Dr Hussein Mwinyi awe rais wa Tanzania 2015

Status
Not open for further replies.
Kwa vile Zitto ameonekana kuwa ana nia ya kugombea uraisi mwaka 2015 baada ya muda wa maendeleo ya uhakika yanayoletwa na Kikwete kuisha. Ni vyema sasa ikaangaliwa kwa upande wa ccm ni kina nani wenye uwezo wa kugalagaza wapinzani kwenye uchaguzi. Ni ukweli kuwa ccm itashinda tena kwa kishindo 2010 na kwa kishindo zaidi 2015, 2020, 2025, 2030, 2035 nk, mimi naanza na huu uchaguzi wa 2015 na kumpendekeza Dr Mwinyi kwa hii nafasi muhimu kabisa.

Ni msomi na mchapakazi mzuri. Ni mchamungu na msafi. Mwenzetu huyu ni mpole na mkarimu kama baba yake. Ruhusa na maendeleo ya watanzania wote kama aliyoleta baba yake. Ataendeleza sera za maendeleo za ccm na kuwanyima wahafidhina nafasi ya kuvuruga nchi.

Dr Hussein Mwinyi for president of Tanzania - 2015

Alikwenda JKT? au ndie aliyesababisha JKT ivunjwe? ni KIROBOTO Huyo
 
Ndege wa rangi moja huruka pamoja.Unaweza kuwaona wengine wanakunyakunya ovyo wakiwa wamekusanyika ardhini ukamwona mmoja hanyi ukaanza kumsifia "ndege wangu huyu msafi" na kumbe ukiwafungulia wakaruka angani yule mmoja uliyesema "msafi"ndio kwanzaa anaachia mzigo mzito na kwa vile yuko juu anatembea atasambaza mzigo wake kila mahali juu ya paa,kwenye nguo ulizoanika,kwenye nafaka ulizoanika na hadi kwenye utosi wako mwenyewe!utabaki unasema "mbona chini alikuwa msafi?"waungwana watakuambia "ulipowaona wenzie wanakunya haukupaswa kufungua banda,ungesubiri hadi wote wanye,maana hawa ni ndege wa aina moja,wana rangi moja,ama la,unataka ndege mwenye tofauti nenda kanunue wengine wapya!"...aargh,nisonge nguna yangu nile mie!
 
Hii nchi urais imekua kitu cha kawaida sana.ni lini tutaiheshim hii taasisi?kama kila mtu anajiona anaweza kuwa rais.majanga majanga...
 
Sijui kama itawezekana. Kuna kasystem ndani ya ccm ka wakristo na waislam kupokezana kijiti. Hako kasystem kanaonyesha Rais ajaye kama atatoka CCM, believe or not, atakuwa mkristo! Hiyo ndiyo hali halisi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom