Dkt. Mathayo na Ana Kilango: Same "Wachina" wa Tanzania mpaka "VILAZA" wa Kilimanjaro

bangusule unashindwa kutofautisha P(private candidate wanaotumia kituo husika kama same) na S wanafunzi watahiniwa wa shule(lets say same)?
leo YNIM yuko sahihi he is sober.......
 
Usilete utani wala siasa zenu zilizojaa longolongo na majungu ktk suala nyeti kama elimu......jamaa anapindisha kwa makusudi!! Ina bore kichizi yaani.!
Nimeona mkuu analeta data za private candidate......yaani kilango awashike vichwa wanafunzi wasome?
 
Bandugu........changamoto iliyoletwa na bangusule ni nzuri.....kwani ina-apply na sehemu nyingi tu Tanzania........swali la kujiuliza......je ni tuwatizame wabunge pale tunapofeli?.........

.....kwa maoni yangu....nafikir zinahitajika jitihda za kila mmoja wetu ktk kuhakikisha viwango vya elimu...vinakuwa.....everyone of us has a role to play.........

hivyo basi......ni vyema mkaji/tukaji-organise.....na kuelewa matatizo ya shule zetu ili tuzisaidie..........kunyoosheana vidole pekee hakutaondoa tatizo........

..........Bangusule tuambie wewe umefanya nini....au una mpango wa kufanyia nini jimbo lako?.........
 
..........Bangusule tuambie wewe umefanya nini....au una mpango wa kuifanyia nini jimbo lako?.........

Well said Ogah, Bangusule ameona kiwango cha elimu kinaporomoka jimboni mwake na inaonekana ameamua kumtwisha lawama mbunge wake, binafsi siamini kama ameanza kampeni za ubunge kama baadhi ya wachangiaji wanavyodai hapa. In general matatizoya elimu jimboni Same ndio haya hayo yanayozikabili wilaya nyingine nchini. Labda hii mada iwe approached kwa mtazamo huu..."kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani Same, nani alaumiwe?"
 
Yoyo,

matokeo kati ya P1000 na S1000 hayana tofauti yoyote kubwa. sasa sijui anayejaribu kupindisha ukweli hapa ni nani. ushahidi wa matokeo ya S1000 ulioutaka huu hapa. lakini pamoja na hayo kuna uhalali gani wa wanafunzi wa P1000 kufeli namna hii?

na taarifa kwamba shule 9 kati ya 10 zilizoshika mkia ktk mtihani wa darasa la 7 ktk mkoa wa Kilimanjaro zinatokea wilaya Same mtaleta kisingizio gani?

sitamuita mtu majina, wala sitamjaji mchangiaji yoyote yule. hizi data za baraza ni ushahidi tosha wa hali ilivyo mbaya.

S0498 DINDIMO SECONDARY SCHOOL

DIV-I = 0 DIV-II = 0 DIV-III = 1 DIV-IV = 18 FLD = 8 ABS = 1

S0875 GONJA SECONDARY SCHOOL

DIV-I = 2 DIV-II = 2 DIV-III = 5 DIV-IV = 41 FLD = 41 ABS = 6

S0615 KIRANGARE SECONDARY SCHOOL

DIV-I = 0 DIV-II = 1 DIV-III = 6 DIV-IV = 50 FLD = 8 ABS = 0

S0872 NDUNGU SECONDARY SCHOOL

DIV-I = 0 DIV-II = 0 DIV-III = 1 DIV-IV = 12 FLD = 15 ABS = 6

S0901 KISIWANI SECONDARY SCHOOL

DIV-I = 0 DIV-II = 0 DIV-III = 2 DIV-IV = 25 FLD = 12 ABS = 0

S0354 JITENGENI SECONDARY SCHOOL

DIV-I = 0 DIV-II = 0 DIV-III = 2 DIV-IV = 61 FLD = 61 ABS = 0

S0419 CHOME SECONDARY SCHOOL

DIV-I = 0 DIV-II = 0 DIV-III = 10 DIV-IV = 25 FLD = 0 ABS = 0

S0802 MAKANYA SECONDARY SCHOOL

DIV-I = 1 DIV-II = 1 DIV-III = 6 DIV-IV = 36 FLD = 6 ABS = 0
 
Yourname lakini kuna watoto wengine akili zao zimelala tu, hata uwapeleke kwenye best school au uwapige matuitions kila siku- bado watafeli tu, yani ndivyo walivyo!

Shule nyingi za Same vijijini (hasa za miaka ya karibuni) ni za day, hazina walimu wa kutosha, na hata mazingira yenyewe ya shule hayavutii. Tatizo kubwa na tofauti iliyopo kati ya wanafunzi wa boarding na day ni kwamba hawa wa day vijijini wakitoka shule wanakumbana na kazi za nyumbani, kuna mashamba, mifugo, mazao na shughuli mbalimbali za wazazi, hawana muda wa kusoma, na giza likiingia ndio imetoka hiyo kwa kuwa umeme nao hakuna! Kwa mwanafunzi kufanya vizuri kwenye mazingira kama haya anatakiwa 'awe' kichwa kwelikweli lakini kama akili zenyewe za kushikiwa kama za nanihii lazima azunguke!
 
Mbunge alaumiwe kwa kata kutokua na sekondari-SAWA,
Mbunge alaumiwe kwa sekondari kutokua na maabara au vifaa vya maabara-SAWA,
Mbunge alaumiwe kwa sekondari kutokua na walimu wa kutosha-SAWA,
Mbunge alaumiwe kwa wanafunzi kufeli-SI SAWA.

Kwa mtazamo wangu huku sasa ni kulilia spoon feeding ya kila kitu tufanyiwe na viongozi. Ni wapi familia zinachukua majukumu ya kuhimiza watoto kuzingatia elimu?...Wazazi wanakuta chumba cha kusomea kimejaa magazeti ya udaku, excuses za kutega kujisomea kibao, halafu tunataka tumlaumu Mbunge?... Tunataka awe Matron wa hizo shule asimamie Prep au? muda huo utatoka wapi? What if kwa wabunge wa Dar ambao wana sekondari zisizohesabika!...

Mbunge ana majukumu ya kuchochea maendeleo ya jimbo kwenye kila aspects na sio elimu peke yake...Kwa hili tutakua tunamuonea kumshushia mzigo wa lawama za wanafunzi kufeli squarely on Mbunge.
 
Kwa maoni yangu toka nchi ipate uhuru na serikali kuanza kuwafanyia kila kitu, watu mmesahau kuwajibika.

Hao waliokuwa wanaitwa waChina wa Tanzania, walikuwa wanafanya shughuli za maendeleo kwa kutegemea mapato yao. Walikuwa wanalima hili kupeleka watoto shule au kupata huduma zingine.

Na mkirudi kwenye misingi ya kutotegemea serikali maendeleo yatakuja tu.
 
Mkuu Bangusule malalamiko yako kutokana na Utendaji wa Wabunge watajwa katika Post Mama sio ya kuupuzwa.Kwa wengi inaonekana kama Malalamiko ya Bangusule yamekaa kama kampeni ya kuwang'oa wabunge watajwa,Sioni kama hilo ni tatizo,kwa upande wangu naona kuwa malalamiko hayo ni changamoto kwa Wabunge hao.

Bangusule kama upo Dar mtafute Mama Mbunge...Ni mtu mcheshi na mpenda kushauriwa...kutokana na mawazo yako kuhusu suala la kudorora kwa Elimu Same Mashariki unaweza kutoa ushauri mzuri kwa Mbunge na ukaleta matunda mazuri kwa Vijana wetu......masuala haya ya maendeleo ya jamii si ya Mbunge peke yake,kila mwana-same/Mtanzania anapaswa kushriki ktk maendeleo ya Eneo lake!Mfano wa kijana wa Iowa ni wa kupongezwa na kuigwa na watanzania wengine wenye nafasi za kuweza kufanya mambo kama hayo.......Namkumbuka hata Mbunge Nyalandu Lazaro pia alitumia nafasi yake ya kuwepo huko Iowa kujenga mahusiano ya karibu kati ya Wordolf university-Iowa na sehemu aliyotoka Singida.

Hata hivyo Mawazo yako yatafika kwa Mbunge kwa sababu naamini kwa maandishi ya baadhi ya members humu inaelekea wanajua hata schedule za Mheshimiwa......Hoja kama hizi zinajenga na unamfumbua macho Mbunge...tusiwalundikie sifa tu!! bado kama wawakilishi wetu wana mengi ya kufanya kuboresha maisha ya wananchi wa Majimbo yao.....Hili la Elimu ni muhimu mno,kwa sababu Elimu ndio ufunguo wa kila kitu,Tusitegemee kujikomboa kwenye huu umaskini kama tunajenga Taifa la Vilaza!!!
 
Haya ndio maneno na si kuingiza siasa za "ubunge" 2010 kwenye elimu!! Mie nadhani tatizo lipo kwenye familia kwanza...familia ambazo zimeweka msisitizo na kufuatilia kwa karibu masuala ya elimu ya watoto wao basi kwa kiasi kikubwa watoto nao wamekuwa wanafanya vizuri!! Na hiyo haijalishi ile socio-economic status ya hiyo familia, cha muhimu ni familia kuweka msisitizo na kujali......kwa bahati mbaya na kwa mtazamo wangu hicho ndicho kinacho-miss kwa kiasi kikubwa sana ktk familia nyingi nchini Tanzania!

Kumbuka ubunge ni kiti cha kisiasa kama hii ingekuwa directed kwa afisa elimu wa Same kungekuwa na sababu ya kupiga kelele kwamba tunaingiza siasa; long as it's to the politicians then I think its part of their portion implying their education policy has something to do with the results of the schools; kama atashindwa kueleza what happened then ni mtaji wa kisiasa kwa wale kama mimi wanao inspire kugombea kiti hicho 2010. nikija na sera mbadala nikaelezea how it will work out into bringing the changes to the results mpaka irudi kuwa Same wachina na with the true democracy backed with analytical minds of wapiga kura then I dont think if there would be any thing wrong; tatizo ni je Bangusilo na mimi will we walk the talk? au ndo tuko kwenye MKUBITA? Mkakati wa Kuondoa Umaskini Binafsi Tanzania.
 
Bandugu........changamoto iliyoletwa na bangusule ni nzuri.....kwani ina-apply na sehemu nyingi tu Tanzania........swali la kujiuliza......je ni tuwatizame wabunge pale tunapofeli?.........

.....kwa maoni yangu....nafikir zinahitajika jitihda za kila mmoja wetu ktk kuhakikisha viwango vya elimu...vinakuwa.....everyone of us has a role to play.........

hivyo basi......ni vyema mkaji/tukaji-organise.....na kuelewa matatizo ya shule zetu ili tuzisaidie..........kunyoosheana vidole pekee hakutaondoa tatizo........

..........Bangusule tuambie wewe umefanya nini....au una mpango wa kufanyia nini jimbo lako?.........

Ogah,

Nakubaliana na mengi uliyoyaandika hapo juu. Tatizo kubwa la Tanzania sio resources ni management, kwenye siasa utasema ni leadership. Hapo ndipo suala la mbunge linapoingia.

Sidhani kama Bangusule anataka mbunge pekee ndiye atatue matatizo ya Same na badala yake anaona kuna tatizo, who should stand up and be ready to be counted? Mbunge ndio mwakilishi wa wananchi kwenye hiyo wilaya na kama elimu iko chini inatakiwa yeye ndio awe wa kwanza kwenda kwa wanachi na kuwaunganisha pamoja ili kukabiliana na tatizo. Rudia definition yangu ya leadership huko nyuma (Direction and mobilization of resources). Kuna watu hapa wanafikiri mbunge anapolaumiwa ni kwasababu hajatoa pesa zake mfukoni kuendeleza elimu, hayo mimi nitaita mawazo finyu. Mbunge atalaumiwa kwa kushindwa kutumia resources zilizopo ikiwa ni pamoja na wananchi wote wa wilaya husika.

Huu mjadala umenifundisha jambo moja, Watanzania ndio maana tunachagua viongozi wabovu kwasababu expectations zetu kwa hawa viongozi ziko chini mno.

Japo huu mjadala umeanzishwa na kulenga Same, nafikiri ni mjadala muhimu sana maana unalenga kwenye matatizo sugu ya Tanzania ya uhusiano wa elimu mbovu na viongozi wa kisiasa, uhusiano wa matatizo yetu ya kila siku na uongozi.

Using football analogy, kuna watu watasema kwanini umlaumu Scolari kwa kuchemsha kwa Chelsea wakati wanaocheza ni wachezaji? Kwanini umlaumu Bush kwa kuanguka kwa uchumi wa USA? Narudia pale pale japo resources ni ile ile (watu) lakini visions na mobilization techniques za kiongozi mmoja dhidi ya mwingine ni tofauti. Hapo ndipo inapokuja kiongozi bora dhidi ya kiongozi mbaya.

Ukisoma baadhi ya maoni ya watu hapa inaelekea hata hawajui nini wajibu wa kuwa kiongozi. Standards zetu ziko chini mno ndio maana hata wasanii akina Komba wanaweza kuwa wabunge. Kazi ipo kweli kweli.
 
Last edited:
Hivi tunategemea tutainua kiwango cha elimu cha taifa letu bila kila mmoja wetu kupigania kuwa elimu katika jimbo lake ipewe kipaumbele? Badala ya kumbeza Bangusule, kila mmoja wetuanatakiwa kumuiga katika jimbo lake.

Kusema kuwa watanzania wamezoea spoon feeding ni kutowatendea haki. Nguvu za wananchi hazitafika mbali kama hazitaunganishwa na kuelekezwa kunakotakiwa. Wanaopaswa kufanya hivi ni wabunge ambao waliomba kazi hiyo ili walete mabadiliko katika hali ya wananchi wa jimbo lake na sii wale wa jimbo lingine. Kisingizio kuwa hali ya taifa ni duni kwa hiyo hawawezi kuleta maendeleo katika jimbo lao does not hold water. Kama ni hivyo, basi wananchi watakuwa na haki ya kuwatosa na kumweka mbunge ambaye hali duni ya taifa haitamzuia kupigania maendeleo kwa watu wa jimbo lake. Ukitaka uongozi basi kuwa kiongozi. Tunapenda mno kulaumu victims wa mapungufu yetu.

Amandla.......
 
Mapambano yaendelee
 
Bangusule and all,

Kwanza Mkuu Bangusule, samahani siingilii uhuru wako wa kuji-express lakini reference ya Mwalimu kufufuka inaanza kukarahisha...I mean mwalimu angekuwepo, mwalimu alisema, mwalimu akifufuka...mwalimu, mwalimu, mwalimu, nadhani Mwalimu tuendelee kumuenzi, ila pia tumuache apumzike kwa amani.

Naomba nikuhakikishie kwamba Mwalimu Nyerere hafufuki mpaka wakati utakapofika kwa muongozo wa imani yake! Na pia wakati huo atakapofufuka atakua yuko busy na personal-individual issues za maswala ya ni wapi ata-spend eternity, kama wewe, na Mama Kilango, na Dr. Mathayo na sisi wengine wote tutakavyokuwa kiasi kwamba hataulizia hata kama Mama Maria, wakina-Makongoro na nk wako wapi, achilia mbali kuulizia Same imekuwaje!

So, maisha ni kwa walio hai na responsibility zinawakuta walio hai! Nje ya Swala la Mwalimu, haya mengine nakuunga mkono kuwa una kila sababu za kuwahoji wabunge wako! (Hata kama watakujibu hayo maswala ni nje ya job description zao, sawa, ila unahaki ya kuwahoji)

Ila naomba nianike jambo moja hadharani, hii swala la kudhani wabunge na other political posts people vie for them kwasababu wanataka kuwatumikia wananchi tuli-revisit! Kwa wakati huu wanasiasa wenye nia ya dhati kiasi hicho ni wachache sana sana! Wengi wanaingia kwa maslahi yao binafsi, hivyo usishangae sana kwanini wananeemeka na maswala uliyodhani watafuatilia hawafuatilii! Wako busy sana kufuatilia kile ambacho kiliwa-prompt kuingia kwenye siasa na kutaka Ubunge...but certainly sio darasa la saba wamefeli, sijui mifereji, sijui mpunga haupo no no no no, hayo sio priority kwao! (Siyo yaliyowapeleka kwenye Ubunge): Hivi kweli unaweza kukubali (na huu ni mfano) kuwa mtu anatumia muda na fedha kwa mamia ya mamilioni -, ana-acha career yake ama shughuli zake nyingine na kuwa M'bunge ili ahamasishe maendeleo, basi, kwakuwa anauchungu na kijijini kwao! I mean si angetumia hizo kuhamasisha maendeleo zikawa mtaji wakuingia Bungeni free!

The only reason that is possible ni kwasababu kuna -incentive kubwa sana ya kuwa M'bunge lakini hakuna TORs, Performance Indicators wala Consequences za M'bunge kutokuwajibika zaidi ya labda kukosa Ubunge kwenye uchaguzi ujao, which is not a very big deal or probability!

Swala la wewe kujiuliza na sisi wa-Tanzania wengine tunaodhani wabunge hawatendei haki majimbo yao ya uchaguzi, tuwawajibishe vipi ili wajue kutokuwajibika kuna-personal consequences kama ambavyo Ubunge una-personal incentives!
 
FMES,
mpelekee mbunge malalamiko yetu, na mwambie ushirikiano uleule aliotoa ktk kujenga visima autumie kuinua elimu katika wilaya yetu. pia hizi changamoto asizichukulie kama ni vita dhidi yake. Mama Kilango akiyatatua matatizo haya, wananchi wake watamkumbuka na kumuenzi.

- Mkuu huwezi mpa changamoto mbunge kwa kumtukana kwanza kwamba ni kilaza, wakati huna ukweli wowote kuhusu jimbo lake, la kumuita kilaza ni matusi ya nguoni kwa mbunge ningeomba uombe radhi kwa hilo hata kama Mods na wenye nguvu humu hawawezi kuona kwamba hayo matusi, yanahitaji kuondolewa na kufutwa mara moja, mbunge amechaguoliwa na wananchi wengi sana wa jimbo lake, sasa kumuita kilaza bila facts ni ajabu sana kwamba this kind of lugha chafu na ya chooni inakubaliwa hapa JF, ndio maana siku hizi tumepunguza speed maana angeandikwa Mengi haya matusi yako ingefutwa mara moja.

tunachotaka toka kwake, ni maelekezo kuhusu mkakati endelevu wa kushughulikia tatizo hili. wananchi/wazazi wana mwamko mkubwa wa elimu na ndiyo maana wanaendelea kupeleka watoto wao shule ingawa matokeo yanawaangusha.

- Mbunge wa huko amewaletea contena kubwa lilokuwa limejaa vitabu kutoka UK, na nilikuwa wa kwanza ksuema hapa, sasa tatizo la elimu ni la taifa kwa sababu baada ya kuwapa vitabu sasa inatakiwa juhudi za wananchi pia, waalimu kama hawalipwi mishahara mbunge atafanya nini hilo ni tatizo la taifa mkuu sio la mbunge, kwenye hili la elimu wewe na wote wanaokuunga mkono ni mawazo mufilisi kwa sababu mbunge amejitahidi kuwaletea vitabu na pia mpaka waalimu, sasa what else unatka aende darasani kufundisha tena au?

- Maelekezo ya mbunge ni wapi yaliwahi kuinua elimu ya jimbo mkuu kama sio nonesense! Hebu niwekee jimbo ambalo unaweza kulilinganisha na Same East, kwamba miaka mitatu iliyopita kulikuwa na elimu kubwa sasa imeshuka kwa sababu ya mbunge mpya, yaani una maana Yona alilisaidia hili jimbo kuliko mbunge wa sasa? Are you serious au unatania mkuu? Mbunge wa sasa amewasaidia hata kumtoa fisadi wa hatari sana kwa taifa ungetegemea watu kama wewe muwe na shukrani lakini ndio yale yale maneno mengi ya uongo, huku ukweli uko wazi kwamba mbunge huyu anakubalika tena ni aibu mkuu wakikusikia kwenye jimbo lake, hivi unajua rais wa jamhuri amefika huko mara ngapi mkuu? Mara ya mwisho alikwenda kufungua mradi wa bara bara ambao ndio hasa uliomfanya mbunegw a sasa kuomba awe kwenye kamati ya miundo mbinu ya bunge, leo Same East unaweza kuongea na simu ya mkono baada ya mama mbunge kuweka miti ya simu huko, muwe na aibu kidogo basi kwenye kulaumu viongozi bila sababu.
 
rasilimali ya wilaya ya Same ni watu wake. watoto ndiyo hazina yetu. hatukubarikiwa dhahabu, almasi,au mafuta, kama maeneo mengine ya Tanzania. kwa msingi huo yeye kama Mbunge, huku akishirikisha wananchi anapaswa kuwa makini sana, tena sana, katika kuinua kiwango chetu cha elimu.

- Wananchi ni rasilimali ya taifa mkuu sio Same East tu ambako wewe sio mwananchi wa huko kwa sababu wananchi wote wa huko wanajua vizuri kazi ya mbunge wao, anayetakiwa kuwa makini hapa ni wewe kabla ya kukurupuka, kama taifa linadidimia kwenye elimu sio tatizo la mbunge wa Same East, hili neno ya sisi taifa kushuka kielimu nimeliskia New York, in the 90s, likisemwa na Mwalimu, tena akiwa amesha-retire, lakini sikumsikia akimlaumu mbunge yoyote wa Tanzania, acha haya majungu mkuu na fitina, maana haviwezi kuleta maendeleo ya wananchi wa Same East, kama ni wananchi wa huko hilo mbunge wao hana hata tatizo katika kuwasadiai na kuwaiskiliza wananchi wake, lakini sio warukia forums za wkenye mitandao hapana mkuu mbunge amechaguliwa jimboni na wananchi wake, sio huku kwenye forums,

- Naomba nikuhakikishie kua kwa kazi anayofanya mama Kilango kwa Same East, hahitaji kabisa ushauri wako uchwara wa kumtukna kwanza eti ni kilaza halafu ukibanwa na facts unadai ni ushuair nonesense, tke it back mkuu hahitaji huu ushauri wako, keep it to yourself, next jaribu kwua na heshima kwa mbunge aliyechaguliwa na wananchi wa jimbo, ambao amewafanyia wonders so far na wanaelewa hilo, ndio maana hata mafisadi wanaliogopabo hawajapeleka mtu huko maana wanajua huwezi mtoa Mama Kilango, ambaye sasa hivi yuko wkenye siasa za juu mno mkuu sio hizi za kupakana ujinga ujinga.

naomba kupumzika na hii topic, maana haina lolote zaidi tu ya majungu na upotoshaji, next time fanya homework kwanza kabla ya kukurupuka, ngoja niwahi wakuu wa JF hapa DC maana tunakwenda kupata moja baridi na moja moto sasa, kama kawaida huwa tunawatafuta JFs kwanza popote pale na shukrani wka JFs wote mliojitokeza hapa DC, saafi sana tudumishe undugu wakuu na umoja wetu na mshikamano.

Respect!

Wazee wa sauti ya umeme - FMES!
 
Last edited by a moderator:
hali ya maendeleo katika wilaya ya Same imedorora tangu Dr.Mathayo na Anna Kilango wachaguliwe kuwa wabunge wa same magharibi na same mashariki. hali ya ELIMU ni mbaya sana. wilaya ya same imeshika mkia katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba na ule wa kidato cha nne. katika suala la KILIMO ule mradi maarufu wa kilimo cha umwagiliaji Ndungu una hali mbaya sana. kuna maradhi ya mpunga yameingia na wakulima hawana msaada wowote toka kwa mbunge wao Anna Kilango. milimani upande wa Dr.Mathayo ukataji MITI na uharibifu wa MISITU ambayo ni vyanzo vya maji umezidi kuongeza. BARABARA ya mkomazi-bendera-ndungu-gonja-kisiwani-same bado ni kero kubwa kwa wananchi.

Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuisifu wilaya yetu na kutuita "Wachina" wa Tanzania. nina hakika akifufuka leo na kushuhudia uongozi mbovu wa Dr.Mathayo na Anna Kilango, akaona na matokeo ya mitihani ya watoto wetu atageuza kauli yake na kutuita "VILAZA" WA KILIMANJARO.

Bangusule hakusema hawa wabunge ni vilaza. Alichosema ni kuwa Mwalimu akifufuka atawaita watu wa Same ( yeye mwenyewe akiwemo) kuwa vilaza wa Kilimanjaro. Kuuita uongozi wa wabunge waliopo mbovu ni haki yake kama mpiga kura. Hakuna alipotukana.
 
hali ya maendeleo katika wilaya ya Same imedorora tangu Dr.Mathayo na Anna Kilango wachaguliwe kuwa wabunge wa same magharibi na same mashariki. hali ya ELIMU ni mbaya sana. wilaya ya same imeshika mkia katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba na ule wa kidato cha nne. katika suala la KILIMO ule mradi maarufu wa kilimo cha umwagiliaji Ndungu una hali mbaya sana. kuna maradhi ya mpunga yameingia na wakulima hawana msaada wowote toka kwa mbunge wao Anna Kilango. milimani upande wa Dr.Mathayo ukataji MITI na uharibifu wa MISITU ambayo ni vyanzo vya maji umezidi kuongeza. BARABARA ya mkomazi-bendera-ndungu-gonja-kisiwani-same bado ni kero kubwa kwa wananchi.

Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuisifu wilaya yetu na kutuita "Wachina" wa Tanzania. nina hakika akifufuka leo na kushuhudia uongozi mbovu wa Dr.Mathayo na Anna Kilango, akaona na matokeo ya mitihani ya watoto wetu atageuza kauli yake na kutuita "VILAZA" WA KILIMANJARO.

Bangusule hakusema hawa wabunge ni vilaza. Alichosema ni kuwa Mwalimu akifufuka atawaita watu wa Same ( yeye mwenyewe akiwemo) kuwa vilaza wa Kilimanjaro. Kuuita uongozi wa wabunge waliopo mbovu ni haki yake kama mpiga kura. Mimi sioni alipotukana.
 
hali ya maendeleo katika wilaya ya Same imedorora tangu Dr.Mathayo na Anna Kilango wachaguliwe kuwa wabunge wa same magharibi na same mashariki. hali ya ELIMU ni mbaya sana. wilaya ya same imeshika mkia katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba na ule wa kidato cha nne. katika suala la KILIMO ule mradi maarufu wa kilimo cha umwagiliaji Ndungu una hali mbaya sana. kuna maradhi ya mpunga yameingia na wakulima hawana msaada wowote toka kwa mbunge wao Anna Kilango. milimani upande wa Dr.Mathayo ukataji MITI na uharibifu wa MISITU ambayo ni vyanzo vya maji umezidi kuongeza. BARABARA ya mkomazi-bendera-ndungu-gonja-kisiwani-same bado ni kero kubwa kwa wananchi.

Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuisifu wilaya yetu na kutuita "Wachina" wa Tanzania. nina hakika akifufuka leo na kushuhudia uongozi mbovu wa Dr.Mathayo na Anna Kilango, akaona na matokeo ya mitihani ya watoto wetu atageuza kauli yake na kutuita "VILAZA" WA KILIMANJARO.

Mtanzania

.....umeeleza vizuri sana ni kw anji agani kiongozi anahitajika kwa jamii.....na anategemewa vipi.......

........bangusule kaleta concern....which is ok as a concern citizen....na concern yake.............does apply sehemu nyingi tu nchini.........

.....now.......check hiyo highlight ya kwanza in red...........tell me how do one arrive to such a conclusion.......!!!

....sidhani kama itakuwa ni kumtendea haki Mh Mbunge kumsema Mbunge eti kuna maradhi ya mpunga na yeye hakuwa na msaada wowote kwa wakulima.........how do one substantiate this claim...........kwa ambao tumekulia kule kajunjumele....tunatakiwa tulielewe hili jambo better than anybody........nafikiri unanisoma............

........Mtu unaweza kuwa na hoja nzuri sana........lakini ukishindwa namna ya kui-present.............mtu anaweza kuku-ignore.....ukashangaa........

......bangusule ana valid concerns......lakini zinaelea......na ndio maana akina Ogah.....wame-comment walivyo -comment..........

.......bangusule should now tell us amelifanyia nini au ana mpango wa kulifanyia nini jimbo lake.........

Kuna mtu hapa kazungumzia suala la wabunge kuwa na ToRs na Performance indicators........wow it might be good idea to start with.....however, we should be able to see and say Mh Mbunge did 1, 2, 3..........to the satisfaction of who......this is debatable.......
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom