Dr. Ndodi kutoa dawa bure!

Ameahidi baada ya kusikia kauli tu kutoka kwa huyo mdhamini wake hapo studioni, ingawa hajasema hiyo bure itaendelea kwa muda gani maana mdhamini mwenyewe nalipia vipindi vitano tu, na pili huyo mdhamini asipotimiza ahadi yake itakuaje?
 
Wakuu, kwa namna ya pekee kabisa kapatikana "mfadhili". Mfadhili huyo kamwahidi dk ndodi kuwa atagharimia vipindi/masomo yake kwa njia ya tv na redio kwa muda wa wiki tano mfululizo kuanzia sasa. Kwa hali hiyo ndodi naye katoa ofa ndani ya kipindi hicho kutoa dawa zake BURE! na kuwa gharama itakuwa kwenye kiingilio tu. Naam naam, kwa hatua hii sasa nadhani si lazima tusongamane loliondo kwa babu maana ndg yetu huyu wa mango_tea bei yake nayo sasa ni rizonabo. Sosi ni ndodi mwenyeweeee! Nawasilisha.
 
Nahisi babu atakuwa amewakomba wateja wake kwa zaidi ya asilimia tisini.
Hivyo anatafuta kishawishi cha kuwarejesha.
.
 
Wakuu, kwa namna ya pekee kabisa kapatikana "mfadhili". Mfadhili huyo kamwahidi dk ndodi kuwa atagharimia vipindi/masomo yake kwa njia ya tv na redio kwa muda wa wiki tano mfululizo kuanzia sasa. Kwa hali hiyo ndodi naye katoa ofa ndani ya kipindi hicho kutoa dawa zake BURE! na kuwa gharama itakuwa kwenye kiingilio tu. Naam naam, kwa hatua hii sasa nadhani si lazima tusongamane loliondo kwa babu maana ndg yetu huyu wa mango_tea bei yake nayo sasa ni rizonabo. Sosi ni ndodi mwenyeweeee! Nawasilisha.

Naona waganga wa kienyeji wote watajitokeza kwenye competition, Mungu utusaidie wanao tunaangamia kwa kukosa maarifa. Na yeye alitoka na lebel ile ile ya dini sasa anaona imekuja album nyingine anajaribu atoke vipi. Yetu macho mwisho wote watakutwa na dhambi zao zikiwazimewatangulia watakapo maliza uwongo wote na mwisho wao utakuwa ni kushushwa mavumbini maana waliamua kujikweza badala ya kunyenyekea na kusujudi kwenye kiti cha enzi ili sifa na utukufu uwe na Mungu wetu Yesu milele na milele.
 
Dr.dondi acha unafiki bana,ulikua wapi siku zote?umewafilisi watu kwa kuwatoza pesa nyingi na hawakupona unadai uwezo kakupa mungu WAPI BANA mnaingia intanet mkipata maarifa mwadai god.
Jamani we ukiugua kwa mfano heartfailure,google that utapata majibu yote achana na matapeli
 
Ametangaza leo Star tv.

Nadhani ni baada ya kuzidiwa kete na babu.
Alikwina?(Alikuwa wapi)Babu wa loliondo amekuwa kama Tigo kwenye makampuni ya simu,kwani Tigo ndio wamefanya makampuni mengine washushe viwango vyao,kwa hilo big up babu wa Loliondo
 
Hivi huyo Dr. Ndodi yeye hana makazi yake? Nauliza swali hili kwa sababu katika matangazo yake huwa anasema anapatikana Itumbi Hotel, Dar; hivyo hivyo kwa Mwanza, Arusha na kwingineko huwa anakuwa hotelini na kwa maana hiyo gharama kubwa anzotoza nafikiri zinatokana na yeye kukaa hotelini badala ya nyumbani kwake au ofisi ya kudumu. Sasa ajifunze kwa Babu wa Loli.
 
Mzushi huyo hana lolote siku zote alikuwa wapi.
Anaelewa kipato cha wa TZ lakini amekuwa akiwakamua laki tatu na kuendelea kwa kuwapa ushauri ambao sometime haujaweza hata kuzaa matunda.

Babu kaset standard
 
anaweza akatoa dawa bure lakini akaongeza gharama za kumwona.
Kwani mpaka sasa kukalia benchi lake tu ni shiling 20,000/- so si ajabu akafidia humo humo.
 
Back
Top Bottom