatukuunganisha nguvu Zitto anasema yuko bizena shughuli za bunge..Zitto kwa ujumla wake amepoteza sifa zakuwa mpambanaji. Ameshindwa kabisa kuwamsaada kwa wanyonge. Amekuwa mtu wakutupa makombora kwa mbowe kwambaanapewa pesa na Nimrod Mkono wakati sikweli na Mkono alikiri kumpa Zitto magari 2na siyo Mbowe. Kila analofanya ni kwa ajili yakuomba huruma ya watanzania.

Rashid Hamad yeye pia amekuwa akiungamkono ccm.Amekuwa akifanya kwa vitendona kwa siri ama wazi.Ukweli wake ni palealipoungana na ccm kwenye bunge maalum lakatiba kuhubiri serikali 2 na kutukana UKAWAhuku akijua anasaliti kabisa nafsi.Hii ni hatarisana.Dk Slaa mwenyewe amekuwa mwiba mzitokwa ccm na ufisadi.Ameendelea kuaminiwana watanzania.Amekataa katakata kuchezangoma za ccm.Amekataa kuwa sehemu yawahujumu uchumi na mafisadi.Amekubalikuwa na maisha ya kawaida kuliko kupokeamamilioni kama siyo mabilioni kutoka kwaccm.Amekuwa akipambana kwa udi nauvumba dhidi ya ufisadi, uonevu,manyanyaso, DHULUMA,hujuma na kulindarasilimali za taifa.

Ameendeleza kujengachama na sasa UKAWA,Ameendelezakuzungukia sehemu nyingi za Tanzaniakuhubiri UKOMBOZI WA PILI.Ametishwamaisha,kuwindwa na kutukanwa,amekuwajasiri na kuendeleza Mapambano zaidi nazaidi.Amepewa tuzo za kimataifa na mtumakini bara la Africa.Dk Slaa amekuwa ndiyeNyerere wa pili wa leo.Dk Slaa umebaki hazina pekee Tanzania katikakupigania ukombozi wa pili.Ndiye atabakikuwa kioo cha wazalendo.Zitto na Hamadwamesaliti nafsi zao,wamekubali kuwamateka.

Dk Slaa mungu akupe afya njema zaidiukishirikiana na wapiganaji wengineakina Julius Mtatiro,James Mbatia,Prof Lipumba, John Mnyika David Kafulila,Mchungaji Mtikira, Maarim Seif, Machali, Tundu Lissu, Freeman Mbowe



NK.danielezekiel69990@gmail.com

Jifunze kuandika kwa kuacha nafasi
 
Hahahahahaha.......Dr wa
Gongo kwishney,amejizika mwenyewe,amesoma upepo akaona hata
kura.alizopata 2010 hazitafika nusu......
Si ndo walijitangaza na DJ wake ndo atagombea 2015? au kasahau? UKAWA
hamwezi mkayapita haya MaCCM,siyapendi ila hakuna upinzani murua
Tanzania....enzi zile hii ndo ilikua dream team yangu.
1.Dr Wilbrod P. Slaa
2.Zitto Z.Kabwe
3.John Mnyika
4.Tundu Lisuu
5.Halima Mdee
Lakini baada ya chuki kuingia,baada ya shetani kuingia ,baada ya watu
kuitwa wasaliti wengine kuitwa wahafidhina...niliamua kitu
kimoja,"mstakabali wa maendeleo yangu uko chini ya mikono yangu"
hayataletwa na maintarahamwe (MaCCM) au Ma-alshababi (MaCDM) hata haka
ka pimbi kalikojileta ATC-Tanzania.
My fellow youths,your future is on your hands...

Kama unamanisha ulicho kipost, usingekuwa member wa hili jukwaa!?
 
MUNGU WA MBINGUNI ALIYE HAI AKUBARIKI SANA MLETA UZI huu , kiwango CHA DR SLAA KATIKA UKOMBOZI WA NCHI HII NI KAMA CHA NELSON MANDELA ENZI ZILE ZA UBAGUZI WA RANGI , dr slaa ni TUNU YA TAIFA HILI , KWA VILE UKOMBOZI NI KAZI YA MUNGU , TUNAAMINI ATASHINDA NJAMA ZOTE DHIDI YAKE .
 
MUNGU WA MBINGUNI ALIYE HAI AKUBARIKI SANA MLETA UZI huu , kiwango CHA DR SLAA KATIKA UKOMBOZI WA NCHI HII NI KAMA CHA NELSON MANDELA ENZI ZILE ZA UBAGUZI WA RANGI , dr slaa ni TUNU YA TAIFA HILI , KWA VILE UKOMBOZI NI KAZI YA MUNGU , TUNAAMINI ATASHINDA NJAMA ZOTE DHIDI YAKE .
Nani anawadanganya? Mandela hakukwiba hovyo hovyo wake za watu. Mandela hakuacha ya Mungu na kumtumikia Kaisari.
 
UBORA WA DR SLAA KATIKA UKOMBOZI WA TAIFA hili HAUTAFUTWA KWA MAPOVU HATA YA FOMA LIMAO .

mkuu achana nao wewe unatumia kichwa kufikiri hawa wanatumia tumbo kufikiri wasipo fanya wanachofanya hawali
 
Sometimes tuwe wakweli kama hivi,toka uwepo wa Dr.Slaa na jeshi lake bungeni mpaka leo,serikali inapashwa moto,ni basi tu CCM wabishi na wagumu kuelewa
 
Back
Top Bottom