Dr.kitine yanaweza kumpata yaliompata kolimba?

kama hivyo ndivyo basi Kombe alisitahiri kuuwawa na majasusi wenzake kwani alikiuka kiapo alichokula kwa hiari yake cha kutunza siri alizoziona akiwa mtumishi wa ujasusi. Hii inatokea duniani kote...... kumbukeni yule jasusi wa KGB wa urusi aliyepewa sumu baada ya kukimbilia uingereza na kuanza kuropoka. KGB wakamfutilia na kuingia kimya kimya kijasusi pale Uingereza na kumpa sumu iliyopelekea kifo chake na ilibaki kidogo uhusiano wa Urusi na Uingereza uingie matatani.

Mimi ninavyooona ukitoa siri za majasusi baada ya kuwatumikia au ukiwa bado ndani utahesabika kama msaliti uliyetumwa kwa mission maalum kwenda kuwachunguza na kwa maana hiyo unatumikia mabwana wawili kwa mpigo.... hakika hutabaki salama kwani majasusi hao hawawezi kujua una siri ngapi zingine ambazo hujazimwaga hadharani.

Hivi ni vimbwanga vya Wikileaks jamaa wakamsingizia kubaka mwanamke huko sweden na kama angekuwa jasusi mstaafu pengine kwa sasa angekuwa amekata roho.

Dr Kitine hakutoa siri za majasusi anazozijua channel Ten kamwe hawawezi kumuacha kama angewalipua majasusi wenzie .....kilichobaki kaingia kwenye mchezo wa siasa za maji taka huko ruksa kujilipua, kujitoa mhanga atamwaga upupu kadri atakavyoona roho yake itabaki nyeupe.

Mh! I doubt this, what about, Stan Katabalo, Gilman Rutihinda, Steven Kibona, Horace Kolimba, Imrani Kombe, Edward Sokoine, Koplo Rashid Lema e.t.c.

Inasemekana imran kombe alishugulikiwa na mzee mwenyewe baada ya wakuu wa intelejentia kumweleza anavujisha siri za serekali ya ccm kwa mzee wa kiraracha, ndiyo mana mzee wa kiraracha alikua kila kukicha anawalipua
 
Mh! I doubt this, what about, Stan Katabalo, Gilman Rutihinda, Steven Kibona, Imrani Kombe, Edward Sokoine, Koplo Rashid Lema e.t.c.
Hata hawa nao walisema CCM imepoteza muelekeo? Mmoja alikuwa anaandikia gazeti la mfanyakazi, mwingine akawa gavana wa fedha na mwingine waziri wa fedha, huyu nae akasababisha mtu azikatae pesa zake zikiwa ndani ya gunia.......aah huyu si alikuwepo wakati mwenzake anamwelekeza kwa simu kuwa wawaue wote wasimwache hata dereva taxi!
 
tangu lini mtu ukanyamazishwa eti uongee kupitia vikao tu? alichoongea kitine ni sahihi
 
Wimbi la mparanganyiko wa ccm linazidi kushika kasi kila kukicha,baada ya mtoto wa mkulima kuwataka viongozi wastaafu kutumia vikao kueleza mawazo yao.Agizo hilo limepuuziwa baada ya mmoja wa viongozi wastaafu Dr Hans Kitine kukiponda wazi wazi chama hicho.Akiongea ktk kipindi kinachorushwa na Channel ten cha Je tutafika? Kitine amesema kuwa ccm IMEPOTEZA MWELEKEO maneno yaliowahi kumgharimu aliewahi kuwa katibu mkuu wa ccm wakati huo marehemu Horace Kolimba.Swali langu kwa great thinkers je Dr kitine atasalimika kweli kwa hiyo kauli? maana ukweli unauma!


Hongera Dr Kitine. Nyinyi ndo jicho la taifa, na unaposema kitu chema kwa ajili ya CCM atakaejaribu kukudhuru ni mwendawazimu. Ukweli CCM hawana dira, falsafa, muongozo, imani. Sasa ni hovyohovyo tu.:msela:
 
Tena nilifurahishwa sana na kiusemi kuwa ,Miluzi mingi imempoteza Mbwa.
Kile chama kishakufa, kiko vipande vipande.
 
inategemea ukweli gani,chama kilichokomaa kisiasa hakitakiwi kuteteleka kwa statement za watu kama kitine.swala la kuangaliwa ni je chama hicho kinafanikiwa kupata na kutimiza malengo yake?mfano kushinda uchaguzi,idadi ya wabunge wengi nk halafu ndipo utakapojua mwelekeo wa chama.kifo cha kolimba ni ccm au mungu?na kitine siku zake zikifika ataenda mbele za haki kama wengine wote binadamu itakavyokuwa.

HAPO KWENYE RED AM STL CONFUSED!!!! KISHINDE TU KWA NJIA YOYOTE ..I MEAN KIBAKI MADARAKANI HUKU MAISHA YA WATU WAKE IKIDIDIMIA??????? Eg Tanzania na CCM ya leo.:hatari:
 
Kama kawiva alishindwa vipi kucoverup scandal yake hadi wakamlipua mnasifia mijitu kishabiki.ama mlikua bado kindergaten hamjui alifanyaga nini

Nakushukuru kwa kuwakumbusha vijana. Tatizo letu tunasahau mambo haraka na kukimbilia kushabikia watu hovyo hovyo. JK alishabikiwa weee leo wanamwona muoga. Scandal za watu kama Kitine hazikanushwi kwa ushahidi ili tujue kama ni mzalendo wa kweli aliyezushiwa kwa fitna au la je tutajuaje kama anastahili sifa zinazotolewa na baadhi ya wachangiaji.
 
Hata mie nilitazama kipindi hicho jana cha channel ten.Dr Kitine ameweka wazi na kwa mifano halisi udhaifu uliopo ndani ya CCM.Moja ya kitu alichotanabaisha ni pale aliposema kuwa baadhi ya viongozi waliopo na wastaafu wameamua kuongea nje ya vikao kwa sababu siku za hivi karibuni vikao hivyo vya CCM vimekuwa havina agenda za maana, na badala yake vimegeuka kuwa ni ulingo wa kukejeri wenye mawazo tofauti, fitina, kushambuliana miongoni mwa makundi yanayosigana ndani ya chama.Kutokana na hali hiyo watu wenye akili zao wanaona ni bora watoe maoni yao kwenye umma kwa kupitia vyombo ya habari ambapo watasikiwa na wananchi ambao kimsingi ndiyo wenye nchi.

Na hata alienda zaidi na kutukumbusha kuwa huko nyuma hata uteuzi wa viongozi kwenye taasisi nyeti ulizingatia vigezo ambavyo vilikuwa clearly stated, kama vile uzalendo (patriotism), jitihada (diligence), kutokuwa mwizi na mbinafsi.Na akaweka wazi kwa kusema hata usalama wa taifa walisaidia kuwapata viongozi wa kutimikia maeneo hayo nyeti.Lakini hivi sasa, alisema Dr Kitine, utaratibu huo haupo, mambo yanakwenda kiholela holela."Mtu yeyote atakayeonyesha kutetea maslahi ya walio wengi nchi hii siku zote ataandamwa sana, kwa hiyo inataka ujasiri sana" Mi binafsi namkubari sana Dr Kitine, na Mungu amjalie maisha marefu zaidi ili aendelee kuisaidia nchi hii kifikra.
 
kazi kweli kweli tanzania, huyo mzee anamaisha ya kawaida kabisa ya mtanzania sio hawa wa kujilimbikizia mali, siku hizi usalama wananukia perfume! wanalamba bia na kujitamba kwenye mabaa na magari ya kifahari! zamani ulikuwa mtu hadi mkewe hajui kama mtu ni usalama. kitine hawamuwezi bado anawatu na wanampa information zote! ile kazi haina kustaaafu, kustaafu kwake ni kuingia kaburini
 
..ukiona mtu mwenye scandals kama Kitine anapata ujasiri wa kuongea hadharani ujue hao anaowasema wamechafuka zaidi yake.

..utawala huu ungekuwa umesheheni watu wenye maadili na hekima watu kama Kitine wasingejitokeza na kuanza kuushambulia.
 
Wakati Dr. kitine anaongelewa kama shujaa, najiuliza kama ametakasika na ile shutuma ya kutumia mamilioni ya serikali kumtibu mkewe na jinsi alivyomfanyia Jenerali Ulimwengu kwa kuibua ile habari kwenye gazeti la Rai. Labda ile habari ya Kitine imeshasahaulika... Wasiwasi wangu ni kuwa isije kuwa watu wanapiga kelele kwa kuwa wako nje ya 'game' na sio kwasababu ni wazalendo.
 
Hata mie nilitazama kipindi hicho jana cha channel ten.Dr Kitine ameweka wazi na kwa mifano halisi udhaifu uliopo ndani ya CCM.Moja ya kitu alichotanabaisha ni pale aliposema kuwa baadhi ya viongozi waliopo na wastaafu wameamua kuongea nje ya vikao kwa sababu siku za hivi karibuni vikao hivyo vya CCM vimekuwa havina agenda za maana, na badala yake vimegeuka kuwa ni ulingo wa kukejeri wenye mawazo tofauti, fitina, kushambuliana miongoni mwa makundi yanayosigana ndani ya chama.Kutokana na hali hiyo watu wenye akili zao wanaona ni bora watoe maoni yao kwenye umma kwa kupitia vyombo ya habari ambapo watasikiwa na wananchi ambao kimsingi ndiyo wenye nchi.

Na hata alienda zaidi na kutukumbusha kuwa huko nyuma hata uteuzi wa viongozi kwenye taasisi nyeti ulizingatia vigezo ambavyo vilikuwa clearly stated, kama vile uzalendo (patriotism), jitihada (diligence), kutokuwa mwizi na mbinafsi.Na akaweka wazi kwa kusema hata usalama wa taifa walisaidia kuwapata viongozi wa kutimikia maeneo hayo nyeti.Lakini hivi sasa, alisema Dr Kitine, utaratibu huo haupo, mambo yanakwenda kiholela holela."Mtu yeyote atakayeonyesha kutetea maslahi ya walio wengi nchi hii siku zote ataandamwa sana, kwa hiyo inataka ujasiri sana" Mi binafsi namkubari sana Dr Kitine, na Mungu amjalie maisha marefu zaidi ili aendelee kuisaidia nchi hii kifikra.

Hivi huyu Dr Kitine ndo mwandishi anayejiita msomaji raia mwema nini? Maana naona kuna dots zinazoshawishi hivyo. Kwa wale waliosoma raia mwema la leo watakubaliana nami. Makala zake kwenye raia mwema huwa zinanivutia sana maana inaonekana mwandishi huyu (hata kama si Dr Kitine) atakuwa ana connection kali sana na system maana huwa anaongea mambo ya jikoni sana.

Hoja alizoongea Dr Kitine ni nzito sana na zimejaa mantiki. Halafu, hivi mtu hata kama aliwahi kuwa mwizi na siku hizi haibi akikwambia kuwa kuna mtu anaiba mali zako utakataa kumsikiliza eti kwa vile na yeye huko nyuma aliwahi kuiba? Huu unaanza kuwa ugonjwa mkubwa sana kwenye jamii yetu. AKitokea mtu anaongea mambo mazito ya kuonya watu huacha kuangalia hoja na badala yake wanaanza kumjadili mtu. Sijui kama Dr Kitine amewahi kufanya ufisadi huko nyuma na hata kama ikiwa kweli hatuwezi kupuuzia mambo anayoongea yenye maslahi ya taifa eti kwa sababu huko nyuma aliwahi kufisadi. Sitetei ufisadi na pia sikubaliani na tabia ya kuponda hoja zenye mashiko eti kwa sababu tu zimeongewa na mtu fulani. Kuna wakati wa kujadili hoja na si watu...
 
..ukiona mtu mwenye scandals kama Kitine anapata ujasiri wa kuongea hadharani ujue hao anaowasema wamechafuka zaidi yake.

..utawala huu ungekuwa umesheheni watu wenye maadili na hekima watu kama Kitine wasingejitokeza na kuanza kuushambulia.

wewe ndo umeongea......gud
 
ACHENI JAKAYA KIKWETE AISHI KWENYE MABAWA YA MIDEGE ANGANI AKICHAGUA ILMRADI GHARAMA YA KODI ZETU KUIFADHILI MIRADI HIYO HAIZIDI ROBO YA TIJA TUNAYOVUNA KWENYE MAPENZI YAKE HAYO!!!

Hivi PakaJimmy, huenda huyu mwenye bandiko lake,anayeshabikia ovyo matembezi ya Mhe Jakaya Kikwete Wizara moja baada nyingine bila kutupa VERIFIABLE FACTS and FIGURES juu ya ushabiki wake, akawa ni Rweyemamu wa Ikulu kule Magogoni, Katibu Mwenezi na Propaganda CCM au ndio tuseme Zilipendwa Mzee Tyson Wassira Waziri wa Uhusiano leo hii kaamua kutoka Ki-Doti-Komu vile nini??

Tathmini ya huu Mradi wa ziara ya Mhe Kikwete Mi-Wizarani kamwe haitofanywa na akili za kilabuni hivi; tutakwenda mbele kidogo na kutaka ripoti iliyoandaliwa baada ya kutumia vigezo vya kisayansi (Project Monitoring and Evalution) ili kubaini kwamba tangu anapanga ziara hii.

Ni sharti JK atujibu kwa mtaji wa kodi zetu anazoendelea kutumia hivi sasa katika 'Kikwete Tembelea Wizara Project' (KTWP) na wal si kutupigia kelele za kishabiki hapa; huko kwenye siasa za kishabiki Vijana hatumo bali ni kwamba TIJA tu ndio tuwekewe mezani kweupe. Washiriki wa KTWP watujibu maswali kama vile Kikwete: (1) alikua na makusudio yepi, (2) kakuta hali halisi ikoje, (3) hali hiyo inajilinganisha vipi na kipinda cha mara ya mwisho mradi kama huo ulipotendeka, (4) Wa-Tanzania tumelazimika kuwekeza kiasi gani katika hiyo Month-Long Kikwete Project na iko wapi thamani ya kodi zetu mle????

Dr Bila ripoti tunaomba tangu ziara na familia yako mbugani na kote huko mikoani. Wapinzani na wabunge wote kwa ujumla nanyi tutawabana sana juu ya jinsi gani Viongozi Waandamizi wanavyotumia kodi zetu na TIJA za wazi zinazopatikana kwenye kile watendalo tukilinganisha na gharama iliotumika. Tukizingatia nidhamu kama hii tangu ikulu hadi nyumba kumi mitaani kwetu basi wananchi tutaona ACCOUNTABILITY wa hali ya juu!! Huko nyuma JK ameripotiwa kuwa na ziara nyingi sana na hata wakati mwingine kudaiwa kuwakera walipa kodi.

Kwangu mimi sitojali ziara zake ni nyingi kiasi gani ba ni thamani ya tija iliyopatikana ukilinganisha na gharama tulizowekeza mle. Tena mimi nitamuunga mkono sana JK akiweza basi kila siku awepo tu kwenye pipa angani kila kukicha ilmradi UNPOLITICISED WATCHDOG POLITICAL GROUPS AND PARLIAMENT wanaturidhisha katika hili bila swali kubaki kichwani mwetu.

Tunasupibi ripoti bungeni juu ya matumizi kwenye mradi huu na vile vile kwenye hotuba ya mwisho wa mwezi akajikite katika TIJA zenye kugusika na kuonekana tulizozivuna kwenye KTWP. Hatutaki blaa blaa na longo longo nyingi za mwaka wa 47 ambayo ndio haswa imetunashisha kama taifa kwenye huu umasikini gundi mabegani.

Mhe Kikwete kama CEO wa Tanzania kwa sasa, kama angelikua anaongoza kampuni ya kibiashara lazima angelazimika kuridhisha Wajumbe wa Bodi (Wahe Wabunge, nchi wahisani na Asasi za Kiraia husika) na haswa wamiliki wa kampuni (sisi wananchi) juu ya kila atendalo na faida ya kuonekana bila siasa, kwa nini ishindikane kwa ngazi ya taifa endapo kweli hatukusudii kuja kupata misaaada to Rwanda au hata Kenya kutupa LIFTI KWENYE NDEGE YAO toka kwenye hatari Libya????
 
TUSIMLAUMU DR KITINE PAKA WAKE KULA SAMAKI WETU KWA KITENDO TU CHA SIE HUKU KUACHA CHUNGU WAZI!!!

Hivi hizo hela za tiba ya mamsap alizipewa Mhe Dr Kitine au kuna ripoti mahala kwamba alivunja lango la benki kuu??

Kutibiwa kwa mke wa aliyekua TISS Director si tatizo bali kosa ni misingi iliotumika na mruhusu fedha kufanya jinsi ambavyo walipa kodi hatukupata kuridhika.

Naamini mahala kuna kanuni na taratibu jinsi gani kugharamia tiba za viongozi na familia zao. La sivyo nasema tusimlaumi Dr Kitine kitenda cha paka ya kula samaki wetu kwa sababu tu ya uzembe wa sisi kuacha chungu wazi!!

Wakati Dr. kitine anaongelewa kama shujaa, najiuliza kama ametakasika na ile shutuma ya kutumia mamilioni ya serikali kumtibu mkewe na jinsi alivyomfanyia Jenerali Ulimwengu kwa kuibua ile habari kwenye gazeti la Rai. Labda ile habari ya Kitine imeshasahaulika... Wasiwasi wangu ni kuwa isije kuwa watu wanapiga kelele kwa kuwa wako nje ya 'game' na sio kwasababu ni wazalendo.
 
CCM wanatambua hilo kuwa sasa hivi itawagharimu kwa kumuondoa mtu yeyote awe CCM au upinzani kwa njia ya kum-kolimba.

Kwa mazingira ya Tanzania ya leo, "You get what you pay for" Wakiamua kutumia hiyo njia haramu kwa msemo wa wakenya "Wataona Kanga Aliona" wakimaanisha wataona kilichomtoa Kanga manyoya.

Watanzania hawawezi kuruhusu huo upuuzi wa kupunguza siku za mtu kuishi kwa sababu tu ya kuambiwa ukweli.
 
WanaJF nimepoteza kumbukumbu!! Hivi huyu Kitine ndiye yule aliyekumbwa na kashfa ya kuongopa kuwa mkewe alienda kutibiwa ughaibuni na kulipwa mipesa ambayo si halali, au?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom