Dr Mwakyembe hapaswi kuhurumiwa, amevuna alichokipanda

Ajabu sana utakuwa umetumwa na mafisadi tu. Kuna hela nyingi zilitengwa kuwasafisha mafisadi kama bwama Manyama yeye kazi yake ni kumkosoa Sita, Mwakyembe na wengine na kumpamba mwenye mvi mwizi wa kutupwa. Anajjita mwalimu wa watu!
Weka tone kidogo tu la fikra kichwani mwako. Bila shaka unawafahamu hao wanaoitwa nafisadi wapo katika chama gani na serikali gani. Jiulize sasa kwa nini wao bado wako nao? Jiulize je hilo la hao kuwa mafisadi wamelifaha,u limi? Je wewe kuwafahamu hao jamaa ni mafisadi ilikuwa baada ya kuambiwa na makamanda wa mafisadi? Je hawa jamaa hawakuwahi kuwa pamoja? Halafu utaamua kuacha ushabiki na utafanya uchambuzi wa kina.
 
Aliyoyasema yapo, yaliandikwa kwenye magazeti na yalijibiwa na watu makini, kama wewe hukuwepo angalau basi upate nafasi ya kufanya utafiti, lakini kama moyo wako utaridhika kwa kusema mleta thread hii ni mzushi haya sitakuwa na la kukusaidia

Wewe mtoa hoja ndio utuletee nukuu za hayo maneno aliyosema sio kuzunguka zunguka hapa!
 
tatizo kubwa letu ni kutokutaka kuona hata mtu mwingine anapotuonesha. Hatuwezi kufika kamwe, tukiendelea kushabikia watu wanaotufanya sisi wajinga, watu ambao wanaposhindwa ndipo wanakumbuka kuwa kuna wananchi. Lakini hao si wabaya kama wale ambayo wanajaribu kuharibu majadiliano yenye lengo la kutafuta jawabu kwa kupindisha hoja na kusema mambo ya hovyo hovyo na mepesi katika koja nzito na zenye kutaka tafakuri

huyu mtu kwa ubaya wake na unafiki wake ndiye anajivua ngamba kikweli kweli
na hakika mnafiki moto anauona hapa hapa duniani sasa yeye anajifanyianya eti
ana uchungu na tz watu wanaiba matrilion kwenye mafuta na yeye yupo awasemi
tanzania ni shamba la bibi kila mtu mwizi
 
Narudi nyuma miaka kadhaa wakati DR Mwakyembe alipoona siasa inalipa kuliko taaluma alipoamua kukimbia chaki Chuo Kikuu cha Dar es laam na kwenda kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. Mwakyembe kwa kutaka kupendwa na chama chake aliyatamka maneno ambayo yalikuwa dhihaka kwa wananchi wa nchi hii, maneno ambayo, yaliidhalilisha taaluma yake, maneno yaliyodhalilisha wasomi na maneno yaliyodhalilisha jumuiya ya chuo kikuu cha Dar es salaam. Aliyasema hayo kwani alijua chama chake kinapenda kuyasikia, na alisema akijua akiyasema hayo atapata nafasi moja ya kuwa mbunge kilaini.

Nakumbuka yote, nakumbuka kila kitu. Nakumbuka hasira za wenye tafakuri nziti zilivyomrukia na kumsuta, alionekana dhahiri anajitongozesha kwa gharama ya wananchi kuumia ili yeye aneemeke. Nakumbuka jinsi alivyomuudhi Jenerali Ulimwengu hata wakaanza kujibizana kwa kalamu na maneno ya vinywani.

Nakumbuka, sijasahau ni Dr Mwakyembe huyu huyu chaguo kipenzi cha CCM. Alishirikiana nao kuwagandamiza wananchi, akataka kwenda mbali kushiriki zaidi kuwagandamiza ili aendelee kufaidi na kuneemeka yeye na familia yake. Alipowekewa kigingi akijifanya yeye na wanafiki wenzake eti wanatetea wananchi. Kumbe wapi wamekutana na kichaka cha simba sasa wanataka sapoti ya kukishinda, wote wao na kile kichaka lengo lao ni kutufanya kitoweo.

Dr Mwekyembe ni mmoja wa watengenezaji mifumo hiyo michafu na ya kinyama ambayo leo imemrudi yeye mwenyewe. Wanajua na wanajuana namna ya kuzitengeneza hizo sumu na kuwalisha sijui kuwagusisha watu. Wameshawau wengine wengi tu leo imefika zamu yao wanapiga kelele.

Wenye kumbukumbu nzuri watakubaliana nami kuwa Mwenyekiti wa CCM alilizungumzi hili katika sherehe za kuzaliwa chama mwaka juzi. Alisema wazi watu ndani ya chama wamehasimiana kiasi cha kushindwa kuachiana glasi mezani.

Hivyo ndivyo siasa za CCM zilivyo na kila mwenye upeo kidogo tu anafahamu hilo achilia mbali DR wa sheria. Ukiwa nao fanya kama wanavyofanya wao na malengo ya chama chao. Uongo, uzandiki, wizi, uzabizabina, kujipendekeza, ulafi, majivuno, dharau na uchafu mwingine mwingi waufanyao. Ukikiuka haya umekiuka miiko, umekuwa msaliti lazima uadhibiwe.

Kuna waliosema chama kimekosa dira na mwelekeo wakakiona cha moto. Kuna alioaga kwenda London eti akirudi awaambie watanzania ukweli kuhusu nchi yao ilivyotafunwa na kubaki makapi, lakini thubutu yake hakurudi. Mifano ni mingi hata ile ya waliotaka kusema ukweli kuhusu jambo fulani wote wamepotea, kuanzia Stan Katabalo mpaka ile tume ya unga wa ngano wa sumu, tume nzima ilipotea. Walipita kulalamika kuwa wanataka kuuliwa hakuna aliyewasikiliza, wakaishia. Yote haya Mwakyemba anayafahamu na bado akaenda kujiunga na kusaidia kutekeleza haya, sasa leo zamu yake anang'aka. Anang'aka nini mwache aone shida wanazopata watanzania wengine ambayo kwa sababu ya yeye na wenzake kujenga mfumo wa kidhalimu kuna watanzania wanakufa kwa kukosa barabara za kuwafikisha mahosipitalini, aone jinsi watanzania wanavyojilundika hospitalini wakisubiri vifo vyao huku wakipozwa na panadol, bora yeye amepelekwa Appolo.

Hili liwe fundisho kwa watu wote wenye kutumia migongo yetu wanyonge kujipatia nafasi ya kujilimbikizia mali na madaraka. Kuna siku madaraka na mali havitatosha sasa wataanza kunyang'anyana walivyopeana kwani kila mtu atataka kumzidi mwenzie. Mbinu zingine zinaposhindikana na msaliti anapoelekea kutoa siri ndipo watarudi kwenye ile mbinu yao ya "Costra Nostra" maiti haisemi.

Dr Mwakyembe na wenzake wasilie kama zamu yao imefika basi wajue kuwa hata wenzao waliowatanguliza walipitia machungu hayo hayo, zaidi wajue kuwa maisha ya watanzania waliootaabika na kufa kwa ajili ya udhalimu wao ni dhaidi ya wao kunyweshwa sumu. Wanavuna walichopanda
era na katiba ya CCM siyo hiyo uliyoanisha hapo ya Uongo, Uzandzki, wizi, ulafi, majivuno, dharau na uchafu mwingine unaoujua wewe. Kwa mtazamo wangu mimi naona Mtanzania msomi anapenda prestige, si muwazi, hapendi wenziwe wawe na elimu kama yake, na siyo mbunifu. Mfano Mkoa wa mbeya una madini ya zinc,copper, silver,gold, tantilite,neobium, chuma,nickel iliyo ndani ya copper ore n.k. kwa sababu ndani ya bunge hakuna wabunifu kusaidia jamii , wao hukimbilia kutwaa maeneo yenye madini kwa majina yao au ya ndugu zao, kisha hukimbilia bungeni kuimba wimbo wa uwekezaji ili wapate 10% tu. kwa upande wangu huu ni uvivu. Lakini ukiwaelimisha wananchi wakachimba wenyewe na kuuza kwa serikali mfano, tuseme serikali ichukue % kutoka kwa local wachimbaji au wachimbaji wawe watanzania na wawekezaji wawe wakutoka nje lakini hawaruhusiwi kuchimba, wanunue kwa wachimbaji Watz. Ninamaana iwe kama hivi WACHIMBAJI LOCALS-----SOKO LIJENGWE NA SERIKALI------WAWEKEZAJI WANUNUE MALIGHAFI SOKONI-------UTAONA MBEYA ITAKUWA LONDON METAL EXCHANGE MARKET YA AFRICA. lakini huku kutiana sumu nani awe nani haina faida kwa taifa letu lenye rasilimali kibao ambazo wote tutazifuata huko baada ya kufukiwa ardhini.
 
1. alitoa kebehi kwa taaluma yake..
2. akagandamiza wananchi..
3. mmoja wa watengenezaji wa mifumo michafu na ya kinyama..

kwenye red mbona imekuwa tofauti..? so kosa kubwa la Dr. Mwakyembe ni kuingia kwenye chama na kujaribu kupambana (kwa mujibu wa andishi lako) dhidi ya hao mafisadi..? kwa hiyo kwako ww wale wote wanaonekana kutaka kupigania wanyonge wanastahili hili alilolipata Dr na hao wengine uliowataja..? ingekuwa vzuri kama ungejiweka wazi..

Maswali mazuri. Tukiendelea kujiuliza zaidi tutapata majibu ya maana. Dr aliingiaje kwenye Siasa, alikuwa na nafasi gani katika kundi la wanamtandao, kipi kilichowaunganisha yeye, Sitta na wengineo. Je aliufahamu ufisadi kabla ya kuingia ndani ya chama? je alizifahamu mbinu hizi chafu za mafisadi aliojiunga nao kabla au alizifahamu baada? Kama alizifahamu kabla kwa nini asiseme kabal hajajiunga ilhali wakati huo fisadi mkubwa wakimfanya mweka hazina wa chama?

Je taarifa za Richmond alizotoa ni zote au kuna alizobakiza? Kama zipo zilizobaki je aliingia deal yeyote na mafisadi iwe chini ya kivuli cha chama au serikali? Nini yalikuwa makubaliano? Je hayo makubaliano yalikuwa yana faida yoyote kwa wananchi?
 
era na katiba ya CCM siyo hiyo uliyoanisha hapo ya Uongo, Uzandzki, wizi, ulafi, majivuno, dharau na uchafu mwingine unaoujua wewe. Kwa mtazamo wangu mimi naona Mtanzania msomi anapenda prestige, si muwazi, hapendi wenziwe wawe na elimu kama yake, na siyo mbunifu. Mfano Mkoa wa mbeya una madini ya zinc,copper, silver,gold, tantilite,neobium, chuma,nickel iliyo ndani ya copper ore n.k. kwa sababu ndani ya bunge hakuna wabunifu kusaidia jamii , wao hukimbilia kutwaa maeneo yenye madini kwa majina yao au ya ndugu zao, kisha hukimbilia bungeni kuimba wimbo wa uwekezaji ili wapate 10% tu. kwa upande wangu huu ni uvivu. Lakini ukiwaelimisha wananchi wakachimba wenyewe na kuuza kwa serikali mfano, tuseme serikali ichukue % kutoka kwa local wachimbaji au wachimbaji wawe watanzania na wawekezaji wawe wakutoka nje lakini hawaruhusiwi kuchimba, wanunue kwa wachimbaji Watz. Ninamaana iwe kama hivi WACHIMBAJI LOCALS-----SOKO LIJENGWE NA SERIKALI------WAWEKEZAJI WANUNUE MALIGHAFI SOKONI-------UTAONA MBEYA ITAKUWA LONDON METAL EXCHANGE MARKET YA AFRICA. lakini huku kutiana sumu nani awe nani haina faida kwa taifa letu lenye rasilimali kibao ambazo wote tutazifuata huko baada ya kufukiwa ardhini.
Bravo. Hilo ndio la maana hasa, wote hawa wezi tu, watiliane sumu hata waogeshane sumu, hatupaswi kuwahurumia bali tushukuru Mungu anawaumbua na sasa zile zilizokuwa siri zao wanaziweka hadharani. Hawana lolote, wameongoza miaka kibao bila impact yoyote sasa wanataka tuwahurumie na tuwashabikie katika vita yao ya kulishana sumu. Walishane tu, hamna mwenye huruma na sisi, wote ni mafisadi, wapo chama kimoja na serikali yao, wamezoea kuwalisha wenzao sasa wakilishwa wao wanpiga kelele.
 
Wewe std seven? Najua ni ticha kihiyo wa udsm haueleweki kabisa. Ebu rudia uone umeaddress nini kwenye post yako. Sisi regardless what as long as Dr. bado anaumwa priority ni kumuombea uzima mambo mengine na kama kuna jambo subiri apone um-face.

Narudi nyuma miaka kadhaa wakati DR Mwakyembe alipoona siasa inalipa kuliko taaluma alipoamua kukimbia chaki Chuo Kikuu cha Dar es laam na kwenda kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. Mwakyembe kwa kutaka kupendwa na chama chake aliyatamka maneno ambayo yalikuwa dhihaka kwa wananchi wa nchi hii, maneno ambayo, yaliidhalilisha taaluma yake, maneno yaliyodhalilisha wasomi na maneno yaliyodhalilisha jumuiya ya chuo kikuu cha Dar es salaam. Aliyasema hayo kwani alijua chama chake kinapenda kuyasikia, na alisema akijua akiyasema hayo atapata nafasi moja ya kuwa mbunge kilaini.

Nakumbuka yote, nakumbuka kila kitu. Nakumbuka hasira za wenye tafakuri nziti zilivyomrukia na kumsuta, alionekana dhahiri anajitongozesha kwa gharama ya wananchi kuumia ili yeye aneemeke. Nakumbuka jinsi alivyomuudhi Jenerali Ulimwengu hata wakaanza kujibizana kwa kalamu na maneno ya vinywani.

Nakumbuka, sijasahau ni Dr Mwakyembe huyu huyu chaguo kipenzi cha CCM. Alishirikiana nao kuwagandamiza wananchi, akataka kwenda mbali kushiriki zaidi kuwagandamiza ili aendelee kufaidi na kuneemeka yeye na familia yake. Alipowekewa kigingi akijifanya yeye na wanafiki wenzake eti wanatetea wananchi. Kumbe wapi wamekutana na kichaka cha simba sasa wanataka sapoti ya kukishinda, wote wao na kile kichaka lengo lao ni kutufanya kitoweo.

Dr Mwekyembe ni mmoja wa watengenezaji mifumo hiyo michafu na ya kinyama ambayo leo imemrudi yeye mwenyewe. Wanajua na wanajuana namna ya kuzitengeneza hizo sumu na kuwalisha sijui kuwagusisha watu. Wameshawau wengine wengi tu leo imefika zamu yao wanapiga kelele.

Wenye kumbukumbu nzuri watakubaliana nami kuwa Mwenyekiti wa CCM alilizungumzi hili katika sherehe za kuzaliwa chama mwaka juzi. Alisema wazi watu ndani ya chama wamehasimiana kiasi cha kushindwa kuachiana glasi mezani.

Hivyo ndivyo siasa za CCM zilivyo na kila mwenye upeo kidogo tu anafahamu hilo achilia mbali DR wa sheria. Ukiwa nao fanya kama wanavyofanya wao na malengo ya chama chao. Uongo, uzandiki, wizi, uzabizabina, kujipendekeza, ulafi, majivuno, dharau na uchafu mwingine mwingi waufanyao. Ukikiuka haya umekiuka miiko, umekuwa msaliti lazima uadhibiwe.

Kuna waliosema chama kimekosa dira na mwelekeo wakakiona cha moto. Kuna alioaga kwenda London eti akirudi awaambie watanzania ukweli kuhusu nchi yao ilivyotafunwa na kubaki makapi, lakini thubutu yake hakurudi. Mifano ni mingi hata ile ya waliotaka kusema ukweli kuhusu jambo fulani wote wamepotea, kuanzia Stan Katabalo mpaka ile tume ya unga wa ngano wa sumu, tume nzima ilipotea. Walipita kulalamika kuwa wanataka kuuliwa hakuna aliyewasikiliza, wakaishia. Yote haya Mwakyemba anayafahamu na bado akaenda kujiunga na kusaidia kutekeleza haya, sasa leo zamu yake anang'aka. Anang'aka nini mwache aone shida wanazopata watanzania wengine ambayo kwa sababu ya yeye na wenzake kujenga mfumo wa kidhalimu kuna watanzania wanakufa kwa kukosa barabara za kuwafikisha mahosipitalini, aone jinsi watanzania wanavyojilundika hospitalini wakisubiri vifo vyao huku wakipozwa na panadol, bora yeye amepelekwa Appolo.

Hili liwe fundisho kwa watu wote wenye kutumia migongo yetu wanyonge kujipatia nafasi ya kujilimbikizia mali na madaraka. Kuna siku madaraka na mali havitatosha sasa wataanza kunyang'anyana walivyopeana kwani kila mtu atataka kumzidi mwenzie. Mbinu zingine zinaposhindikana na msaliti anapoelekea kutoa siri ndipo watarudi kwenye ile mbinu yao ya "Costra Nostra" maiti haisemi.

Dr Mwakyembe na wenzake wasilie kama zamu yao imefika basi wajue kuwa hata wenzao waliowatanguliza walipitia machungu hayo hayo, zaidi wajue kuwa maisha ya watanzania waliootaabika na kufa kwa ajili ya udhalimu wao ni dhaidi ya wao kunyweshwa sumu. Wanavuna walichopanda
 
greatsinkers wa jf hawajui ile tume ya mwakiembe kuhusu mauaji ya pemba ilisema nini.

asante ya ccm ikawa kumpa kura nyingi ubunge afrikamashariki.

shule za kata ni ukimwi wa taifa. sisi tuliosoma shule zenye mshiko tunajua mambo bana.
 
Hamna kitu hapa porojo porojo ndo zimejaa.Maneno aliyosema huweki umebaki kuzunguka tu.
 
Aliyoyasema yapo, yaliandikwa kwenye magazeti na yalijibiwa na watu makini, kama wewe hukuwepo angalau basi upate nafasi ya kufanya utafiti, lakini kama moyo wako utaridhika kwa kusema mleta thread hii ni mzushi haya sitakuwa na la kukusaidia
Sasa mkuu, umelea uzi ili twende library tukatafute magazeti ya zamani au ili iweje?
Kwa nini usifanye uungwana kuweka hayo mambo hapa, hata kwa uchache?
 
Hata kama unayoyasema ni ya kwli we mtoa mada bt mwakyembe didnt deserve this! Dont u have a sense of humanity??
 
Maswali mazuri. Tukiendelea kujiuliza zaidi tutapata majibu ya maana. Dr aliingiaje kwenye Siasa, alikuwa na nafasi gani katika kundi la wanamtandao, kipi kilichowaunganisha yeye, Sitta na wengineo. Je aliufahamu ufisadi kabla ya kuingia ndani ya chama? je alizifahamu mbinu hizi chafu za mafisadi aliojiunga nao kabla au alizifahamu baada? Kama alizifahamu kabla kwa nini asiseme kabal hajajiunga ilhali wakati huo fisadi mkubwa wakimfanya mweka hazina wa chama?

Je taarifa za Richmond alizotoa ni zote au kuna alizobakiza? Kama zipo zilizobaki je aliingia deal yeyote na mafisadi iwe chini ya kivuli cha chama au serikali? Nini yalikuwa makubaliano? Je hayo makubaliano yalikuwa yana faida yoyote kwa wananchi?

Mkuu hapa naanza kukusoma! Keep on answering...
 
Lowassa alisema namnukuu "Tatizo ni uwaziri Mkuu" .Mwakyembe na Sita walikuwa wana ajenda zao binafsi wala sio wapiganaji wa ukweli.Utasemaje Lowasa, Rostam na Chenge ni mafisadi umwache JK? .Hawa walipiga kelele wakapewa uwaziri wakanyamaza ,walichokuwa wanapigania wakawa wanakipinga bungeni bila aibu.Acha apate mshahara wa dhambi zake.

Jiulize hali ya mwakyembe ingempata moja kati ya wanaharakati/wapiganaji Dr. Slaa,Lissu,Ananilie Nkya ama K. Bisimba kusinge kalika kwa hizo kelele za wanaharakati.Ila wanaharakati wapo kimya kwa kuwa wanawajua hawa ni wanafiki maji yamewafika shingoni ndio wanakimbilia nguvu ya umma.
 
domokaya anatumia vbaya uhuru wa kuongea nna mashaka kama ametumia ubongo kufikiri. ameonyesha uzembe wa hali ya juu ktk kujaji issues hadithi yake haina mashiko nashauri afikiri kabla ya kutoa mada
 
Wewe ni tatizo na huhitajiki uwanjani na kauzi kako ka unakumbuka,unakumbuka,unakumbuka,sema watu wakuelewe,ama wewe ni tunda wa zile shule zetu zilizoanzishwa na kaka ENL kwa nguvu nyingi sana....aibu kwelkweli..Umechosha mkuu?
 
Kuna point hapo kwenye KUSAHAU kwa wabongo!

Hii nchi tungekuwa na mfumo mzuri wa media kijamii na kisiasa matukio mengi ya kisiasa yangekuwa hayasahauliki na wengi wasingekuwa hapo walipo.

Ila sio mbaya kama wewe "domokaya" utujuze hizo taarifa, sio kwa faida yetu tu bali kuweka kumbukumbu sahihi pale ambapo wabongo tunajifanya tumesahau.

Bila hivyo thread yako itapunguza uzito unaosatihiki.
 
Nafikiri Domokaya anataka turejee kwenye mauaji ya wandamanaji wa CUF mwaka 2001 yaliyoua watu 21..kama kumbukumbu ziko sahihi aliwakejeli walioshiriki maandamano hayo na kulipongeza jeshi la polisi kwamba lilifanya kazi sahihi.
Anyway mimi si shabiki wa yeyote yule (wanaomuunga mkono mwakyembe na vita ya ufisadi na wanaomponda).

Ambacho nina hakika nacho ni kwamba Watanzania tu-washabiki mno kwenye mambo ya msingi.Likitokea tukio hakuna anayepata nafasi ya kufikiri..woote tunagawanyika upande.Na wanasiasa wanatujulia sana kwa hili.

Namwombea Mwakyemba apone na arudi salama.Kwanza hilo muhimu.
 
Back
Top Bottom