Dr. Maua Daftari ahukumiwa na mahakama ya Rufani

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
Jamani

Mahakama ya Rufani Tanzania imetoa ukumu ya Naibu waziri Maua Daftrai kumlipa mdeni wake 100.7M aliyemtapeli.

Je kwa hili anastahili kubaki waziri. Kosa ni wizi wa kujiaminisha.
 
angekuwa amefanyakosa la wizi angestakiwa criminal case, hii ilikuwa civil kesi, so huwezi ukasema ni wizi.
 
Jamani

Mahakama ya Rufani Tanzania imetoa ukumu ya Naibu waziri Maua Daftrai kumlipa mdeni wake 100.7M aliyemtapeli.

Je kwa hili anastahili kubaki waziri. Kosa ni wizi wa kujiaminisha.

Kibongo Bongo Atapeta tu
 
Kama serikali ingekua na tabia uwajibikaji wa pamoja kwa kuwa aliyetapeli ni waziri maana yake ni kwamba barara la mawaziri ni tapeli na hivyo halipaswi kuaminiwa. Kitendo pekee cha kuitakasa hii cabinet ni kwa Maua kujiuzulu. Na kama atakaidi inapaswa mkuu wake wa kazi kumwajibisha ikiwa naye atakuwa hataki kufanya kazi na matapeli.
 
Jamani

Mahakama ya Rufani Tanzania imetoa ukumu ya Naibu waziri Maua Daftrai kumlipa mdeni wake 100.7M aliyemtapeli.

Je kwa hili anastahili kubaki waziri. Kosa ni wizi wa kujiaminisha.
Kumradhi wakuu,

Dr. Maua Daftari alifanya kosa gani hasa? Ningependa kujua kwa undani na kesi hii ilifunguliwa lini... Huenda nimepoteza kumbukumbu lakini naamini kwa manufaa ya wengi tuwekeeni hali halisi ili tuelewe hii habari ikoje
 
Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo, Fatma alikuwa akimdai Dk Daftari Sh.210,092, 400 alizompa ili amnunulie vifaa mbalimbali kati ya mwaka 1994 na 1997, lakini mlalamikiwa hakufanya hivyo.

Vitu hivyo ni pamoja mashine ya kusindika matunda kutoka nchini Afrika Kusini, ungo (dish) la satellite, kutoka Uingereza, gari pamoja na vito vya dhahabu.

Mbali na pesa hizo taslimu, pia mlalamikaji alikuwa akimdai Dk. Daftari pesa za vitu mbalimbali alivyovichukua kwake kama vito vya dhahabu, mabati ya kujengea nyumba na milango ambavyo pia hakurudisha.

Mlalamikaji pia alikuwa akimdai mlalamikiwa pesa kiasi cha Sh200 milioni kama fidia kwa kuvunja makubaliano hayo, ambazo kwa jumla zilikuwa takribani Sh410milioni, ikiwa ni pamoja na gharama uendeshaji wa kesi hiyo.

Katika hukumu yake Jaji Kalegeya alieleza kuwa licha ya mlalamikiwa pamoja na mumewe kukataa madai hayo katika utetezi, walionekana kuwa ni matapeli.
 
Hukumu ya mahakama ya rufaa imeripotiwa na daiynews:

=========

High Court orders Daftari to pay businesswoman 100m/-

By CONSESA JOHN,
9th July 2010

THE High Court of Tanzania on Friday ordered the Deputy Minister for Communications, Science and Technology, Dr Maua Daftari, to pay a businesswoman, Fatma Salmini, 100,760,000/-.

Judge Fedrica Mgaya also ordered Ms Daftari to pay seven per cent of the said money starting from yesterday until when she will finish paying the claimant the whole amount. She was also ordered to pay all the costs of the case. In his judgment, Judge Mgaya said that it was evident that Dr Daftari owed the claimant and therefore she had to pay her back.

The judge ruled that although there was no direct evidence, details given by the claimant proved that the two had relations and the respondent received money from the claimant. In the case, the claimant demanded 500m/- she had given Dr Daftari so that the respondent could import some goods on her behalf, something which the respondent failed to do and failed to refund the claimant.

According to charge sheet, the claimant told the court that Dr Daftari convinced her she was able to import a fruit processing plant, vehicle spare parts and other equipment which, however, she failed to import despite having been given the money.

Earlier, the High Court under judge Laurean Kalegeya, now Justice of Court of Appeal, ordered Dr Daftari to pay Ms Salmini 100m/- on grounds that such action was a breach of contract and conning.

However, Dr Daftari appealed at the Court of Appeal on grounds that the order was null and void as it was read by registrar of the court and not the judge who wrote it, contrary to the law. The court ruled that the case be determined afresh and read by the presiding judge.

Meanwhile, hearing of an office abuse case facing two former ministers Basil Mramba and Daniel Yona and former Permanent Secretary Gray Mgonja has been adjourned to July 12, this year.

================

Imetolewa hapa: Daily News | High Court orders Daftari to pay businesswoman 100m/-
 
Thanks mkuu Nemesis,

Sasa si unaona ishakuwa rahisi kwa yeyote kujua nini kilijiri na kwanini ahukumiwe! Again, ahsante mkuu
 
Maadam mashtaka yamefika mahakamani na amehukumiwa kuwa na makosa.. hili ni dosari kubwa kwa kiongozi huyo kiutendaji. Vingozi hupoteza wadhifa wao kwa maswala madogo sana maadam imeashiria kutofuata sheria na kuaminika. Ni matumizi mabaya ya wadhifa alokabidhiwa kwani uwezo wake kuingiza vitu hivyo kumetokana na wadhifa alokuwa nao wakati huo..

Na kama asipolipa fedha hizo bila shaka atakwenda jela hivyo hukumu ya kulipa fedha ni option tu ya adhabu iliyotolewa kulingana na madai kwa makosa aloyafanya..
 
Huyu mama kaishapoteza sifa ya kuwa naibu waziri,kwangu mi binafsi afadhali ya mwizi kuliko tapeli.Lakini kama anaelewana na mabosi zake hilo la civil case linaweza kumuokoa akaendelea kupeta Bongo ambapo tuna mawaziri/manaibu wasanii,mafisadi,wagushi vyeti na wenye mapungufu ya kila aina mradi MWENZETU.
 
what the hell is "an office abuse"? maana mawazo yaliyonijia sidhani kama yanaendana na tuhuma dhidi ya hawa jamaa.
 
Nani anajua historia ya huyo mlalamikaji Fatma Salimini? Hebu jaribuni kuchunguza yake na utaona huyu mama ni wa aina gani tangu enzi ya gazeti ya Fahari. Dr. Maua ameingizwa mkenge na mtoto wa mjini na yeye akatumbukia kwenye shimo.

Siyo kwamba namtetea Dr. Daftari lakini hukumu iliyokwenda kwa amount kubwa yote hiyo bila ya kuwa na ushahidi wa maandishi (kwa kuaminiwa) mimi naona haikukaa sawa hata kidogo. Hiyo value imepatikana vipi na hasa kwa dhahabu na vyombo vyengine?

Wataalamu wa sheria naomba mutuelimishe kuhusu hili.
 
  • Waziri Daftari Maua alitaka kununua vifaa hivyo huko nchi za nje bila kulipa kodi!
  • Waziri Maua Daftari alitaka kusafirisha vifaa hivyo kutoka nchi za nje hadi Dar bila kulipia ushuru wa forodha.
  • Waziri Maua Daftari Maua alitaka kuingiza vifaa hivyo bila kulipa ushuru wa forodha Tanzania.
Utapeli wa kutolipa kodi kwa marafiki wasio na diplomatic immunity = conflicts of interests!
 
angekuwa amefanyakosa la wizi angestakiwa criminal case, hii ilikuwa civil kesi, so huwezi ukasema ni wizi.
Mkubwa, wizi upo kwenye mashauri ya madai pia, si lazima jinai. Kisheria waita kwa kiingereza conversion.
 
Kama serikali ingekua na tabia uwajibikaji wa pamoja kwa kuwa aliyetapeli ni waziri maana yake ni kwamba barara la mawaziri ni tapeli na hivyo halipaswi kuaminiwa. Kitendo pekee cha kuitakasa hii cabinet ni kwa Maua kujiuzulu. Na kama atakaidi inapaswa mkuu wake wa kazi kumwajibisha ikiwa naye atakuwa hataki kufanya kazi na matapeli.

Ah, that will be the day. Talk about wishful thinking...! :sick:
 
Nijuavyo mimi hakuna jipya katika hukumu hii.

Mtakumbuka kuwa hukumu hii ilishatolewa siku za nyuma lakini haikuwa valid kisheria kwa kuwa nadhani haikusomwa na Judge anayehusika. Nadhani kuna thread hapa yenye kumbukumbu hii.

Dr. Maua alitaka kukata rufaa lakini haikuwezekana kwa kuwa hukumu haikuwa imekaa vema kwani ilisomwa na msajili. Ni wazi kuwa Dr. Maua atakata rufaa ili haki itendeke. So hakuna jipya katika habari hii.

Kwa wanaomfahamu mlalamikaji inasemekana kwamba tuhuma nyingi ni za kubambika na ana historia ya utapeli pia. Wanaomfahamu Dr. Maua na style yake ya maisha na familia yake wanaujua ukweli katika matapeli au mafisadi mama huyu hayumo. It is only katika siasa na mahakama za Kitanzania lolote linawezekana.

Pole sana Dr. Maua. Kaza buti haki itapatikana.
 
  • Waziri Daftari Maua alitaka kununua vifaa hivyo huko nchi za nje bila kulipa kodi!
  • Waziri Maua Daftari alitaka kusafirisha vifaa hivyo kutoka nchi za nje hadi Dar bila kulipia ushuru wa forodha.
  • Waziri Maua Daftari Maua alitaka kuingiza vifaa hivyo bila kulipa ushuru wa forodha Tanzania.
Utapeli wa kutolipa kodi kwa marafiki wasio na diplomatic immunity = conflicts of interests!

this is what we call critical thinking, thanks mkuu. Wakuu wengi wanafanya makosa haya, kwakuwa wana-diplomatic passports basi wanazitumia kuhujumu nchi na kujinufaisha.
 
Back
Top Bottom