Dr. Kaborou aiacha CHADEMA, Ajiunga CCM

kizazi cha kina Kaborou,Hiza na Kasaka ni kizazi chakavu hakina uwezo tena wa kuleta mabadiliko.Wamefikia ukomo wao wa kufikiri na kubuni.

Kizazi kipya kinapaswa kutafsiri mauzauza haya kama filimbi ya kuwaita waingia ulingoni.Maana sasa badala ya kujadili hoja tutakuwa tunajadili fulani katoka CHADEMA kaenda CCM,siasa zinachukua sura za watu badala ya hoja.Tunataka ushindani wa hoja ambazo hatimae zitaleta maendeleo badala ya kujadili watu!

Nimesikia jana kwenye vyombo vya Habari,anadai eti CCM ina sera nzuri,sasa hakuzisikia hizi sera wakati wa kampeni?

Makamba nae anachekelea galasa! Hakika wamejichokea! Tunataka siasa zitakazo sababisha mruko,siasa zitakazo chochea maendeleo sio hizi za kizamani!

Cha kuchekesha ni namna Habari ilivyoripotiwa kwenye gazeti la Mtanzania la Tarehe 20 septemba! Wanasema moja ya sababu ya kujitoa ni kwa kuwa Freeman ameonyesha upendeleo kwa wanasiasa vijana na wasomi! Hainingii akilini kuchukuziwa na jambo chanya kama hili! Chama chochote makini kinahitaji vijana wasomi!

Hu ni wakati wa kizazi kipya kuchukua nafasi yake!
 
Tufike mahala tuwe watu wazima na tukumbuke na kujiuliza .Kwanza katika wote akiwemo Kaburu hajasema kitu gani kinamwondoa Chadema .Habari za ndani ni kwamba amekuwa hawezi kuendana na kasi ya Chama kwa sasa .Pia ameona mwazo yake yamepitwa na yeye aliandaliwa na CCM siku nyingi kuondoka bado angali Mbunge.Dalili zale zilikuwa wazi tangia akiwa Mbunge na watu walipiga kelele.

Kaburu hakuwa agent wakati anaingia Upinzani hapana ila amekuwa agent baada ya kuanza kueleweka kwenye Siasa ndipo CCM wakaanza kumtafuta na wamempata lakini bado si pengo kwa Upinzani maana Kaburu kwanza ni nani ?

Mzee Es hapa kuna mada inasema CCM kummaliza Mbowe nawe umekuwa ukipinga sana sana .Sijui ulikuwa unapinga nini mzee.Ni swala la kujiuliza kama mtu akisema juu ya Kuimaliza CCM ama Serikali basi lazima uongozi wake utakwua unahusika na hasa wakisema sema Mbowe .Sasa ndiyo majibu kwamba CCM inataka kummbomoa Mbowe na Chadema lakini wana safari ndefu sana . Ongara umesema maneno mazito na CCM na wewe Es mjue kwamba si rahisi mkawanunua watu na kila mwanzo una mwisho.Kaburu mwacheni aende ni hai yake na wote wana ondoka baada ya kukosa madaraka na hawana impact yeyote end of the day . CCM wanajimaliza wenyewe kwa mikataba feki na kuleta longolongo wandhani kuja Bush Tanzania ni sifa kwa Nchi wakatii watu wana mateso makubwa na hata Elimu wanakosa kulipiwa na serikali yao .

Ni kweli CCM inambomoa Mbowe haya ni baadhi ya majibu hakuna ubisihi.
 
Tibwilitibilwi, umetibilwi!. Si ni huyu huyu Kaburu aliyekula dili na wana CCM kuficha kashfa ya Kitine? Sikushangaa.
 
Huyu Kaborou jamani kachungulia ubunge wa Africa Mashariki.
Kwenye mada nyingine lilijadiliwa suala kuhusu hawa viongozi kuhama,maana ukiangalia trend ya viongozi wa upinzani kurudi au kuhamia CCM ya wakati huu wa Kikwete inasikitisha.Huko nyuma tulikuwa tunasikia majina ya viongozi ambao hata hatujawahi kuwasikia,lakini sasa unasikia Tambwe,Kaborou etc Hii ni dalilli tosha kuwa upinzani sasa ndio basi.Hata kama Freeman anajaza vijana wasomi kwenye chama chake,ambao wengi wao kawapa ubunge,lakini hata hawa mwisho wao ni huohuo.Sasa hawa wabunge waliopewa viti maalum ,ule muda ukiisha,na majimboni huko ni kama tunavyojua,baada ya uchaguzi wa kwanza 1995,wapinzani idadi yao bungeni imezidi kupungua na itaendelea kupungua,which means viti maalum idadi yake itapungua pia,wengi wa hawa utasikia wamejiunga na CCM.
Loathe it or love it,lakini CCM will rule for a very long time to come.Wakati muafaka wa kuishinda CCM,ulikuwa ni 1995.Kwa sababu here was the 1st time voters of this country had an alternative.Lakini upinzani ulishindwa kuitumia nafasi hio vizuri.Uchaguzi uliopita watu walikuwa na imani kuwa Freeman angezoa kura nyingi sana,asingeweza kuishinda CCM,lakini angalau angemshinda Lipumba,that never happened,so whats next?
Ni kama alivyosema Mwalimu,ni mpaka CCM igawanyike,na uwezekano huo ulijitokeza kidogo katika kutafuta mgombea wa rais mwaka jana,lakini wenyewe wakayarekebisha na wakaweka mambo sawa.
Baada ya mda utaona watu wanajijengea umaarufu upinzani ili wajiunge na CCM baadae,maana sasa hio ndio itakuwa shortcut to ubunge,u-DC,RC n.k Tanzania imebarikiwa jamani,wacheni mchezo!
 
Jamii zenye kujali maendeleo, suala la ustawi wa demokrasia ni muhimu. Mfum wa vyama vingi umeonwa ni mfumo mbadala wa kuweza walau kutoa challenge kwa serikali yoyote iliyoko madarakani. Suala la afya ya upinzani nchini Tanzania kama ni dhaifu linatia hofu dhana nzima ya ustawi huu wa demokrasia kama chachu ya maendeleo.
Chanzo ni kipi? sera mbovu za upinzani,sababu za kimazingira na kihistoria au..?Tanzania ya leo siioni kama iko tofauti na nchi kama Kenya,Zambia, Malawi,nk. Nchi hizi kutokana na rekodi ya matokeo ya uchaguzi yanaonyesha kama wapinzani huweza kufurukuta, Tanzania tatizo liko wapi?

Mawazo yangu (naweza nikayaita mawazo hewa), serikli iliyoko madarakani kama kweli inajali maendeleo, kwa upande wangu naamini hivyo..iwachukulie wapinzani kama kioo chao na si maadui,wasaliti na watu wakuogopwa. Vyombo vya habari vitambue kazi zao na maadili ya kazi zao ikiwa ni pamoja na kuonya, kuadabisha na kuadilisha bila kujiweka karibu na wanasiasa.Mihimili mingine nayo ifuate mwendendo huu, polisi,mahakama, nk.
 
Guys,

Points nzito, lakini wote mna-miss the big picture nayo ni kwamba hao wote waliorejea CCM,

Ukweli ni kwamba hawakuwa upinzani toka mwanzoni, isipokuwa walikuwa waongo tu huhitaji kuwa professor, kuelewa hilo,

ninachosema ni kuwa, kama kuna wafuasi wa upinzani humu, hii ni wake up call kuviangalia vyama vyenu kwa makini na kuvichunguza ili kujua nani ni wenu au sio wenu, ni bora kuwa na wanachama wawili na kiongozi mmoja tu!, kuliko kuwa na wanachama maelfu na viongozi kama mlionao sasa hivi,

ninasema hivi, the only way kwa kiongozi yoyote wa upinzani kushamiri na biashara bongo leo, kama kina Freeman, Ndesamburo, na Slaa, ni lazima uwe na something na CCM, ama sivyo muulizeni Mzee Mapesa jinsi CCM walivyomnyang'anya nyumba!

Amukeni musafishe vyama vyenu kwanza ndio mutuongoze kwenye taifa!
 
Ni Hatari kuwa na fikra kwamba CCM itatawala milele! Na kama hali itaendelea kuwa kama ilivyo sasa na maendeleo yakiwa duni Tanzania italekea pabaya!

Watu watakata tamaa na vyama vya upinzani,baada ya hapo watakata tamaa na siasa! Matokeo yake watatafuta mfumo mbadala wa kuleta mabadiliko nchini,ole wake Tanzania.

Nashangalia kila ninaposikia vijana wanajiunga na vyama vya upinzani kwa maana ina maanisha bado watu wanaamini mabadiliko yatapatikana kupitia mfumo wa siasa.

Pamoja na uwizi wa CCM kwenye uchaguzi,bado CCM inacheza ligi ya peke yake! Ndio yenye rasilimali ambayo matokeo yake huvutia wataalaam,matajiri na wanafiki wengi!

Kwani mapambano ya kisiasa yako maeneo gani? Si ni Rasilimali,sera na watu.Kwa kuwa kuna tofauti kubwa katika eneo la rasilimali CCM inakuwa imekamata eneo moja la mapambano,kisha inakamata watu maeneo haya mawili yanafunika sera! Siasa za Tanzania hazina sura ya sera,watu hawapigi kura kulingana na sera na sehemu kubwa ya kampeni watu hawazungumzii sera! Kama tungekuwa tunachagua kwa sera CCM isingeshinda mwaka jana.

Kampeni za Kikwete hazikuwa na sera! Aliaahidi mambo kulingana na mahitaji ya eneo na sio kulingana na ilani ya uchaguzi.Mwenyewe alidai kuna ahadi za ilani na ahadi za papo kwa hapo! Haya ni masihara,kwa sababu ilani inapoandaliw,vyama huangalia rasilimali zilizopo na zitakazo patikana na kisha kuanisha vipaumbele! Ahadi za papo kwa hapo zina ulikini mkubwa! Kisha alithibitisha kuwa ilani yao ni kiini macho,alipokuwa anamponda Mbowe kwa Kuruka na chopper,walidai wanaenda kwa usafiri wa barabara ili watambue matatizo ya wananchi,sasa unawezaje kuwa na ilani kama hufahamu matatizo ya wananchi?

Tatizo la siasa za Tanazania sio kwa upinzani pekee! Tuna wanaisasa makini wachache mno,iwe ndani au nje ya CCM!

Ni lazima kuwe na wimbi kubwa la watu na rasilimali kuelekea upinzani na hatimae tuanze ushindani wa sera.Na huu ndio utakuwa mwanzo wa utungu!
 
Eric,

Wananchi wamelala, ni wavivu wa kufikiri kwasababu hawana shule. Ni rahisi sana kuwadanganya hawa wananchi. Hawajui faida ya kulipa kodi wala hasara ya kutoa rushwa wala kiongozi serikalini anamuathiri vipi!

CCM itatawala milele mpaka kizazi hiki kiishe!

FD
 
Ila hii ya Kaborou ni njaa na usaliti. Mi ningekuwa JK au Makamba watu kama hawa wala siwapokei, tena naweza hata kuwanyima kadi ya uanachama.

FD
 
Jasusi, niwe shabiki wa CCM au sio ,huo ndio ukweli ninavyouona mimi.
Kweli unaweza kuniambia kuna dalili ya CCM kushindwa kwenye chaguzi zijazo?
Serikali ndio inayovipa pesa hivi vyama kujiendesha,sasa kwa mantiki hiyo kweli inawezekana kumshinda mtu anayekulisha?
Kwa mfumo wa vyama vya siasa tulionao hapa,ni rahisi sana kwa serikali kuvimaliza.Maana tulishasikia huko nyuma msajili wa vyama akitishia kukifuta chama fulani,na hii post ya msajili wa vyama sio ya kuchaguliwa,anateuliwa na rais baada ya kupendekezwa na jaji mkuu,kama sikosei.
Kuna mifano imetolewa kuwa Tanzania haina tofauti na nchi kama Kenya,Zambia na Malawi....inawezekana,ila kilichotokea Kenya ni kwamba ile ni KANU iligawanyika,kutokana na wengi kutopendezewa na choice ya Professor wa politics(Moi) kumweka Kenyatta kama mmgombea wa chama cha Kanu.Wakajitoa na kujiunga na chama cha Mwai Kibaki,vinginevyo kama Raila Odinga angekuwa ndio mgombea wa Kanu,wangeshinda tena.
Zambia,chama cha Chiluba kilishinda uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi,Kaunda aliombwa hata na Mwalimu aachie ngazi,awapishe vijana kwenye chama chake wagombee,akabisha,na matokeo yake akashindwa,Banda wa Malawi nae alikutwa na hilohilo,uchaguzi wa kwanza akapigwa chini.Hata hapa Tanzania,Mrema pamoja na timu yake ya wakina Marando,Lamwai,Mbatia etc,walionyesha dalili kuwa lingewezekana wakati ule.Watu walicho sahau wakati ule ni kuwa CCM mradi wake unaanzia kwenye wenyeviti wa nyumba kumi,ina maana chi nzima katika kila nyumba kumi kuna mtu au familia ya CCM,wapinzani wao waliangalia mijini tu kwenye 25% ya population,ile 75% ya vijijini wakaipuuzia,matokeo yake ni kushindwa uchaguzi na kusema wameibiwa kura.
Wengine tunasikia wanaingia kenye kugombea urais,kwa sababu ukigombea urais,na ukapata wabunge,au juu ya asilimia fulani ya kura za urai(sina uhakika na hizo details,mwenye nazo anisaidie) kuna pesa nyingi serikali inalipa hicho chama kila mwezi,ukiachilia mbali ruzuku ya kawaida inayopatikana na kuwa na wabunge,sasa kweli hapa upinzani si ni jina tu?
 
Binafsi sifurahishwi na hali ya siasa zetu Bongo, yaani CCM vs Upinzani (Ushindani). Ndiyo maana napenda tujiulize, ikiwezekana tutafiti, kisha tujadili (inakuwa kama jina la mwanabodi fulani humu ndani!) NINI TATIZO LETU KAMA TAIFA?
Sijaridhika na hoja kuwa Watanzania/wananchi ni wavivu wa kufikiri na/au kwamba hawana shule/elimu. Huenda ni suala la kukata (kukatishwa) tamaa na siasa ndiyo maana watu wengi wanaona siasa kama eneo la "kupata kula" na "kwa kutoa kura". Haijalishi unampa nani kura ili mradi wewe unakula. Tusione wananchi wa Manzese wanampa kura fulani baada ya wao kula pilau na kupewa doti za khanga, tukachukulia tu kuwa hawana elimu au hawakufikiri kuhusu athari za uamuzi wao.
Hao waliosoma wamefanya nini? Kuna utafiti uliowahi kuonyesha kuwa wasomi wengi huwa hawaendi kupiga kura! (utafiti ulifanywa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 kama sikosei). Nakumbuka pia kuna kitabu kilitolewa baada ya uchaguzi wa mwaka 1995, Who Votes in Tanzania and Why.

Tukiangalia mchango wa wasomi wetu, wakiwemo maprofesa na madaktari (baadhi yao ndiyo hao kina Dk Kaborou), katika kuleta siasa za ushindani na maendeleo ya taifa kwa ujumla mi bado naona shaka. Naamini wangeweza kufanya zaidi. Unaweza kurejea uchapaji kazi na mchango wa baadhi ya maprofesa na madaktari mawaziri na wabunge katika kipindi cha miaka 10 iliyopita upime uzito wa hoja yangu (mfano Mbilinyi, Mporogomi, Kapuya, Mgombelo, Ngasongwa). Pamoja na hayo hivi sasa ndiyo kuna wimbi la wasomi (achilia mbali kama wana PhD zene kutia shaka pia) kuingia kwenye siasa (active politics). Sasa kama wanaingia huko kwa maslahi yao binafsi au kama wanataka kuleta mabadiliko ya dhati hilo ni suala linaloweza kujadiliwa pia. Huenda Bw Fred naye akarudi na PhD yake ili aje arejee tena kwa kishindo au kasi mpya katika ulingo wa siasa (soma si hasa) za Bongo!

Nitoe rai tena, tujadili NINI TATIZO LETU KAMA TAIFA?
 
Maneno mengo mliyosema hapo juu ni kweli tupu, kwa kuongeza ni kwamba kama kawaida yetu wabongo, huwa tunarukia mambo bila kuyaelewa. Ninaamni kwamba suala zima la vyama vya upinzani halikuwa linaeleweka toka tulipojiunga nalo, tukarukia tuu kama wendawazimu, bila ya kuangalia facts na vile vile kui-underestimate CCM na tamaa yao na madaraka,

tukaruhusu watu very weak politicians kuanzisha upinzani, watu kama Mtei ambao hawakuwa wanasiasa by any world standards za siasa, kina Mrema ambaye aliingia upinzani only baada ya kugundua kuwa hataruhusiwa kugombea akiwa CCM,

tukaruhusu CCM kuweka chini the rules of the game, tena kuwekwa na Mzee JM, ambaye alikuwa tu anaweka idea zake yeye na Kingunge, na Kinana, huku Mwalimu pembeni akipiga chapuo ndogo ndogo, Mwanzilishi wa CCM akituambia namna ya kuujenga upinzani, kina Mrema wakapiga kelele kuwa hata Mwalimu ananiunga mkono, NONESENSE!

Watu kama Kambona, Kassela Bantu, Fundikira, hawa ndio watu ambao tungewategemea kutusaidia, kumbe ni mabomu matupu kwa hiyo ukweli ukasimama kwamba Mwalimu peke yake ndiye aliyekuwa mwanasiasa wa kweli, wengine wote ni Mungu nisaidie, sasa taifa letu limekwama, tizama watu wanaopewa vyeo sasa hivi hivi kweli unategemea nini? Hawa watamwambia nini rais?

Serikali yetu leo imjeaa manyang'au watupu, kila kiongozi anaji-a-line mkao wa kula tu, ebu nimabieni ni lini mmesikia waziri wa awamu ya nne anapiga kelele? Hawa viongozi wa upinzani they have no choice isipokuwa kuwa-join CCM kwenye kula, maana wamejaribu kuwaamsha wananchi lakini hawaaaamshiki, kwa sababu inawezekanaje baada ya kashfa zote za Mkapa Dodoma wakati wa uchaguzi wa rais, wananchi watoke waipigie kura CCM tena kwa 80%? Unajua hata Freeman ninajua kuwa alivunjika nguvu na sidhani kama bado ana ile spirit tena ya kuing'oa CCM,

Jamani hebu once and for all, na sisi wananchi tubebe hii lawama, kuwa sisi nasi ndio chanzo cha kuchezewa na hawa viongozi, kina Kaburu hawana choice bali kujiunga na sisi wananchi tunaoichagua CCM na uozo wote tunaouona!
 
Mzee ES, unachosema kiko karibu na ukweli kuliko mawazo mengi hadi sasa.. let me digest it.. it is heavy stuff
 
Huyu Kaborou jamani kachungulia ubunge wa Africa Mashariki.
Kwenye mada nyingine lilijadiliwa suala kuhusu hawa viongozi kuhama,maana ukiangalia trend ya viongozi wa upinzani kurudi au kuhamia CCM ya wakati huu wa Kikwete inasikitisha
Kama nilivyotabiri hapo mapema,gazeti la leo la Nipashe limeripoti kuwa Dk Kabourou kugombea ubunge EAC.
 
To me kaborou ni opportunist, ningekuwa decision maker wa CCM hata huo ubunge asingeupata. In the mean time CCM haina haja ya mamluki toka upinzani strengthen their grip on power, they only have to deliver their promises. Naomba kumradhi kwa wanaupinzani ndani ya bodi, ila kwa mtizamo wangu upinzani uko ICU kwa hiyo the likes of Kaborou hawatasaidia CCM lolote. Sintoshangaa hata mzee wa Kiraracha naye akirudi
 
mTz,

Hakuna upinzani Tanzania. Tanzania kuna chama cha mapinduzi tu!, ukisikia kuna chama kinaitwa Chadema au CUF basi ujue ni kwenye makaratasi na ni Dar es salaam au Pemba respectively.

Waliudhika na statement hii samahani, lakini kubalini ukweli sulio wazi.

FD
 
Mzee Es umenenena! Umezungumzia maneno mazito sana.Heko ndugu. Hali ya siasa za Tanzania zinasababishwa na wananchi wenyewe. Hata kama CCM wanaiba,sisi tunawaangalia tu?! Hivi Kenya,Zambia,Malawi hakukuwa na uwizi? wao hawakuwa na usalama wa Taifa?!

Fikra duni ndugu yangu mbona unakataa tamaa sasa? Hata CCM katika mizania ya chama ni chama cha siasa? Itikadi si ni sehemu muhimu ya chama? CCM wanaamini nini? wana muelekeo gani? Kuna demokrasia ya kutosha kweli ndani ya CCM?

Angalia namna wanavyoteua wenyeviti? angalia namna wanavyoteua wabunge? Hiki ndio chama cha kileo kinavyopaswa kuendeshwa?

Ni kweli vyama vya siasa vina udhaifu mkubwa sana lakini hii ni habari njema kwa mustakabali wa Tz? sura ya siasa za Tanzania zinaakisi mawazo na matakwa ya wananchi wote.

Ni jukumu letu sote kubadilisha mambo! Vyama vya upinzani kama kilivyo CCM ni vya UMMA na si mali au kampuni ya mtu! Havina watu(kwa sababu hatuendi),havina pesa(kwa sababu hatuvichangii).

Shabaha inapaswa kuviamirisha na sio kuviponda! Ni hatari sana kama kizazi kipya kinakataa tamaa sasa! Hata CCM yenyewe inahitaji mabadiliko makubwa sana!

Tushike kazi!
 
Hii inamaana huko chama tawala hapakuwa na watu vichwa kama Kabouru! Ndo maana wakamghilibu ili akagombee Ubunge EAC! Hapa naona CCM wamejidhalilisha kwamba woote wabunge karibu 260 ni makaputi.....hadi wampate mpinzani awaokoe....!

.............................
:U Can't Change The Nature:
 
Wabunge wa CCM na watu kama FD mawazo yao ni kuwa na chama kimoja.Japokuwa namjua FD hapa kasema mawazo yako tu na anapenda mabadiliko lakini Mzee Es anapenda mabadiliko si kwa CCM kuondoka no kwa CCM kubakia madarakani ila pawe na strong opposition . Kwa Nchi ambayo wanadhani walipewa wao madaraka ya kuitawala Tanzania na si kuiongoza itakuwa mi ndoto sana kukubali upinzani ufanye kazi . Ndiyo maana hata Lowasa anafikia mahala pa kukaripia ama kutoa hongo kwa mapati makubwa ili kupitisha bajeti za uozo leo sitashangaa CCM kumchukua Kaburu na kutaka kuua upinzani maana ndiyo ndoto kubwa na RA na JM .
 
Back
Top Bottom