Dr. Hoseah apata kigugumizi kuhusu DOWANS..................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Hoseah abanwa kuhusu Dowans Send to a friend Monday, 31 January 2011 20:25 0diggsdigg

hoseah.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah

Ramadhan Semtawa na Sadick Mtulya

MZIMU wa mkataba tata wa Kampuni ya Richmond kisha Dowans, umezidi kumtafuna Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah, baada ya wabunge kumbana wakimtaka afafanue tena usahihi wa taarifa yake ya awali iliyosafisha mkataba huo ambao umeibua utata kwa Kampuni ya Dowans.

Takukuru iliwahi kufanya uchunguzi wa mkataba huo wa Richmond uliosaniwa Juni 23, 2006, ikitumia Sheria ya Rushwa ya mwaka 1971 na kutoa ripoti iliyobainisha ulikuwa halali, lakini uchunguzi wa Kamati Teule ya Bunge ulibaini ulikuwa wa kifisadi.

Ikiwa sasa ni miaka karibu minne tangu Takukuru kutoa ripoti hiyo huku kukiwa na mjadala mzito kuhusu malipo ya Sh94 bilioni kwa Dowans , baadhi ya wabunge jana wameamua kugusa majeraha hayo wakimtaka Dk Hoseah ataje wamiliki wa Richmond anaowafahamu ili kufungua njia kuwabaini wamiliki halali wa Dowans.

Vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya kikao cha semina ya siku 10 kwa wabunge kinachoendelea jijini Dar es Salaam, kilifafanua kwamba Dk Hoseah alitakiwa afafanue ilikuaje aisafishe Richmond ambayo sasa inaletea nchi matatizo kupitia Dowans.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, Dk Hoseah alirushiwa makombora hayo wakati akipokea maoni kutoka kwa wabunge mbalimbali kuhusu mada yake aliyoiwasilisha, na wakati wa majumuisho ndipo alipogeuka mbogo na kujibu mapigo kwa jazba.

"Hosea kabanwa kaambiwa yeye aliisafisha Richmond ambayo baadaye ilirithi mkataba wa Dowans, vipi sasa mkataba huo unaonekana kuitesa Serikali... ndipo alipoanza kujibu kwa ukali," alifafanua mbunge mmoja ambaye aliomba kuhifadhiwa jina.

"Amegoma kuwataja wamiliki na amekuwa mkali kweli kweli na kwambia..., amesema kabisa siwezi kuwataja. Aliulizwa kama Richmond haina matatizo mbona Dowans ina matatizo wakati mkataba ndiyo huo iliorithi?"

Hata hivyo, baada ya kubanwa sana, Dk Hoseah alijitetea akisema atakuwa tayari kuwataja wamiliki wa Dowans na hata wale wa Richmond endapo akiitwa katika kamati za Bunge na si katika semina hiyo.

Mkataba wa Richmond uliangusha Baraza la Mawaziri la kwanza la Serikali ya Awamu ya Nne baada ya Edward Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu Februari mwaka 2008, kufuatia kashfa hiyo.

Hata hivyo, badaye akiwa nje kwa mapumziko ya mlo wa mchana, Dk Hoseah ambaye awali aliwasilisha mada yenye kichwa cha habari, "Nafasi ya Bunge Katika Mapambano Dhidi ya Rushwa Nchini Tanzania," alipoulizwa yaliyojiri ndani, alijibu, "Ndiyo, nimesema siwezi kujibu kwasababu suala hilo liko bungeni na katika vyombo vya sheria."

"Nyie wenyewe mnajua na wao wabunge wanajua suala hilo angeulizwa spika liko bungeni, lakini pia liko mahakamani sasa nianze kuingilia taratibu za kisheria, siwezi. Lakini, hawa wabunge wanajuana wenyewe pia."

Pamoja na kubanwa huko, Dk Hoseah aliwatahadharisha wabunge kuacha vitendo vya rushwa na akawasisitizia kuwa bado anaendelea kuwachunguza kuhusiana na vitendo vya rushwa vilivyoajiri katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

“Bado ninaendelea na mchakato wa kuchunguza wabunge waliotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa na nikikamilisha uchunguzi, watafikishwa mahakamani,’’ kilisema chanzo chetu.

Kutokana na majibu hayo, wabunge wa CCM walimjia juu Dk Hoseah na kumhoji ni kwa nini aliwachunguza wagombea wa CCM pekee na kuwaacha wa upinzani.

“Dk Hoseah alijibu, ata wagombea wa upinzani aliwafuatilia nyendo zao na pia wapo ambao anakamilisha uchunguzi ili awafikishe mahakamani, lakini aliweka mkazo kwa wagombea wa CCM kutokana na kwamba kama angefanya hivyo kwa wapinzani, angeeleweka kuwa ametumwa na CCM kusambaratisha upinzani,’’ kilisema chanzo kingine.

Chanzo hicho kilisema, Dk Hoseah alijitetea kuwa, Takukuru haipaswi kulaumiwa pekee katika kufikisha kesi mahakamani na kwamba hatua hiyo hutakiwa kufanywa na ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP), baada ya kukamilika kwa taratibu zote.


Katika mada yake ya awali, Dk Hoseah alilipa Bunge changamoto kuisimamia Serikali na kuongeza, "Msisitizo mkubwa katika kuhakikisha rushwa inadhibitiwa ni kwa Serikali kuwa wazi (Transparency) na kuwajibika katika maamuzi yake (Accountability)."

Mkuu huyo wa taasisi yenye dhamana ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini ambaye mara kwa mara mada yake ilipingwa na baadhi ya wabunge waliokuwa wakiguna, "mmm," alifafanua kwamba, uwazi na uwajibakaji wa Serikali unapaswa kuwahikikishia Watanzania maamuzi yake yanazingatia maslahi ya nchi.

"Na Bunge linawajibu huu wa kikatiba kuona kuwa uwazi na uwajibikaji unazingatiwa wakati wote na kuwa ni sehemu ya utamaduni wa utawala bora," alisisitiza Dk Hoseah ambaye hivi karibuni alinukuliwa na mtandao wa Wikileaks akimtuhumu Rais Jakaya Kikwete, akidai hana dhamira ya dhati kupambana na rushwa kubwa.

Kuhusu nafasi ya Bunge na mapambano dhidi ya rushwa, Dk Hoseah aliupongeza mhimili huo wa dola wa kutunga sheria, lakini akautahadharisha, "msisitizo mijadala hii isitawaliwe na chuki, hasira na kukomoana bali izingatie ushahidi na ukweli."

....Ikifanyika hivyo haki itatendeka na mitafaruku kati ya mtu na mtu au vikundi na vikundi haitatawala taswira ya Bunge linalojali maslahi ya Watanzania kwasababu ukweli utabaki na ukweli hauwezi kubadilishwa kwa kutupiana lawama au kuwekeana chuki baina ya mtu au kikundi kimoja dhidi ya kingine."

Katika angalizo lake ambalo liliongeza mguno kwa wabunge, Dk Hoseah alisema, umefika wakati sasa tuhuma zozote za rushwa zijadiliwe kwa kuangalia ushahidi unaothibitika na si hisia, kitu alichokiita hakitaweza kuleta tija katika mapambano dhidi ya rushwa.

Huku akinukuu tafiti mbalimbali duniani, Dk Hoseah alisema rushwa inachangiwa na sababu mbalimbali zikiwemo utumiaji wa madaraka vibaya, tamaa na uroho wa mali, migongano ya maslahi, kujuana katika kutoa ajira na zabuni mbalimbali, mmomonyoko wa maadili na kukosekana kwa uwazi na uwajibikaji.

Dk Hoseah aliwalipua wabunge akiwataka kuacha kutumia rushwa katika kupata nafasi ya uwakilishi kwa kutumia njia za rushwa wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Hoseah tangu kuibuka sakata la Richmond, amejikuta akiwa katika vita pana na wabunge hasa wapambanaji wa ufisadi mvutano ambao ulikorezwa zaidi na uamuzi wake wa kuchunguza kile alichokiita ni posho mbili.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments




+1 #2 CAROLINE 2011-02-01 07:08 Hosea abadilishwe kwenye nafasi aliyo nayo hafai katika nafasi hiyo ni mropokaji sana.
Quote









+1 #1 kipepeo 2011-02-01 05:34 Ningemshauri dr Hossea kuwa makini sana anapoongea na sio kuropoka ,juzi tulisikia kupitia wikileaks akisema kuwa rais hataki mafisadi wafikishwe mbele ya sheria, ili nalo alisema dowans na richmond ziko safi sasa imegundulika kuwa hazina usafi, je Bwana dr hossea kwanini usiresign kwa manufaa ya serikali na wananchi wa Tanzania, Je huoni kama wewe pia unahusika kwenye rusha na kudidimiza harakati za Mr President katia kuinua uchumi wetu kwa namna moja au nyingine, TAFAKARI
Quote







Refresh comments list

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!
 
Wabunge wapaswa kuja na muswada binafsi wa kuhalkikisha Takukuru inakuwa taasisi huru nje ya Ofisi ya Raisi kama ilivyo kwa Kenya..................

Nafasi zote lazima zitangazwe magazetini ili kutoa fursa sawa kwa watanzania wote wenye sifa kuziomba...............

Bodi ifanye zoezi la kuwapunguza waombaji na kuwasahili na kutoa mapendekezo yao kwa Bunge .......................

kamati husika ya Bunge iliruhusu wananchi wenye maoni juu ya mapendekezo yaliyotolewa kutoa maoni yao ya kupinga au kuyaafiki mapendekezo tajwa..................................

Baada ya hapo Bunge lipige kura ya kuyapitisha au kuyakataa mapendekezo hayo..............na Raisi kazi yake iwe ni kuthibitisha uteuzi wa watendaji wa ngazi ya ukurugenzi na wakuu wa idara ndani ya taasisi hiyo............

kuwaondoa baada ya uteuzi huo ni lazima Bunge lihusishwe ili kuzilinda ajira zao na waweze kufanya kazi zao bila ya kuiogopa Ikulu ambayo hivi sasa inawazuia wasitekeleze majukumu yao................

Bila ya Takukuru kuwa Taasisi huru kama ilivyo ya Kenya ufisadi utaendelea kushamiri na huku Takukuru wakiendelea kutafuna hela zetu pale hazina lakini hawatakuwa na mchango wa maana kwenye ujenzi wa taifa hili...............
 
PHP:
hana jipya, hizo ndo zilezile kauli za wateule wa mkwere[IMG]https://www.jamiiforums.com/images/styles/JamiiForums/smilies/A%20S%20thumbs_down.gif[/IMG]https://www.jamiiforums.com/images/st...humbs_down.gif

Thank you, Bukanga for this very useful post............................
 
PHP:
hana jipya, hizo ndo zilezile kauli za wateule wa mkwere[IMG]https://www.jamiiforums.com/images/styles/JamiiForums/smilies/A%20S%20thumbs_down.gif[/IMG]https://www.jamiiforums.com/images/st...humbs_down.gif

Tatizo ndugu yangu Bukaga ni kuwa ..............hiyo site uliyoibandika hapo haina lolote lile......................
 
Back
Top Bottom