Dr. Kaborou aiacha CHADEMA, Ajiunga CCM

Duuh! Ndiyo siasa za Bongo. Usishangae siku moja Mzee wa Kiraracha au Profesa wa Unyanyembe nao wakatangaza kujiunga na CCM!
 
Mbona hapa naona picha bila ya maelezo zaidi huyu kahama lini na habari hizi zimetokea wapi tuwekeni sawa tujue siasa za Tanzania zilivyo .Siamini kama ni kweli ila lolote laweza kutokea mbele ya mtu kutaka kula nk .Dalikli zake pia zilionekana mapema sana akiwa Bungeni sasa sijui tuwekeni sawa .
 
Hii habari ilitoka katika Gazeti la Uhuru,. as seen online today 20th Sept 2006
http://www.uhuru.info/

Habari kamili ni kama ilivyo hapo chini:
________________________________________________________________

Kabourou alonga kilichomkimbiza CHADEMA
Ajiunga CCM na vigogo wengine watatu wa upinzani
Makamba asema ni ishara tosha Chama kinakubalika
Na Omar Shaaban, Hai
------------------------------------------------------------------------
mataji8.JPG

Maelezo ya picha:
KATIBU Mkuu wa CCM.Yussuf Makamba akiwa na aliyekuwa makamu Mwentekiti wa Chadema, Dk Walid Kaborou (Kulia) na aliyekuwa katibu Mkuu wa chama cha Sauti ya Umma,Jacob Nkomola, baada ya viongiozi hao kutangaza kuvihama vyama hivyo na kujiunga na CCM, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana, uwanja wa Bamang'ombe, wilayani Hai
------------------------------------------------------------------------


MAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA Dk. Walid Kabourou, amesema amejiunga na CCCM baada ya kuvutiwa na Ilani ya Uchaguzi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika uwanja wa CCM wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro, Dk. Kabourou alisema, ameamua kwa hiari yake bila kulazimishwa na mtu yeyote kurudi CCM, baada ya kuvutiwa na Ilani ya CCM, inayotekelezeka.
Kabourou alisema wengi wanapenda maendeleo yanayofanywa na CCM na hawezi kuendelea kuyapinga hivyo kuamua kuwafuata watu wengi ambao wanakipenda Chama Cha Mapinduzi.
Uamuzi wa kiongozi huyo wa juu wa CHADEMA, na mbunge wa zamani, ni pigo kwa chama hicho cha upinzani ambacho kimekimbiwa wanachama wake wengine wawili.
Mbali na Kabourou wanachama wengine waliojiunga na CCM, wakitokea CHADEMA ni Katibu wa Wilaya, Florence Meela na Anna Samweli, Mjumbe Halamshauri Kuu Taifa.
Chama cha Sauti ya Umma (SAU) nacho kimempoteza Katibu Mkuu wake, Jacob Nkomola, ambaye naye alirejea CCM jana.
Viongozi hao wa upinzani walijiunga na CCM mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba katika mkutano huo wa hadhara.
Wanachama hao wapya wa CCM, waliapishwa tayari kwa utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo na nchi kwa ujumla.
Nkomola alisema kuhama chama si dhambi na kwamba sera nzuri za CCM zinazotekelezeka na uongozi wa serikali ya awamu ya nne vimemvutia kurudi CCM.
Alisema kuwa upinzani ni sawa na kujinyima haki, na kukosa uhuru wa kujiamini, kwa hiyo kurudi kwake CCM, ni sawa na kurudi kwenye wokovu wa kweli na kutenda mema yaliyopo ndani ya CCM.
Katibu Mkuu Makamba alisema, kujiunga na Chama kwa wapinzani hao, ni ishara tosha ya CCM kukubalika miongoni mwa Watanzania.Makamba alisema wananchama wapya hao, watakuwa na kazi kubwa ya kuiendeleza CCM, na kuwaletea wananchi maendeleo.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbrod Slaa, amesema uamuzi Dk. Kabourou kurejea CCM, hauna tofauti na mtu kuhama dini.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Dar es Salaam, alisema kila mtu ana uhuru wake.
Dk. Slaa alisema anachofahamu CHADEMA haina ugomvi na Dk. Kabourou.
Katika harakati za kisiasa, Dk. Kabourou alipata kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini. Akiwa mbunge pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali.
 
Dk. Kaburu kafuata ulaji na si muda mrefu atapewa ulaji huyu, hamna lolote, eti ilani zinazo tekelezeka!!! acheni utani jamani
 
Hawa ndiyo wasomi wetu ambao tunawategemea kutuongoza kwa kuwa wana mwanga .Naamini Kaburu hakuwa na haja ya kufanya haya maana kama ni chakula anacho kwa umri wake .Kushindwa Kigoma ni sawa kama hakufanya la maana wakati akiwa Mbunge .Lakini Kaburu alionekana kwa muda sana kwamba angalienda CCM tangia akiwa Mbunge na nyendo zake watu walisha zipigia kelele mno .Chadema ipo na itaendelea kuwepo .Imetulia na wenye nia njema tu watabakia .Kaburu na kuyatafuta madaraka kwa nguvu alianza zamani sana .Nani hajui historia yake ? Chadema ipo bwana mwache akatafute kula na atapata huko na mgawanyiko ndani ya CCM utaanza maana kama mtu atahaa leo na kesho kuwa Mbunge kama ilivyokuwa kwa akina Mtemvu basi CCM wenye akili lazima kujinga .Kaburu muda sana alisha onekana kutaka kuhama Chama na ni haki yake kabisa kuhama na kuishia CCM.
 
Pale Kigoma kuna kesi ya ubunge ambayo tayari inaelekea mbunge alioko sasa atashindwa na mahama ku-declare uchaguzi urudiwe,

Kwa hiyo huyu mzee amepiga picha na kugundua kuwa ili apite ni bora kurudi kwa maagenti wake wa siku zote, ndizo habari za ndani!
 
Mzee ES!

kumbe jamaa yupo strategic katika kuangalia maslahi ya tumbo lake, no wonder opposition will take ages to achieve benefits anticipated by ndugu wananchi.
 
Halafu ES akiwaambia kuwa mwenyekiti wake ni CCM mnakataa wakati hamna hata vithibitisho.

Kazi kwenu, sisi tunapeta

fd
 
Jamani msimlaumu sana.Siasa bongo ni ajira wala sio service to society.Ndio maana mnaona wasomi wetu (including wale wenye PhD za kuchonga) wanajiingiza kwenye siasa badala ya kusaidia kuinua kiwango cha elimu nchini.Kaburu kazidiwa na njaa na kaamuwa liwalo na liwe lakini mkono shurti uende kinywani.

Mimi sintashngaa mwaka 2010 tukiwa na mgombea mmoja tu wa Urais,Jakaya.Ukichanganya njaa inayovikabili vyama vya upinzani na hujuma wanazofanyiwa na CCM hivi tunategemea kuwa na upinzani kweli,say in 10 yrs time?Hizi habari sio njema hata kidogo,na sio kwenye maendeleo ya demokrasia bali kwenye hatima ya Taifa letu kwa ujumla.Maana upinzani dhaifu ni sawa na kuwa na de-facto single party politics.Sasa angalau zama za chama kimoja tulikuwa na mjamaa Julius Nyerere ambaye pamoja na failure za itikadi zake angalau alikuwa na uchungu wa dhati na nchi yake.Zama hizi za watu kujali matumbo yao bila kuwa na hofu ya upinzani si ndio nchi itauzwa kwa mkopo?

At last nimekuja kugundua umuhimu wa kile kipande cha kwenye wimbo wa Taifa "Mungu Ibariki Tanzania".Tunahitaji sana baraka za Mungu ili nchi yetu iende tunakohitaji sie walalahoi,na wa kutufikisha huko sio wanasiasa wetu bali baraka zake Maulana.Once again,Mungu Ibariki (na kuihurumia) Tanzania.
 
Kuna wakati fulani alipewa uenyekiti wa kamati fulani Bungeni!

Na baada ya hapo nikaanza kuona makali yake yanapungua taratibu.

Lakini kitendo cha kuua upinzani ni kibaya! tunaua upinzani kwa lengo gani?

(1)kuongeza ruzuku kwa CCM?

(2)Au CCM indelee kupitisha mikakataba kwa maslahi ya ccm na viongozi wachache?

Kitendo au utaratibu huu wa kudhalilisha wapinzani siupendi! Japo miye ninaamini upinzani wa kweli uko ndani ya CCM.

kichoendelezwa hapa ni usemi wa jukwaani kuwa tutapambana na rushwa wakati practically tunaiimarisha!

Tutashirikiana na wapinzani wakati practically tunawamaliza!
 
kizazi cha kina Kaborou,Hiza na Kasaka ni kizazi chakavu hakina uwezo tena wa kuleta mabadiliko.Wamefikia ukomo wao wa kufikiri na kubuni.

Kizazi kipya kinapaswa kutafsiri mauzauza haya kama filimbi ya kuwaita waingia ulingoni.Maana sasa badala ya kujadili hoja tutakuwa tunajadili fulani katoka CHADEMA kaenda CCM,siasa zinachukua sura za watu badala ya hoja.Tunataka ushindani wa hoja ambazo hatimae zitaleta maendeleo badala ya kujadili watu!

Nimesikia jana kwenye vyombo vya Habari,anadai eti CCM ina sera nzuri,sasa hakuzisikia hizi sera wakati wa kampeni?

Makamba nae anachekelea galasa! Hakika wamejichokea! Tunataka siasa zitakazo sababisha mruko,siasa zitakazo chochea maendeleo sio hizi za kizamani!

Cha kuchekesha ni namna Habari ilivyoripotiwa kwenye gazeti la Mtanzania la Tarehe 20 desemba! Wanasema moja ya sababu ya kujitoa ni kwa kuwa Freeman ameonyesha upendeleo kwa wanasiasa vijana na wasomi! Haniingii akilini kuchukuziwa na jambo chanya kama hili! Chama chochote makini kinahitaji vijana wasomi!

Hu ni wakati wa kizazi kipya kuchukua nafasi yake!
 
Mlalahoi,
Acha kumbipu Mungu...yaani kwenye Mungu Ibariki tuongeze na Kuihurumia!
Sisi wenyewe hatuhurumiani (soma viongozi wetu hawatuhurumii) kwa hiyo Sir God anaweza akaghairi kutuhurumia!

Admin,
Vipi ukianzisha mjadala kuhusu "Nini tatizo (matatizo) letu kama taifa?" Najua huu ni mjadala mpana sana ambao unaweza kugusa kila nyanja ya maisha yetu. Je, tatizo ni Elimu?(kwamba wananchi wengi hawana, na vyombo vya habari pia vimo kwenye mkondo huo huo, mambo ya Mzumbe kwa mfano kadri yalivyojitokeza na kujadiliwa humu, vyeti feki, etc), Uzalendo? (viongozi na sisi sote), Rushwa? Uvivu wa Kufikiri? (Che Nkapa aliwahi kudai hivyo), Wivu-kwa ujumla, au wa kijinga? (ref. Mzee wa Lupaso) au wa kike (ref. Msekwa ) au Siasa mbovu? Kutoheshimu Taaluma (ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wasomi na hasa wazalendo)? Je, mkazo tuweke wapi ili tujikwamue?

Ama kweli Mungu Ihurumie Tanzania!
 
Sera bomba CCM ulaji ukiyeyuka
http://darhotwire.com/dar/Habari/2006/09/21/24285.html

Kwani wapinzani kurejea tena CCM baada ya mambo kuanza kwenda kombo imekuwa ni fashion, au ni kweli wana machungu ya kweli na nchi hii.

Inabidi tujiulize baada ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Dk. Walid Kabourou kurejea tena Chama cha Mapinduzi kwa madai ya kuvutiwa na sera za CCM zinazotekelezeka.

Hakuna kilichobadilika sana katika sera za CCM (kuwa nzuri)ila kilichobadilika ni kuwa Dk Kabourou alishindwa kufurukuta katika Ubunge wa Kigoma Mjini na hivyo kumwondolea ulaji huo na viulaji vingine ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali alipokuwa Mbunge.

Dr Kabourou anaungana na akina Thomas Ngawaiya (Tanzania
Labour Party), na Richard Tambwe Hiza (Chama cha Wananchi -CUF) waliorejea CCM wakimwaga sifa tele za uzuri wa CCM baada ya boti yao kutoboka walipokuwa katikati baharini.

Ngawaiya aliyekuwa Mbunge wa Moshi Vijijini msimu uliopita,
alirejea CCM baada ya kukorofishana na Mwenyekiti wake wa TLP, Augustine Mrema ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa dalili za kutimuliwa uanachama wa chama hicho.

Mkurugenzi wa Habari na Ueneza wa Sera wa Chama cha Wananchi (CUF), Tambwe Hiza alichepuka na kurejea CCM baada ya Prof Ibrahim Lipumba kumwengua kwenye cheo hicho.

Baadhi ya wengine waliorejea CCM kwa nyakati tofauti na kwa
maneno ya kufurahisha baraza ni Evarist Maembe (CHADEMA), Frank Magoba (CUF) na Teddy Kasela-Bantu (UDP).

Wote hawa walipokuwa kuwa upinzani walikuwa wanaipaka vilivyo CCM na sasa wamegeuka.

Sasa tuseme basi kuwa, sera za CCM huwa bomba na hasa mambo yanapokwenda mrama.
 
Back
Top Bottom