Dr. Mwakyembe: Nikirudi nitamwaga yote kwa watanzania nimechoka sasa....

Huyu bwana hatapona!


unatumia kinywaji gani mkuu? ....mi nilishasema na ninarudia kama anataka watz wajue asemee akiwa huko huko.....tutasikia...huku hawezi kurudi kama alivyokwenda huku akirudi anarudi kivingine kabisa
 
afanye press conference akiwa hapo hapo Hospital, tena ndio media mingi mingi hata za kimataifa ziko, afanye hivo.

Getwell Mwaki
 
Namtakia Mwakyembe afya njema,apate nafuu ya haraka .Hata hivyo,wanasiasa Tanzania tuache unafiki,tuwape watanzania wale ambao tumekuwa tukidai kwamba tunawapigania haki yao.Tuache tabia hii ya kuuficha umma wa watanzania siri nzito.

Dhana ya demokrasia hapa inakuwa mashakani ikiwa mtu uliyepewa mamlaka na umma unawaficha kile wanachostahili kujua kwa sababu au kwa maslahi yako binafsi au chama chako tu.Mtu unakikuka katiba ambayo umeapa kuilinda,haki ya kupata taarifa iko katika katiba.Sijui ni kwa nini Mwakyembe alificha baadhi ya sehemu katika Ripoti ile ya RICHMOND.Vitu vingine huwa tunajitakia kwa sababu za kinafiki nafiki tu.Let the truth be told!
 
Ningependa kusikia hawa jamaa zetu wanasema kile kinachowatesa, Sioni umuhimu wa kusema nitasema wakati unacho cha kusema, kisha watu wanasubiri wakithani kuna cha maana kumbe stori tu kwamba eti wakati ukifika nitasema, Niliposikia EL anataka kusema nikakaa tayari kupata jambo kubwa la maana lakini sikuona ki2. this people should say what they want to say and not Nikirudi nitasema, Hata hapo alipo sauti inasikika. Dunua ni kama kijiji sasa, Come on daktari wa ukweli speak now you dont know tommorow
 
another kuku journalism!!

alikua wapi siku zote

we dramatize hawa drama queens.............

naomba niseme kitu kimoja na mods this time msidiliti

WAPUMBAVU WOTE INCLUDING MWAKYEMBE.......... WANALETA SIASA ZA KIPUUZI, KAMA KWELI ANAIPENDA NCHI ALIKUA WAPI???

hiyo ni kweli kwanini matatizo yampate ndiyo ajifanye kusema kweli kwa hiyo asingeuugua angelea kula buyu kweli huu ndiyo uzalendo.je akifariki nani atasema huo ukweli lakini simuombei mabaya.
 
Bila ya mwanzisha thread kutupa authentic source ya hii habari, I will give this thread a deserved "trash" tag.

Needless to mention that all the subsequent contributions which haven't questioned the auntencity of the source are (sorry guys) equally "trash"!
 
Mbunge wa Kyela na Naibu waziri wa Miundombinu Dr Harrison Mwakyembe ametamka maneno magumu akiwa kwenye matibabu nchini India,Mwakyembe amesema akirudi salama atamwaga yote yanayomsibu bila kuficha hata nukta moja maana amechoka na hawezi kuvumilia tena...

Akaendelea kusema Watanzania waendelee kumuombea maana anaendelea vyema na Allah akimsaidia akanyanyuka kitandani basi wategemee siri nzito ambayo haikuwai kufahamika Tanzania....

Hii imekuwa ni baada ya kuibuka kwa hoja nzito kuwa kuna Watanzania wanataka kuuwawa akiwemo Dr Harrison Mwakyembe,hoja yangu ngoja tusubiri tuone mambo yatakuwaje baada ya kufika,naamini Mungu mkubwa atamnyanyua toka kitandani.

Get well soon Dr Harrison Mwakyembe and Prof Mwandosya...


Wana JF,

Sasa Naona nae Mwakyembe kaja na style nyingine ya kutaka kusema kilicho kweli na kinacho msibu huku Juzi Juzi Lowassa nae alikuja kivyake vyake akipiga mkwala vyombo vya habari kuacha tabia ya kumfuata fuata na kutumia jina lake kupata mitaji yao kibiashara.
My Take,

Mwakyembe yeye tunavyo jua ni mbunge wa kyela na anastyle zake za utendaji wa kazi na mabo mengi mbali na hilo twajua mwakyembe alisha tishiwa kifo na akaijulisha Police na idala zingine za Usaklama baada tu ya kutoa report ya Richmond na Dowans na hapo ndipo palipo tengeneza uhasama mkubwa baina ya wanao miliki Richmond na Dowans na baadae katika awamu hii ya pili kuchaguliwa kuwa Naibu waziri wa Ujenzi na kukutwa na mkasa wa kuumwa ugonjwa wa ngozi from no where. Na sasa yuko matibabu India na akirudi atatupa alicho nacho.

Baba Mkwe wangu E Lowassa nae tunavyo mfahamu alikuwa PM na ni mbunge wa Monduli Huko Arusha, Nae ana sekeseke zake baada tu ya kujiuzuru as PM juu ya kashifa ya Richmond & Dowans na aliondoka na mawaziri wengine Msabha na karamagi, Katika hili timbwiri timbwiri la Dowans & Richmond ni zigo ambalo kila kiongozi esp mawaziri husika na Rais Jk wanakana zigo hili na kila kukicha vyombo vyetu vya habari haviachi kuliongelea kwani halijulikani mwenyewe ni nani kwani watanzania walitaka kuuliza huo mkataba ulikubaliwa vipi na ulitekelezwaje na kusababisha janga kubwa la umeme na kuta kulipwa tena vidia ambayo watanzania hawataki kulipa na kuwataka walio husika walipe. Na ndicho kizungu mkuti ambacho kila kukicha vyombo vya habari vinamwanika Lowassa magazetini kwani nae twaitaji tamko lake kuwa alihusika au hakuusika kwanini alijiuzulu cheo cha PM?
Kama Lowassa hutosema iliyo kweli kwa wananchi kuwa ni nani alihusika na sekeseke hili la Dowans na Richmond basi kamwe vyombo vya habari pamoja na wananchi hawato kupa muda wa kupumua kukuongelea itakuwa ni kama histori na dawa yake ni kukata mzizi wa fitna sema yote kwa wananchi wao ndio watachambua mchele na pumba yanini utishie watu ati utawapeleka vyombo vya sheria haaa umesahau kuwa watu bado wana kidonda cha wewe kujuuzulu kwa ajili ya Dowans na Richmond na Taneso wanantakiwa kulipa deni huku hatujui alieingiza taifa kwenye huo mkataba fake please EL kuwa mungwana na kuwa mzalendo kweli kama wewe huna lolote juu ya hilii


 
Kua na Huruma,kumbuka kinachomtesa kule India ni ktk kutupigania sisi.


TOka amekua waziri ame kupigania nini? , hala lolte huyu alikua anataka cheo tuu na chuki binasfi , alitanguliza maslahi yake binafsi kwanza kwnye wizara ya nishati na madili.Augue pole na apone aje aendelee kufisadi wa TZ tuu, Kwanz ahii habari nahizi ndio zile za kutunga,sidhani kama inaukweli wowote.
 
another kuku journalism!!

alikua wapi siku zote

we dramatize hawa drama queens.............

naomba niseme kitu kimoja na mods this time msidiliti

WAPUMBAVU WOTE INCLUDING MWAKYEMBE.......... WANALETA SIASA ZA KIPUUZI, KAMA KWELI ANAIPENDA NCHI ALIKUA WAPI???


Wewe kila nchi ina mfumo wake na siasa hazina mantiki wala hisia ndugu yangu kwa hiyo kanuni unazozijua (au unazowish zingetumika kwa kiongozi wa nafasi ile haziwezi kufanywa namna wewe ulie nje unavyofikiri). hii inakua kama kwenye mpira tunalaumu sana mtu akikosa goli au akitoa pasi badala ya kushuti ingia wewe uwanjani uone hali halisi. Siasa zingeendeshwa kishabiki unavyofikiria wewe tusingekua hapa JF tunawasiliana mbona watz mnakua hivyo kama watoto ah!! tumshukuru hata kwa ujasiri wake aliouonyesha kwani wangapi wameshindwa hata kile aclichokifanya? tume ngapi zinasafisha watu kila siku na kupoteza hela zetu? kua makini kijana hii siyo serikali ya kimapinduzi iliyoingia katika uongozi bikira hii ni serikali ya miaka kama 50 hivi. kama unajua siasa pima mwenyewe.
ahsante
 
Get well Soon Mwakyembe

Ingawa Wewe Mzee ni MNAFIKI

Inasikitisha kuona watu kama akina Mwakyembe na Sitta viongozi wawili waliojitahidi kufanya angalau kazi zao kwa maslahi yetu kwa viwango vya kuridhisha wanavyotukanwa na kuitwa wanafiki. Sasa sijui mlitaka nini? kuna viongozi wangapi wameleta +ve "impact" kwenye siasa zetu toka 2005 zaidi ya hawa wawili? yaani tumefikia hatua ya kuwaona wale mabubu au wanaoiba hela zetu wazi wazi kuwa ni wazalendo zaidi ya hawa kwa sababu ripoti haikusomwa yote? huu ni umbumbumbu . Narudia tena hii siyo nchi ya kimapinduzi na dola hii imekaa miaka 50 huwezi kukurupuka kwa ushabiki na kufanya kazi kitoto eti kwa sababu watu wasinione mnafiki? kwanza nani amesema kwenye siasa kuna unafiki? kama ni hivyo wanafiki ni wote kuanzia Rais anayeshabikia makundi, lowassa anayejifanya anaonewa wakati ndiyo kinara wa vita ya kimakundi CCM, SLaa anayejifanya mpambanaji wakati analainishwa na hela za mwanachama wa CCM, Zitto anayejipendekeza kwa CCM na kuanza kufuata sera za CCM akiwa bado mpinzani na wengine wengi. Acheni kuwaonea hawa na lebo ya unafiki, kwa sababu siasa kama kuna unafiki basi wanasiasa wote ni wanafiki.
Politics is neither rational nor emotional
 
Mwakyembe na wenzake walikuwa na choice ya kubaki nje ya serikali kama waliamini misimamo yao ni nje ya serikali. Hii imekuwa ni nchi ya wanasiasa kila kukicha kutishia wanataka kuuawa na maadui wao.

Nje ya serikali wakati yuko CCM haina maana kuna calculations za kisiasa, mtu ambaye angekataa uwaziri ingebidi awe Sitta ambaye uzoefu wake mkubwa na wizara waliyompa ni kama kumdemote. mwakyembe alichukua position ili kupata angalau uzoefu na kuongeza nguvu zake kimtandao na kisiasa ili. kumbuka haya mapambano ni marefu mpaka 2015 ndiyo kitaeleweka na mustakabali wa nchi utaamuliwa.

ugua pole dr na hata mungu akikuchukua haitakua mbaya. ulichofanya tayari kina impact kwenye nchi hii na siasa zimegeuzwa juu chini, wananchi wamefunguka, upinzani wameongeza nguvu, wale waliokua wanataka kupeana urais 2015 sasa itabidi watuombe sisi wananchi tuwape na siyo kuwekana tu kama tuko kwenye ukomonisti.
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Similar Discussions

Back
Top Bottom