Dr. Kitila Mkumbo aipa ITV hadhi ya Television ya Taifa

Wanabodi ITV Imerusha mjadala wa vijana leo chuokikuu Dar es salaamu katika kumuenzi MwL Nyerere bure ambapo wachokoza mada wasomi, vijana, wazazi viongoz wameufikia umma kutukumbusha mwalimu kama mwalimu, mwanasiasa, kiongoz, mkulima, mwandishi, raisi na mwanasia alitenda kwa ajili ya Tanzania tuitakayo wakamulika Tanzania baada yake nini kinatendeka. ITV Imesababisha hayo kufika nje ya ukumbi, mkoa,nchini nje ya nchi au hapo ulipo kama uliangalia bure Je kutokana na kutambua mchango wa mwalimu na mambo mbalimbali ITV Ilirusha ni wakati wa kusema ni TV ya Taifa kwa sasa mambo ya kizalendo na kimabadiliko na hata ya kidemokrasia ya uhuru wa maoni yanazimwa kama yanamulika watawala. Mie naungana na Dr Kitilia Mkumbo, "ITV ni TV ya Taifa" Nini maoni yako juu ya chombo hiki kusababisha mabadiliko yanayotokana na jitihada za MwL katika nyanja tajwa hapo kwa Tanzania tuitakayo kulinganisha na TBC. Nia ni kupata maoni ya kukisaidia chombo hiki kwa vipindi kama kipima joto, malumbano ya hoja, mijadala na habari
Anauliza ndonya Msumbiji?
 
Kwani CNN ni tv ya taifa la marekani hadi itumie mda wake kutangaza debate ya romney na obama badala ya voice of america.haya ni maamuzi ya kituo cha tv .wangeonyesha wote baba wa taifa nani angecover uzimaji mwenge shy.?.
Hivi huyo dr kitilya.udr wake ni wa elimu au.maana sioni issue ya kuongelea hapo.
 
Sijui Dr slaa alikufanyia nini maana upumui bila kumtaja!

Badala muwe na Chadema Tv mnalialia Kama watoto.Katibu mkuu kajenga Hekalu kuliko Makao Makuu ya Chama chenu.Nikipitaga pale Makao yenu utafikiri Banda la KUKU.
 
Ni baada ya kukubali kurusha kongamano la vijana kuhusu mwl Nyerere.
Kasema kuwa TV ya taifa sio lzm gari lako liwe na SU au STK, bali matendo.

Mzee Mengi mwenyewe aliwahi kunukuliwa akisema kuwa TBC haiwezi kushindana na TV binafsi, alipokuja Tido TBC ilifurukuta kidogo, ikaitangaza kuwa ITV ina madeni sana huko nje na haiwezi kuonesha michuano ya Kombe la Dunia, TBC ikajinadi kwa kauli mbiu ya ukweli na uhakika, miaka miwili baadae TBC imekuwa televisheni ya kawaida sana huku ITV ikirejea hadhi yake ya kawaida, bila shaka ITV ishalipa madeni yake inayodaiwa huko nje ili mwakani tutazame AFCON moja kwa moja toka kwa Mzee Madiba.

Hongereni sana ITV
 
Badala muwe na Chadema Tv mnalialia Kama watoto.Katibu mkuu kajenga Hekalu kuliko Makao Makuu ya Chama chenu.Nikipitaga pale Makao yenu utafikiri Banda la KUKU.

Chadema inatokea wapi tena na mambo ya ITV????
 
Ni baada ya kukubali kurusha kongamano la vijana kuhusu mwl Nyerere.
Kasema kuwa TV ya taifa sio lzm gari lako liwe na SU au STK, bali matendo.

madaktari mgomo baridi, walimu mgomo baridi, polisi mgomo baridi (mpaka kamanda wao kauwawa bila upinzani wowote),
kila idara mgomo baridi hata taasisi nyeti ya mkuu wetu nayo mgomo baridi wa kuongoza(rejea kutotoa matamko na miongozo ya msingi ktk kutatua matatizo ya raia wake), KWA NINI TBC WABAKI BILA KUGOMA?
wapo kwenye mgomo baridi wa kuwa tv ya taifa toka jembe lao lilipoondolewa, Ahsanteni ITV kwa kuziba pengo!
 
Nashangaa watu kutaka kuitumia vibaya siku ya mwalimu kufanya siasa au kuendeleza malumbano yasiyo na faida kwa nchi yetu. Kama ITV wakiamua kurusha makongamano ya Kitila Mkumbo Live na hii si mara ya kwanza hiyo ni ridhaa yao. Lakini kwenda mbali na kutaka kuwaghiribu wa Tanzania kuamini eti ITV ni ya Kitaifa zaidi hayo ni mambo ya mtu bunafsi anayesema hivyo na anajua anachokifanya. Si vema watu kutaka kuharibu hii siku muhimu ya Baba wa Taifa.
 
Ni kweli lakini kwa nini wasiuze share kama presion air au crdb kwa watu wengine ili ifunge mitambo yake nchi nzima!!!! yani huwezi amini moro na bukoba ndo wamefungiwa juzi!!!!
IPP kama pesa ushapata bana fanya mpango itv iwe ya watu bana! watu wa karibu kamshaurini huyu mzee Mengi.. yule dada pale anamlia pesa tu aampi mawazo endelevu!

Ebwana Moro hatuipat hawajafunga?
 
Hata chadema ikibahatika kuongoza nchi itaiitaji tbc na vyombo vingine vyote vya dola, kwa hili rafiki yzangu wana chadema mnakuwa na mumkali usiopimika
 
Mapovu ya nini sasa?

Nimemsikia JK kupitia TBC ametaja jina la Mwalimu Nyerere mara mbili tu!
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom