DR. Mwakyembe na Natural Justice

Kiranga,

..kwa kweli nikupongeze kwa moyo uliokuwa nao ktk kuitetea hoja yako.

..anayekupinga hapa ama ni mgumu wa kuelewa au ana lake jambo.

..hakuna maelezo ya kutosha kueleza kwanini Tume ya Mwakyembe haikumhoji Edward Lowassa.

..ni bahati tu kwamba Lowassa naye alikurupuka akajiuzulu. kitendo hicho kimeficha a big flaw ikaonekana Mwakyembe na timu yake wamefanya kazi nzuri.

..Lowassa angeweza kukomaa ktk nafasi yake kwa kisingizio kwamba hakuhojiwa, na "amejipima" akaona hana sababu ya kujiuzulu.



mtu wa madili na mishen town kama lowassa hainiingii akilini kuwa alikurupuka kujiuzuru sema tu na ww umepokea vijisent

ndugu yangu muda bado upo na anao arudishe hiyo mada tena bungeni jamani mbona wagumu wa kuelewa mambo lol, dual process was not completed because aliona mziki mzito akajiuzuru

kama alionewa kama anavyosema kila siku kwenye tv na makanisani kwa nini asiende hata kesho aseme alionewa bungeni then ansard ivutwe issue irudi tena bungeni?
 
mtu wa madili na mishen town kama lowassa hainiingii akilini kuwa alikurupuka kujiuzuru sema tu na ww umepokea vijisent

ndugu yangu muda bado upo na anao arudishe hiyo mada tena bungeni jamani mbona wagumu wa kuelewa mambo lol, dual process was not completed because aliona mziki mzito akajiuzuru

kama alionewa kama anavyosema kila siku kwenye tv na makanisani kwa nini asiende hata kesho aseme alionewa bungeni then ansard ivutwe issue irudi tena bungeni?

Dual process ndio nini?
 
[h=2]Serikali yagoma kueleza ugonjwa wa Mwakyembe[/h]
Mwakyembe%2818%29.jpg

Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe.



SerikaliI imekataa kutoa taarifa ya ripoti iliyopewa na madaktari bingwa wa Hospitali ya Apolo, India ambao walimtibu Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni, alipoulizwa kuhusiana na ripoti hiyo, alisema kuwa suala hilo haliwahusu na kama wameipokea hawezi kuzungumzia suala hilo.

Alisema Dk. Mwakyembe ndiye anaweza kuzungumzia na hajui kama imepokelewa au la.
"Hata kama tumeipokea sina ruhusu ya kuzungumza na kama hiyo ripoti yake mfuate mwenyewe Dk. Mwakyembe akueleze

kwani sisi hatuwezi kutaja ugonjwa uliokuwa unamkabili," alisema Nyoni.
Akizungumzia hali ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami. ambaye alikuwa India kwa matibu, alisema kuwa hali yake inaendelea vizuri, lakini alisema hana taarifa za kurejea kwake.

Hivi karibuni, Dk. Mwakyembe alisema hospitali ya Apollo alikokuwa amelazwa alikuwa, imetuma ripoti kwa serikaali ya Tanzania kueleza walichobaini baada ya kumfanyia uchunguzi.



CHANZO: NIPASHE​
 
Nashauri Dr . Mwakyembe atoe ultimatum kwa serikali kuwa isipotoa tamko kuhusu ugonjwa wake kufika muda fulani i.e 5[SUP]th[/SUP] January 2011, basi yeye ataitangaza ripoti ya ugonjwa wake. Hebu awasikilize hata wanafamilia na rafiki zake, na ndugu ambao wanataka aweke wazi ripoti ya ugonjwa wake kama alivyofanya kuhusu ajali na ''Alshababy"

Serikali imetoa tamko muda mwafaka, kama sijakosea tarehe tano (5) ni kesho kutwa- stay tuned...............
 
Tanzania ni nchi ya amani tena yenye kuheshimu misingi ya demokrasia kwa nchi na wananchi wake.Kila mmoja ana haki sawa ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake kwa mujibu wa sheria.Kila mwananchi anayo haki sawa na uhuru wa kutoa mawazo yake bila kuvunja sheria kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 18.Pia ukisoma madaraka ya bunge katika katiba ya jamhuri wa muungano utaona kwamba, bunge ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka,kwa niaba ya wananchi,kuisimamia serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba ibara 63(2).Pamoja na maelekezo haya ya bunge serikali inachelea kujibu hoja na majukumu iliyoagizwa kuyatekeleza na bunge hili.

Nimetanguliza nukuu za katiba yetu kutokana na serikali yetu kushindwa kutekeleza ama kukaidi kwa makusudi kabisa maazimio ya bunge bila kujali kodi za wavuja jasho wa nchi kwa kuunda tume zisizo na tija.Kitendo cha serikali yetu kupuuza maagizo ya bunge ni uvunjaji wa katiba ya Jamhuri ya Muungano,kama ibara ya 63(2) kinavyozungumza.Napenda kuungana na mh. Mnyika kumsihi mh.Spika wa bunge si vyema suala la Richmond kuachiwa hivi hivi likapita bila kujua nini hatima ya mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali katika kuhakikisha haki inatendeka.Ukimya huu wa bunge kusimamia serikali kutekeleza maazimio ya bunge ni aibu kubwa kwa bunge na wabunge wake.

Wote ni mashahidi,wakati mh. Lowasa alipopewa nafasi ya kuchangia hoja kutokana na kashfa ya sakata la Richmond,alisema kilichokuwa kinatafutwa ni uwaziri mkuu,sasa basi kwa mantiki hiyo na ukimya wa bunge,tunaamini kweli kilichokuwa kinatafutwa kilikuwa ni wadhifa wa mtu na si sakata la Richmond ndo maana hakuitwa na tume ya mh.MWAKYEMBE kujibu tuhuma zilizomkabili.Kitendo cha serikali kushindwa kuwajibisha watendaji wake kama ilivyoagizwa na ukimya wa bunge ni ishara tosha bunge lilitumika kukandamiza haki ya raia wake kwa chuki binafsi.Mbaya zaidi kitendo cha bunge kulifunga rasmi suala la Richmond bila kujua hatima yake ni uonevu mkubwa uliofanywa katika kuchafua utu na heshima ya mh,Lowasa.Na kwa mantiki hiyo tunalitaka bunge limuombe radhi muathirika huyo wa siasa za makundi ndani ya chama chake ama litoe ultimutum kwa serikali kwa kushindwa kutekeleza maazimio yote iliyoyapokea toka kwa mhimili huo wa bunge.Hoja iliyoko hapa si kumtetea mh.Lowasa,la hasha bali ni kuona haki ikitendeka kwani sheria ni msumeno.

Serikali kama ilishindwa kutekeleza maagizo iliyopewa na bunge letu,aidha kwa kuona kuna uonevu uliotokea,ingewasilisha taarifa rasmi za utetezi wa watendaji wake kuliko kunyamza kimya,ilihali watendaji wake wamevuliwa utu wao.Kitendo cha serikali kukaa kimya ni ishara mbaya na taswira chafu mbele ya wananchi wake.Tunaomba serikali kupitia waziri husika wa bunge na sera kutoa taarifa juu ya uwajibikaji wake katika sakata hili.Kushindwa kwa serikali kutekeleza maazimio ya bunge,na bunge kukaa kimya ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu.Kama kweli ule usemi usemao funika kombe mwanaharamu apite ulitimia,sasa tunaitaka serikali na bunge kupeleka hoja ya dharura kumuomba radhi mh.Lowasa.

Mh. Lowasa ni wakati wako sasa kwa kuungana na waheshimiwa wabunge walionyesha nia ya kutaka hoja ya Richmond kurudishwa bungeni umefika.Hapo hata ile natural justice ambayo hukutendewa,utaipata. Fursa ya kuelezea umma wa Watanzania nani hasa mhusika mkuu wa Richmond.Kauli yako inasubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi wa nchi yako ambao uliapa kuwatumikia kwa uadilifu na kumtaka Mungu akusaidie.Ukiwa muumini katika kusimamia ukweli bila kumung'unya maneno kama ulivyofanya kwenye NEC,utakuwa umejijengea heshima kubwa zaidi ya kujiuzulu na kufanywa mbuzi wa kafara.kama lengo lilikuwa kukinusuru chama na serikali yako,wote wamekugeuka!

Nawakilisha
 
Mkuu we have so many issues to discuss

1.Lowassa kiherehere chake ndicho kilimuondoa u-PM, angeweza kutojiuzulu na hakuna yeyite angemfanya chochote!
2.Richmond ndiyo ikawa dowand ndiyo symbion!!! inaonyesha hakuna tatizo
3. naona unataja katiba, serikali ya tanzania chini ya ccm na wabunge wake hawafuati katiba so you are wasting your valuable time
4. Kikwete anajua A-Z ya richmond, Lowassa kiserikali aliishajihukumu, unafikiri kuwa nn kitafanyika
5.mwakyembe mnafiki hakusema kila kitu
6. mitandao ilikuwa kazini je leo haipo

issue hii imetokea lini? unataka isemwe leo

ondoa ccm madarakani utamu wa yote haya utakuja tu ccm isipokuwepo madarakani

sawa??
 
Ni wakati sasa wa richmond kurudi bungeni na natural justice kuchukua mkondo wake

Mkuu, bunge lipi unaloliongelea hapa, hili linaloongozwa na Makinda au lipi? Natural justice? Dont make me laugh! Kama hata wananchi wenyewe wanapopewa rungu waweze kuitetea haki, wanachagua kuipa kichapo, utegemee nini? Haya ya Richmond yangekuwa historia kama wananchi hawakuchagua hovyo mwaka 2010 lakini WaTZ? mmh, wewe wasikie tu!
 
[QOTE=Kiranga;3022428]Tukienda kwa first principles, huwezi kuandika ripoti bila kumpa mtu nafasi ya kujieleza. Hiyo ni fundamental principle ya fair hearing, ina maana hiyo ripoti imeandikwa bila kumsikiliza Lowassa.

Sisemi kwamba Lowassa ni safi, nasema katika kuandika ripoti Mwakyembe alichemsha. Katika sheria unaweza ukawa una m prosecute mtu kafanya kosa kweli, lakini ukikosea steps katika kukusanya evidence unaweza kushindwa kesi mtuhumiwa akaachwa huru. kwa nini Mwakyembe hakumuhoji Lowassa? Regardless of the answer, Lowassa amepewa mwanya wa kusema hakutendewa haki, kwa sababu hakutendewa.[/QUOTE]....kaka me nadhan ungejifunza vzr nadharia ya ntural justice thn njoo utoe mawazo yako
 
Back
Top Bottom