Dr. Kigwangala: another Lucas Selelii

Kwanza ni Mrundi. Aende kwao akaonyeshe makali yake wamsulubishe mara moja

Siasa za magamba hizi na huchelewi kusikia uchaguzi ujao yeye ataaambiwa sio raia wa Tz na wakampa bashe, magamba kweli siwawezi
 
Aliwekwa na Jakaya Kikwete kwa nguvu... Walimziba Msomali, sasa wamempata mgushi jina...

Yatawatoka Macho CCM... GOOD 4 them...
 
WanaJFMhe. Dr. Kigwangala ni kijana na ana elimu nzuri, hivyo ni vema akasimama kidete bila unafiki kuwatetea wananchi wa Nzega. Nchi hii imezidi na ahadi za uongo na unafiki mkubwa.......Subirini 2015.....hata kama CCM watashinda lakini bado wabunge wake takribani 80% watakuwa vijana zaidi ya akina Mhe. Dr. Kigwangala

Wana JF,

Tuwe wazi kama katetea issue kwa maslahi ya nchi tumpe credit yake. na tuone hiyo serikali yake itatekeleza au? Tatizo la CCM ni kukitetea chama na maslahi yao binafsi ukiwapinga wanakuona hapana sielewi kwanini?
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Wana JF tuwe fair..
siyo ukimpongeza mtu wa CCM basi na wewe ni magamba au umelipwa kuna waadilifu ndani ya sisi ingawa wamefunikwa na baadhi wanafanya kwa malengo yao binafsi zaidi...Mbona Mbowe alipongeza January Makamba

Suala siyo kuwa fair, hapa tunaongelea uadilifu wa mtu katika hali ya uhalisia
na si jinsi anayovutia vyombo vya habari. Kwa taarifa yako mimi si shabiki wa
kiongozi au chama chochote bali nachangia kutokana na jinsi nijuavyo, siandiki
ili kumfurahisha mtu...
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Wala msiende mbali wana JF mna macho mliyaona mna masikio mlisikia kuweni waangalifu sana na hao magamba,huyu Dr.HK KITU GANI ??????issue sio tuwe fair G55 WALIPOTISHWA hawakuthubutu kufanya maamuzi magumu kukiacha chama chao kipasuke walinywea,ni wabunge haohao mwaka jana tu ilipozuka suala la Richmond wengi tuliwaona ni mashujaa walijipiga vifua wakisema pangechimbika waaaapi!!!!!!upupu mtupu
walipotishwa wakanywea leo Dr.hk namuunganisha na hao ambao leo hii kati yao ni mawaziri na wengine manaibu.anatafuta umaarufu tuu.
 
Sigma
Re: Dr. Kigwangala: another Lucas Selelii
Mi sijui anakoenda.
j3 akiongea anaiponda serikali,
jumanne akiongea anaisifia serikali yake ilivo makini.
Kind of he is pondering which side to take.
Ni kama Tanzania enzi ya Cold war na Non-aligned movement ili kumega ugali huku na kuchovya mboga kule.

HANA LOLOTE HUYO, ALITUAMBIA WANA NZEGA TUANDAMANE KWENDA MGODINI, HALAFU AKASIFIA WAWEKEZAJI KUWA WANALETA UJUZI.KUMBUKENI ALIVYONYAMAZISHWA NA TUNDULISU SIKU ILE BUNGENI​
 
lile jembe, lucas selelii angefaa kuwa waziri kuliko mawaziri wengi wa jk. Hata pinda mwenyewe hafikii uwezo wa selelii, tuwe wakweli.
 
huyu jamaa anatafuta umaarufu kwa kutetea wananchi kwa sera zisizo za chama chake lengo nikuwa karibu na wananchi mwaka 2015 wamrudishe mjengoni la sivyo bashe nae anataka kupita hapo hapo!
tafadhari siungi mkono hoja yako hawa watu walidhani moto wa selelii umezimwa sasa chipukizi limekuja na moto mpya huyu bwana japo alipewa ubunge kapuni lakini nadhani hata yule bashe asingekuwa moto kama huyu dr ni maarufu haitaji umaarufu pia ni mzalendo wa kweli kama kikwete angekuwa na mshauri makini kama mimi january makamba na dr kigwangara angewapa wizara very simple angemwondoa maua daftari ,wasira ,sophia simba wangemsaidia bada ya yeye kuwa saidia maziri wake, dr wa ukweli siungi mkono hoja yako
 
Kigwangala amejitahidi lakini bado hajafanya lolote la tofauti na wana ccm wengine. Porojo tumezizoea toka enzo zile za "ifikapo mwaka elfu mbili", sera na mipango katika maandishi na maneno tumeiichoka, kiu yetu ni vitendo katika kutekeleza sera na mipango ili kukuza uchumi wa Taifa na kuleta maeendeleo ya mtu mmoja mmoja. Atueleze mpango wa Maandamano kushinikiza kufungwa kwa mugodi wa Buzwagi umefikia wapi na utahitimishwa lini?
 
Huyu Dr. Kigangwala sio mtu mwema, chambo tu, amewekwa hapo kwa maslahi ya serikali.

Kama mnakumbuka wakati bajeti ya kilimo inapitishwa, aliwakera wabunge na wananchi wa kanda ya ziwa, bahada ya kuondoa shillingi na kuungwa mkono na wabunge wengi, kusema ukweli wananchi wengi walitegemea pale ndipo wabunge wao pa kuibania serikali ili itoe majibu yanayoeleweka kuhusu bei ya pamba.

Lakini alichofanya Dk Kigangwala, kama kawa akatoa shillingi, na akaungwa mkono na wabunge kibao, mpaka wakateua bahadhi ya wabunge wakakaa kikao kujadili hili swala.

Bahada ya hapo Waziri Mkuu akasimama kutetea bajeti ya wizara ya kilimo, Bahada ya hapo akaulizwa mtoa shillingi "vipi Dk bahada ya maelezo hayo ya waziri mkuu, bado unaendelea na msimamo wako wa kutoa shillingi"

Dk Kigangwala akacheka alafu akatamka "nairudisha shillingi yangu"
Tangu siku hiyo mpaka hivi leo wafanyabiashara wanajinunulia pamba kwa bei wanayoitaka, ma DC walikuwa wanawatetea wakulima wameacha, wanasema kama wabunge wenu wameshindwa kuwatetea, na ndio mliowapigia kura sembuse sisi.

Pale Dr Kigwangala alikuwa anawazingua wabunge ili wamuunge mkono alafu awatose, na ndivyo alivyofanya.
Nionavyo mimi ni kuwa, huyu ameandaliwa na serikali ili atoe shillingi watu wamuunge mkono alafu awatose, kama alivyowatosa wazee wa pamba, mpaka leo umeshasikia kelele za kwenye pamba. Serikali imetangaza bei 1100 na watu wananunua 600, hapo mpo?
 
and we think we are great thinkers......... poooooooooooooooooooooooooooooof!!!
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Hongera Dr. Kigwangala kwa kazi uliyoifanya ila sasa unatakiwa usahihishe kwa kumrudia mwenye jina lake na mumalize tofauti nae vinginevyo nawewe ni kati ya hao mapunguani
 
..kuna mahali Hussein Bashe amedai Selelii alikuwa akifadhiliwa na Rostam Azizi.
 
Mi sijui anakoenda.
j3 akiongea anaiponda serikali,
jumanne akiongea anaisifia serikali yake ilivo makini.
Kind of he is pondering which side to take.
Ni kama Tanzania enzi ya Cold war na Non-aligned movement ili kumega ugali huku na kuchovya mboga kule.

Mkuu kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo utakubaliana na mimi kwamba behaviour za wabunge wa CCM ni kama hali ya hewa: Mara jua mara mvua baada ya muda baridi. Tatizo ni kwamba wabunge wa CCM wanaona kwamba uwezekano wa CCM kurudi mwaka 2015 unaenda ukififia kila kukicha. Sasa wale wabunge wajanja wameanza taratibu kujifanya wako kwa wananchi ama kwa wapinzani ili ikifika muda wakiona meli yao inazama waweze kupata maboya yaani wahamie upinzani hasa CDM na kupokelewa kwa kuwa watakuwa wamejipambanua kuwa walikuwa ni wapinzani ndani ya CCM. Hakika nakuambia kuelekea 2015 tutaona mengi ya ajabu.
 
Kigwangala ni mwenzetu humu JF. tatizo linalowapata wana-CCM wanaojichanganya kama huyu ni kwamba anaona jinsi wananchi tulivo wakali na tulivyo na hoja.

Kuna mbunge anaitwa Rozi Kirigini nilimshangaa sana eti alipomshangaa Magufuli kusoma bajeti kwa kutumia laptop. Watu kama huyu mdada Kirigini hawajui kuwa mtu kama Kigwangala anashinda kwenye blacberry anaona tunavotembeza hoja.

Kigwangala anajua wazi akileta unafiki mle bungeni basi inabidi ajiondoe humu JF awaachie kina Zitto.

Binafsi sikuamini nilipomuona Kigwangala kwenye WANABIDII FORUM akiwaponda Spika na Naibu wake kwamba hawapendi sana hoja binafsi na kwamba yeye kapeleka mara tano na zimekataliwa. SIna hakika na hoja zake lakini nadhani aiha zilihusu mambo ya madini, au benki.

Ukikataliwa hoja binafsi haitangazwi. Hivyo sishangai akisema hivi kwamba anajua bajeti itapitishwa kwa wingi wa kura lakini basi walau yeye asije kulaumiwa na watakaosoma hansard.

Ni kweli tunasoma hansard na tunawabana humu JF wala hatusubiri wajukuu zetu watufanyie hiyo kazi.

Siko CHADEMA, siko CCM lakini big upa Kigwangala na wabunge wote walioko mitandaoni kama JF wakiwemo Zitto, Regia Mtema.
 
Kwa mtu anayeuelewa mchezo wa kupita kwenye kamba iliyofungwa kwenye miti miwili tofauti atagundua kwamba this is a kind of game Dr, HK is playing - a balancing act, whereby the doc's trying to remain on the rope afloat making sure that he doesn't fall whilst impressing the audience.
Gamba ni gamba, kapinga hoja kwa 100% ilibidi aende mbali na kutoa shilling kwenye bajeti ya maji.
Usanii wa CCM ni mkubwa kwani hao mavuvuzela wa magamba wakikataa bajeti ya serikali rais anavunja bunge! Magamba mangapi yatarudi?
 
Back
Top Bottom