Dr. Hosea aitikisa Ikulu...

Hakuna faida ya kumwondoa dr hossea na kumwacha kikwete ambaye ni mtuhumiwa wa rushwa na ametajwa kwenye kagoda.
Je, ukimwondoa hosea ni nani atateua mtu mwingine????
Rais katuhumiwa na kuwalinda mafisadi na mwaka huu kaingia madarakani kwa nguvu , akimwondoa hosea atamuweka mtu ambaye atatakiwa asiseme ukweli kama alivyo sema hosea
 
Mabere marando alisema kikwete, lowasaa, mkapa na lowassa ni wasisi wa epa na kagoda .
Kikwete hajakanusha mpaka leo!!!!
Huu ni ukweli mtupu.
Hapa wa kulaumiwa ni kikwete
 
Gazeti la Tanzania Daima la leo linatutaarifu ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Dr. Hosea ameitikisa Ikulu baada ya kubainika aliongea na Shushushu wa Marekani juu ya JK kuwa ni kikwazo cha vita dhidi ya rushwa kubwakubwa.............na ya kuwa JK amekuwa akizuia mafisadi kushitakiwa kwenye mahakama zetu..........kwa visingizio vya ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kuwafikisha mahakamani kazi ambayo ni ya DCI na DPP.......

Gazeti hili limebaini ya kuwa JK amesononeshwa na madai hayo ya Dr. Hosea pamoja ya kuwa tayari amekwisha kuyapinga hadharani kuwa alinukuliwa vibaya...........

Nionavyo mimi Dr. Hosea ataondolewa hivi karibuni kwa makosa ya kutathmini utendaji wa bosi wake na kwa kufanya hivyo alikosa imani na ni utovu wa nidhamu..................Hii tukiachilia mbali ukweli kuwa JK ni mtu wa visasi sana.....................

Ni ukweli usio pingika kwamba Kikwete ndiye kikwazo cha mafisadi kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa kutoa sababu za kitoto kwamba huwezi kumhukumu mtu mpaka ithibitishwe kwamba ana hatia.Hata kama mtandao wa WikiLeaks usinge m-quote Hosea haya tunayajua.Compelling evidence is everywhere.Kinachonikera hapa ni kwamba Hosea anamtupia lawama mwenzie ili aonekana kwamba yeye hana matatizo,mwenye matatizo ni Kikwete.Hizi ni tabia za kitoto.Kwanza yeye mwenyewe ana usafi gani mpaka awe tayari kushughulia mafisadi?Ni mapapa yale yale.Ana tuhuma chungu nzima.
 
Acha wafukuzane Hossea mwenyewe angekuwa muungwana angeachia ngazi kama JK alikuwa kikwazo ktk kutimiza wajibu wake na watanzania tungemwelewa sasa huku kulalamika wakati umekalia TAKUKURU huu ni unafiki, namlaani kwa unafiki huu. ni fisadi pia kwani ana usafi gani.
 
labda sijui vizuri lakini nafikiri PWC ni accounting firm!wamfanyie interview mkurugenzi wa TAKUKURU kwani anatafutwa mhasibu mkuu wa serikali au CAG!!mi nadhani hawtakiwi watu wenye CPA'S na ACCA takukuru

Mdg wangu usiclem maisha,umeckia PWC ni auditing we hutak kusikia kingine,hawa jamaa wanafanya kaz kma TAX consultants na pia kma recruitment agent pia,nazan hadi ajira ya mkurugenzi wa NHC wao ndo walisimamia mchakato mzima
 
labda sijui vizuri lakini nafikiri PWC ni accounting firm!wamfanyie interview mkurugenzi wa TAKUKURU kwani anatafutwa mhasibu mkuu wa serikali au CAG!!mi nadhani hawtakiwi watu wenye CPA'S na ACCA takukuru

pwc ni reqtment firm wanafanyia inteview feld mbalimbali
 
Mkuu, mimi nahisi wewe unajitahidi kumjenga na kumtetea huyu Hosea fisadi mkubwa kwa kutaka kum empty Kikwete ili amuache mahali alipo!!! Hosea si ndiye huyu huyu aliye msafisha fisadi Chenge juzi juzi? Hivi aliambiwa au kulazimishwa na Kikwete ili kumsafisha chenge? I will very glad akifungashiwa virago vyake, tena siyo kesho afungashiwe leo, kama hakutimuliwa jana!! Hosea ameigeuza TAKUKURU kuwa kitu tofauti na madhumuni ya kuanzishwa kwake.

Hosea hana cha kujitetea kwetu hata kwa hao Wamarekani maana hakuna la maana alilokwisha fanya la kufanya tumuonee huruma! kama kweli alizuiwa kumkamata Mkapa na Mwinyi, je alizuiwa pia kumkamata Tannil Somaiya? Chenge? Manji? Mkono?Subash? Lowasa na Rostam?

Hawa wote ni wasanii wanafanya mchezo wa kuigiza. Kikwete akiwa kwenye kona zake anasema kuwa anaangushwa na maafisa wa takukuru na wale wa ofisi ya upelelezi na mwanasheria mkuu lakini hachukui hatua dhidi ya hao wanaomwangusha akianzia kwa wakuu wa taasisi hizo. Then hosea naye anakuja anasema nimezuiliwa kufanya kazi zangu, Mkurugenzi wa upelelezi na Mwanasheria Mkuu nao wanasema hatujawezeshwa kufanya upelelezi au hakuna ushahidi wa kutosha wa kupeleka mahakamani!! ....... na Sinema inaendelelea hivyo hivyo na nchi inaendelea kuliwa tu

Hujanielewa nionavyo ni kuwa Hosea na Jk.....................are birds of a feather.........................na ndiyo maana JK alimuweka hapo kuwalinda JK na mswahiba wake........................hakuna aliyemsafi kati yao.........................
 
Hakuna faida ya kumwondoa dr hossea na kumwacha kikwete ambaye ni mtuhumiwa wa rushwa na ametajwa kwenye kagoda.
Je, ukimwondoa hosea ni nani atateua mtu mwingine????
Rais katuhumiwa na kuwalinda mafisadi na mwaka huu kaingia madarakani kwa nguvu , akimwondoa hosea atamuweka mtu ambaye atatakiwa asiseme ukweli kama alivyo sema hosea
Good point..................JK na Hosea wake waishie ndipo vita dhidi ya ufisadi itaanza kufanyiwa kazi
 
Bora amuondoe na akambakishie uhai wake.

Na mara baada ya hapo, kiongozi wa TAKUKURU ajaye nafasi yake itangazwe magazetini na PriceWatersCoopers wakawafanyie interview ya kufa mtu kisha majina sita yatakayo bakishwa kwenye mchakato yapelekwe Bungeni Dodoma ili nao wakawachuje na kubakisha majina matatu ambayo ndio yatakayopelekwa kwa rais kuteua mmoja tu kati yao kushika wadhifa huo nyeti. Kusiwepo na mambo ya u-KADA wala urafiki katika hili.

Mara baada ya uteuzi, rais atangaze kumachia mikono huru mtu huyo afanye kazi jinsi taaluma yake inavyomelekeza.

Hoja nyeti ila marekebisho ya katiba hususani tunahitaji katiba mpya kuvalia njuga huu ushenzi............wa ufisadi.........................
 
Wikileaks, the guardian uk na wengine wametuhabarisha waliohusika ktk ufisadi wa manunuzi ya rada toka Bae ni waziri mkuu wa zamani, maofisa wawili wa ngazi za juu JWTZ, afisa mmoja wizara ya ulinzi. Wenye majina yao watujulishe. Raisi mstaafu tunajua ni Mkapa
 
Kinachohitajika zaidi in my opinion ni mabadiliko ya katiba ili wakuu wa vyombo kama Takukuru na Tume ya Uchaguzi (among others) wateuliwe na Bunge. That, in my opinion, is critical to development in Tanzania. Na kama CCM wangekuwa na vision, wasingekataa hili na badala yakwe wangerukia ili wapate credit. Short-sightedness yao ndiyo ugonjwa mkubwa kwa nchi yetu na ndiyo itakayoiweka nchi yetu hapo ilipo for a long time.
 
Tanzania ingekuwa nchi ya utawala wa kisheria Kikwete angekuwa "impeached" kwa kukiuka kiapo cha kulinda katiba ya Jamhuri wa Mwungano wa Tanzania. Kwa kumwambia Hosea kuwa rais na waziri mkuu wasipelelezwe amevunja katiba. Mnakumbuka yaliyompata Richard Nixon wa Marekani 1973? Ilibidi ajiuzulu kuepusha kupelekwa jela.
 
Nilishasema humu, Dr Hosea na Sitta wanahitaji sala zetu kwani serikali hii si ya kuambiwa ukweli wasikushike uchawi. JK mwenyewe mara kibao kanukuliwa na vyombo vya habari akisema vita dhidi ya mafisadi ni hatari mno na kwamba inahitaji tahadhari mkubwa mno.

Sasa hebu jiweke katika vyatu vya huyu mtumishi wa chini yake (Dr Hosea) ambaye angependa kuona anafanikiwa na jukumu ambalo Wa-Tanzania tumempa kupiga vita rushwa.

Sasa hata wewe unapokuta ya kwamba wanaotajwatajwa katika mambo ya rushwa ni maswahiba wakubwa wa bosi wako kiasi kwamba wao wakifika ikulu hupita ndani moja kwa moja.

Kwa hali hiyo hata wewe utapata wapi jeuri ya kuwashtaki watu ambao hata bosi wako mwenyewe keshasema mwenyewe kwenye vyombo vya habari kwamba ni hatari mno na kwamba wala hawawezekani??? Isitoshe, Rais wetu huyo huyo amesikika akiwasifika watu tunaowatuhumu kwa UFISADI kwamba ni majemadari kweli kweli na watu mashuhuri sana katika maendeleo ya jamii yetu.

Kama kweli JK naye alikua anasumbuliwa na UFISADI wa baadhi ya watuhumiwa wetu, sehemu nzuri zaidi pa kuwatupilia nje tena mbali kabisa ni kuwazuia watu kama hawa wasipitishwe na chama chao kugombea nafasi ya uongozi yoyote lakini yeye alienda mbali zaidi na kufikia hata hatua ya kuwapigia chapuo ili wakachaguliwe kuongoza.

Sasa kwa lugha ya mwili wa Mhe rais wetu katika hatua hizi zote inatoa ujumbe wowote unaopingana na hayo madai Wikileaks?? Tunawaangalieni kwa mbali huku uraiani. Mauaji na visasi visianzie mambo ambayo wala si siri kwa umma wa Tanzania.

Dr Hosea asiwe kisingizio wala mbuzi wa shughuli katika masuala ya UFISADI unaotisha nchini mwetu.

Alichokisema yule ofisa wa ubalozi wa Marekani kwamba kaambiwa na Hosea ni kweli kabisa na ushahidi uliokuwepo unathibitisha hivyo. Kama JK angekuwa haogopi kuwafungulia mashtaka watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini basi wote (akina Mkapa, Karamagi, Chenge, Rostam na wengineo) wangekuwa wamepandishwa kizimbani na kuiacha sheria ifuate mkondo wake na wale ambao wangeonekana wana hatia kuchukuliwa sheria zinazostahili bila kujali nyadhifa zao zilizopita au za wakati tulionao, lakini wamefanya usanii ili kuhakikisha hawa wote hawapandishwi kizimbani.

 
Tanzania ingekuwa nchi ya utawala wa kisheria Kikwete angekuwa "impeached" kwa kukiuka kiapo cha kulinda katiba ya Jamhuri wa Mwungano wa Tanzania. Kwa kumwambia Hosea kuwa rais na waziri mkuu wasipelelezwe amevunja katiba. Mnakumbuka yaliyompata Richard Nixon wa Marekani 1973? Ilibidi ajiuzulu kuepusha kupelekwa jela.
in Tanzania this will never happen
 
Bora amuondoe na akambakishie uhai wake.

Na mara baada ya hapo, kiongozi wa TAKUKURU ajaye nafasi yake itangazwe magazetini na PriceWatersCoopers wakawafanyie interview ya kufa mtu kisha majina sita yatakayo bakishwa kwenye mchakato yapelekwe Bungeni Dodoma ili nao wakawachuje na kubakisha majina matatu ambayo ndio yatakayopelekwa kwa rais kuteua mmoja tu kati yao kushika wadhifa huo nyeti. Kusiwepo na mambo ya u-KADA wala urafiki katika hili.QUOTE]


Na kwa maoni yangu naona kwa attitude aliyoionesha Slaa anafaa kushika ubosi wa Takukuru kama hosea akifukuzwa, sio urais atachemsha
 
Hosea is nothing, and I don't think if we are doing right to discuss this stupid person.


This is out of wisdom, it is an hypothesis that soldiers do not have a wisdom; prove the alternative if this Null is not true!

We are discussing the issues and events not people; i.e. "JK ni Kikwazo katika Rushwa" was the argument and not otherwise
 
Back
Top Bottom