DR. Mwakyembe na Natural Justice

Si lazima kuangalia au kuhoji mambo kwa upande mmoja wa shilingi.Mimi nietoa possble scenario ambayo inawezekana ilitumika kutoumhoji Lowasa kwa faida yake mwenyewe. Hakutendewa haki kivpi na Yeye ni waziri Muu na ripoti iisomwa bungeni. Kwa nini hakujibu au kujitungia maswali na kuyajibu bungeni ili wanachi wajue ukweli tofauti na uwongo wa tume uliosowa bungeni.

Badala yake yeye akaamua kuzira. Na ukungu wa maswali hata angehojiwa lowasa ulikupwepo na utakuwepo sababu kuna wengine walipewa rehersal laini tatizo ni offiacial document zipo.

May be ikifika sehemu Lowasa mwenyewe aombe hizo official document zake zote ziwe public

Tukienda kwa first principles, huwezi kuandika ripoti bila kumpa mtu nafasi ya kujieleza. Hiyo ni fundamental principle ya fair hearing, ina maana hiyo ripoti imeandikwa bila kumsikiliza Lowassa.

Sisemi kwamba Lowassa ni safi, nasema katika kuandika ripoti Mwakyembe alichemsha. Katika sheria unaweza ukawa una m prosecute mtu kafanya kosa kweli, lakini ukikosea steps katika kukusanya evidence unaweza kushindwa kesi mtuhumiwa akaachwa huru. kwa nini Mwakyembe hakumuhoji Lowassa? Regardless of the answer, Lowassa amepewa mwanya wa kusema hakutendewa haki, kwa sababu hakutendewa.
 
Kiranga kwani Tume za bunge zinatakiwa kufanya kazi kama mahakama
 
Kiranga kwani Tume za bunge zinatakiwa kufanya kazi kama mahakama

Hili si swala la principles za mahakama.

Hata mwanao wakija jirani kumsemea kaharibu maua yao, huwezi kumuadhibu au kumuandikia ripoti mbaya kabla ya kumuita na kumuhoji ilikuwaje.

Ndiyo maana ikaitwa "Natural Justice", sio law, constitution wala court justice.
 
Nashauri Dr . Mwakyembe atoe ultimatum kwa serikali kuwa isipotoa tamko kuhusu ugonjwa wake kufika muda fulani i.e 5[SUP]th[/SUP] January 2011, basi yeye ataitangaza ripoti ya ugonjwa wake. Hebu awasikilize hata wanafamilia na rafiki zake, na ndugu ambao wanataka aweke wazi ripoti ya ugonjwa wake kama alivyofanya kuhusu ajali na ''Alshababy"

Ugonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari, usifundinshe watu namna ya kuishi utakavyo.... akiamua kusema alikua anaumwa nini ni yeye... ni serikali pumbavu tu inayoweza kutoa tamko la ugonjwa wa mwananchi wake unless kuna kibali cha daktari au ni kwa ajili ya takwimu tu, ndio unaambiwa kuna wagonjwa milioni mbili wa tegu, huwezi kupewa orodha ya wagonjwa kama udhanivyo

Sanasana serikali ndio inatakiwa itoe ultimatum kwa Mwakyembe kutimiza ahadi alizotoa

it is very difficult when it comes to human body, ndio maana Litvinyenko pamoja na data zote waingereza walizokua nazo waliishia kulalama tu kama pinda na suala la jairo
 
kuwa mwakyembe hakumuhoji Lowassa kwenye ile kamati...yet watu wanaisifia ile kamati ..imetuacha uchi wa mnyama!!

Word.... jamaa anaweweseka, BTW, si kwamba MWakyembe is immune to all diseases except sumu au chuki.... PEOPLE SHOULD KNOW THAT!! NA DALILI ZOTE ALIZONAZO SI YEYE WA KWANZA KUWA NAZO NA SI KILA ALIYEPATA DALILI ZILE AMEWEKEWE RAIOACTIVE MATERIA OR AT LEAST DANGEROUS POISON
 
Ukimnyima mbongo chakula inaweza isiwe issue, lakini ukitaka kumtesa na kumsababishia mahangaiko moyoni basi mnyime maneno....yaani mnyime kile ukijuacho, atahangaika sana.

TUNAITA CHOYO... NA NDIO HUUA MATAJIRI NA PESA KWENYE VYUNGU

pamoja na hayo your mfano doesnt hold water....
 
Huku kulia lia kwa wafuasi wa Lowassa kunaonyesha kabisa kwamba huyu bwana yuko desperate kujisafisha wakati alishapa nafasi ya kuyasema hayo na mbele ya bunge lakini kwa woga wake na kwa sababu ya kujua kwamba yeye ni mhalifu katika hilo, akakimbilia kuhusisha ripoti ile na uwaziri mkuu wake.

Leo kwa ulevi tu, watu wanaanza kuingiza concept za natural justice ambao hata hawana weledi nazo na kudhani kwamba uchafu uliomtapakaa bwana huyu utasafishwa kwa porojo za humu JF. Awadaganye hao hao wajumbe wa NEC na wafuasi na wapambe wake mbumbumbu, siyo watanzania wenye ufahamu.

mkuu si kila anayeleta post against mwakyembe ni pro-lowassa, unless una akili fupi kama website admin wa ikulu
 
mkuu si kila anayeleta post against mwakyembe ni pro-lowassa, unless una akili fupi kama website admin wa ikulu

Hahaha, eti website admin wa ikulu.Umezibuka, mi headphone hiyo nini?

Nilisema hapo mwanzo wazi kabisa ili kuondoa confusion.

Kusema kwamba Lowassa hakutendewa haki na Mwakyembe alichemsha hakuna maana kwamba Lowassa ni msafi.

Lowassa hakutendewa haki, Mwakyembe amechemsha, lakini Lowassa corrupt.
 
hizo headphones ni beat by dre mkuu... super

Watanzania tuna tatizo kubwa sana la kuelewa kwamba si kila anayepinga hoja yako basi hayuko upande wako na yupo kwa adui yako... ndio degedege la wana ccm wengine wasiompenda lowassa, ni degedege la wanaCCM wakidhani kila akosowae ni chadema na kosa la baadhi ya wanachadema wakidhani kila awakowae ni ccm

BTW, website admin wa ikulu ni issue... ni bora kutembea US agencies or private companies website kuijua bongo
 
Lowassa aliuachia uwaziri mkuu kwasababu ali aim at presidency, ndo maana JK alisema wazi kuwa ni ajali ya kisiasa.

Na alipoulizwa huo NEC alinyamaza na gamba likagoma, everthing else ni porojo tu.
 
SITALIPIZA KISASI
Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari wa IPP, aliweka mbele nguvu za Mungu, ambapo alisema kama kuna watu walitaka kumuangamiza anawasamehe na hana sababu ya kulipiza kisasi.“Sitalipiza kisasi hiyo sio kazi yangu bali Mungu anajua cha kufanya na watu wenye kulipiza visasi maisha yao sio marefu,”​

What are the rules of natural justice?

The principles of natural justice concern procedural fairness and ensure a fair decision is reached by objective decision maker. Maintaining procedural fairness protects the rights of individuals and enhances public confidence in the process. A word used to refer to situations where audi alteram partem (the right to be heard) and nemo judex in parte sua (no person may judge their own case) apply.

Kutokana na matukio ya hivi karibuni mpaka sasa nampa Lowasa ‘the benefit of the doubt’’, kwasababu inawezekana kweli kamati ya Mwakyembe haiku exercise natural justice. Kama Mwakyembe yeye mwenyewe ameshindwa kujipa natural justice je ataweza kumpa mtu mwingine?. Watu wameongea kuhusu ugonjwa wake, , watu wamenusurika kuuwawa na kupoteza kazi kwa ajili yake, watu wamefunga na kuomba kwa ajili yake ili tu Mungu ampe uzima na aseme kuhusu sababu ya ugonjwa wake.

Lakini cha ajabu yeye anarudi anasema sitalipiza kisasi! Kwa maana nyingine tayari kisha jenga visasi na watu. Maana yake nini? Je Mwakyembe anaweza kulipa kisasi? Ana nguvu gani za kumlipa kisasi mtu aliyetaka kumuua?. Je kisasi cha mtu anayetaka kukutoa roho ni nini?. Kwa utaratibu wa natural justice mtu hawezi kuwa hakimu wa kesi yake mwenyewe. Inatkiwa aseme anayoyajua kuhusu ugonjwa wake, kisha sisi wananchi (natural court) ndo tutoe maamuzi. Kwanini hataki kuwa muwazi kama hajalishwa sumu mambo ya visasi yanatoka wapi? Na kama ni sumu kwanini hataki kusema ukweli?. Mtu mwenye PHD ya sheria ni mtu ambaye anatakiwa kuwa sio muoga na kikubwa asimamie ukweli daima. Sasa hizi kauli za ‘’kiswahili’’ kuwa sitalipiza kisasi maana yake nini?

Amesema ameiachia serikali; hakuna mtu anaweza kujali uhai wa mtu mweingine. JB katueleza humu kuwa LTK’s ndo wanaohusika, halafu leo yeye anatuambia ameiachia serikali sisi tumueleweje?. Toka nimezaliwa sijawahi kusikia serikali au bunge likitangaza ripoti ya ugonjwa wa mtumishi wake, kwanini iwe kwa Mwakyembe tu? Ingekuwa bora asingetoa kauli ya kusema hatalipiza visasi, angewashukuru watz basi ingetosha. Kama anaficha mambo ya kuhusu uhai wake mwenyewe, angeshindwa vipi kuficha mambo mengine ya Richmond kama alivyosema mwenyewe bungeni?

Nashauri Dr . Mwakyembe atoe ultimatum kwa serikali kuwa isipotoa tamko kuhusu ugonjwa wake kufika muda fulani i.e 5[SUP]th[/SUP] January 2011, basi yeye ataitangaza ripoti ya ugonjwa wake. Hebu awasikilize hata wanafamilia na rafiki zake, na ndugu ambao wanataka aweke wazi ripoti ya ugonjwa wake kama alivyofanya kuhusu ajali na ‘’Alshababy”

Nimefarijika kusoma msimamo wa Dr. Mwakyembe; for sure your miracle is now made permanent because of what you have publicly declared. Dont get provoked by agents of dark places who take the word of God in vain; "For the wisdom of this world is foolishness with God. As it is written, 'He catches the wise in their own craftiness'; and again, 'The Lord knows the thoughts of the wise, that they are futile.'" 1 Corinthians 3:19-20.

Since "...the natural man does not receive the things of the Spirit of God, for they are foolishness to him; nor can he know them, because they are spiritually discerned." 1 Corinthians 2:14-15. Thats why "The fool has said in his heart, 'There is no God.' Psalm 53:1 and "Fools mock at sin, but among the upright there is favor." Proverbs 14:9. Beside "A fool has no delight in understanding, but in expressing his own heart." Proverbs 18:2

Because of the work of God in my life I take charge and responsibility over your situation asuring that nothing shall by any means hurt you and you shall live to the fullest of your age. In this I have confidence that its is not because am wiser or intelligent but because of who lives inside me who is greater than that who is in the camp of the enemy.

As it is written 'In coming to you brothers and sisters, I come proclaiming to you the testimony of God not according to excellence of word or of wisdom. For I decided not to know anything among you but Jesus Christ and this one crucified. I come to you in weakness and in much fear and trembling. My word and proclamation are not in persuasive words of human wisdom but by the demonstration of the Spirit and power, so that your faith might not be in the wisdom of men but in the power of God!' I know the word of God is settled in heaven and I myself stand on it to proclaim your victory in Jesus name. It is for this course the children of God are made manifest that they can destroy the work of the devil.

May the peace of our Lord Jesus bestowed unto you and may you live to declare his wonderful deeds in your life AMEN!
 
Lowassa aliweza na alikuwa na haki ya kujitetea. Hakunyimwa haki ya kujitetea. Alipopewa nafasi ya kujitetea au hata kujenga hoja kuwa kamati haikufanya kazi vizuri hivyo apewe muda aende kuzungumza na kamati Lowassa alizira. Alipewa kamba akajifunga mwenyewe. Kamati ilieleza kilichofanywa na "nguvu kuu" yaani Waziri Mkuu lakini Waziri Mkuu anapitishwa na Bunge na ni mtu wa tatu katika urais. Ni kweli wangeweza kumhoji lakini unamhoji vipi mtu mwenye nguvu kama Lowassa (personally) na kama Waziri Mkuu? Leo hii mnaona watu wanavyohangaika juu yake na siyo Waziri Mkuu - imagine alivyokuwa Waziri Mkuu.

Tena kina Mwakyembe hata kugusa tu ofisi ya Waziri Mkkuu ni kitu ambacho kinabakia katika historia. Leo hii hata kumgusa Waziri ni kazi. NI kweli tungependa labda ingekuwa perfect lakini ndio siasa ilivyo - you win some you lose some. Labda leo huko aliko anajuta kutomhoji Lowassa. Lakini, kwamba walimnyima Lowassa haki ya kujitetea haina hoja kwa sabababu alituhumiwa ndani ya Bunge mbele ya Bunge na alipoomba nafasi ya kuzungumza kila mtu alitegemea angejitetea na kuishambulia kamati na kuifanya duni. Alijaribu kidogo (soma hotuba yake ya kujiuzulu) lakini kitu pekee ambacho hakikufanya ni kujitetea.

Alitambua kosa hilo ndio sababu siku chache baadaye akazungumza na Tido Mhando (TVT wakati huo) na kujaribu kujitetea na kama watu wanakumbuka matangazo yale yalikatishwa si kwa amri ya Mwakyembe... Leo hii anajaribu kujielezea na amebaki kulalamika kuwa alionewa ukweli ni kuwa yeye mwenyewe alitaharuki na kuchukua uamuzi wa KUuzira uwaziri mkuu .. nakumbuka maneno yake "There is a wish and I'm going to grant it". "Wanachotaka ni Uwaziri Mkuu" alisema. Na akajiuzulu.

Ndio maana wengine tunamuona hafai kuwa kiongozi. Alishindwa kujitetea na kutetea msimamo wake na wakati alipotakiwa kuonesha kuwa anaweza kupigana aliweka "manyanga chini". Leo tunahangaika naye si kwa sababu hakupewa nafasi ya kujitetea! Tunahangaika naye kwa sababu alipopewa nafasi ya kujitetea yeye alizira! Well.. hakuhumiwa na Bunge wala na Kamati ya Mwakyembe. Alituhumiwa na alipewa nafasi ya kujiteeta kwenye Bunge (ambalo Kamati ya Mwakyembe iko chini yake). Lowassa angeweza kama anatkaa siku ile kutoa baada ya kujitetea vizuri kuwa Bunge lipige kura ya kuwa na imani naye au la. Baada ya kujitetea na kuweka ushahidi wake (Spika kisheria anampa nafasi ya kwanza ya kuzungumza Waziri Mkuu) basi wabunge wangekuwa na picha zote mbili. Lowassa hakufanya hivyo, hakujitetea, hakutoa nafasi kwa chama chake kuona ushahidi ambao anaamini ulifichwa na alishindwa hata kutoa nafasi ya Bunge kuonesha imani dhidi yake au la. Alijiuzulu. Hakulazimishwa na Rais, hakulazimishwa na Mwakyembe na hakulazimishwa na Bunge. Alijiuzulu baada ya kushauriana na mke wake Bi. Regina.

Sasa Mwakyembe anapewa lawama ya kujiuzulu kwa Lowassa? Really?
 
Sio kila anayepinga CCM yuko Upinzani (CHADEMA), na siyo kila anayepinga CCM yuko Upinzani wengine wanapinga wakiwa ndani ya hivyo vyama. So kila anayesema mawazo tofauti kuhusu Mwakyembe basi ni mfuasi wa Lowassa, na kinyume chake ni kweli.

Mimi nina msimamo wa kujitegemea, husema jambo kulingana na ukweli unaoprevail kwa wakati huo, kwa hiyo ni makosa kunisema ni mfuasi wa Lowassa. Ukisoma vizuri nilichoandika unaweza kuona kuwa ni njia ya kistaarabu ya kumprovoke Mwakyembe aseme.....

Utanufaika nini na Mwakyembe akisema? Hapo ndipo hujaweka wazi, ni kipi hasa unalenga? Thread yako nimeisoma vizuri lakini haijaweka wazi hili, unaposema kajinyima natural justice kwani kuna mashtaka ama tuhuma gani ambazo kwazo anahitajika kujipa natural justice? Kumbuka madhila haya ya ugonjwa iwavyo vyovyote vile si mashtaka ama tuhuma.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Huku kulia lia kwa wafuasi wa Lowassa kunaonyesha kabisa kwamba huyu bwana yuko desperate kujisafisha wakati alishapa nafasi ya kuyasema hayo na mbele ya bunge lakini kwa woga wake na kwa sababu ya kujua kwamba yeye ni mhalifu katika hilo, akakimbilia kuhusisha ripoti ile na uwaziri mkuu wake.

Leo kwa ulevi tu, watu wanaanza kuingiza concept za natural justice ambao hata hawana weledi nazo na kudhani kwamba uchafu uliomtapakaa bwana huyu utasafishwa kwa porojo za humu JF. Awadaganye hao hao wajumbe wa NEC na wafuasi na wapambe wake mbumbumbu, siyo watanzania wenye ufahamu.

Mbopo,

kwa bahati mbaya unaimba wimbo ule ule...kumsafisha EL, EL hawezwi kusafishika JF...anatakiwa awe jela, why is he on streets?

SISI TUNAOAMINI CCM wote ni wezi akiwemo Membe..tunalaumu kuwa kamati ile INGEFANYA KAZI KWA UADILIFU NA UKWELI...TUNGEKUA NA RAIS MWINGINE!!!

Lowassa aliweza na alikuwa na haki ya kujitetea. Hakunyimwa haki ya kujitetea. Alipopewa nafasi ya kujitetea au hata kujenga hoja kuwa kamati haikufanya kazi vizuri hivyo apewe muda aende kuzungumza na kamati Lowassa alizira. Alipewa kamba akajifunga mwenyewe. Kamati ilieleza kilichofanywa na "nguvu kuu" yaani Waziri Mkuu lakini Waziri Mkuu anapitishwa na Bunge na ni mtu wa tatu katika urais. Ni kweli wangeweza kumhoji lakini unamhoji vipi mtu mwenye nguvu kama Lowassa (personally) na kama Waziri Mkuu? Leo hii mnaona watu wanavyohangaika juu yake na siyo Waziri Mkuu - imagine alivyokuwa Waziri Mkuu.

Tena kina Mwakyembe hata kugusa tu ofisi ya Waziri Mkkuu ni kitu ambacho kinabakia katika historia. Leo hii hata kumgusa Waziri ni kazi. NI kweli tungependa labda ingekuwa perfect lakini ndio siasa ilivyo - you win some you lose some. Labda leo huko aliko anajuta kutomhoji Lowassa. Lakini, kwamba walimnyima Lowassa haki ya kujitetea haina hoja kwa sabababu alituhumiwa ndani ya Bunge mbele ya Bunge na alipoomba nafasi ya kuzungumza kila mtu alitegemea angejitetea na kuishambulia kamati na kuifanya duni. Alijaribu kidogo (soma hotuba yake ya kujiuzulu) lakini kitu pekee ambacho hakikufanya ni kujitetea.

Alitambua kosa hilo ndio sababu siku chache baadaye akazungumza na Tido Mhando (TVT wakati huo) na kujaribu kujitetea na kama watu wanakumbuka matangazo yale yalikatishwa si kwa amri ya Mwakyembe... Leo hii anajaribu kujielezea na amebaki kulalamika kuwa alionewa ukweli ni kuwa yeye mwenyewe alitaharuki na kuchukua uamuzi wa KUuzira uwaziri mkuu .. nakumbuka maneno yake "There is a wish and I'm going to grant it". "Wanachotaka ni Uwaziri Mkuu" alisema. Na akajiuzulu.

Ndio maana wengine tunamuona hafai kuwa kiongozi. Alishindwa kujitetea na kutetea msimamo wake na wakati alipotakiwa kuonesha kuwa anaweza kupigana aliweka "manyanga chini". Leo tunahangaika naye si kwa sababu hakupewa nafasi ya kujitetea! Tunahangaika naye kwa sababu alipopewa nafasi ya kujitetea yeye alizira! Well.. hakuhumiwa na Bunge wala na Kamati ya Mwakyembe. Alituhumiwa na alipewa nafasi ya kujiteeta kwenye Bunge (ambalo Kamati ya Mwakyembe iko chini yake). Lowassa angeweza kama anatkaa siku ile kutoa baada ya kujitetea vizuri kuwa Bunge lipige kura ya kuwa na imani naye au la. Baada ya kujitetea na kuweka ushahidi wake (Spika kisheria anampa nafasi ya kwanza ya kuzungumza Waziri Mkuu) basi wabunge wangekuwa na picha zote mbili. Lowassa hakufanya hivyo, hakujitetea, hakutoa nafasi kwa chama chake kuona ushahidi ambao anaamini ulifichwa na alishindwa hata kutoa nafasi ya Bunge kuonesha imani dhidi yake au la. Alijiuzulu. Hakulazimishwa na Rais, hakulazimishwa na Mwakyembe na hakulazimishwa na Bunge. Alijiuzulu baada ya kushauriana na mke wake Bi. Regina.

Sasa Mwakyembe anapewa lawama ya kujiuzulu kwa Lowassa? Really?

Mkuu hapa unamwonea EL, Kweli ajitetee mbele ya wabunge 300! na bomu limeishapigwa? au unasema kuwa aliishajua mapema mwakyembe atasema nini? tunaweza kumhukumu Lowasa kushindwa kujitetea kama aliipata report mapema na alijua Mwakyembe atasema nini kinyume na hapo...kisaikolojia ni ngumu, lets be honest in this!

Pili mkuu siyo siri, report ile ingekuwa honest Kikwete naye angekuwa hayupo leo!

Kibaya zaidi unazungumza kuw kamati haikuwa na uwezo wa kumuhoji Lowassa kwa sababu ya nguvu kubwa! haya ni mawazo yako mkuu..kikanuni Kamati ya bunge ilitakiwa kuwa na TOR....Kuwa Terms of Reference ya kamati ile haikutwakiwa kumuhoji Lowassa? au kushindwa kwao kumuhoji Lowasa ni failure yao? na hii barrier ya 'uwaziri mkuu' kuwa ni ngazi kubwa itafutwa vipi na nani? leo Pinda akikosea hakuna wa kumuhoji kwa sababu u-PM wake ni ngazi kubwa?? what are you approving here??
 
HIvi Lowassa ambaye tunaambiwa na wengine kuwa is the best thing that is waiting to happen to Tanzania alishindwa kujitetea mbele ya watu 300 halafu siku chache baadaye aliweza kusimama kujitetea mbele ya watu milioni 40? Really? Lowassa ambaye alisimama kubishana juu ya hoja ya kupaa kwa ndege yake na kuzungumza kwa umahiri kila hoja za serikali zilipokuja kweli unaamini alishindwa kupangua hoja za Kamati ya Mwakyembe moja baada ya nyingine? Umejaribu kuipitia hotuba ya Lowassa kujiuzulu uone jinsi alivyoanza vizuri lakini akafikia kuachia ngazi?

Lowassa abebe lawama ya kujiuzulu kwake. Siyo Kamati ya Bunge wala Bunge lililomtaka ajiuzulu. Tuwe wa kweli Lowassa kama Waziri Mkuu alikuwa na nafasi ya kujitetea na kwa hiari yake alikataa kuitumia. Alipomuomba Spika nafasi ya kuzungumza asubuhi ile Spika alimpa. Ikumbukwe asubuhi ile ilikuwa ni kwa ajili ya mwendelezo wa michango ya wabunge (kukaangwa kwa kina Lowassa - angalia kwenye youtube yangu bado ninazo zile clips). Lakini Lowassa alitoa taarifa kwa Spika kuwa angependa kuzungumza.

Spika anafuata taratibu za Bunge - Waziri Mkuu ana priority ya kuzungumza Bungeni halafu anayefutia ni msemaji wa Kambi ya Upinzani. Lowassa aliposimama asubuhi ile angeweza:

a. Kuonesha kuwa hoja za wabunge ni kali dhidi yake lakini siyo sahihi kwa sababu hawajui ukweli wote.
b. Angeweza kuonesha kidogo sehemu ya ukweli kwa upande wake - hakuna ambaye angeweza kumkatisha. Ila angeweza kujibiwa.
c. Lowassa hakutaka kusema alichokuwa anakijua (siyo Mwakyembe). Watu wengi hawajui kuwa Lowassa lolote ambalo angelisema pale lingejibiwa na kina Mwakyembe na ndio mtego ambao aliwekewa (sehemu ya siasa hiyo). Lowassa angesimama na kusema kuwa x, y, na z kilichotajwa na Mwakyembe siyo kweli kina Mwakyembe wangetakiwa kujibu na wabunge kuwez akuamua. Lowassa hakutaka kufanya hivyo. Alijiuzulu.
d. Angeweza kutoa hoja ya kuomba Bunge liahirishwe ili akutane na Kamati Teule na kuwapa sehemu ya maelezo yake maana hawakumpa nafasi hiyo.
e. Lowassa alikuwa na haki kama Watanzani awengine kutoa mawazo yao kwa Kamati TEule. Uzuri wa Kamati teule ni kuwa inaweza kukuuita au kama kuna mtu anaweza kutoa ushahidi wowote anayo haki ya kuutoa. Lowassa alitulia kimya na alijua hajaaitwa kwa kadiri muda ulivyokuwa unapita. Angeandika barua kuuliza au hata yeye mwenyewe kuwapelekea maelezo yake - si lazima aitwe. Hakufanya hivyo. Alipeleka maelezo yake kwa Spika siku moja kabla ya ripoti ya Mwakyembe (nje ya muda). Rejea hotuba ya kujiuzulu kwake. Lowassa hakufanya hivyo. Alitarajia kuwa yeye ni Waziri Mkuu basi lazima angefuatwa au kuombwa well.. hakufanyiwa hivyo. Kama maelezo yake kuwa angeweza hata "kutembea kwa miguu" ni ya kweli well alijua vikao vinapofanyika kwanini hakujipeleka?
f. Lowassa angeweza kutoa hoja kwa Spika Bunge liahirishwe ili akutane na wabunge wa chama chake. Kama Waziri Mkuu alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo na Spika angemsikiliza (wote chama kimoja); angeweza kutumia hata hoja ya kutaka kuzungumza na Rais wake (mwenyekiti wa CCM). Bunge lingeahirishwa au hata ile hoja ingeahirishwa kwa muda wakati Waziri Mkuu anazungumza na Rais. Hakufanya hivyo. Alijiuzulu. Siyo kosa la Mwakyembe wala Bunge.

Pili mkuu siyo siri, report ile ingekuwa honest Kikwete naye angekuwa hayupo leo!

Of course, lakini siyo ripoti tu, kama Lowassa angeamua kujitetea yeye na Rais wake wangeondoka. Lowassa ndiye mtu anayejua ukweli wote wa kuhusika kwa Kikwete, kwanini hakufanya hivyo? Leo tunasikia ametumia ujuzi huu kule Dodoma kuweza kuzuia kujivua gamba? Kwanini hakutumia siku ile kujitetea? Kwanini hakusimama na kusema kuwa "Jamani, miye nilimuambia Rais..." Hakufanya hivyo. Alijiuzulu.

Kibaya zaidi unazungumza kuw kamati haikuwa na uwezo wa kumuhoji Lowassa kwa sababu ya nguvu kubwa! haya ni mawazo yako mkuu..kikanuni Kamati ya bunge ilitakiwa kuwa na TOR....Kuwa Terms of Reference ya kamati ile haikutwakiwa kumuhoji Lowassa? au kushindwa kwao kumuhoji Lowasa ni failure yao? na hii barrier ya 'uwaziri mkuu' kuwa ni ngazi kubwa itafutwa vipi na nani? leo Pinda akikosea hakuna wa kumuhoji kwa sababu u-PM wake ni ngazi kubwa?? what are you approving here??

Hapana simaanishi Waziri Mkuu ni nguvu kubwa ambayo haiwezi kuhojiwa na Kamati. La hasha, ninaamini - kama Kamati ilivyoamini - suala la Waziri Mkuu ni suala la Bunge zima. Kamati TEule haiwezi kumpigia kura ya kutokuwa na imani Waziri Mkuu bali Bunge. Na Kamati ilileta suala la WAziri Mkuu kwenye Bunge. Kumbuka kuwa Kamati Teule ni sehemu tu ya Bunge ambayo imekasimiwa madaraka ya Bunge. Bunge zima linaweza kukaa kama Kamati Teule! Na wangeweza hata kufunga milango kwanza kama Kamati na kuzungumza! Walichofanya kina Mwakyembe ni kurudisha kwa Bunge ambalo ndilo linamuidhinisha Waziri Mkuu kumhoji. Lowassa alitakiwa kujitetea mbele ya Bunge ambalo lilimpitisha miaka miwili nyuma. Ndicho chombo sahihi cha kumwajibisha Waziri Mkuu. Lowassa alijua hili. Alijua moto wa Wabunge wa CCM jana yake asingeweza kuuzima kwa kuzungumza. Lowassa hakutaka kupambana na kujitetea. Aliogopa kwa sababu alijua kuwa amewekwa kona isiyowezekana (an improbable angle).

a. Ajiteteee lakini wabunge wakatae wampigie kura ya kutokuwa na imani na hivyo alazimishwe kujiuzulu na kupoteza haki zake kama Waziri Mkuu.
b. Ajitetee na kumtaja Rais wake na Rais amruke na kulivunja Bunge na hivyo kuanzisha mgongano mkali.
c. Ajitetee halafu kina Mwakyembe wayaweke wazi yale mengine ambayo walimuachia kiporo halafu aonekane kuwa ujanja wake wa maneno haukuwa na njia ya kumuokoa.

Lowassa aliamua njia rahisi - the path of least resistance. Ndio maana wengine tunakebehi kabisa wazo ati ni kiongozi mzuri na kwamba wapo watu wanafikiria ati anaweza kuwa Rais anayefaa wa Tanzania.

Mwanadamu huru anaweza kuletwa na mtu mwingine huru hadi kwenye genge la jiwe lenye kina kirefu. Anaambiwa kuwa anatuhumiwa kufanya x,y na z. Wanaomtuhumu wanamwambia ajipime "yeye mwenyewe na kuchukua uamuzi unaostahili". Sasa yule mtu huru baada ya kutafakari anaamua kuruka na kupoteza maisha yake. Haulizi, habishi, wala hajaribu kuwaambia wanaomtuhumu kuwa tuhuma zao si za kweli. Hachambui ushahidi uliotolewa dhidi yake anaamua tu kuruka. Well, mtu yeyote aliyekaa pembeni ambaye anaona kuwa hakuna mtu aliyemshikia Bunduki kumwambia aruke au aliyemsukuma. Wanamuona ametumia kutemba kidogo, kukaa chini kufikiria na kisha anaomba nafasi ya kuzungumza. Nafasi hii ya kuzungumza angeweza kujitetea maana wale wanaomtuhumu wanatarajia kuwa atajitetea. Badala yake anasimama na kusema.

"kweli hamkuniuliza muda wote huo hadi mmenifikisha hapa, ningeweza kuja hata kwa miguu hadi kwenye ofisi zenu lakini hamkufanya hivyo. Ningeweza kujitetea kwani ushahidi mliotoa hauna msingi. Kwa kweli hamkunitendea haki na natural justice haikufuatwa. Najua mnachokitaka, mnataka nyumba yangu, mnataka magari yangu na kwa hakika mnataka cheo chengo".

Halafu anaruka kwenye genge!

Bahati nzuri ananusurika japo amejeruhiwa. Anarudi na kusema "mmenisukuma nijirushe"?

Wanamuuliza

"Kwanini uliruka?"

anasema
"Nisingeruka ningeonekana mbishi!"

"Sasa huoni kwa kuruka watu waliona una hatia?" wanamuuliza.

"Nisingeruka bosi wangu angeonekana vibaya"

"Kwanini sasa uliruka kama ushahidi haukuwa mzito hivyo"?

Hajibu na badala yake anaanza kueneza kampeni kuwa "nilionewa nilionewa". Bahati nzuri kuruka kwake kulitangazwa kwenye televishenina kurekodiwa.
 
Ukimnyima mbongo chakula inaweza isiwe issue, lakini ukitaka kumtesa na kumsababishia mahangaiko moyoni basi mnyime maneno....yaani mnyime kile ukijuacho, atahangaika sana.

Kama hataki kusema angekaa kimya sio kupiga kelele!
 
Personally najua Lowassa ni corrupt na hata sihitaji hata ripoti ya Mwakyembe, najua from reliable sources tangu enzi za serikali ya Mwinyi.

Lakini bado nina swali moja zito sana.

Kwa nini Mwakyembe hakumhoji kabla ya kuandika ile ripoti?

Great question. Lakini nianze kwa kulijibu kutoka mbali kidogo. Anayehojiwa katika uchunguzi wa uhalifu ni mtuhumiwa au mshukiwa. Uchunguzi wa kujaribu kujenga kesi wakati mwingine hata mtuhumiwa hata hajui uchunguzi unafanyika (FBI na polisi wanafanya hivi sana). Wakishakuwa na sababu ya kutosha kuleta mashtaka basi wana mshtaki (indictment) na mtu anakamatwa na kutoka hapo ndio wanampeleka kuanza kumhoji. Maelezo yake hayatoshi hivi hivi kwani baadaye atafikishwa mahakamani ambapo licha ya kushtakiwa atapewa nafasi ya kuwahoji watuhumu wake (cross examination).

Hapa ndio msingi wa hiki tunachozungumzia "natural justice". Kwamba, mtu anayechunguzwa ana haki ya kuhojiwa lakini vile vile anahaki ya kujibu mashtaka yanayotolewa dhidi yake. Kwa maneno mengine, uchunguzi huwa una mtu au chombo kinachochunguzwa.. sasa along the way yawezekana katika uchunguzi huo ikaonekana kuna watu wengine au vyombo vingine vinahusika kwa namna moja au nyingine. Sasa hivi vinaweza kutajwa na vinaweza hata kuletwa mahakamani kuelezea upande wao chini ya kiapo na wengine wanaweza kujikuta matatani kama wanagundulika kuwa wakati uchunguzi unafanyika walijaribu kuficha au kuharibu ushahidi au taarifa - hivyo wanaweza kupata obstruction of justice charges.

Sasa swali lako linauliza "kwanini hawakumuuliza Mwakyembe". Ili tuweze kuona angalau the reasoning turudi kwenye Kamati Teule ilipewa majukumu ya kuchunguza kitu gani na ni nani alikuwa ni "object of the investigation".

Hii hapa sehemu ya taarifa ile katika utangulizi wake (msisitizo wa rangi kali nyeusi wangu) :

Mheshimiwa Spika, tarehe 15 Novemba, 2007 uliipa Kamati Teule siku thelathini kukamilisha kazi yake na Hadidu za Rejea zifuatazokwa ajili ya kutekeleza kazi hiyo ya uchunguzi:

1. Kubainisha Richmond Development Company LLC ni kina nani, nani kampuni ya shughuli zipi na hivyo kupima uwezo wake kupatiwazabuni ya kuleta nchini na kujenga mtambo wa umeme wa gesi waMW 100;

2. Kutathmini mchakato mzima wa jinsi zabuni waliyoshinda Richmond ilivyoshughulikiwa kuanzia Kamati ya Zabuni hadi mwisho ili kujiridhisha kuwa sheria, taratibu, miiko na maadili ya zabuniyanayotawala zabuni za aina hiyo vilifuatwa au vipi;

3. Kutathmini mkataba baina ya Richmond Development Company LLC na TANESCO ili kujiridhisha kuhusu uhalali wa masharti yamkataba huo ukizingatia gharama na masharti mengine ukilinganishana masharti yaliyomo katika mikataba ya aina hiyo iliyoafikiwa naTANESCO/Serikali;

4. Kubainisha huduma na misaada mbalimbali waliyopewa Richmond kama vile kufunguliwa Letter of Credit na kupima uhalali wake;

5. Kuziangalia na kuzitolea maoni taarifa za TAKUKURU, PPRA nataarifa zozote nyingine zilizoangalia utaratibu wa zabuni ya Richmond; na

6. Kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na mchakatomzima wa Richmond ili kutoa mapendekezo ya kuboresha taratibu zazabuni kwa siku zijazo, kwa maslahi ya Taifa letu.

sasa swali tunaweza kuuliza: Je, Kamati Teule iliundwa ili kuchunguza nini - jibu tukiangalia hadidu rejea ni "RICHMOND". Tunaweza hata kubadilisha kidogo swali na kuuliza kama iliundwa kumchunguza nani? - jibu bado tunaona katika hadidu zote sita kuwa ni "Richmond". Kwamba, Waziri Mkuu wala afisa yeyote wa serikali hakuwa the OBJECT OF INVESTIGATION. Uchunguzi wa Kamati Teule ulihusiana na Kampuni ya Richmond. Tena Spika aliwakataza kabisa kuwa wasichunguze hata suala la Dowans (rejea maelekezo ya Spika siku ile).

Hii ina maana ya kwamba - vitu na watu wengine wote ambao walijikuta kwenye uchunguzi ule (akiwemo Waziri Mkuu) walikuwa ni incidental to the investigation. Ni katika uchunguzi wake wa Richmond ndio Kamati Teule ikajikuta inakutana na majina mbalimbali ya watu na ofisi zao. Ukisoma vizuri hiyo ripoti utaona kuwa mwisho wa siku jina lililokuwa linatajwa tajwa sana ni la Waziri Mkuu kuwa ndiye aliyefanikisha. Remember - he was not the object of investigation.

Hii ndio sababu walipofika mwisho wa ripoti yao walitoa mapendekezo tu mbalimbali ambayo yaliendana na kile walichokikuta. Kwamba kina Karamagi walifanya hivi n.k wawajibike na hata ilipofika kwa Waziri Mkuu walisema kuwa jina lake lilitajwa sana na wao walitaka yeye mwenyewe ajipime kutokana na uzito wa kuhusika kwake na cheo chake.

Sasa, ndio Mwakyembe akasema maneno haya yafuatayo ambayo yanaendana kabisa na hoja kuwa Lowassa hakuwa anachunguzwa na Kamati Teule (msisitizo wa mistari wangu) :

Kamati Teule haikufurahishwa hata kidogo na taarifa hizo zinazomgusa moja kwamoja Mhe. Waziri Mkuu katika kuipendelea Richmond DevelopmentCompany LLC. Hata hivyo Kamati Teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu Tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mhe. Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge. Vilevile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibuwa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake. Kuangalia ikiwa matokeoya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge.

Sasa, hicho ndicho Mwakyembe alisema kuhusu yote yaliyosemwa kwenye uchunguzi. Mwakyembe hakusema ajiuzulu, Mwakyembe hakusema anapaswa kujiuzulu; alisema "mwenyewe ajipime". Sasa akajipima akaruka! Iweje Mwakyembe abebeshwe lawama?
 
Back
Top Bottom