DR. Mwakyembe na Natural Justice

Na wewe king'ang'anizi mno, wenziyo wamejenga hoja zenye mashiko lkn wewe unatupotezea muda na hoja zako zisizoeleweka. Sasa unataka kutuhamishia kulinganisha powers za ma-PM waliopita! Acha kuzungusha mada kijana.

Mwanakijiji, Kiranga na sasa Malecela wameku-preempt hoja zako zote.. kwanini usikubali yaishe ? Tuna mengi ya kujadili pia.

unataja majina ya akina mwanakiji yanakusaidia nini? huyo kiranga naye aliuliza kwa nini mwakyembe hakumhoji Lowasa naona naye unasema hoja yake ina mashiko!

uko bize? leo hii , hii ni post yako ya pili kwa siku nzima ya leo! jana umepost post tatu tu, yet uko bize mno na unasema nakupotezea muda!!! unafiki huu na kugawa watu makundi hakukufikishi popote pale na kunakuabisha tu

kama ni slow learner bear with me, kama ni low thinker nibebe tu, kama nina logic jibu, na ukishindwa potezea.. thread nyingi sana humu!

huyo malecela anatapatapa tu na CCM yake, wanataka kutuaminisha mwizi ni Lowassa wakati na mwakyembe ni hero! wote ni wezi tu , sikuwa na divert mjadala..umewaza hivyo...kutaka kukomaza unafiki wake anasema the powerfull PM?? this doesnot make sense at all?? tabia za kinafiki mbaya..sisi wengine tunawawasha tu na HUNA UWEZO WALA MAMLAKA YA KUNINYAMAZISHA labda uje unipokonye L/top yangu, ofisi yangu na ufunge cafe zote...niache kwa sababu umesema haiwezekani...na kwa haraka nimeishajua wewe unajikomba watu wenyewe hauwajui..tunashindana na hoja, wewe kaa pembeni kajadili tunda alilokula adamu na eva..that is your limit!
 
Jamaa(EL) bado hata hivyo alikuwa na nafas ya kujitetea mbele ya pilato(bunge) na hakufanya hivyo,-akasusa! Sasa kushinikiza ripot ya ugonjwa hadharan itatusaidia nini sie?
 
Wabe sitaki kuingilia ugomvi usionihusu lakini kwa ukweli kama unampenda huyo ndugu mwambie aache kuwa too ambitious na hata kutaka kupata utukufu wa Mungu ambao ni dhambi ya kupitiliza. I myself has experience with his characters ambapo once he wanted to plant his person kwa lazima hata pale wananchi wa mahala pale walipomkataa kwa nguvu zote. Hakujua kwamba si kila jamii inaweza hongeka kirahisi ndipo walipomshangaza kwa huyo mtu wake kupata kura za aibu hadi kutoa machozi hadharani. Ninampenda sana lakini matendo yake si mazuri nami nikinyamaza bila kumwambia ukweli dhamira yangu itanisuta milele.

You being a born again usije ingia kwenye dhambi ukaangamia kwakukosa maarifa. Kama kweli ameamua kumrudia Mungu atulie na kumwamini maana ni kwakurudi na kutulia ndipo tunapopata ushindi na siyo kuhangaika kama anavyofanya sasa. Mfikishie huu ujumbe hata nikipata nafasi ya kukutana naye will tell him before his face. The word of God says in prov 16:18 Pride goeth before destruction, and an haughty spirit before a fall. Labda utasema how proud is he, kwakutopenda kusikia kuwa he has to moderate his ambitions and desires kama amepangiwa kuwa Rais atakuwa tu wakati ukifika hata bila kuwa desparate kiasi hicho.

Mkuu Ame, asante kwa ushauri mzuri

hakuna anayemsafisha Lowassa, Lowassa ameishajifia na hana uwezo kama wengi wanavyofikiria, ila lile doa la nini kilitokea litaendelea tu siku nyingine zote. EL anavuna alichopanda, na Mwakyembe anavuna alichopanda, vita hii na nyuma yake kuna nini haielezeki kwa maelezo ya wengi humu. Mwakyembe hata yeye anajua kuwa alitakiwa kumuuliza Lowassa. Ila alizuiliwa. Anayetaka kumuua Mwakyembe ni hao hao waliomwambia asimuulize Lowassa!

to cut short, CCM ni mafia na hakikisha wanaondoka madarakani!! kundi fulani kusema hivi kwa kundi fulani ni kupalilia waendelee kukaa kitu ambacho ni hatari

Ame unasema kama nampenda nimwambie? yaani unaamini ninaweza kusema nao na kuwaona kwa macho yangu, I have never met EL zaidi ya kwenye magazeti, mwakyembe ndio ninafhamu vizuri mpaka blood group lake!! wengi humu wanatoa maoni kwa upenzi na si kuwa wanawajua hao wanaowatetea...mtavunja hadhi ya jukwaa, huu ni uwanja unawakusanya watu wote....TABIA NA MWAZO TOFAUTI SANA na tukiwa wote na akili ya invisible why are we having JF?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mkuu Ame, asante kwa ushauri mzuri

hakuna anayemsafisha Lowassa, Lowassa ameishajifia na hana uwezo kama wengi wanavyofikiria, ila lile doa la nini kilitokea litaendelea tu siku nyingine zote. EL anavuna alichopanda, na Mwakyembe anavuna alichopanda, vita hii na nyuma yake kuna nini haielezeki kwa maelezo ya wengi humu. Mwakyembe hata yeye anajua kuwa alitakiwa kumuuliza Lowassa. Ila alizuiliwa. Anayetaka kumuua Mwakyembe ni hao hao waliomwambia asimuulize Lowassa!

to cut short, CCM ni mafia na hakikisha wanaondoka madarakani!! kundi fulani kusema hivi kwa kundi fulani ni kupalilia waendelee kukaa kitu ambacho ni hatari

Ame unasema kama nampenda nimwambie? yaani unaamini ninaweza kusema nao na kuwaona kwa macho yangu, I have never met EL zaidi ya kwenye magazeti, mwakyembe ndio ninafhamu vizuri mpaka blood group lake!! wengi humu wanatoa maoni kwa upenzi na si kuwa wanawajua hao wanaowatetea...mtavunja hadhi ya jukwaa, huu ni uwanja unawakusanya watu wote....TABIA NA MWAZO TOFAUTI SANA na tukiwa wote na akili ya invisible why are we having JF?

so unasema Lowassa hana nafasi ya kuwa Rais?
na waliompa sumu Mwakyembe sio watu wa Lowassa???????
 
"mwenyewe ajipime"-Mwakyembe

where the hell this statement is coming from kama swala halikuwa kumchunguza Lowassa? why comments like this was accepted were they in TOR? kuwa kamati ile itoe ushauri wa nini cha kufanya hawa waliohusika kwenye ile chain?

Sasa ulitaka waseme nini. Hiyo ni lugha sahihi ya ntu anayejua mipaka yake. All the facts still stand. Lowassa alijiuzulu si jwa sababu aliombwa au kulazimishwa bali alijipima na akaona ni uamuzi sahihi. Hivi jwa nini baada ya kujipima kama anavyojipima sasa hakusema kutajwa kwa jina lake hakuna msingi na hivyo analiachia bunge liamue? Lowassa aliamua kujiuzulu yeye mwenyewe na yeye mwenyewe akubali lawama ya hivyo. Hivi kweli Rostam aibuke leo kulalamika kuwa chama chake hakikumpa nafasi ya kujitetea ndio maana alijiuzulu ubunge? Kweli watu walaumu ccm kwa ra kujuzulu?
 
mwakyembe ni kiongozi wa umma, kiutaratibu, taarifa (report) kuhusu ugonjwa wake inapaswa itolewe na daktari wake/ waziri wa afya/ msemaji wa familia... zaidi ya hapo sioni cha kumlaumu DR.

Nashukuru sana mkuu
maana waliowengi wanadhani DR Ni mtu wa kijiweni, basi akijisikia kusema anasema,hapana ni kama mkuu alivyonena hapo juu kuwa serikali ndio msemaji wake mkuu kupitia wizara ya afya na hata Daktari wake akitaka kutoa taarifa ni lazima apate baraka kutoka sehemu husika

na tusitegeme wizara itasema eti Dr alipewa sumu hahahaha hilo halipo hata kama alipewa lakini kikawaida haitowekwa hadharani kama mfikirivyo ni kwa usalama wa nchi na watu wake kwa ujumla
 
  • Thanks
Reactions: Ame
HIvi Lowassa ambaye tunaambiwa na wengine kuwa is the best thing that is waiting to happen to Tanzania alishindwa kujitetea mbele ya watu 300 halafu siku chache baadaye aliweza kusimama kujitetea mbele ya watu milioni 40? Really? Lowassa ambaye alisimama kubishana juu ya hoja ya kupaa kwa ndege yake na kuzungumza kwa umahiri kila hoja za serikali zilipokuja kweli unaamini alishindwa kupangua hoja za Kamati ya Mwakyembe moja baada ya nyingine? Umejaribu kuipitia hotuba ya Lowassa kujiuzulu uone jinsi alivyoanza vizuri lakini akafikia kuachia ngazi?

Lowassa abebe lawama ya kujiuzulu kwake. Siyo Kamati ya Bunge wala Bunge lililomtaka ajiuzulu. Tuwe wa kweli Lowassa kama Waziri Mkuu alikuwa na nafasi ya kujitetea na kwa hiari yake alikataa kuitumia. Alipomuomba Spika nafasi ya kuzungumza asubuhi ile Spika alimpa. Ikumbukwe asubuhi ile ilikuwa ni kwa ajili ya mwendelezo wa michango ya wabunge (kukaangwa kwa kina Lowassa - angalia kwenye youtube yangu bado ninazo zile clips). Lakini Lowassa alitoa taarifa kwa Spika kuwa angependa kuzungumza.

Spika anafuata taratibu za Bunge - Waziri Mkuu ana priority ya kuzungumza Bungeni halafu anayefutia ni msemaji wa Kambi ya Upinzani. Lowassa aliposimama asubuhi ile angeweza:

a. Kuonesha kuwa hoja za wabunge ni kali dhidi yake lakini siyo sahihi kwa sababu hawajui ukweli wote.
b. Angeweza kuonesha kidogo sehemu ya ukweli kwa upande wake - hakuna ambaye angeweza kumkatisha. Ila angeweza kujibiwa.
c. Lowassa hakutaka kusema alichokuwa anakijua (siyo Mwakyembe). Watu wengi hawajui kuwa Lowassa lolote ambalo angelisema pale lingejibiwa na kina Mwakyembe na ndio mtego ambao aliwekewa (sehemu ya siasa hiyo). Lowassa angesimama na kusema kuwa x, y, na z kilichotajwa na Mwakyembe siyo kweli kina Mwakyembe wangetakiwa kujibu na wabunge kuwez akuamua. Lowassa hakutaka kufanya hivyo. Alijiuzulu.
d. Angeweza kutoa hoja ya kuomba Bunge liahirishwe ili akutane na Kamati Teule na kuwapa sehemu ya maelezo yake maana hawakumpa nafasi hiyo.
e. Lowassa alikuwa na haki kama Watanzani awengine kutoa mawazo yao kwa Kamati TEule. Uzuri wa Kamati teule ni kuwa inaweza kukuuita au kama kuna mtu anaweza kutoa ushahidi wowote anayo haki ya kuutoa. Lowassa alitulia kimya na alijua hajaaitwa kwa kadiri muda ulivyokuwa unapita. Angeandika barua kuuliza au hata yeye mwenyewe kuwapelekea maelezo yake - si lazima aitwe. Hakufanya hivyo. Alipeleka maelezo yake kwa Spika siku moja kabla ya ripoti ya Mwakyembe (nje ya muda). Rejea hotuba ya kujiuzulu kwake. Lowassa hakufanya hivyo. Alitarajia kuwa yeye ni Waziri Mkuu basi lazima angefuatwa au kuombwa well.. hakufanyiwa hivyo. Kama maelezo yake kuwa angeweza hata "kutembea kwa miguu" ni ya kweli well alijua vikao vinapofanyika kwanini hakujipeleka?
f. Lowassa angeweza kutoa hoja kwa Spika Bunge liahirishwe ili akutane na wabunge wa chama chake. Kama Waziri Mkuu alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo na Spika angemsikiliza (wote chama kimoja); angeweza kutumia hata hoja ya kutaka kuzungumza na Rais wake (mwenyekiti wa CCM). Bunge lingeahirishwa au hata ile hoja ingeahirishwa kwa muda wakati Waziri Mkuu anazungumza na Rais. Hakufanya hivyo. Alijiuzulu. Siyo kosa la Mwakyembe wala Bunge.




Of course, lakini siyo ripoti tu, kama Lowassa angeamua kujitetea yeye na Rais wake wangeondoka. Lowassa ndiye mtu anayejua ukweli wote wa kuhusika kwa Kikwete, kwanini hakufanya hivyo? Leo tunasikia ametumia ujuzi huu kule Dodoma kuweza kuzuia kujivua gamba? Kwanini hakutumia siku ile kujitetea? Kwanini hakusimama na kusema kuwa "Jamani, miye nilimuambia Rais..." Hakufanya hivyo. Alijiuzulu.



Hapana simaanishi Waziri Mkuu ni nguvu kubwa ambayo haiwezi kuhojiwa na Kamati. La hasha, ninaamini - kama Kamati ilivyoamini - suala la Waziri Mkuu ni suala la Bunge zima. Kamati TEule haiwezi kumpigia kura ya kutokuwa na imani Waziri Mkuu bali Bunge. Na Kamati ilileta suala la WAziri Mkuu kwenye Bunge. Kumbuka kuwa Kamati Teule ni sehemu tu ya Bunge ambayo imekasimiwa madaraka ya Bunge. Bunge zima linaweza kukaa kama Kamati Teule! Na wangeweza hata kufunga milango kwanza kama Kamati na kuzungumza! Walichofanya kina Mwakyembe ni kurudisha kwa Bunge ambalo ndilo linamuidhinisha Waziri Mkuu kumhoji. Lowassa alitakiwa kujitetea mbele ya Bunge ambalo lilimpitisha miaka miwili nyuma. Ndicho chombo sahihi cha kumwajibisha Waziri Mkuu. Lowassa alijua hili. Alijua moto wa Wabunge wa CCM jana yake asingeweza kuuzima kwa kuzungumza. Lowassa hakutaka kupambana na kujitetea. Aliogopa kwa sababu alijua kuwa amewekwa kona isiyowezekana (an improbable angle).

a. Ajiteteee lakini wabunge wakatae wampigie kura ya kutokuwa na imani na hivyo alazimishwe kujiuzulu na kupoteza haki zake kama Waziri Mkuu.
b. Ajitetee na kumtaja Rais wake na Rais amruke na kulivunja Bunge na hivyo kuanzisha mgongano mkali.
c. Ajitetee halafu kina Mwakyembe wayaweke wazi yale mengine ambayo walimuachia kiporo halafu aonekane kuwa ujanja wake wa maneno haukuwa na njia ya kumuokoa.

Lowassa aliamua njia rahisi - the path of least resistance. Ndio maana wengine tunakebehi kabisa wazo ati ni kiongozi mzuri na kwamba wapo watu wanafikiria ati anaweza kuwa Rais anayefaa wa Tanzania.

Mwanadamu huru anaweza kuletwa na mtu mwingine huru hadi kwenye genge la jiwe lenye kina kirefu. Anaambiwa kuwa anatuhumiwa kufanya x,y na z. Wanaomtuhumu wanamwambia ajipime "yeye mwenyewe na kuchukua uamuzi unaostahili". Sasa yule mtu huru baada ya kutafakari anaamua kuruka na kupoteza maisha yake. Haulizi, habishi, wala hajaribu kuwaambia wanaomtuhumu kuwa tuhuma zao si za kweli. Hachambui ushahidi uliotolewa dhidi yake anaamua tu kuruka. Well, mtu yeyote aliyekaa pembeni ambaye anaona kuwa hakuna mtu aliyemshikia Bunduki kumwambia aruke au aliyemsukuma. Wanamuona ametumia kutemba kidogo, kukaa chini kufikiria na kisha anaomba nafasi ya kuzungumza. Nafasi hii ya kuzungumza angeweza kujitetea maana wale wanaomtuhumu wanatarajia kuwa atajitetea. Badala yake anasimama na kusema.

"kweli hamkuniuliza muda wote huo hadi mmenifikisha hapa, ningeweza kuja hata kwa miguu hadi kwenye ofisi zenu lakini hamkufanya hivyo. Ningeweza kujitetea kwani ushahidi mliotoa hauna msingi. Kwa kweli hamkunitendea haki na natural justice haikufuatwa. Najua mnachokitaka, mnataka nyumba yangu, mnataka magari yangu na kwa hakika mnataka cheo chengo".

Halafu anaruka kwenye genge!

Bahati nzuri ananusurika japo amejeruhiwa. Anarudi na kusema "mmenisukuma nijirushe"?

Wanamuuliza

"Kwanini uliruka?"

anasema
"Nisingeruka ningeonekana mbishi!"

"Sasa huoni kwa kuruka watu waliona una hatia?" wanamuuliza.

"Nisingeruka bosi wangu angeonekana vibaya"

"Kwanini sasa uliruka kama ushahidi haukuwa mzito hivyo"?

Hajibu na badala yake anaanza kueneza kampeni kuwa "nilionewa nilionewa". Bahati nzuri kuruka kwake kulitangazwa kwenye televishenina kurekodiwa.

Mkuu Mwanakijiji,

Mjadala huu unanikumbusha jambo moja lililotamkwa na Mwanasheria Alex Mgongolwa akihojiwa na Clouds FM mara baada ya kusomwa kwa taarifa ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu Richmond, alisema ripoti imeandaliwa na mtaalamu wa mitego ya kisheria, kwamba kwao wao wanansheria kile kilikuwa kitanzi ambacho kila unapojitahidi kujisafisha ndipo kinapozidi kukaza, na akashauri wahusika wote wakae kimya ama sivyo watazidi kujiumiza kwa kujiumbua.

Kinachojidhihirisha hapa ni Lowasa kuzidi kujiumbua na kujimaliza kupitia mikakati yake hii ya kujisafisha anasahau kuwa ni yeye mwenyewe aliyepima akajiona ni mhalifu akajiuzulu, hili hata watetezi wake wanashindwa kuliona au hawataki makusudi kulizungumzia!
 
Mkuu Ame, asante kwa ushauri mzuri

hakuna anayemsafisha Lowassa, Lowassa ameishajifia na hana uwezo kama wengi wanavyofikiria, ila lile doa la nini kilitokea litaendelea tu siku nyingine zote. EL anavuna alichopanda, na Mwakyembe anavuna alichopanda, vita hii na nyuma yake kuna nini haielezeki kwa maelezo ya wengi humu. Mwakyembe hata yeye anajua kuwa alitakiwa kumuuliza Lowassa. Ila alizuiliwa. Anayetaka kumuua Mwakyembe ni hao hao waliomwambia asimuulize Lowassa!

to cut short, CCM ni mafia na hakikisha wanaondoka madarakani!! kundi fulani kusema hivi kwa kundi fulani ni kupalilia waendelee kukaa kitu ambacho ni hatari

Ame unasema kama nampenda nimwambie? yaani unaamini ninaweza kusema nao na kuwaona kwa macho yangu, I have never met EL zaidi ya kwenye magazeti, mwakyembe ndio ninafhamu vizuri mpaka blood group lake!! wengi humu wanatoa maoni kwa upenzi na si kuwa wanawajua hao wanaowatetea...mtavunja hadhi ya jukwaa, huu ni uwanja unawakusanya watu wote....TABIA NA MWAZO TOFAUTI SANA na tukiwa wote na akili ya invisible why are we having JF?

Wabe kwakua wewe unaamini basi jua wazi vita hii ni vita yenye maelezo ya wazi. Tupo tulioamua kusimama kwa zamu zetu ili kuitafuta Tanzania iliyo njema ambayo uwezo wa kuipata umo mikononi mwetu maana tumepewa nguvu uwezo na mamlaka kupata kila tunachokitamani kama kiko sawa sawa na mapenzi ya Mungu. Kama ujuavyo katika hili tunataka wote tutoke salama isipokuwa wale tu wana wa uovu ambao kwa hiari yao wameamua kumtumikia muasi; hao watajimaliza wao wenyewe kwa panga walizo jifulia kwa mikono yao. Ni hilo tu kwa mengine yote tuombeane tu ili jina la Mungu lisitukanwe kupitia sisi.
 
ndo mana mleta mada kamshauri mwishoni kua aitake serikali hadi tar 5 january itoe tamko otherwise ripot ataitoa mwenyewe ndo matatizo ya kusoma tu heading halafu unadandia kujibu

Mungu kamponya na ugonjwa, nyie mnataka ataje ugonjwa na sababu ili ziwasaidie nini? Kwa nini mnataka azidi kuwanufaisha wasiohitajika?

Hapa JF wapo walioshabikia kuumwa kwake na wengine kumtakia kifo. Sasa kapona kwa nguvu ya YESU KRISTO, mnataka aitishe serikali ambayo yeye ni Waziri. Mkijua mtampa nini kama compesations au mtawaua mnaotaka awataje? Kibaya tayari mnahisia zenu mnazotaka zithibitishwe, poleni.

Mh. Mwakyembe, keep calm, mshukuru Yesu aliyekuponya na umtangaze yeye. Shetani ndiye aliyekusababishia ugonjwa na Yesu kakuponya, MWISHO. Malumbano ya nini?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Lowassa aliweza na alikuwa na haki ya kujitetea. Hakunyimwa haki ya kujitetea. Alipopewa nafasi ya kujitetea au hata kujenga hoja kuwa kamati haikufanya kazi vizuri hivyo apewe muda aende kuzungumza na kamati Lowassa alizira. Alipewa kamba akajifunga mwenyewe. Kamati ilieleza kilichofanywa na "nguvu kuu" yaani Waziri Mkuu lakini Waziri Mkuu anapitishwa na Bunge na ni mtu wa tatu katika urais. Ni kweli wangeweza kumhoji lakini unamhoji vipi mtu mwenye nguvu kama Lowassa (personally) na kama Waziri Mkuu? Leo hii mnaona watu wanavyohangaika juu yake na siyo Waziri Mkuu - imagine alivyokuwa Waziri Mkuu.

Tena kina Mwakyembe hata kugusa tu ofisi ya Waziri Mkkuu ni kitu ambacho kinabakia katika historia. Leo hii hata kumgusa Waziri ni kazi. NI kweli tungependa labda ingekuwa perfect lakini ndio siasa ilivyo - you win some you lose some. Labda leo huko aliko anajuta kutomhoji Lowassa. Lakini, kwamba walimnyima Lowassa haki ya kujitetea haina hoja kwa sabababu alituhumiwa ndani ya Bunge mbele ya Bunge na alipoomba nafasi ya kuzungumza kila mtu alitegemea angejitetea na kuishambulia kamati na kuifanya duni. Alijaribu kidogo (soma hotuba yake ya kujiuzulu) lakini kitu pekee ambacho hakikufanya ni kujitetea.

Alitambua kosa hilo ndio sababu siku chache baadaye akazungumza na Tido Mhando (TVT wakati huo) na kujaribu kujitetea na kama watu wanakumbuka matangazo yale yalikatishwa si kwa amri ya Mwakyembe... Leo hii anajaribu kujielezea na amebaki kulalamika kuwa alionewa ukweli ni kuwa yeye mwenyewe alitaharuki na kuchukua uamuzi wa KUuzira uwaziri mkuu .. nakumbuka maneno yake "There is a wish and I'm going to grant it". "Wanachotaka ni Uwaziri Mkuu" alisema. Na akajiuzulu.


Ndio maana wengine tunamuona hafai kuwa kiongozi. Alishindwa kujitetea na kutetea msimamo wake na wakati alipotakiwa kuonesha kuwa anaweza kupigana aliweka "manyanga chini". Leo tunahangaika naye si kwa sababu hakupewa nafasi ya kujitetea! Tunahangaika naye kwa sababu alipopewa nafasi ya kujitetea yeye alizira! Well.. hakuhumiwa na Bunge wala na Kamati ya Mwakyembe. Alituhumiwa na alipewa nafasi ya kujiteeta kwenye Bunge (ambalo Kamati ya Mwakyembe iko chini yake). Lowassa angeweza kama anatkaa siku ile kutoa baada ya kujitetea vizuri kuwa Bunge lipige kura ya kuwa na imani naye au la. Baada ya kujitetea na kuweka ushahidi wake (Spika kisheria anampa nafasi ya kwanza ya kuzungumza Waziri Mkuu) basi wabunge wangekuwa na picha zote mbili. Lowassa hakufanya hivyo, hakujitetea, hakutoa nafasi kwa chama chake kuona ushahidi ambao anaamini ulifichwa na alishindwa hata kutoa nafasi ya Bunge kuonesha imani dhidi yake au la. Alijiuzulu. Hakulazimishwa na Rais, hakulazimishwa na Mwakyembe na hakulazimishwa na Bunge. Alijiuzulu baada ya kushauriana na mke wake Bi. Regina.

Sasa Mwakyembe anapewa lawama ya kujiuzulu kwa Lowassa? Really?

umeongea sana, lakini malezo yako ni kama vile yanaonyesha kamati was right kumuogopa Lowassa, very difficult kukuelewe na kuielewa kamati...

Hayo ya Lowassa kupambana, sidhani kama wewe unaweza kusimama kwenye mahakimu 200+ ukapambana unless utuambie wewe umetoka MASS na sio duniani... TUKUBALI TUSIKUBALI, KAMATI YA MWAKYEMBE IMECHANGIA KULINDA BAADHI YA WATU WALIOTAKIWA KUWA JELA SIMPLY BY JUSTIFYING KWAMBA KUNA TAARIFA WALIHIFADHI ILI KUTOIVUA NGUO SERIKALI, SO EVERY GUILTY PERSON ANATUMIA HIYO UMBRELLA KUSEMA KWAMBA KUNA YALIYOFICHWA... WHICH TRANSLATE KWAMBA KAMATI USED RESOURCES T GATHER INFO AND DELIVERED JUST A PORTION OF IT, AND YET THY USED FULL RESOURCES

DOESNT MAKE SENSE TO ME, NAKUPA SOW NA WEWE UNANIPA RIPOTI ISIADREES KILA AREA YA TOR NA SOW
 
Sasa ulitaka waseme nini. Hiyo ni lugha sahihi ya ntu anayejua mipaka yake. All the facts still stand. Lowassa alijiuzulu si jwa sababu aliombwa au kulazimishwa bali alijipima na akaona ni uamuzi sahihi. Hivi jwa nini baada ya kujipima kama anavyojipima sasa hakusema kutajwa kwa jina lake hakuna msingi na hivyo analiachia bunge liamue? Lowassa aliamua kujiuzulu yeye mwenyewe na yeye mwenyewe akubali lawama ya hivyo. Hivi kweli Rostam aibuke leo kulalamika kuwa chama chake hakikumpa nafasi ya kujitetea ndio maana alijiuzulu ubunge? Kweli watu walaumu ccm kwa ra kujuzulu?

kweli kaka, nimekubali ...tuko pamoja.

Mkuu x-mass njema, kama uko Tanzania tengeneza pilau ya asili , kama uko 'kule' duni nyingine najua umeishaisherekea mwezi wote huu....

Christmas-Cards-300x240.jpg


nadhani haujasahau nikisema mwana kondoo ameshinda unajibu nini!
 
Wabe kwakua wewe unaamini basi jua wazi vita hii ni vita yenye maelezo ya wazi. Tupo tulioamua kusimama kwa zamu zetu ili kuitafuta Tanzania iliyo njema ambayo uwezo wa kuipata umo mikononi mwetu maana tumepewa nguvu uwezo na mamlaka kupata kila tunachokitamani kama kiko sawa sawa na mapenzi ya Mungu. Kama ujuavyo katika hili tunataka wote tutoke salama isipokuwa wale tu wana wa uovu ambao kwa hiari yao wameamua kumtumikia muasi; hao watajimaliza wao wenyewe kwa panga walizo jifulia kwa mikono yao. Ni hilo tu kwa mengine yote tuombeane tu ili jina la Mungu lisitukanwe kupitia sisi.

Christmas-Cards-300x240.jpg
x-mass njema
 
  • Thanks
Reactions: Ame
umeongea sana, lakini malezo yako ni kama vile yanaonyesha kamati was right kumuogopa Lowassa, very difficult kukuelewe na kuielewa kamati...

Hayo ya Lowassa kupambana, sidhani kama wewe unaweza kusimama kwenye mahakimu 200+ ukapambana unless utuambie wewe umetoka MASS na sio duniani... TUKUBALI TUSIKUBALI, KAMATI YA MWAKYEMBE IMECHANGIA KULINDA BAADHI YA WATU WALIOTAKIWA KUWA JELA SIMPLY BY JUSTIFYING KWAMBA KUNA TAARIFA WALIHIFADHI ILI KUTOIVUA NGUO SERIKALI, SO EVERY GUILTY PERSON ANATUMIA HIYO UMBRELLA KUSEMA KWAMBA KUNA YALIYOFICHWA... WHICH TRANSLATE KWAMBA KAMATI USED RESOURCES T GATHER INFO AND DELIVERED JUST A PORTION OF IT, AND YET THY USED FULL RESOURCES

DOESNT MAKE SENSE TO ME, NAKUPA SOW NA WEWE UNANIPA RIPOTI ISIADREES KILA AREA YA TOR NA SOW

MTM usisahau X-mass mkuu!!





X-MASS NJEMA!!!!
Christmas-Cards-300x240.jpg
 
Ndiyo maana Sugu anaitwa Mbilinyi. Hawa kina Mwa baadhi yao hawana maana hata kidogo.
 
Great question. Lakini nianze kwa kulijibu kutoka mbali kidogo. Anayehojiwa katika uchunguzi wa uhalifu ni mtuhumiwa au mshukiwa. Uchunguzi wa kujaribu kujenga kesi wakati mwingine hata mtuhumiwa hata hajui uchunguzi unafanyika (FBI na polisi wanafanya hivi sana). Wakishakuwa na sababu ya kutosha kuleta mashtaka basi wana mshtaki (indictment) na mtu anakamatwa na kutoka hapo ndio wanampeleka kuanza kumhoji. Maelezo yake hayatoshi hivi hivi kwani baadaye atafikishwa mahakamani ambapo licha ya kushtakiwa atapewa nafasi ya kuwahoji watuhumu wake (cross examination).

Hapa ndio msingi wa hiki tunachozungumzia "natural justice". Kwamba, mtu anayechunguzwa ana haki ya kuhojiwa lakini vile vile anahaki ya kujibu mashtaka yanayotolewa dhidi yake. Kwa maneno mengine, uchunguzi huwa una mtu au chombo kinachochunguzwa.. sasa along the way yawezekana katika uchunguzi huo ikaonekana kuna watu wengine au vyombo vingine vinahusika kwa namna moja au nyingine. Sasa hivi vinaweza kutajwa na vinaweza hata kuletwa mahakamani kuelezea upande wao chini ya kiapo na wengine wanaweza kujikuta matatani kama wanagundulika kuwa wakati uchunguzi unafanyika walijaribu kuficha au kuharibu ushahidi au taarifa - hivyo wanaweza kupata obstruction of justice charges.


Sasa swali lako linauliza "kwanini hawakumuuliza Mwakyembe". Ili tuweze kuona angalau the reasoning turudi kwenye Kamati Teule ilipewa majukumu ya kuchunguza kitu gani na ni nani alikuwa ni "object of the investigation".

Hii hapa sehemu ya taarifa ile katika utangulizi wake (msisitizo wa rangi kali nyeusi wangu) :



sasa swali tunaweza kuuliza: Je, Kamati Teule iliundwa ili kuchunguza nini - jibu tukiangalia hadidu rejea ni "RICHMOND". Tunaweza hata kubadilisha kidogo swali na kuuliza kama iliundwa kumchunguza nani? - jibu bado tunaona katika hadidu zote sita kuwa ni "Richmond". Kwamba, Waziri Mkuu wala afisa yeyote wa serikali hakuwa the OBJECT OF INVESTIGATION. Uchunguzi wa Kamati Teule ulihusiana na Kampuni ya Richmond. Tena Spika aliwakataza kabisa kuwa wasichunguze hata suala la Dowans (rejea maelekezo ya Spika siku ile).

Hii ina maana ya kwamba - vitu na watu wengine wote ambao walijikuta kwenye uchunguzi ule (akiwemo Waziri Mkuu) walikuwa ni incidental to the investigation. Ni katika uchunguzi wake wa Richmond ndio Kamati Teule ikajikuta inakutana na majina mbalimbali ya watu na ofisi zao. Ukisoma vizuri hiyo ripoti utaona kuwa mwisho wa siku jina lililokuwa linatajwa tajwa sana ni la Waziri Mkuu kuwa ndiye aliyefanikisha. Remember - he was not the object of investigation.

Hii ndio sababu walipofika mwisho wa ripoti yao walitoa mapendekezo tu mbalimbali ambayo yaliendana na kile walichokikuta. Kwamba kina Karamagi walifanya hivi n.k wawajibike na hata ilipofika kwa Waziri Mkuu walisema kuwa jina lake lilitajwa sana na wao walitaka yeye mwenyewe ajipime kutokana na uzito wa kuhusika kwake na cheo chake.


Sasa, ndio Mwakyembe akasema maneno haya yafuatayo ambayo yanaendana kabisa na hoja kuwa Lowassa hakuwa anachunguzwa na Kamati Teule (msisitizo wa mistari wangu) :



Sasa, hicho ndicho Mwakyembe alisema kuhusu yote yaliyosemwa kwenye uchunguzi. Mwakyembe hakusema ajiuzulu, Mwakyembe hakusema anapaswa kujiuzulu; alisema "mwenyewe ajipime". Sasa akajipima akaruka! Iweje Mwakyembe abebeshwe lawama?

Kama Lowassa alikuwa implicated kwa mujibu wa uchunguzi wa Kamati ya Mwakyembe, na Mwakyembe akaandika ripoti bila kumuhoji na kupeleka ripoti bungeni, at the very least anakuwa hajakamilisha aspects hizi mbili za objectives alizopewa.

2. Kutathmini mchakato mzima wa jinsi zabuni waliyoshinda Richmond ilivyoshughulikiwa kuanzia Kamati ya Zabuni hadi mwisho ili kujiridhisha kuwa sheria, taratibu, miiko na maadili ya zabuniyanayotawala zabuni za aina hiyo vilifuatwa au vipi;

3. Kutathmini mkataba baina ya Richmond Development Company LLC na TANESCO ili kujiridhisha kuhusu uhalali wa masharti yamkataba huo ukizingatia gharama na masharti mengine ukilinganishana masharti yaliyomo katika mikataba ya aina hiyo iliyoafikiwa naTANESCO/Serikali;
 
Waberoya Lowassa alijiuzulu kwa sababu ni mwizi kama ripoti ya Mwakyembe ilivyosema au kwa sababu hakuitwa kwenye kamati? Ha! Ha! Ha! Hebu chagua moja tuendelee na mjadala! Ha! Ha!
 
Back
Top Bottom