IsangulaKG
JF-Expert Member
- Oct 14, 2010
- 706
- 386
Wadau, taarifa nilizozipokea muda mfupi uliopita zimethibitisha kuwa Dr. Swakala, kiongozi wa kamati ya madaktari walioomba msamaha ni kada mkubwa wa CCM.
Dr.Swakala, akiwa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo cha BUGANDO alifikia hatua kukigeuza Chuo kama Tawi la CCM kwa kuwashawishi wanafunzi wenzake kujiunga na CCM pamoja na kusambaza kadi. Pia daktari mwingine aliyetajwa, ambaye pia ni mmoja wa wale walioomba msamaha na mmoja kati ya wapishi wa move nzima Dr.Nuru Mwambola, aliwahi kutuhumiwa kuwahujumu wanafunzi wenzake wa udaktari akiwa Makamu wa Rais pale Kairuki mpaka kufikia kupigiwa kura ya kutokuwa imani nae.
Dr.Nuru, ambaye amekuwa Mwanachama mtiifu kwa CCM alikuwa akitumika kushawishi wanafunzi wenzake kujiunga na CCM akiwa chuoni. Ni kwa kutumia nafasi hiyo, yeye Nuru, pamoja na Swakala walikwenda kwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni Wakili Makene tar 21.08.2012 na kumuomba awakutanishe na Stephen Wassira ili waweze kuonana na Rais.
Wakili Makene aliwajibu kuwa Wassira yupo nje ya Dar ila ametoa maelekezo kuwa Rais yupo tayari kuwaona ila waombe msamaha kwanza kwa rais, serikali na wananchi. Baada ya agizo hilo ndipo wakaendelea na mchakato wa kukusanya majina ya interns, na kwa taarifa zilizopo ni kwamba ni inters 150 tu kati ya 319 ndio waliotuma majina yao.
Baada ya kutekeleza agizo la kuomba msamaha hapo jana, baadhi ya wajumbe wa kamati ya Madaktari wa CCM walikwenda wizarani ili kupata mrejesho, na Naibu Waziri aliwajibu kuwa Mwizi akikiri ameiba kinachofuata ni hukumu.
Habari hii ni kwa hisani ya Daktari ambaye hakupenda jina lake litajwe.
Shukrani Ritz kwa angalizo lako!