Dr Magufuli & NSSF na ujenzi wa daraja la Kigamboni

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,377
58,384
Dr Magufuli awataka NSSF kuanza ujenzi wa daraja la Kigamboni mwaka huu

By admin– March 25, 2011Posted in: Habari Mchanganyiko

Na Tiganya Vincent_MAELEZO-Dar es salam

Serikali imeliagiza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF) kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa maeneo ya Kigamboni na jirani yake.

Daraja hilo linatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 130 hadi litakapokamilika kwa ajili ya matumizi ,ambapo NSSF itatoa bilioni 100 na Serikali bilioni 30.

Agizo hilo lilitolewa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kutembelea eneo la Kurasini Vijibweni ambapo Daraja hilo linatarajiwa kujengwa.

Alisema kuwa asilimia 60 ya fedha walizonazo NSSF ambazo ni sawa na bilioni 100 zinatosha kuanza ujenzi wa daraja hilo wakati Wizara ya Ujenzi inatafuta asilimia 40 sawa zaidi ya bilioni 30 zilizobaki ili kukamilisha ujenzi wa daraja zima.

“Tumezungumza siku nyingi kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni ifike wakati tuanze kwani Serikali haiwezi kukosa asilimia 40 ya fedha zinazohitajika kukamilisha ujenzi huo” alisema Magufuli.

Alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Serikali itajitahidi kutafuta fedha ikiwemo kutenga katika bajeti ya Wizara ya Ujenzi ili kuhakikisha kuwa ujenzi wa Daraja hilo unakamilika kabla ya uongozi wa awamu ya nne haujamaliza muda wake.

“NSSF nawaomba mjitahidi kukamilisha taratibu zote na kisha wiki ijayo (Ijumaa ) mtangaze zabuni ili ikiwezekana ujenzi uanze mara moja …ili likikamilika litusaidie katika kupunguza msongamano katikati ya Jiji kwani feli zitaanza kusafirisha abiria kwenda Tegeta na Bagamoyo badala ya kutumia barabara” alisistiza Dkt Magufuli.

Alisema kuwa ki msingi NSSF kutokuwa na asilimia 100 za fedha zinazohitajika katika ujenzi wa daraja hilo hakuwezi kuwafanya wasianze mradi kwani katika mradi wowote mkandarasi anaanza kwa kulipwa fedha kiasi na kisha anaongezewa kulingana na anavyoondelea na mradi.

Dkt. Magufuli alisema kuwa ujenzi wa Daraja la Kigamboni ni muhimu kwa kuwa eneo hilo linachukua wananchi wengi wanaofanyakazi katikati ya Jiji la Dar es salam halikadhalika kuna miradi mingi inayotarajiwa kuanzishwa ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Mabasi yaendayo katika Mikoa ya Mtwara na Lindi na kuwepo kwa viwanja 10,000 vya NSSF.

Kufuatia umuhimu wa Daraja hilo Waziri huyo aliwahakikishia viongozi waandamizi wa NSSF kuwa Serikali kupitia Wizara yake watachangaia asilimia 40 ya fedha zinazohitajika ili kukamilisha ujenzi wake.

Alisema watatumia kipindi cha miaka mitatu kuhakikisha wanamaliza fedha hizo ambazo Serikali inapaswa kuchangia.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Crescentius Magori alisema kuwa NSSF hadi hivi sasa ina kiasi cha bilioni 100 kati ya bilioni 130 zinazohitajika ili kukamilisha ujenzi haraka.

Alisema kuwa daraha hilo litakuwa na njia nne za magari na mbili kwa ajili ya watembea kwa miguu kupita.

Hivyo Magoro amemuhakikishia Waziri huyo kuwa watajitahidi kutangaza zabuni wiki ijayo mara baada ya kuhakikishiwa kuwa Serikali itachangia asilimia 40 ya gharama za ujenzi wa daraja hilo.

Daraja la kigamboni linatarajia kuchukua miaka mitatu hadi kukamilika pindi ujenzi wake utakapoanza.

MWISHO
 
Dr Magufuli awataka NSSF kuanza ujenzi wa daraja la Kigamboni mwaka huu

By admin– March 25, 2011Posted in: Habari Mchanganyiko

Na Tiganya Vincent_MAELEZO-Dar es salam

Serikali imeliagiza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF) kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa maeneo ya Kigamboni na jirani yake.

Daraja hilo linatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 130 hadi litakapokamilika kwa ajili ya matumizi ,ambapo NSSF itatoa bilioni 100 na Serikali bilioni 30.

Agizo hilo lilitolewa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kutembelea eneo la Kurasini Vijibweni ambapo Daraja hilo linatarajiwa kujengwa.

Alisema kuwa asilimia 60 ya fedha walizonazo NSSF ambazo ni sawa na bilioni 100 zinatosha kuanza ujenzi wa daraja hilo wakati Wizara ya Ujenzi inatafuta asilimia 40 sawa zaidi ya bilioni 30 zilizobaki ili kukamilisha ujenzi wa daraja zima.

"Tumezungumza siku nyingi kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni ifike wakati tuanze kwani Serikali haiwezi kukosa asilimia 40 ya fedha zinazohitajika kukamilisha ujenzi huo" alisema Magufuli.

Alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Serikali itajitahidi kutafuta fedha ikiwemo kutenga katika bajeti ya Wizara ya Ujenzi ili kuhakikisha kuwa ujenzi wa Daraja hilo unakamilika kabla ya uongozi wa awamu ya nne haujamaliza muda wake.

"NSSF nawaomba mjitahidi kukamilisha taratibu zote na kisha wiki ijayo (Ijumaa ) mtangaze zabuni ili ikiwezekana ujenzi uanze mara moja …ili likikamilika litusaidie katika kupunguza msongamano katikati ya Jiji kwani feli zitaanza kusafirisha abiria kwenda Tegeta na Bagamoyo badala ya kutumia barabara" alisistiza Dkt Magufuli.

Alisema kuwa ki msingi NSSF kutokuwa na asilimia 100 za fedha zinazohitajika katika ujenzi wa daraja hilo hakuwezi kuwafanya wasianze mradi kwani katika mradi wowote mkandarasi anaanza kwa kulipwa fedha kiasi na kisha anaongezewa kulingana na anavyoondelea na mradi.

Dkt. Magufuli alisema kuwa ujenzi wa Daraja la Kigamboni ni muhimu kwa kuwa eneo hilo linachukua wananchi wengi wanaofanyakazi katikati ya Jiji la Dar es salam halikadhalika kuna miradi mingi inayotarajiwa kuanzishwa ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Mabasi yaendayo katika Mikoa ya Mtwara na Lindi na kuwepo kwa viwanja 10,000 vya NSSF.

Kufuatia umuhimu wa Daraja hilo Waziri huyo aliwahakikishia viongozi waandamizi wa NSSF kuwa Serikali kupitia Wizara yake watachangaia asilimia 40 ya fedha zinazohitajika ili kukamilisha ujenzi wake.

Alisema watatumia kipindi cha miaka mitatu kuhakikisha wanamaliza fedha hizo ambazo Serikali inapaswa kuchangia.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Crescentius Magori alisema kuwa NSSF hadi hivi sasa ina kiasi cha bilioni 100 kati ya bilioni 130 zinazohitajika ili kukamilisha ujenzi haraka.

Alisema kuwa daraha hilo litakuwa na njia nne za magari na mbili kwa ajili ya watembea kwa miguu kupita.

Hivyo Magoro amemuhakikishia Waziri huyo kuwa watajitahidi kutangaza zabuni wiki ijayo mara baada ya kuhakikishiwa kuwa Serikali itachangia asilimia 40 ya gharama za ujenzi wa daraja hilo.

Daraja la kigamboni linatarajia kuchukua miaka mitatu hadi kukamilika pindi ujenzi wake utakapoanza.

MWISHO
my take: Magufuli hizi zisije zikawa ni siasa tena na tunaomba haya uliyoyaongea yatendeke kwani tumechoka kusikia huu wimbo
 
Binafsi mpaka nione wanaanza kupeleka vifaa vya ujenzi site otherwise sitaki kuisumbua akili yangu kuamini vitu visivyoaminika - hivi project ya Mji mpya wa Kigamoni nayo inaanza April Mosi 2011?
 
Daraja linawezekana. Muhimu utashi wa dhati.
Kutokana na muda uliobaki ya 4yrs na umuhimu wa daraja,nashahuri NSSF pamoja na serikali watumie design and build tendering kwani itapunguza muda mwingi wa procurement.
 
mi naona hyo miaka 3 maana yake nin! Mpka kukamilika ndo itakuwa gia ya kuombea kura yaleyale ya machinga complex ndo yatajitokeza muda si mrefu
 
Binafsi mpaka nione wanaanza kupeleka vifaa vya ujenzi site otherwise sitaki kuisumbua akili yangu kuamini vitu visivyoaminika - hivi project ya Mji mpya wa Kigamoni nayo inaanza April Mosi 2011?
VP bado upo ktk ndoto
 
Dr Magufuli awataka NSSF kuanza ujenzi wa daraja la Kigamboni mwaka huu

By admin March 25, 2011Posted in: Habari Mchanganyiko

Na Tiganya Vincent_MAELEZO-Dar es salam

Serikali imeliagiza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF) kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa maeneo ya Kigamboni na jirani yake.

Daraja hilo linatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 130 hadi litakapokamilika kwa ajili ya matumizi ,ambapo NSSF itatoa bilioni 100 na Serikali bilioni 30.

Agizo hilo lilitolewa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kutembelea eneo la Kurasini Vijibweni ambapo Daraja hilo linatarajiwa kujengwa. Redtube Beeg Spankbang

Alisema kuwa asilimia 60 ya fedha walizonazo NSSF ambazo ni sawa na bilioni 100 zinatosha kuanza ujenzi wa daraja hilo wakati Wizara ya Ujenzi inatafuta asilimia 40 sawa zaidi ya bilioni 30 zilizobaki ili kukamilisha ujenzi wa daraja zima.

Tumezungumza siku nyingi kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni ifike wakati tuanze kwani Serikali haiwezi kukosa asilimia 40 ya fedha zinazohitajika kukamilisha ujenzi huo alisema Magufuli.

Alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Serikali itajitahidi kutafuta fedha ikiwemo kutenga katika bajeti ya Wizara ya Ujenzi ili kuhakikisha kuwa ujenzi wa Daraja hilo unakamilika kabla ya uongozi wa awamu ya nne haujamaliza muda wake.

NSSF nawaomba mjitahidi kukamilisha taratibu zote na kisha wiki ijayo (Ijumaa ) mtangaze zabuni ili ikiwezekana ujenzi uanze mara moja ili likikamilika litusaidie katika kupunguza msongamano katikati ya Jiji kwani feli zitaanza kusafirisha abiria kwenda Tegeta na Bagamoyo badala ya kutumia barabara alisistiza Dkt Magufuli.

Alisema kuwa ki msingi NSSF kutokuwa na asilimia 100 za fedha zinazohitajika katika ujenzi wa daraja hilo hakuwezi kuwafanya wasianze mradi kwani katika mradi wowote mkandarasi anaanza kwa kulipwa fedha kiasi na kisha anaongezewa kulingana na anavyoondelea na mradi.

Dkt. Magufuli alisema kuwa ujenzi wa Daraja la Kigamboni ni muhimu kwa kuwa eneo hilo linachukua wananchi wengi wanaofanyakazi katikati ya Jiji la Dar es salam halikadhalika kuna miradi mingi inayotarajiwa kuanzishwa ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Mabasi yaendayo katika Mikoa ya Mtwara na Lindi na kuwepo kwa viwanja 10,000 vya NSSF.

Kufuatia umuhimu wa Daraja hilo Waziri huyo aliwahakikishia viongozi waandamizi wa NSSF kuwa Serikali kupitia Wizara yake watachangaia asilimia 40 ya fedha zinazohitajika ili kukamilisha ujenzi wake.

Alisema watatumia kipindi cha miaka mitatu kuhakikisha wanamaliza fedha hizo ambazo Serikali inapaswa kuchangia.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Crescentius Magori alisema kuwa NSSF hadi hivi sasa ina kiasi cha bilioni 100 kati ya bilioni 130 zinazohitajika ili kukamilisha ujenzi haraka.

Alisema kuwa daraha hilo litakuwa na njia nne za magari na mbili kwa ajili ya watembea kwa miguu kupita.

Hivyo Magoro amemuhakikishia Waziri huyo kuwa watajitahidi kutangaza zabuni wiki ijayo mara baada ya kuhakikishiwa kuwa Serikali itachangia asilimia 40 ya gharama za ujenzi wa daraja hilo.

Daraja la kigamboni linatarajia kuchukua miaka mitatu hadi kukamilika pindi ujenzi wake utakapoanza.

MWISHO
Hivi kweli hili litafanyika kabla ya 2015? Yangu macho!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom