Dr. (PhD) Slaa Akishinda, Kikwete atakubali matokeo?

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Nimekuwa natafakali sana kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu. sasa naona Dr. Slaa amemfunika Kikwete. Mimi nasafiri jijini dar mara kwa mara. nina ndugu, jamaa na marafiki katika mikoa mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Morogoro, dar es salaam, Mwanza, Arusha, Kagera, mara, Shinyanga, Dodoma n.k. Kote huko, Dr. Slaa anaongoza mijini na vijijini. hata ukifanya utafiti humu JF utaona kuwa JK anafunikwa vibaya sana.

Najua kesho ndo tunaenda kumhukumu Jk kwa mabaya yote aliyotufanyia kwa miaka mitano ikiwa ni pamoja na kushindwa kusimamia rasilimali za nchi ziwanufaishe watanzania badala ya wageni.

Sasa Dr. Slaa kura zake zikiongoza
  1. Kikwete ataruhusu mkurugenzi wa NEC amtangaze Dr. Slaa kuwa ndiye Mshindi?
  2. Je Mkurugenzi wa NEC akimtangaza Dr. Slaa kuwa ndiye mshindi kinyume na matakwa ya JK, JK atakubali matokeo hayo na kukabidhi ikulu?
  3. Je kama JK akimkataza Mkurugenzi wa NEC na akakubali kumtangaza JK kama ndo mshindi halali, siri ikavuja (kwa maana hata NEC kuna wafuasi kibao wa Dr. Slaa) itakuwaje?
Maswali haya nimejiuliza sana, jibu sipati.
mwenye jibu?
 
Kikwete hana ujanja wa kuzuia matokeo. Kama matokeo yametangazwa na kashindwa, lazima akubali tu....na atakubali tu.
 
asiye kubali kushindwa si mshindani itabidi tu akubali vinginevyo hiyo injili yake ya amani na utulivu anayoihubiri itatoweka, ila mwenyewe napata wasiwasi sana na ka usemi kao kamoja hivi eti "USHINDI NI LAZIMA KWA CCM" hivi huwa wanamaanisha nini?
kwamba aidha watachakachua matokeo au ndio kama unavyowaza kuwa hawata kubali matokeo.
 
Nimekuwa natafakali sana kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu. sasa naona Dr. Slaa amemfunika Kikwete. Mimi nasafiri jijini dar mara kwa mara. nina ndugu, jamaa na marafiki katika mikoa mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Morogoro, dar es salaam, Mwanza, Arusha, Kagera, mara, Shinyanga, Dodoma n.k. Kote huko, Dr. Slaa anaongoza mijini na vijijini. hata ukifanya utafiti humu JF utaona kuwa JK anafunikwa vibaya sana.

Najua kesho ndo tunaenda kumhukumu Jk kwa mabaya yote aliyotufanyia kwa miaka mitano ikiwa ni pamoja na kushindwa kusimamia rasilimali za nchi ziwanufaishe watanzania badala ya wageni.

Sasa Dr. Slaa kura zake zikiongoza
  1. Kikwete ataruhusu mkurugenzi wa NEC amtangaze Dr. Slaa kuwa ndiye Mshindi?
  2. Je Mkurugenzi wa NEC akimtangaza Dr. Slaa kuwa ndiye mshindi kinyume na matakwa ya JK, JK atakubali matokeo hayo na kukabidhi ikulu?
  3. Je kama JK akimkataza Mkurugenzi wa NEC na akakubali kumtangaza JK kama ndo mshindi halali, siri ikavuja (kwa maana hata NEC kuna wafuasi kibao wa Dr. Slaa) itakuwaje?
Maswali haya nimejiuliza sana, jibu sipati.
mwenye jibu?

Je Dr Slaa naye akishindwa atakubali matokeo? Mbona unaagalia upane mmoja tu? Na wewe je ambaye umefanya utafiti usio rasmi kutokana na safari zako na kujiamnisha kuwa Slaa anamfunika Kikwete je ikitokea utafiti wako ukawa kinyume utakubali matokeo?
 
Akubali akatae historia itakuwa imejiandika kuwa kiwete ndiye aliyeiingiza nchi katika machafuko na mahakama ya the hague itakuwa inamsubiri.....
 
Ukweli ni kuwa JK hatakubali. Mimi si nabii lakini ikitangazwa Dr Slaa jeshi litaingilia kwa maagizo ya JK. Kama aliwatishia wafanyakazi ambao hata hawakupanga kuandamana, ni dalili mbaya. JK ni mshari sana sana kuliko sura yake inavyoonyesha.
 
Je aliishajenga nyumba Dar? Manake alikataa zile zaserikali walizogawiwa/uziwa na Mkapa. Kama hajajenga itakuwa kazi kuachia Ikulu
 
Akubali akatae historia itakuwa imejiandika kuwa kiwete ndiye aliyeiingiza nchi katika machafuko na mahakama ya the hague itakuwa inamsubiri.....[/QUOT

Mhuuuuuuuuuuuuuuuu, yangu macho baada ya kupiga na kulinda kura yangu
 
Tusubiri, ni masaa machache tu yamebakia, tuhakikishe tukapige kura zetu na tusubiri.
Worry of the problem when it comes
 
Kama uchaguzi utakuwa wa haki, thithiem haina chao. Mikoa ifuatayo Dr Slaa na Chadema watazoa kura nyingi sana zikazomuwezesha Rais Mtarajiwa kumpiga chini Kikwete. Mikoa hiyo ni Mwanza, Shinyanga, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Dodoma, Dar, Kigoma, Musoma, Kagera na Rukwa. Tabora bado uko katika hati hati kama utaingia kwa chadema. Go Slaa Go! :peace::peace::peace:
 
Je Dr Slaa naye akishindwa atakubali matokeo? Mbona unaagalia upane mmoja tu? Na wewe je ambaye umefanya utafiti usio rasmi kutokana na safari zako na kujiamnisha kuwa Slaa anamfunika Kikwete je ikitokea utafiti wako ukawa kinyume utakubali matokeo?

Ndiyo watanzania watakubali akiwemo Dr. Slaa. Ingawaje sijui hizo kura za kumwezesha Jk kushinda zitatoka wapi, labda nje ta TZ na nje ya sanduku la kura. Kwa vile wewe ni mwana JF, angalia pia kura za maoni zilizoshindikana kuchakachuliwa!!!!!

Hii ni bendera ya chama cha upinzani kuanzia kesho
 
Dr Slaa atashinda lakini mshindi atatangazwa Kikwete kwa lazima. Historia ya Kenya's last election bila mapanga.
 
Nakubali kuwa chance kubwa ni kuwa Dr. Slaa atashinda lakini Kikwete atatumia shari kuchukua nchi. Ndiyo maana view yangu ni kuwa unless Watz waendelee na mwamko walio nao sasa wa kukataa kupachikiwa kiongozi wasiomkubali, JK atattangazwa mshindi come Tuesday morning. Na kwa Avanti ambaye anauliza kwa nini hatuangalii pande zote mbili, i.e. kama Dr. Slaa akishindwa itakuwaje, ujue kuwa Dr. Slaa hayuko Ikulu kwa hiyo akishashindwa atakataa matokeo halafu ang'ang'anie nini? Obviously JK ana uwezo wa kutumia vyombo vyote vya dola kwa faida yake (including media as we have seen during the last two months) kwa hiyo there's no chance chama cha upinzani kitashindwa halafu kiweze kukataa matokeo. The only way JK atashindwa kuchakachua matokeo ni kama ushindi wa Dr. Slaa ukiwa ni mkubwa sana (landslide) kiasi cha kuwa no matter what they do hawataweza kuficha matokeo. Tukapige kura asubuhi hii na tuchague direction ya nchi yetu. Watanzania wote wajue kuwa kura yao ni siri yao na hamna anayeweza kuwaamulia kiongozi wanayemtaka. EVERY VOTE COUNTS. Waambie wote unaowafahamu. Usipochagua vizuri utajilaumu kwa miaka mitano. Please vote.
 
Inawezekana ndugu.
Halafu nchi hii hakuna wa kufanya fujo.puto tu likipasuka mbio pia wana jf ni mdomo tu lakini vitendo 00. Mmenenepeana kama maboko hata kukimbia mita 50 wengi wenu hamuwezi
leo kapigeni kura tuonyeshe mabadiliko makubwa kwenye tanzania mpya.
Muda huu naenda kwenye kituo changu cha kupigia kura mwere-morogoro
kila la heri
 
Je Dr Slaa naye akishindwa atakubali matokeo? Mbona unaagalia upane mmoja tu? Na wewe je ambaye umefanya utafiti usio rasmi kutokana na safari zako na kujiamnisha kuwa Slaa anamfunika Kikwete je ikitokea utafiti wako ukawa kinyume utakubali matokeo?
kama Dr slaa akishinda Kikwete lazima aondoke ikulu amasivyo hatangaze hamepindua nchi kijeshi na hafute vyama vyote vya siasa.kibaki chama chake kama kinavyo jiita chamapinduzi.
 
Vipi, kwani huko Geshini wote ni maisha bora yaani ile ahadi ya 2000 imetimizwa kwao kwa 100% au nao tunadunda nao kama kawa! Yaani, shule bila mwalimu, huduma duni za afya, mfumko wa bei, rasilimali za taifa kugawiwa bure nk nk; kama hiki kibwagizo wao hakiwahusu tunawatakia kila la kheri ktk kulinda mipaka ya nchi yetu; na maandalizi ya kumtii amiri jeshi watakayekabidhiwa na watanzania ifikapo hapo kesho 1 Nov 2010.
 
Uyu mkwele kuna kila dalili kuwa atayakataa matokeo na kitakachofuata Mungu anajua
 
nadhani matokeo watayatangaza baada ya week mbili wakati wakiendelea kutafuta namna ya kuyachakachua matokeo
 
Back
Top Bottom