Dr Hussein Mwinyi awaomba madaktari kusitisha mgomo

Mbona kaka unaongea uongo! Nani kakwambia kuwa Hosen Mwinyi kuwa Ni Mzenji ???

Hata angekuwa hapana tatzo kwani Wizara ya ni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, au hujui kama Tanganyika haipo?

Tuitafute Tanganyika ndio tuanze kujidai.

Ni kweli kwamba Hussein Mwinyi ni Mzenji, ni Mbunge wa Kwahani-Unguja.
Pia ni kweli kuwa Mambo ya Afya si mambo ya Muungano.
Sijui unachobisha na kutetea ni nini hasa!
 
Kweli vilaza kama Mch Rwakatare, Munde, Vick Kamata, Nyangwine, Mkumba, Nchemba wanastahili Tsh 6,000,000 halafu Daktari anapata laki 9. Give me a break!!!!!!

Wabunge wengine pale wanatoa maoni juu ya mambo ya economics wakati hawana qualification zozote[hawana CV zinazoonyesha kwamba wanaweza kutoa maoni kuhusu mambo ya economics,kwa hiyo wanafanya usanii] za kutoa maoni hayo. Wanazungumza maneno ya mitaani tu,and then they want to walk away with millions of shillings.
 
Sasa Speaker anasema '' Wabunge kaeni kimya,hili swala tumeshalipeleka Mahakama Kuu'' Sasa sijui hiyo Mahakama Kuu itatoa uamuzi kabla ya leo saa sita usiku,au sijui vipi. Hapa naona,mgomo ukianza,the hospitals must be secured,ama sivyo madaktari wanaweza kukung'utwa na ndugu za wagonjwa.
 
Alicho ongea Waziri wa Afya ni kweli,Madhara ya Mgomo wa madaktari ni mkubwa sana kuliko tudhaniavyo.

Amewaomba wasitishe mgomo.

Mambo ambayo wameshindwa kuyafikia muafaka serikali ipo teali pia kuzungumza Nao tena.

Watanzania tumechoshwa na usanii wa hii Serikali dhaifu.

Wanayajua yote ambayo Madaktari wanayataka. Wameshafanya mazungumzo mara mbili bila kuwepo na utekelezaji wowote toka Serikalini.

Watangaze hadharani kwamba madai yao yatatekelezwa mara moja badala ya kutaka kuendelea kupiga soga lisilokwisha.
 
Twambie Hussein Mwinyi ni mbunge wa toka Zanzibar au Tanganyika? Acha unafiki na kujipendekeza kama kawaida yenu wana CCM!
Mbona kaka unaongea uongo! Nani kakwambia kuwa Hosen Mwinyi kuwa Ni Mzenji ???

Hata angekuwa hapana tatzo kwani Wizara ya ni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, au hujui kama Tanganyika haipo?

Tuitafute Tanganyika ndio tuanze kujidai.
 
Back
Top Bottom