ChaMtuMavi
JF-Expert Member
- Oct 15, 2008
- 330
- 8
R.I.P Dr. Gama
Huyu mzee aliwahi kuanzisha, kuonyesha mfano na kusimamia mapinduzi ya kilimo (kama sikosei iliitwa 'kilimo mlale/ulale') sina uhakika na programu hiyo iliitwaje. Ruvuma hawakuwa wazalishaji wakubwa wa mahindi kabla ya programu hiyo.
Huyu Mzee amejenga kiwanda cha kusaga mahindi (Msamala milling co.) sembe za Azam haziendi Ruvuma. Kule unga unakula kwa bei karibu na bure na unasambazwa hadi ktk maeneo ya makazi na wabeba baiskeli. Upo packed ktk mifuko ya ujazo mbalimbali. Anazo mashine za kisasa kabisa.
Wananchi wa mkoa Ruvuma hawataweza kumsahau huyu mzee.
Bujibuji, you are very right, huu ni msiba mzito sana kule Ruvuma, hususani mji mzito wa songea na vitongoji vyake ambako aliwahi kuwa mbunge kwa miaka mingi.
Sio kwamba aliisaidia tu timu ya Majimaji, ila huyu ndio Mwanzilishi wa hii timu, na alihusika sana katika kuiimarisha pia akihamasisha ujenzi wa Uwanja a Majimaji na pia akileta wachezaji hodari kama vile Abdallah "King" Kibaden (Mputa), Madaraka Seleman (Mada), Peter Tino, Mhando Mdeve, Octavian Mrope, Celestine "Sikinde" Mbunga na wengineo,.
RIP LMG.Amen