JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,442
- 55,017
Mkandara said:Recta,
Mkuu wangu sasa hivi sina muda ila nitakujibu baadaye..(Mwakyembe vs Rostam)..
Kifupi tu kuwepo kwa watu hao (mafisadi alowatosa) ktk Central Committe ya CCM na pia members wa NEC -CCM haina maana kabisa kuwa hawa watu wana wadhifa ndani ya Uongozi wa nchi hii, hata Asha Baraka ni member wa kamati za chama.. na kuamini kwamba member wa chama CCM ni mtu mkubwa sana ni imani ya kupotosha Demokrasia inavyofanya kazi.. CCM ni chama tu kama kilivyo chama Chadema au CUF, hivyo hizo Committe zinafanya kazi za chama na wakivuruga ktk maslahi ya Taifa wanatakiwa kushtakiwa kwa taratibu sawa na raia mwingine yeyote.. Na mfano mzuri ni Chenge kama nilivyosema hapo awali..JK hakushirikishwa ktk kumkamata, na kumfungulia mashtaka kwa sababu ni member wa kamati za CCM...
Kuhusiana na Ditto, nimesema kwa Lugha ya mtaani inawezekana nikasema Mkulu alijiua kutokana na JK kumbwaga..
Recta, mkuu kwa lugha nayotumia usidhani najaribu kumlaumu JK kumbwaga Ditto isipokuwa ni kuonyesha jinsi anavyoweza kuwa tofauti na viongozi wengine waliopita na hasa viongozi wa Kiafrika..Nyerere asingeweza kumtupa Ditto, Mwinyi asingeweza na wala Mkapa asingeweza kufanya hata nusu ya aliyofanya Kikwete ktk swala la Mafisadi tena watu wake wa karibu... Pamoja na sifa zote ambazo mimi humbwagia Nyerere naelewa kabisa kuwa alikuwa akiwalinda baadhi ya watu na kila walipoharibu aliwabadilisha wizara au madaraka tu. Mwinyi ambaye alihusika na mauaji ya vizee huko Shinyanga alikuja kuwa rais wa nchi.. Lakini tunaona JK kawabwaga kabisa viongozi wote aliowaondoa ktk serikali yake na sehemu za chama ambazo ana madaraka... Kikwete hana madaraka wala mamlaka ya kuwavua Mafisadi nafasi zao ktk kamati za chama ikiwa wamechaguliwa kulingana na taratibu za chama..Yeye ni mwenyekiti tu na inatakiwa nguvu kubwa ya wajumbe kuwavua uanachama au ujumbe wa kamati hizi..nguvu hiyo hana na ndicho nachotaka kuwaambia..He is (almost) standing alone!
Hivyo tusijaribu kumbebesha mzigo usio kuwa wake...
Mkandara,
..wacha kutufanya wana JF watoto wadogo. kesi ya Ditopile ushahidi wake ulikuwa wa waziwazi. hakuna mtu yeyote yule ambaye angeweza kumuepusha Ditopile na mashtaka yale.
..lakini pamoja na kufanya mauaji yale Raisi hakumfukuza kazi marehemu Ditopile. alimsubiri aandike barua ya kujiuzulu kazi na aliikubali. Raisi huyo huyo alikataa barua ya kujiuzulu ya Daudi Balali, na kuamua kumfukuza kazi. sasa jiulize kwanini alikubali barua ya Ditopile ya kujiuzulu, lakini akakataa ile ya Balali? binafsi nasema yote hiyo ilitokana na ushikaji wake kwa Ditopile.
..zaidi dhamana ya kesi ya Ditopile ilikuwaje? sidhani kama mtu mwenye kesi nzito kama Ditopile angeweza kuwa akisafiri freely kwenda Tabora kutafuta asali, mara yuko Morogoro anakagua mashamba etc etc. je, kuna mtu mzito aliyekuwa akimlinda?
..halafu unakwenda mbali na kusema ati Nyerere alikuwa na huruma na marafiki zake. umemsahau Bibi Titi Mohamed? vipi kuhusu Oscar Kambona? Mzee Kasela Bantu, na Balozi Kasanga Tumbo?
..unaposema Mwinyi alihusika na mauaji ya vizee Shinyanga una maana gani? je kuna ushahidi kwamba aliua kwa mkono wake kama alivyofanya Ditopile? Mwinyi alijiuzulu kutokana na makosa na uzembe wa watu waliokuwa chini yake. tena wahusika wenyewe walikuwa Shinyanga na yeye Mwinyi yuko makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani DSM.
..kama unataka kumtetea Raisi Kikwete ufanye hivyo kwa kutumia maelezo yenye kueleweka. pia ingekuwa vizuri kama ungefanya hivyo bila kuanza kuwachafua wale waliomtangulia.
..yanayoendelea kati ya JK na maswahiba zake yananikumbusha ile michezo ya watoto watukutu ambapo husema hivi:-
..mtoto wa kwanza: "twende."
..mtoto wa pili: "wapi?"
..mtoto wa kwanza: "tukaibe"
..mtoto wa pili: "tukikamatwa?"
..mtoto wa kwanza: "SIMOOO!"