Dr. Kigwangala: another Lucas Selelii

Brothers and Sisters,

Nawashukuru walioponda na waliofagilia, nyote mna haki ya kusema na kutazama mambo kama mnavyoona inafaa.

Haki mliyonayo nyie na mimi pia ninayo.

Naomba sasa niwaambie tu kuwa, kwa kutumia haki yangu, na nafasi niliyopewa na wananchi wa Nzega, ninafanya kazi yangu kwa nguvu zangu zote kwa kadri ninavyoona inafaa. Mnayo haki ya kuona vinginevyo, lakini nadhani wananzega wanajua zaidi kama kazi yangu inawalipa au la, na wataniambia wiki ijayo nikirudi nyumbani na kuongea nao. Nzega tumekuwa na kawaida ya kukaa kwenye vijiwe formal na informal na kuhojiana mustakabali wa maendeleo ya jimbo letu na nini wanachokitaka wananzega Mbunge wao akifanyie kazi. mengi ya mnayoyaona ninayafanya ni zao la mapendekezo yanayotokana na wananchi wa Nzega, kwa maandishi, kwa vikao, kwa sms na hata kwa email.

Naomba pia mfahamu tu kwamba, mimi kama mimi nafanya kazi yangu ya leo, ya 2015 anajua Mungu.

Siwezi kusema hapa leo kuwa mimi ni Mbunge bora kabisa kuliko wote, nafahamu wazi kabisa kuwa pengine mimi si mjinga kuliko wote, lakini najifunza kwa bidii sana kuwawakilisha wananchi wa Nzega na watanzania kwa ubora wanaostahiki na wanaoutarajia.

Hata hivyo, ninawashukuruni nyote kwa kunipa feedback. kwa wapenzi wa maandiko ya Hayati baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere, ni lazima viongozi wajikosoe na wakubali kukosolewa, na mimi ni muumini wa yote mawili, hivyo nawashukuruni kwa kunikosoa wale wote mlioniponda ....kama inavyosomeka kwenye kitabu cha 'Kujikosoa na Kukosoana'

Wakatabahu,
HK.
 
Jamani kwenye ukweli tusifie, hata kama chadema kuna mabaya na mazuri lakini sio kweli kwamba kwasababu yuko ccm basi ndo kila mtu hafai. Huyu Daktari mi namkubali saaaaaaaaaana, hamumunyi maneno, kama ovyo atasema hiyo ni ovyo, kama kweli basi atasifia. Tuwe wakweli, huyu jamaa kama unamfuatilia huwa ana contributions nzuri sana. Wasiwasi wangu ni kama atadumu ndani ya chama chake au jimbo lake.

Hebu nikumbusheni huyu jamaa naitwa nani tena?
 
Ndugu HK vipi kuhusu ahadi yako ya kuandamana na wananchi kwenda mgodini? Lini utekelezaji wake?! Ukitimiza ili hakika nitakuona upo kwa ajili ya maslahi ya wananzega.
 
Huyu Dr. Kigangwala sio mtu mwema, chambo tu, amewekwa hapo kwa maslahi ya serikali.

Kama mnakumbuka wakati bajeti ya kilimo inapitishwa, aliwakera wabunge na wananchi wa kanda ya ziwa, bahada ya kuondoa shillingi na kuungwa mkono na wabunge wengi, kusema ukweli wananchi wengi walitegemea pale ndipo wabunge wao pa kuibania serikali ili itoe majibu yanayoeleweka kuhusu bei ya pamba.

Lakini alichofanya Dk Kigangwala, kama kawa akatoa shillingi, na akaungwa mkono na wabunge kibao, mpaka wakateua bahadhi ya wabunge wakakaa kikao kujadili hili swala.

Bahada ya hapo Waziri Mkuu akasimama kutetea bajeti ya wizara ya kilimo, Bahada ya hapo akaulizwa mtoa shillingi "vipi Dk bahada ya maelezo hayo ya waziri mkuu, bado unaendelea na msimamo wako wa kutoa shillingi"

Dk Kigangwala akacheka alafu akatamka "nairudisha shillingi yangu"
Tangu siku hiyo mpaka hivi leo wafanyabiashara wanajinunulia pamba kwa bei wanayoitaka, ma DC walikuwa wanawatetea wakulima wameacha, wanasema kama wabunge wenu wameshindwa kuwatetea, na ndio mliowapigia kura sembuse sisi.

Pale Dr Kigwangala alikuwa anawazingua wabunge ili wamuunge mkono alafu awatose, na ndivyo alivyofanya.
Nionavyo mimi ni kuwa, huyu ameandaliwa na serikali ili atoe shillingi watu wamuunge mkono alafu awatose, kama alivyowatosa wazee wa pamba, mpaka leo umeshasikia kelele za kwenye pamba. Serikali imetangaza bei 1100 na watu wananunua 600, hapo mpo?

Mkuu naomba nikukumbushe kwamba kwenye suala la bei ya pamba usije kutarajia lolote la kuwafaa wakulima wa pamba kutoka kwa hamis kigwangala mbunge wa nzega.

hamis kigwangala mbunge wa nzega naye ni mfanyabiashara ya pamba na kuna fununu kwamba hata ile stimulus package alifaidika nayo. Huyu mkulu ana kampuni yake inakwenda kwa jina la MSK Solutions ambayo pamoja na shughuli zingine inazofanya ni pamoja na kununua pamba.

Labda kitu ambacho hakuwaeleza wananchi pamoja na wabunge wenzake, ni kutoku-"declare interest" alipokuwa anachangia bajeti ya wizara ya kilimo. Kwahiyo katika mazingira kama hayo asingekuwa na jeuri ya kung'ang'ania shilingi "yake".
 
sasa mwita, kama mimi nilikuwa nadai bei ya pamba iongezeke bado utasema nilikuwa nina maslahi binafsi kama 'mfanyabiashara?'

Nyanda,

Ipo siku ahadi itatimi9a, kuahirisha kitu si kuacha kutekeleza. Kuna mazungumzo yalianza baina ya serikali, watu wa mgodi na mimi nikiwawakilisha wananzega - yalianza kwenda vizuri japokuwa sasa hivi yanasuasua na hivyo lolote linaweza kutokea very soon

Ndugu HK vipi kuhusu ahadi yako ya kuandamana na wananchi kwenda mgodini? Lini utekelezaji wake?! Ukitimiza ili hakika nitakuona upo kwa ajili ya maslahi ya wananzega.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Huyu jamaa kwa ukali anaoendelea nao ndani ya bunge, kwa kitendo cha kupinga sera na itikadi za ccm, na kutetea maslahi ya wananchi wa Nzega, hatadumu. Nawaambieni 2015 watamfanya walichomfanya Selelii kwenye kura za maoni. Amepinga bajeti ya wizara ya maji kwa 100%. Anasema naweka kumbukumbu sahii kwenye hansard, ili baada ya miaka 50 wajukuu zake watakaoingia humu wakaisoma hansard wasije wakamwona ni punguani kwa kuunga mkono hoja. Ghasia kaomba mwongozo wa spika kutaka Dr. Kigwangala afute kauli yake ya punguani, akilalamika kuwa inamaana wabunge wanaounga mkono hoja ni punguani. Spika kamtetea Dr. Kigwangala.

Hamis Andrea Kigwangala (Saidi Bagaile) alianza Bunge Kishamba sana, Na nilishawahi Kumchamba sehemu fulani kwamba anajisahau anafikiri yeye ni sehemu ya Serikali ( Labda alikuwa analipa Fadhila maana alishika nafasi ya tatu Nzega).

Kama mnasema amejirekebisha basi itakuwa ni kwa Sababu ameshawahi kukutana na Rungu la Tundu Lisu, David Silinde na Sugu maana jamaa alikuwa kazi yake ni 'Taarifa Mh Spika', Yeye ilikuwa kazi yake ni kutetea Serikali yake hata kama Utetezi wake uliwaumiza wananchi wake Mfano wakali wa Mjadala wa Sheria Mpya ya Fedha aliwatetea sana wawekezaji Mpaka Lisu akamshushua nadhani From there atakuwa alirudi nyuma akajitathmini na kujuiliza Kazi ya mbunge ni nini

Halafu anatabia za uongo mimi mtu akishakuwa Muongo huwa simfagilii hata Kidogo
 
sasa mwita, kama mimi nilikuwa nadai bei ya pamba iongezeke bado utasema nilikuwa nina maslahi binafsi kama 'mfanyabiashara?'
<br />
<br />
labda alitaka udai bei ya pamba ishuke ili upate hasara, bila kuangalia athari ya mtazamo wake kwa wakulima wa pamba. Labda mwita hajakuelewa, la msingi Mheshimiwa HK nakugongea 5 kwa kufanya kazi uliyotumwa na wapiga kura wako, tambua kuwa wachangiaji wengi humu akiwemo mimi mwenyewe si mpiga kura wako. Tunaweza kukushauri jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wako, na kuweza kuisaidi nchi yako in general. Wapiga kura wako waliokuchagua na kukufanya uwepo hapo mjengoni ni bora kuliko wengine. Japo mimi si mpiga kura wako, na wala si mwana magamba, nimefuatilia sana hoja zako, na nimeona nyingi ni kwa maslahi ya wananchi na taifa, na hata ile hoja ya Butiama was for the public interests, japo mengine unajikanganya it is not very much the case. May be what I have observed is that you were not supposed to be on that part.
 
Kigwangala kwanza tukubaliane kwamba ukiwa mfanyabiashara ya pamba huwezi kuwa mtetezi sahihi wa wakulima wa pamba,kwa vyovyote vile utakuwa upande wa wanunuzi(wafanyabiashara) wenzako,na sina hakika kama uli declare interest ulipochangia hoja hiyo kwakuwa sikuangalia bunge wakati unatoa hoja yako. Na dio maana hadi sasa bado wafanyabiashara ya pamba(MSK Solution ikiwa mmojawapo) wananunua pamba kwa bei ya chini,kwanini usianze kwa kuonyesha mfano kwa wanunuzi wengine ununue kwa beei nzuri?
Na kama ungekuwa mkweli na unasimamia maslahi ya wakulima basi usingekubali kurudisha shilingi yako kwa majibu mepesi kiasi kile. Hapo ungeweza kuonyesha kweli kwamba una dhamira safi. Lakini kwakuwa hukuweza kusimamia hoja yako na sina kumbukumbu ni hoja gani umewahi kuisimamia hadi mwisho tangu uingie bungeni basi sina shaka kwamba ulikuwa unatafuta cheap popularity. Maandamano kuelekea mgodi wa resolute ni mfano wa kulegalega kwako.
 
<br />
<br />
labda alitaka udai bei ya pamba ishuke ili upate hasara, bila kuangalia athari ya mtazamo wake kwa wakulima wa pamba. Labda mwita hajakuelewa, la msingi Mheshimiwa HK nakugongea 5 kwa kufanya kazi uliyotumwa na wapiga kura wako, tambua kuwa wachangiaji wengi humu akiwemo mimi mwenyewe si mpiga kura wako. Tunaweza kukushauri jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wako, na kuweza kuisaidi nchi yako in general. Wapiga kura wako waliokuchagua na kukufanya uwepo hapo mjengoni ni bora kuliko wengine. Japo mimi si mpiga kura wako, na wala si mwana magamba, nimefuatilia sana hoja zako, na nimeona nyingi ni kwa maslahi ya wananchi na taifa, na hata ile hoja ya Butiama was for the public interests, japo mengine unajikanganya it is not very much the case. May be what I have observed is that you were not supposed to be on that part.

FOF usitake kusema kwamba mimi simuelewi Kigwangala,ninamuelewa sana. Kitu kinacholeta wasiwasi ni kwamba huyu mkulu ni mfanyabiashara ya pamba na hawa ndio wanaowanyonya wakulima wa pamba. Serikali ilipotoa pesa ya stimulus package waliofaidika ni hawa wafanyabiashara,wakulima hawakupata chochote huku wafanyabiashara wakizidi kuneemeka.
Ni wafanyabiashara hawa hawa akina Kigwangala ndio walioshusha bei ya pamba sasa unataka kuniambia hiyo jeuri ya kuwatetea wakulima haikuwa ni kuwahadaa wananchi hususani wakulima wa pamba? Fungua macho kidogo tu utanielewa.
 
Nyanda,

Ipo siku ahadi itatimi9a, kuahirisha kitu si kuacha kutekeleza. Kuna mazungumzo yalianza baina ya serikali, watu wa mgodi na mimi nikiwawakilisha wananzega - yalianza kwenda vizuri japokuwa sasa hivi yanasuasua na hivyo lolote linaweza kutokea very soon

Ndugu HK, kwa kumbukumbu zangu mara zote unapoongelea suala la mgodi wa Resolute uwa unaonyesha kuchoshwa na mazungumzo yasiyozaa matunda na ndio maana majuzi ukasema upo tayari kuungana na wananzega kwenda pale mgodini na kufanya yale uliyoyasema bungeni. Sasa huoni kama unakua kigeugeu?! Jaguar- Kigeugeu (Official Ogopa Video ).mp4 - YouTube
 
Jamani kwenye ukweli tusifie, hata kama chadema kuna mabaya na mazuri lakini sio kweli kwamba kwasababu yuko ccm basi ndo kila mtu hafai. Huyu Daktari mi namkubali saaaaaaaaaana, hamumunyi maneno, kama ovyo atasema hiyo ni ovyo, kama kweli basi atasifia. Tuwe wakweli, huyu jamaa kama unamfuatilia huwa ana contributions nzuri sana. Wasiwasi wangu ni kama atadumu ndani ya chama chake au jimbo lake.

Mimi sitaki kuwa mnafiki wala sitaki kupata dhambi bure kwa kutokuwa mkweli au kumpa sifa anayestahili kusifiwa na kumpuuza fisadi na dhalimu. Aisee Kigwangala pambana juhudi zako tunaziona na unajitahidi sana kutetea watu wako na ndicho ulichokifuata humo mjengoni.

Usife moyo ila kama unafanya haya kupoteza lengo ili ufanye hadaa kwa kuwawekea CCM mazingira mazuri ya ushindi 2015 sisi tutakulaani na itakuwa 2015 ni mazishi ya your political career.
 
Mnasifia msichokijua. Hamuwaoni wapambanaji au ndo umetumwa kupiga debe.
 
anachokifanya nikuzoofisha ccm kwa ujumla maana ukiwa ndani ya gamba hutakiwi kuwa msafi bali ukubaliane na uchafu uliomo
 
Back
Top Bottom