kanga
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 1,025
- 494
Nimepata wasiwasi na utendaji wa viogozi wetu jinsi wanatoa maamuzi katika masuala mbalimbali.Sakata la kufukuzwa kazi kwa CEO wa ATCL hivi karibuni Eng,Chizi kwa sababu ya ukiukaji wa taratibu za ajira yake kunaacha maswali mengi kuliko majibu yanayotolewa na ofisi ya Mwakyembe.
Sababu moja kubwa ambayo Mwakyembe ameitoa akiongea na watumishi wa ATCL ni kwamba Eng. Chizi alikuwa amekwisha staafu kazi hivyo hakusathili kuajiriwa na ATCL.Sababu hii naona ni nyepesi sana kuzingatia mifano mbalimbali ambayo ipo kwa jinsi wastaafu wengi wameendelea kuajiriwa kwa mikataba ya ajira kwa kipindi cha miaka miwili au mitatu.Mfano mmojawapo ni uteuzi wa DAVID MATTAKA ambaye aliteuliwa kuwa CEO wa ATCL wakati huo alikwisha staafu kama CEO wa PPF.David Mattaka ndiye alimwachia ofisi Chizi kama mrithi wa ofisi yake kama CEO je swali kwa Mwakyembe Uteuzi wa Mattaka na Chizi una tofauti gani?.Kinachoonekana hapa ni mambo binafsi sana ndiyo yanaleta kelele zote hizi.Na kama kuna sababu nyingine ni ufisadi katika ATCL wakati wa CEO Chizi vyombo vya dola kama TAKUKURU na CAG wanatakiwa waagizwe kufanya ukaguzi maalum na siyo kuteua tume.
Inaonekana Mwakyembe ni mtu asiye jifunza na anapenda umaarufu rahis kwa vitu vyenye kuhitaji uchambuzi wa kina.Na hapa Mwakyembe akionekana ameboronga Lowasa atachekelea vizuri akimaanisha na kuthibitisha Mwakyembe alitumika kwenye Kamati ya Richmond kumuonea na nia ilikuwa UWAZIRI MKUU WAKE.:majani7: