Dr Mwakyembe hapaswi kuhurumiwa, amevuna alichokipanda

Tatizo kubwa letu ni kutokutaka kuona hata mtu mwingine anapotuonesha. Hatuwezi kufika kamwe, tukiendelea kushabikia watu wanaotufanya sisi wajinga, watu ambao wanaposhindwa ndipo wanakumbuka kuwa kuna wananchi. Lakini hao si wabaya kama wale ambayo wanajaribu kuharibu majadiliano yenye lengo la kutafuta jawabu kwa kupindisha hoja na kusema mambo ya hovyo hovyo na mepesi katika koja nzito na zenye kutaka tafakuri

Anayetufanya sisi wajinga ni wewe na group lako la mafisadi, mtu mzima unakazania tu neno nakumbuka bila kusema unachokumbuka nini, huo ndo UNAFIKI mkubwa, unategemea nani mwenye akili zake timamu ataamini tuhuma ambazo hazijatajwa, mtajitahidi sana kutuharibia nchi, lakini hamtaweza kutudanganya, tuna uwezo wa kufikiria kuliko mnavyodhani, labda mtawadanganya wachache tu.
 
Dont hit around the bush weka mambo hadharani tujue mabaya ya mwakyembe naona umeongea mambo mengi lakini umeshindwa kuanika uovu wa mwakyembe au umetumwa nini.
 
Umenikumbusha Mugo, ni kweli ni kama story ya Ngugi. Najiuliza hivi kama kuna mtu angetokea kipindi kile ambacho Mugo anaaminika na kuheshimika kwelikweli kwa ushujaa ambao hakuufanya akasema aliyemsaliti Kihika ni Mugo watu wamgekubali? Namuheshimu sana Ngugi, ama kweli yeye ni nabii
Ni kweli! Wakati Kihika amezungukwa na Mabaunsa ghafla anajitokeza Mugo...Namhurumia sana Dr Mwakyembe. Lakini nalazimika kukumbuka siku ile ya kuhitimisha ripoti ya Richmond. Nilihuzunika sana, Niseme tu nilikata tamaa na siasa za Tanzania. Namkumbuka Fred Mpendazoe ambaye alisema atajaribu kuukumbatia mbuyu hata kama wengine walikuwa wanauzunguka akiwemo Spika Sitta. Namkubuka Ole Sendeka na Anne Kilango walivyokubali kuwa kufa kikondoo. Kwa hali ilivyo sasa namuombea Mwakyembe apone lakini naamini atatuambia nini alificha na kwa Maslahi ya nani kwenye ile ripoti yake.
Naamini pia atatuambia nini maana ya Richmond haramu, Dowans haramu na Symbion halali?
 
umeongea muzuri sana . Amevuna alicho panda.
 
Huyu aliyenzisha thread hii ni wale cheap ones wanaondesha maisha yao kwa usuru mdogo wa kulipwa na kina lowassa,days are numbered and what ever goes around comes around my dear either in the same way or otherwise,chain yote waliohusika polisi usalama na vibaraka wengine dhambi hii ya utumishi kwa ujira wataulipa kwani mzimu wa tendo hilo wanatambea hao,hata akifa mwakyembe his spirit will prevail in a good manner siyo ya lowassa
 
Nimesema humu mara kadhaa na hapa narudia tena, Mwakyembe atateseka sana, hafi upesi, atapukutika kidogo-kidogo kwa dhulma aliyowafanyia Watanzania huku anacheka kwa madoido na mbwembwe, yote hiyo akitazama maslahi yake binafsi. Huyu hana cha sumu wala nini, Hiyo ni laana ya Mwenyeezi Mungu. Na ataishi muda mrefu akipukutika kidogo kidogo na kila anapoendelea kudanganaya ndio mambo yanazidi hayapunguwi.

Hiyo mitambo aliyofanya kila hila isiwashwe, mbona leo ipo na inadunda kama kawa? au Kilintoni kawanyamazisha?
 
Mngepata kujua Dini za hao wanaosapoti hoja za mwanzisha hii sred iliyojaa kila aina ya dalili za ujambazi wa kigaidi ndo mngeshangaa na kuamini kuwa hata darasani watu hao wapoje
 
Mtanunuliwa sana na mafisadi kwa ubinafsi wenu na unafiki.
Natamani haya mateso ya Mkyembe ungeyapata wewe halafu useme umevuna ulichopanda

Wa TZ tusiwe wabinafsi kupita kiasi kumbuka usemi usemao leo kwa mwenzako kesho kwako.

Tushiriki pamoja kumuombea mwenzetu na kukemea kwa nguvu zote haya maovu yanayo endelea yashindwe!
 
sasa we uliyeweka hii thread unatofauti gani na aliyuosema Masaburi kuwa utakuwa ndio unachotumia kufikiri....unakumbuka kebehi na kurudia neno hilo mara zaidi ya 4 halafu husemi kebehi hizo sana sana umemtaja Ulimwengu, kwani ulimwengu ni nani kwenye siasa ya Tanzania??
Unajaribu kuwa"derail" watu kwa maoni yako hilooooooooooooooooo usidhani hii forum wanaingia ma zero brain mkubwaaaaa!!!!
 
Pole sana ndugu yangu unafanya speculation sehemu ambayo haihitajiki kabisa. Acha kumshabikia mtu, kuwa objective, umsifie na kumpongeza mtu kwa mazuri anayoyafanya na umkosoe kwa mabaya yake. Tuache ushabiki, tusishabikie tu na wala tusijaribu kuweka kambi kila jambo linalogusa maslahi ya nchi yanapoongelewa. Hebu jiulize swali wewe mwenyewe je unadhani kuna mwanasiasa yeyote mwenye dhamira ya kweli ya lutukomboa wanyonge wa nchi hii tukapata neema? Unamwona yeyote bila kujali anatoka chama gani? Tuache itikadi na ushabiki, kama yupo tummunge mkono na kumpa ajenda zetu, kama hayupo tujiulize tutampata wapi? je nani atamtengeneza? Je tutasubiri azaliwe? Shida hzina vyama, mgomo wa madaktari hauchagui unashabikia upande upi, elimu mbovu inatuathiri sote, kosefu wa madawa mahospitali ni wetu wote, wao wakilishana sumu wanaenda appolo, sisi tukila sumu bahati mbaya tena kwenye uyoga au kasa tunakufa. Tunazikana bila kuulizana wewe chama gani, tunakaa matanga pamoja huku tukitafuta maji na kuni za kupikia wafiwa. Wakija na Ma land Cruiser yao kutupa pole na kilo mbili za sukari wanakaa dakiak tano haooo wanaondoka, wanamikutano muhimu sisi twabaki kushabikia,wamelishana sumu! upuuuzi mtupu.

Mara useme acha kumshabikia mtu, mara msifie mtu, mara usifanye speculation, mara be objective, vp umegoma kujielewa? Au?
 
Wacha matusi na ushabiki usio na maana, Mwakyembe alimwaga damu lini kupigania haki za wanyonge?
Proposition na presentation ya mada ni tusi tosha linalostahili an eaqual and opposite response.
Tatizo ni kuwa ni ma great thinker tu wanaoweza ku read between the lines
To that end unastahili pole tu.
 
sosoliso hembu rudia tena kuyasoma vizuri na taratibu maandishi ya Domokaya na utayaelewa vyema. Indirect inasaidia kufikirisha, usitake kutafuniwa kilakitu, ubongo wako utalemaa.
Mkuu Domokaya unahoja. Sifurahii bmwanadamu mwenzangu awaye yeyote kuumia namna ile, bali wengine walio kwenye mkondo huo wajifunze kutokana na makosa ya wenzaao, tusisubiri mpaka yatukute. Unafki haufai hata kidogo. Tuwe na nia ya dhati inayotoka mioyoni mwetu ya kuliinua taifa letu.
Tusiwatendee wengine vibaya, na tuenende kwa haki.
Usikubali kujiunga na genge lolote lenye nia mbaya kwa awaye yeyote. Tusimamie haki maana kwa haki kamwe hatutoumbuka.
Kumbuka ukijiunga na genge lauhalifu ukawa mmoja wao, baadae ukijifanya unalipinga kwakuwa umepunjwa mahali ujue hauto poana na nivigumu kulishinda.
Nibora kuyapiga vita hayo magenge tangu awali tukiwa wasafi.

Mkuu nimependa hoja zako. Mtu yeyote anayejiita Great Thinker na anaingia ktk Jukwaa la Siasa anaponda hoja za mleta thread kwa matusi na kashfa basi huyo bado ni mchanga sana ktk siasa za nchi yetu. Kama hujaelewa anazungumza nini basi tafuta habari kamili ya hizo hints ameongelea. Utajiita vipi msomi kama unataka tafunikiwa kila kitu?
 
pole sana dr mwakyembe. wewe ni jasiri usiyeogopa fisadi. usingesoma ile ripoti tungejuaje mafisadi wa nchi hii. mungu akuponye wanaochekelea taabu zako washindwe na walegee. endelea kumtegemea muumba wako utapona.
 
mbona husemi hizo kebehi alizosema,hayo maneno machafu dhidi ya wananchi,..eti unayakumbuka maneno yote halafu huandiki hata neno moja,..hakuna point yoyote mpya uliyoandika hapo...tuambie alikebehi kwa maneno gani,.sio ili mradi kila mtu aandike kitu kuhusu mwakyembe...
Pale Ubungo Plaza Mwakyembe alikuwa mmoja wa wanaotaka waongozewe mishahara ,wandishi walipolalamika aliwaambia wao ni UPE (uandishi pasipo elimu).
Pia uliza kwanini hajaenda huko Kyela,ingekuwa hapo zamani pamoja na kuumwa angeshaenda Kyela
 
Nakuunga mkono, 80%, ila umesahau kuwa ana share kubwa sana katika kampuni fulani ya kufua umeme. Natumai itakuwa fundisho kwa wengine.

inafua umeme kijiji gani na megawatt ngapi inachangia kwenye gridi ya taifa iyo kampuni ya kina mwakyembe??
 
Pale Ubungo Plaza Mwakyembe alikuwa mmoja wa wanaotaka waongozewe mishahara ,wandishi walipolalamika aliwaambia wao ni UPE (uandishi pasipo elimu).
Pia uliza kwanini hajaenda huko Kyela,ingekuwa hapo zamani pamoja na kuumwa angeshaenda Kyela

mbona lowassa hajaenda kumpa pole,unadhani kwanini?
 
Ni kweli! Wakati Kihika amezungukwa na Mabaunsa ghafla anajitokeza Mugo...Namhurumia sana Dr Mwakyembe. Lakini nalazimika kukumbuka siku ile ya kuhitimisha ripoti ya Richmond. Nilihuzunika sana, Niseme tu nilikata tamaa na siasa za Tanzania. Namkumbuka Fred Mpendazoe ambaye alisema atajaribu kuukumbatia mbuyu hata kama wengine walikuwa wanauzunguka akiwemo Spika Sitta. Namkubuka Ole Sendeka na Anne Kilango walivyokubali kuwa kufa kikondoo. Kwa hali ilivyo sasa namuombea Mwakyembe apone lakini naamini atatuambia nini alificha na kwa Maslahi ya nani kwenye ile ripoti yake.
Naamini pia atatuambia nini maana ya Richmond haramu, Dowans haramu na Symbion halali?

piga, pasua kichwa hatokaa ayanene tena aliyoyabakìza mpaka anakuwa mavumbi. Iwapo alipopata nafasi ya kurudi akipumua,akadiriki kusema,nanukuu moja ya kahuli zake "namuachia mungu". Tutegemee jipya lipi hapa??
 
Hakuna alichoficha zaidi ya kuwa yeye alikuwa akiyafanya aliyoyafanya kwa maslahi yake binafsi. nyie mnafikiri ana jipya lingine la kuongeza? sana sana aje kuungama na kukiri kuwa aliwahadaa wa Tanzania kwa tamaa yake binafsi.
 
watu bwana.. hujaona kabisa dr mwankyembe alichoifanyia tz.. tena naamini angeendelea kuwa mwalimu asinge fanya chochote kikubwa zaido ua kuifanyi akazi tu CCM kama huyo ndugu yenu Mkandara/Mukandara(rekebisha mwnyw).. yani we unawafagilia sana hao waalimu wenu wanaowafelisha na kuwalala wanafunzi ili wafaulu????

tafuta huyo mwanasiasa unaemfikiria ambae angesoma ile report kama mwankyembe... MNATAKA MFANYIWE NINI???????

kusema kweli hata mimi sijaona chochote cha "maana" na cha "kukumbukwa" alichoifanyia tz.................. kama ni "kusoma" ripoti mbona hata mimi wangenipa ningesoma!!................... kusoma tu??................. hilo tu ndiyo tumkumbuke na kumshukuru na kumtukuza kama shujaa??................... kwani alitusomea hiyo ripoti bure?? ..................hakulipwa mshahara wake??.................... tena na posho mbilimbili juu!!..................... wangapi wanasoma ripoti kila siku?.................... hata leo kuna nyingine zinasomwa!!....................

kama tutaanza kufunua madudu yote aliyoshiriki kuyafanya akiwa kwenye bodi ya NBC................... nadhani hata nyie mnaomuona shujaa mtanyanyuka kumpiga mawe.........................

tena usitukumbushe jinsi alivyonyofoa nusu ya ripoti na kuificha kisha akaja kutusomea ripoti yake feki!....................... wakati watu wanawakaba kina rostam na lowasa mashati.................. yeye huyooooo kaenda kuanza uzalishaji wa umeme wa upepo bila kutangaza maslahi katika biashara ya nishati kinyume cha kanuni za bunge!!................... hivi nao kama si ufisadi mnaoupigia kelee hapa kila siku, ni nini basi??......................

mi nafikiri muhimu ni kumuombea apone haraka kwa sababu za kibinadamu................. ila hilo la kutaka tumuone shujaa hapa na kumtukuza, nasema nooooo.........................
 
Back
Top Bottom