Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,880
Ndugu zangu,
Suala hili linakuzwa sana bila sababu ya msingi. Kiasi kwamba tunafikia hata kuaminishwa kuwa rushwa nyingine sio rushwa na nyingine ndio rushwa. PCCB wana mamlaka yao ya kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria. Wabunge hatupo juu ya sheria.
PCCB wamepewa kazi hii na ofisi ya Bunge na ndio maana kule PCCB wana nyaraka za Bunge za malipo yote ambayo wabunge tumelipwa toka mwaka 2006. Kuhojiwa sio big deal maana wabunge wengi tumehojiwa. Mimi nilikuwa ujerumani nikaambiwa baadhi ya wajumbe wa kamati yangu wameitwa PCCB. Niliporudi kwa ajili ya kamati nikamwambia Katibu wangu awapigie simu PCCB kuwaambia kuwa ninataka wanihoji maana hawawezi kuhoji wajumbe wangu bila ya Mwenyekiti. Nikaenda kuhojiwa siku ya sikukuu ya Nyrere tarehe 14 Oktoba. Nilihojiwa kwa masaa mawili na kuwapa majibu yote waliyohitaji. Kwanini niogope kuhojiwa iwapo sina kosa?
Kuna watu wanataka kukuza suala hili kwa sababu ni dhahiri kuwa itagundulika makosa fulani fulani katika malipo ya Wabunge. Hivyo makundi yameanza kupigana ili kuonyesha kuwa kila mtu ni mlaji tu hapa nchini na ndio maana suala la Dkt. Mwakyembe limechukua prominance sana. Kwa vyovyote vile maadui wa Mwakyembe wanalishikia bango hili. Mwakyembe nae kama binadamu imebidi ajitetee. Hata hivyo kukataa kuhojiwa sio mwafaka maana kutotoa ushirikiano kwa chombo cha dola nalo ni kosa. Mbona Shelukindo kahojiwa, Mwambalaswa kahojiwa, wajumbe wote wa kamati ya POAC wamehojiwa na wabunge wengine wengi. Hata hivyo labda Mwakyembe kwa kuwa ni mjuvi wa sheria anajua kuwa kuna vipengele vinamlinda.
Suala hili pia halihusu kamati ya Nishati na Madini peke yake na wala halina mahusiano na sakata la Richmond. Kwenye Richmond Bunge haliwezi kuzibwa mdomo hata kidogo. Pia wabunge tusiizibe taasisi ya dola yenye mamlaka ya kisheria kutenda kazi yake.
Wasiwasi wangu ni kuwa tunajenga taswira katika jamii kuwa kuna mambo tunafichaficha kuhusiana na malipo haya ya wabunge. It is a public knowledge that wabunge tunalipwa sana zaidi ya stahili. Taasisi na Mashirika ya Umma pia yanalalamika kuhusu malipo haya. Hata PCCB wenyewe hulipa wabunge kama Mwakyembe alivyosema. Lakini haina maana kuwa hili sio kosa au PCCB wanakosa mamlaka ya kuchunguza.
Ninaamini kabisa uchunguzi wanaofanya takukuru utasema ukweli kuhusiana na masuala haya na hata kuondoa hisia mbaya dhidi ya wabunge kuwa wanalipwa mara mbilimbili kwa kazi zile zile. Ili kuthibitisha kuwa hakuna kosa katika malipo haya, ni vema kutoa ushirikiano kwa chimbo kinachochunguza.
Sasa hapa JF tunajadili watu badala ya kujadili issue. Jambo lililopo hapa ni kwamba je wabunge tunapolipwa zaidi ya mara moja kwa siku kwa kazi ambayo tumeshalipwa na ofisi ya Bunge ni halali au haramu? Is it ethical? Is it corruption? Haya majibu unayapata tu kwa uchunguzi na sio vinginevyo na chombo cha kufanya uchunguzi huo ni PCCB. Tunaipenda au kuichukia PCCB, lakini ndio wenye mamlaka.
Muhimu zaidi ni kuwa PCCB sio Hosea. Hosea anaweza kuwa mtuhumiwa lakini kuna vijana wazuri tu pale wazalendo ambao wanafanya kazi vizuri sana. Vyombo hivi vinafanya kazi kwa maandishi, hivyo ni dhahiri kuwa ni vigumu kupindisha ukweli mahakamani.
Suala hili ni zito sana. Ni kashfa ambayo inaweza kuwa ya historia na ni kashfa ambayo inaweza kubadili mfumo uliojikita ambao sisi wenye madaraka fulani fulani tunafaidika na uoza uliopo. Hili sio jambo la kuchezeachezea hata kidogo. Kumbukeni kashfa ya malipo ya aina hii ilimwangusha Spika wa Uingereza hivi majuzi.
Muhimu zaidi suala hili tusimhusishe Spika kwani yeye hahusiki na posho hizi kwa wabunge maana hatembelei taasisi wala mashirika. Pia Spika alitoa ushirikiano wa dhati kwa PCCB ili kufanikisha kazi yao. Sio kweli kuwa Spika ni kigeugeu katika hili isipokuwa wabunge (ambao ndio wapiga kura wake) tunamyumbisha ili atutetee. Hapana, Spika awe pembeni kwani akichafuka ni Taasisi nzima imechafuka na maadui wake wanamtafuta sana kwa kila hali. Spika aliruhusu uchunguzi ila kwa staha..........