Dr. Karume Apigiwa Wimbo wa Taifa Zanzibar

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Wana JF;

Leo nimesikia Dr. Karume akipigiwa Wimbo wa Taifa wa Zanzibar.

Mjasiliamali naye alikuwepo.

I might be out of touch . . . Hii ya "Dr" na "Wimbo wa Taifa Zanzibar" imekaaje?
 
Wana JF;

Leo nimesikia Dr. Karume akipigiwa Wimbo wa Taifa wa Zanzibar.

Mjasiliamali naye alikuwepo.

I might be out of touch . . . Hii ya "Dr" na "Wimbo wa Taifa Zanzibar" imekaaje?

Yakhe! ndo muungano huo, weye mbona waghafilika!
 
Yakhe! ndo muungano huo, weye mbona waghafilika!

Yakhe! Mie nilikuwa sijui ati! Nadhani nilighafirika . . .

Nshazoea "Mungu Ibariki mie" naye wala sikujua kuwa anao Udakteri eti!

Hayaaa . . . namiombeni radhi . . . Muungano udumu!
 
Muungano wenye mataifa mawili, safi sana. Na ili kunogesha sherehe hizo, wamesombwa wananchi toka mikoa yote ya Zanzibar. Uwanja umefurika, guess the cost!
 
Muungano wenye mataifa mawili, safi sana. Na ili kunogesha sherehe hizo, wamesombwa wananchi toka mikoa yote ya Zanzibar. Uwanja umefurika, guess the cost!

Yakhe asante kwa unayoyasema . . . Ni kweli uwanja umefurika . . .

Halafu yakhe kunogesha Muungano hata site tumeanza kutoa namba mpya za magari . . . .

Huoni sasa Muungano ume-balance?

Haya yakhe, mie bado naangalia gwaride . . . .

Umewaona vijana "Chipukizi wa CCM" wakiongoza maandamano?
 
eti Dr Karume.....

Yakhe kwani weye ulikuwa ujui kuwa Rais wa Zanzbar ni Dakreri? Au mtangazaji kakosea? Maana kila wakati amtaja kama Dr. Karume?

Hebu nielemisheni . . . Au kuna mahali alipewa Udaktari wa Heshima?
 
Yakhe kwani weye ulikuwa ujui kuwa Rais wa Zanzbar ni Dakreri? Au mtangazaji kakosea? Maana kila wakati amtaja kama Dr. Karume?

Hebu nielemisheni . . . Au kuna mahali alipewa Udaktari wa Heshima?

Karume alipewa udaktari wa heshima na chuo kimoja cha Marekani. Ndio maana unasikia wanamwita Dr. Karume.
 
Wakuu kuwa doktor sio kazi sana kama mnavyoweza kudhani. Ukitembelea chuo kikuu fulani mara mbili mara tatu unaweza kuvikwa kigauni na kakofia ka u-doktori.
Au mmesahau jinsi nduli wa uganda alivyowaagiza watu wamwite Dr. HE. General, CBE, Alhaji;;;;;;; yote yawezekana. Hata sio vigumu sana.
 
LOL

Kazi kweli kweli . . . . nimekupata Mkuu.

Cheers!
 
Zanzibar kuwa na wimbo wao wa taifa, bendera, Rais nk, nadhani sio kitu tunachotakiwa kutuumiza kichwa, muhimu ni jinsi gani ya huu Muungano kuuweka ili pande zote angalau ziridhike. Kusiwepo upande unaoona kuwa upande fulani una maslahi zaidi kuliko mwingine. Lakini yote haya yameharibiwa na waliouanzisha, na pia waliotakiwa kuulinda. Yale mambo muhimu yaliyokubalika kwa huu muungano hayafuatwi, ama yameondolewa kinyemela, ama kuna mambo yameongezwa bila kufanya utafiti wa athari zake.

Lakini kubwa ni kutoshirikishwa WANANCHI kuamua Muungano uwe vipi. Viongozi kukaa wenyewe na kupitisha wanavyofikiri/wanavyotaka uwe. Mfano ni pale ulipokuwa unaanza mfumo wa vyama vingi, wakaangalia wakaona yawezekana Bara ikashinda CCM, Zanzibar wakashinda wapizani, na wakati huo Rais wa Zanziba alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, wakaona haitafaa Rais wa Jamhuri ya Muungano atoke CCM, na makamu wake wa kwanza atoke upinzani. Hivyo cheo cha Rais wa Zanziba kuwa makamu wa kwanza wa Rais kikaondolewa.
 
Kikubwa kinachopaswa kufanywa hivi sasa ni kuuangalia Muungano kwa mapana zaidi. Ni kweli kuwa tunauhitaji Muungano lakini si katika sura na muundo uliopo sasa kwa sababu unatuletea matatizo badala ya fanaka tuliyoitarajia. Umefika wakati sasa uandaliwe mjadala wa kitaifa kuhusu Muungano na ifikiwe muafaka wa nini kinachptakiwa na watanzania wengi. mtindo huu wa kuwa watumwa wa hitoria utaendelea kuturudisha nyuma kila siku kwa sababu badala ya kufanya mambo ya maendeleo tunapoteza muda na tasilimali nyingine kujadili masuala ambayo tungeweza kuyajadili mara moja na kukubaliana
 
Yah, yah, yah!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Unanikumbusha enzi za "Zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa....................!!!!!!!!!!"

By the way, Hongera kwa Zanzibar kutimiza miaka 45 ya Mapinduzi!!!
 
Mnalazimisha tu muungano hakuna Mzenj anaetaka muungano wa kijanja. Gesi na mafuta!! Zahabu je?.
 
Karume alipewa udaktari wa heshima na chuo kimoja cha Marekani. Ndio maana unasikia wanamwita Dr. Karume.

Zamani ukipewa PhD ya heshima basi kweli unaheshimika kwa mchango wako uliotukuka kwa jamii au dunia kwa ujumla.
Lakini siku hizi wanajigawia tu kama njugu,mara Dr.Kikwete,mara Karume,Mzindakaya sijui....
 
Mkuu Mtarajiwa, Dr. nini bwana , kuna Maprofesa Maji Marefu!!!
Kila mtu anapenda usomi asiouhenyea.
 
Zamani ukipewa PhD ya heshima basi kweli unaheshimika kwa mchango wako uliotukuka kwa jamii au dunia kwa ujumla.
Lakini siku hizi wanajigawia tu kama njugu,mara Dr.Kikwete,mara Karume,Mzindakaya sijui....
Wacha wivu wewe...!
 
Wazanzibar wananifurahisha sana. Wanafanya mambo yao taratibu, kimya kimya lakini kwa uhakika. Hivi sasa wana bendera yao, wimbo wao wa Taifa, na idara ya serikali inayohusika na usajili wa namba za magari yanayoingizwa huko. Muda si mrefu watakuwa na Idara yao ya kodi ya mapato, currency yao na hatimaye passport yao. Wakikamilisha hayo wanakuwa sawa na nchi yoyote ile duniani.

Sisi bado tumebung'aa na serikali ya Muungano wakati wenzetu wameshauasi muungano siku nyingi sana. Viongozi wa juu serikalini wakisikia unatamka Tanganyika wanakuona kama ni msaliti mkubwa!!!

Kila la heri Wazenj labda nasi tutapata Tanganyika yetu kwa kupitia mlango wa nyuma maana mkishakamilisha yote hayo hapo juu basi itakuwa zamu yetu kudai Tanganyika kwa nguvu zote maana kutakuwa hakuna Muungano tena utakuwa umeshaporomoka kabisa.
 
Back
Top Bottom