Dr. Lawrence Gama ameaga dunia

na najua kuwa kulikuwa na utaratibu unafanywa ili apelekwe ng'ambo kwa matibabu,lakini Mauti yamemfika kabla mipango hiyo haijafanikiwa...

Look at Miafrika! Mbona mizungu ikiugua hailetwi Afrika kwa matibabu?
 
Hivi wabongo hii tabia yenu ya kusubiri mtu mpaka afe ndiyo muanze kumsifia mtaacha lini?
Nway RIP mzee Gama
 
Raha ya Milele umpe ee bwana na Mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani. Amina
 
eh huyo ni mtu wa Mungu eti, huoni Askofu mkuu anakuwa msemaji wa familia?
 
Msiba utakua wapi? Mbezi Beach karibu na Art Gallery au?

Kwa Taarifa za jamaa wa karibu wa Marehemu Msiba upo Mbezi.Na Taarifa kamili za mazishi zitatangazwa Jioni hii au kesho asubuhi kwa saa za Tanzania,baada ya kikao cha ndugu wa karibu wa marehemu/serikali.
 
RIP Dr. Gama...:(
Hivi huyu bwana alikua anafanya nini siku za karibuni, ni muda mrefu sijamsikia.
RIP DR GAMA.
alikuwa yupo tu,baada ya kudondoshwa kwenye kura za maoni na dr nchimbi- kama sikosei.
Huyu alikuwa mwanamichezo haswa,milambo,lipilu hata majimaji.
Mungu awape familia yake nguvu wakati huu wa kipindi kigumu sana.
 
Inna Lillah Wa Inna Ilayhi Raji'oun.

Oh! My uncle Dr. Chief Lawrence Mtazama Gama,

(Baba wa Familia, Former Director usalama wa taifa, Former Songea urban MP na former Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya ulinzi na usalama).

Ndugu zangu walioko uko Dar (Brother John, Willy & Steven, Noela, Flora, Lawrence, May, Anna, Mussa, Pendo na Untie yangu Siwa), mtaniwakilisha kwenye msiba huu mzito wa Baba yetu my uncle Dr. Chief Lawrence Mtazama Gama.
May Allah give you the strength and patience to get through this.


Haya ndiyo matatizo ukiwa mbali na nyumbani.
__________________________________________
 
Habari nilizo letewa leo usiku ni kuwa Mwili wa Marehemu Dr. Chief Lawrence Mtazama Gama utasafirishwa siku ya Ijumaa kuelekea Kijijini Makolo, Songea na Marehemu atazikwa siku ya jumapili Insha'Allah...!
 
WAPI MZEE ES...nadhani hukosi cha kusema kuhusu comrade Gama......hii ndio JF bwana ......hatupondi tu hata walioacha alama za kutukuka kama Gama .....tunawasifia bila kupigiwa debe!!!

- Sawa sawa Mkulu PM, kwanza Mungu amuweke mahali pema peponi, otherwise ni vigumu sana kumhukumu Marehemu kiuongozi kwa sababu most of his time alikuwa ni underground, ni mpaka alipopewa ukatibu wa CCM kwa amri ya Mwalimu, baada ya kumfukuza Kolimba.

- Kwa machache ninayoyajua kuhusu marehemu, ni kwamba alioa dada wa Mwalimu, ni mmoja wa viongozi wachache sana waliokuwa na imani na Mwalimu na mafundisho yake ya ujamaa, huyu aliyafuata kwa moyo mmoja bila unafiki, under utawala wa Mwalimu, huyu alikuwa ni mmoja wa wateule wake na hasa mmoja wa the guards wa siasa za ujamaa na kujitegemea, huyu akienda kwa Mwalimu kukushitaki kwamba hufai, basi hufai, yaani huyu alikuwa kwenye ile line ya kina Butiku, Apiyo, Warioba, Salim, Mkapa, Kahama, Bomani, Kingunge na Rupia.

- Lakini kwenye uchaguzi wa 1995, alimuudhi sana Mwalimu kwa kujaribu kumpitisha Msuya over Mkapa aliyekuwa chaguo la Mwalimu, katika urais, na alifanya hivyo kutokana na kuahidiwa uwaziri kwenye serikali ya Msuya. Kwa mara ya kwanza aka-fall from the grace na Mwalimu mwenyewe akamuondoa ukatibu na kumpa Mangula,

- The next thing akawa-betrayed na Kingunge wa nyumbani mwenziwe na mshiriki wa Mwalimu's line, Kingunge ndiye aliyemchezea kete mbaya kule Kamati Kuu na kumpa Nchimbi ubunge wa jimbo lake kwa wizi, Marehemu could not believe it kwamba among all Kingunge angeweza kumchezea rafu ili kumsaidia kijana mdogo na corrupt kama Nchimbi.

- He never recovered from that Kingunge's thing, akajaribu sana kurudi politically, lakini Mtandao hawakuwa na nafasi kabisa na huyu mkuu, it was over! Atleast ni mmoja wa viongozi wachache sana ambao under Mwalimu, walijaribu sana kuonyesha some independent thinking, lakini kwa bahati mbaya au nzuri viatu vya Mwalimu, vilikuwa vikubwa sana kwa viongozi kama marehemu kuonekana, aliyeweza ni Sokoine peke yake.

- Kwa maoni yangu Gama, was a good man ninasema hivyo kwa sababu huyu angeweza kuwa fisadi na asifanywe lolote, lakini he never did I mean angeweza kujilimbikizia mali za ajabu sana kama angetaka, lakini amekufa akiwa hana kitu, hata alipokubali deal la Msuya, ilikuwa only kwa ajili tu ya kutaka ku-advance kiuongozi, sio kwa sababu ya kutaka kuiba. Taifa letu leo linakosa wazee kama huyu ambao ndio waliokuwa walinzi wa itikadi za maadili ya uongozi. Viongozi kama Gama, Mhaville, Siyovelwa, Chifu Adam Sapi, Mzee Mwangoka, hawa waliweza kumfuata kiongozi yoyote wa taifa na kumpa ukweli kama hakuwa in line na maadili ya uongozi yaliyowekwa na Mwalimu. Alipochezewa rafu na Kingunge, hakuficha mshituko wake, mbele ya kamati kuu alionya kwamba taifa hili limeanza kupotea na linaelekea pabaya sana, guess what? he was damn right sio tu tumepotea ila tuko kwenye dead end! le fin! Kwishney! yaani kwa maneno mengine tumekwisha.

Mungu amuweke Mahali Pema Peponi!

Respect.

FMEs!
 
huyu ni gama bwana ...moja ya boardguards wa [aide camp] wa kwanza wa MWALIMU alitrain ISRAEL .....kwa mwalimu ...akampata dada yake mwalimu[alishakufa zamani]..akawa shemeji wa mwalimu..baada ya hapo...mwanzililishi wa JKT...akiwa na maj gen kaswende[enzi hizo mkuu wa jkt anaitwa director kama TISS]....,akahamia usalama kama director..mkuu wa mikoa mbalimbali ,mbunge ....katibu mkuu wa CCM.

ANAKUMBUKWA KAMA MPENDA MICHEZO ALIJENGA VIWANJA MAJIMAJI,ALI HASSAN MWINYI....AKAANZISHA TIMU MAJIMAJI, na MIRAMBO[YA Akina Feruz telu..mnamkumbuka..?]...kimsingi ni daktari wa uchumi wa kijamaaa na kwa matendo na maendeleo aliyoshirikisha watu ...anastahili kuitwa DR...ma dr wa siku hizi PHD zao zimesaidia nini wananchi??? hakuwa fisadi...?? alikuwa mjamaa wa vitendo...nasikitika comrade mwenzake kama KINGUNGE hatapata bahati ya kuacha alama hizi akifa..kwani ameshaitukana historia yake.....kwa mzee ni muhimu kufa kwa heshima...

huyo ndie CHIFU LAWRENCE MTAZAMA GAMA comrade wa kiukweli ukweli!!
Maneno mazito haya ndugu yangu.Huku ndio kufa umeacha legacy maana hakuna sababu ya kutafuta ma MC waanze kukupigia debe wewe ulikuwa nani.Viwanja vya michezo vikitamkwa tu na jina lako linainuliwa juu juu. Kazi kwenu kina Sophia Simba, Mathias Chikawe, na ma Dr kama Nchimbi na wengineo....sijui mtatuachia legacy gani!!
 
huyu ni gama bwana ...moja ya boardguards wa [aide camp] wa kwanza wa MWALIMU alitrain ISRAEL .....kwa mwalimu ...akampata dada yake mwalimu[alishakufa zamani]..akawa shemeji wa mwalimu..baada ya hapo...mwanzililishi wa JKT...akiwa na maj gen kaswende[enzi hizo mkuu wa jkt anaitwa director kama TISS]....,akahamia usalama kama director..mkuu wa mikoa mbalimbali ,mbunge ....katibu mkuu wa CCM.

ANAKUMBUKWA KAMA MPENDA MICHEZO ALIJENGA VIWANJA MAJIMAJI,ALI HASSAN MWINYI....AKAANZISHA TIMU MAJIMAJI, na MIRAMBO[YA Akina Feruz telu..mnamkumbuka..?]...kimsingi ni daktari wa uchumi wa kijamaaa na kwa matendo na maendeleo aliyoshirikisha watu ...anastahili kuitwa DR...ma dr wa siku hizi PHD zao zimesaidia nini wananchi??? hakuwa fisadi...?? alikuwa mjamaa wa vitendo...nasikitika comrade mwenzake kama KINGUNGE hatapata bahati ya kuacha alama hizi akifa..kwani ameshaitukana historia yake.....kwa mzee ni muhimu kufa kwa heshima...

huyo ndie CHIFU LAWRENCE MTAZAMA GAMA comrade wa kiukweli ukweli!!

Kutuaga kwa Mzee Gama kunamaanisha "Wajamaa" wamemalizika Tanzania.
 
Back
Top Bottom